ufafanuzi wa agano jipya ufunuo - home - african pastors ...d)shabaha ya kitabu e)ujumbe wa kitabu...

140
Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo www.africanpastors.org Na Dorothy Almond mwisho na Askofu Francis Ntiruka

Upload: others

Post on 04-Aug-2020

319 views

Category:

Documents


80 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

Ufafanuzi WaAgano Jipya

Ufunuo

www.africanpastors.org

Na Dorothy Almondmwisho na Askofu Francis Ntiruka

Page 2: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

Kimetolewa na:AFRICAN PASTORS FELLOWSHIP

Station House, Station Approach, AdishamCanterbury, Kent CT3 3JE

United Kingdom

www.africanpastors.org

Ufafanuzi WaAgano Jipya

UfunuoDorothy Almond

© African Pastors Fellowship 2010

Page 3: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1373

UFUNUO WA YOHANAYALIYOMO

UTANGULIZI

a)Mwandishi

b)Walioandik iwa

c)Wakati wa kuandikwa

d)Shabaha ya Kitabu

e)Ujumbe wa Kitabu

f) Mtindo wa Kitabu

UFAFANUZI

SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA1: 1-3 Wito wa Yohana kuandika

4-8 Salaam; na Sifa kuu kwa Baba, Roho, Mwana9-11 Yohana aliagizwa kuandika

12-20 Maono ya Mwana wa Adamu katika utukufu

SURA 2 - 3 UJUMBE KWA MAKANISA SABA2: 1-7 Barua kwa Kanisa la Efeso

8-11 Barua kwa Kanisa la Smirna12-17 Barua kwa Kanisa la Pergamo18-29 Barua kwa Kanisa la Thiatira

3: 1-6 Barua kwa Kanisa la Sardi7-13 Barua kwa Kanisa la Filadelfia

14-22 Barua kwa Kanisa la Laodikia

SURA 4 - 5 MAONO YA MBINGUNI4: 1-11 Maono ya mbinguni: Mungu aabudiwa na uumbaji mzima5: 1-14 Maono ya mbinguni: Mwana-Kondoo wa Mungu

SURA 6: 1 - 8:5 MUHURI SABA: MAONO YA HUKUMU ZA MUNGU6: 1-2 Muhuri ya kwanza: Farasi Mweupe

3-4 Muhuri ya pili: Farasi Mwekundu5-6 Muhuri ya tatu: Farasi Mweusi

Page 4: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1374

7-8 Muhuri ya nne: Farasi wa Kujivujivu9-11 Muhuri ya tano: Maono katika ulimwengu wa kiroho

6:12-7:17Muhuri ya sita: Tetemeko kubwa na kutikiswa kwa vitu vyote7: 1-17 Watumishi wa Mungu watiwa muhuri8: 1-5 Muhuri ya saba: Uhusiano kati ya maombi kwenda juu kwa

Mungu na hukumu kushuka kutoka kwa Mungu

SURA 8:6 - 11:19 BARAGUMU SABA ZA MAONYO YA HUKUMU8: 7 Baragumu ya kwanza

8-9 Baragumu ya pili10-11 Baragumu ya tatu

12 Baragumu ya nne13 Ole tatu

9: 1-12 Baragumu ya tano ambayo ni Ole wa kwanza13-21 Baragumu ya sita ambayo ni Ole wa pili

10: 1-11 Malaika mwenye nguvu na Kitabu kidogo11: 1-14 Mashahidi wawili

15-19 Baragumu ya saba: Tangazo la kufika kwa „Mwisho‟

SURA 12 SHIDA KWA KANISA: UPINZANI JUU YA KRISTONA KANISA

12: 1-6 Maono ya Mwanamke aliyevikwa jua7-12 Vita mbinguni

13-17 Vita kati ya Shetani na Mwanamke

SURA 13 MAONO YA WANYAMA WAWILI13: 1-10 Mnyama atokaye baharini

11-18 Mnyama atokaye nchini

SURA 14 MAONO MBALIMBALI 14: 1-5 Maono ya Mwana Kondoo na waliokombolewa

6-13 Maono ya Malaika watatu14-20 Mavuno - Hukumu ya mwisho

SURA 15 MAONO YA VITASA SABA VYA MAPIGO15: 2-4 Kipengele - Picha ya washindi hali wamefika salama

5-8 Malaika saba kupewa vitasa vya mapigo

SURA 16 VITASA SABA VYA GHADHABU YA MUNGU16: 2 Kitasa cha kwanza

3 Kitasa cha pili4-7 Kitasa cha tatu8-9 Kitasa cha nne

10-11 Kitasa cha tano

Page 5: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1375

12-16 Kitasa cha sita17-21 Kitasa cha saba

SURA 17 MAONO YA KAHABA NA MNYAMA17: 1-18 Maelezo ya Babeli na Tangazo la Kuanguka Kwake

SURA 18 KUANGUKA KWA MJI MKUU BABELI18: 1-8 Hukumu ya Babeli

9-19 Maombolezo ya vikundi mbalimbali

SURA 19 MSHINDO MKUU HUKO MBINGUNI19: 1-5 Sifa kuu kwa Mungu Mshindi

6-10 Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo11-16 Kristo aliyeshinda17-21 Mnyama na Nabii wa uongo waangamizwa

SURA 20 KUFUNGWA KWA SHETANI KWA MIAKA ELFU20: 1-6 Shetani kufungwa kwa miaka elfu

7-10 Shetani kufunguliwa kwa muda mfupi kisha kutupwa katika ziwala moto

11-15 Ufufuo wa wanadamu wote na hukumu ya mwisho

SURA 21 MBINGU MPYA NA DUNIA MPYA21: 1-8 Mungu kuwa pamoja na watu wake

9-22 Yerusalemu, Mji Mtakatifu ukishuka kutoka mbinguni

SURA 22 KUJA KWA KRISTO22: 1-5 Uzima tele

6-22 Hitimisho

UTANGULIZIa. MwandishiMwandishi kama alivyosema ni Yohana (1:4). Alijiita mtumishi (1:1) ndugu namjoli (1:9) na nabii (22:9) ila hakujiita Mtume. Je! alikuwa Yohana Mtume,mwandishi wa Injili na Nyaraka tatu zenye jina lake? Waandishi wote waKikristo walioishi katika karne za kwanza walisema hivyo, Yustini Shahidi,Ireneo, Klementi wa Iskanderia, na Tertulliano, wala hakuna aliyeleta wazo latofauti mpaka Dionysius wa Iskanderia mwisho wa karne ya tatu, na hata yeyehakukataa kabisa. Ni dhahiri kwamba mwandishi alijulikana sana katikamakanisa saba ya Asia yaliyoandikiwa. Upo ushuhuda wa kutosha juu yaYohana Mtume kuishi Efeso wakati wa uzee wake na ya kuwa alifukuzwampaka kisiwa cha Patmo kwa ajili ya kumtetea Kristo. Mwandishi hakuona hajaya kujieleza zaidi, ilitosha ajiite Yohana tu.

Page 6: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1376

Kwa nini mashaka yametokea? Mashaka yametokea kwa sababu ya hali yaKiyunani cha Kitabu cha Ufunuo, hakuna aina yake katika maandishi ya vitabuvingine vyote vya Agano Jipya. Kinatofautiana na kile cha Injili na Nyarakazenye jina lake. Ni Kiyunani cha mtu ambaye lugha yake ya asili ilikuwaKiebrania. Inakubalika kwamba aliweza kuandika Kiyunani cha aina nyingineikiwa aliona vema. Wataalamu wametoa sababu mbalimbali kwa jambo hilo.Sababu moja ya maana ni kwamba mambo yaliyomo ni tofauti na maandishi yakawaida, ni kitabu kilichojaa maono, na njozi, na ushairi. Mara nyingine Mungualisema naye, mara nyingine malaika alimwambia neno n.k. Kwa hiyo mamboyaliyomo ni ya kipekee, ya ajabuajabu. Yohana mwenyewe alisema alikuwa„katika Roho‟ na aliandika kama „nabii‟ hivyo hakuwa katika hali ya kawaida yautulivu wa kuweza kuandika kwa utaratibu. Hakujua atapata maono gani nayatatokea nini, hivyo si ajabu lugha yake ni ya kipekee kulingana na upekee naugeni wa yale aliyoagizwa kuyaandika. Inawezekana Yohana alitumiamkalimani alipoziandika Injili na Nyaraka ila pale Patmo ilikuwa vigumu kumpatamtu wa kumsaidia. Alikuwa amekolewa sana na mambo ya Agano la Kale namarejeo kama 245 yameingizwa katika Ufunuo.

Iwapo tofauti zipo kati ya Kitabu hicho na Injili na Nyaraka, hata hivyo,zinafanana katika mengineyo. Katika Injili na Ufunuo Yesu ameitwa „Neno‟ na„Mwana Kondoo‟ na Yohana ametaja Maji ya Uzima, Mana, Mchungaji nakondoo n.k. Wengine wameona kwamba yaliyomo katika Ufunuo ni tofautisana na tabia ya Yohana Mwenyewe. Kitabu chasema sana juu ya ghadhabuna hukumu za Mungu. Yohana amefikiriwa kuwa mpole, yule mpendwaaliyeegemea kifuani mwa Yesu na kuwa karibu naye zaidi ya wengine, hatahivyo, ni vema tukumbuke kwamba Yesu alimwita „mwana wa ngurumo‟(Mk.3:17). Wakati fulani alitaka kuleta ghadhabu ya Mungu juu ya Wasamaria(Lk.9:54). Huo ukali unahusu ujumbe aliopewa, si yeye.

Mwandishi alisema alikuwa nabii (22:9) na ya kuwa ilimpasa atoe unabii (10:11)na ya kuwa Kitabu ni unabii (1:3; 22:10,18,19). Potelea mbali mwandishi ni yupikatika 1:1 Yohana amekaza kwamba asili ya Kitabu hicho ni Mungu Mwenyewe.

Kanisa Zima lilichukua muda katika kukubali kukiweka katika orodha ya Vitabuvya Kanuni vya Agano Jipya, hasa kwa sababu katika eneo la mashariki Kanisalilikuwa na mashaka juu yake, ila mashaka hayakuhusu Yohana kuwamwandishi bali yalihusu yaliyomo. Jambo moja lililochochea mashaka lilikuwafundisho la „Chiliasm‟ lililotokea wakati wa Montano, karne ya pili, Fundisho hilolilifuliza wazo la Yesu Kurudi na kutawala hapa duniani kwa miaka elfu (Ufu.20).Wafuasi wa Montano walipotosha habari hiyo kwa kuingiza mawazo ya ajabuhata kundi la watu wao walikwenda mpaka mlima fulani kumngojea BwanaYesu n.k. Jambo la namna hiyo lilisababisha dharau kwa fundisho hilo.

Page 7: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1377

Kitabu kilikuwemo katika Orodha ya Vitabu vya Kanuni ya „Muratorian Canon‟iliyotokea sehemu ya pili ya karne ya pili. Orodha hiyo ilitokea kabla ya ileiliyoukamilisha uchaguzi wa Kanisa juu ya Kanuni ya Vitabu. Katika kukiwekakatika Kanuni ya Vitabu vya Agano Jipya ni dhahiri kwamba Kanisa lilikihesabukuwa Kitabu cha manufaa kwa Kanisa Zima na ya kuwa ujumbe wake ulipatanana ujumbe wa Agano Jipya. Mahali pake pa kuwekwa mwisho wa Vitabu vyotevya Biblia panafaa sana kwa sababu Kitabu hicho kinaauhitimisha ujumbe waBiblia ulioanza na Uumbaji wa kwanza, na kufuatwa na Anguko la Wanadamu,ndipo kuendelezwa na habari za shughuli za Mungu katika historia yawanadamu ili aulete wokovu kamili katika Kristo. Kitabu cha Ufunuo kina habariza mwisho, wa Uumbaji mpya na Uzima kupatikana tena, na laana za Angukokugeuzwa kuwa baraka. Kristo aliyezishinda enzi za uovu pale Msalabaniaonekana katika ushindi wa mwisho wakati wa kuziangamiza enzi zote zilizokinyume cha Yeye na Mungu. Ndipo mwisho kabisa Mungu yu karibu kabisa nawatu wake wakiishi pamoja katika Mji/Bustani. Ingekuwaje kama Biblia ingekosakuwa na habari hizo za ushindi wa mwisho?

b. WalioandikiwaWakristo katika makanisa saba ya Asia Ndogo (1:4; Sura 2-3).

c. Wakati wa KuandikwaBaadhi ya wataalamu wanafikiri kwamba kitabu hicho kiliandikwa wakati waKaisari Nero, kama B.K.64; na wengine wanafikiri kiliandikwa muda mfupibaada ya Nero, ila wengi zaidi hufikiri kiliandikwa mwisho wa utawala waKaisari Domitiani (B.K.81-96).Wote hukubaliana kwamba kiliandikwa wakati wa mateso.

Wazo la kufikiri kuwa ni wakati wa Nero latokana na habari iliyoandikwa katikaUfunuo 11 iliyotaja hekalu, na watu kufikiri kwamba hekalu lililotajwa ni lile laYerusalemu lililobomolewa B.K.70. Kwa hiyo lazima Kitabu kiwe kimeandikwakabla ya wakati huo. Ila tukisoma kwa uangalifu 11:1ku. haisemi juu ya„kubomolewa‟ kwa hekalu. Neno „hekalu‟ limetumika kueleza uhalisi wa kiroho sijengo.Pia ulikuwapo uvumi uliosema kwamba Nero hakufa na baadaye wazo hilolilibadilika kusema kwamba alikufa lakini atafufuka (Ufu.13:14; 17:8ku). Baadhiya wataalamu wanafikiri kuwa Kitabu kiliandikwa wakati wa Kaisari Vespasian(BK.69-79) kwa sababu ya Wafalme 7 kutajwa katika sura ya 17. Ugumu nikujua kuanzia na nani katika mfuatano wa MaKaisari na kama ni vizurikuwaingiza katika hesabu hiyo saba wale waliotawala kwa muda mfupi sana.

Watu wasiokubali kwamba Kitabu kiliandikwa wakati wa Nero wanaonakwamba mateso ya Nero hayakufanana na yale yaliyotokea wakati waDomitiani. Mateso ya Nero yalitokea palepale Rumi, na kwa sababu Nero

Page 8: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1378

alitafuta „kisingizio‟ kwa jambo baya ambalo wengi walidhani yeye alilifanya lakuunguza moto majengo ya Rumi kwa sababu alitaka kuyajenga kwa upya.Uvumi huo ulipopata nguvu na kuenea kwamba yeye ni asili ya huo moto basiakatafuta kuupoza uvumi huo kwa kuwanyoshea kidole Wakristo nakuwasingizia kwamba ni wao waliofanya. Hivyo Wakristo hawakuteswa kwasababu ya imani yao, bali kwa mapenzi ya Nero aliyetaka kuondoa mashaka yawatu juu yake. Katika Ufunuo picha ni ya mateso kutokea mahali pengi nakusababishwa na Kaisari kudai afanyiwe ibada. Katika Ufunuo jambo hilolimetajwa kuwa „kumsujudu mnyama‟ (13:4,12,15; 14:9,11; 15:2; 16:2; 19:20;20:4). Wakristo walishindwa kumfanyia Kaisari „ibada‟ ambayo waliona ni hakiapewe Kristo peke yake.

Wakati wa Domitiani hali ya kumwaza na kumwabudu Kaisari na kumfanyakama „mungu‟ iliendelezwa hata yeye alidai aitwe bwana na mungu. Kwa hiyo, sipale Rumi tu, hata katika miji na vijiji vya majimbo siku za kumfanyia ibada nakumkiri kuwa „bwana‟ ziliwekwa. Wakristo walishindwa kutii amri ya kufukizauvumba kwenye sanamu yake na kusema Kaisari ni Bwana, kwa hiyo,waliwindwa na kukamatwa na kuteswa. Neno hilo halikuwasumbua watuwengine kwa sababu waliiamini na kuiabudu miungu mingi. Pia, watu wengiwalikuwa radhi na utawala wa Rumi ulioleta mafanikio mengi kwao, walahawakuona shida yoyote katika kupata nafasi hii ya kuonyesha shukrani yaokwa Dola na Mkuu wake. Ila kwa Wakristo Mungu alikuwa Mmoja tu na Bwanawao alikuwa Mmoja tu, Kristo. Kwa upande wa serikali Kaisari aliona jambo hiloni njia ya kutia nguvu utawala wake katika Dola zima na ilitoa nafasi kwa watuwa desturi na mapokeo na miungu mbalimbali kuufikia umoja wa kuishi katikaDola moja, wote wakijiunga katika tendo hilo mara kwa mara, huku waliruhusiwakuendelea na desturi na mila zao. Desturi hii ilianza polepole ila hakunaushuhuda wa Domitian kutoa amri maalumu bali ni viongozi wa majimbo namaliwali wa maeneo waliofuatia mambo hayo wakitaka kujulikana kama watiifusana wa Dola. Ni hao walioweka siku za ibada kufanyika na nafasi kutolewakwa raia kufukiza uvumba na kumkiri kuwa bwana na mungu. Watu waliokataakuitii amri walihesabiwa wasaliti nao waliteswa hata wengine waliuawa nawengine walifukuzwa makwao na kulazimishwa kufanya kazi za shokoa. Ndiyosababu katika Ufunuo adui mmoja mkubwa ni Serikali na viongozi wa siasa. Hiini tofauti na jinsi serikali ilivyowaziwa wakati wa Paulo na Petro (Rum.13:1ku. 1Pet.5:2,13).

Ipo sababu nyingine ya kufikiri Kitabu kiliandikwa wakati wa Kaisari Domitianinayo ni hali ya makanisa saba yaliyotajwa katika sura 2 na 3. Makanisayanaonekana kama yamekuwapo kwa muda. Antipa ameuawa kwa imani yake(2:13). Pale Smirna Wakristo walionywa watateswa vikali hivi karibuni (2:10)wale wa Filadelfia pia walionywa juu ya saa ya kujaribiwa (3:10). Katika 6:9 rohoza wale waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu zimetajwa na katika sura ya 17„mwanamke amelewa na damu ya watakatifu‟. Wengine wamekuwa

Page 9: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1379

Wakristo kwa muda mrefu na wa kutosha hata baadhi waliambiwa kwambawameuacha upendo wao wa kwanza (Ufu.2:4). Wengine wamekuwa „hai‟ ilawamelegea kiasi cha „kutaka kufa‟. Katika andiko la Polikarpo inaonekanaKanisa la Smirna halikuwepo mpaka B.K.64. Kwa hiyo, ni vigumu kuwazaKitabu kiliandikwa wakati wa Nero.

d. Shabaha Ya KitabuYohana alikuwa mchungaji mwenye mzigo wa kuhifadhi kondoo wake, waleWakristo katika shirika zao, pale Asia Ndogo, hasa wale wa makanisa sabayaliyotajwa katika sura ya pili na ya tatu. Walikuwa wachache waliozungukwa naumati wa watu walio kinyume cha imani yao. Alijua wamekwisha kupatwa namateso (Antipa ameuawa 2:13) ila hayo yalikuwa malimbuko tu ya matesomakali zaidi yatakayofuata. Katika dhiki yake alijisikia kuwa dhaifu sana kwasababu hakuweza kuwa pamoja nao na kuwasaidia. Atawezaje kuwatayarishakwa dhoruba itakayovuma hivi karibuni? Yeye mwenyewe amekwisha kupatwana shida, amefukuzwa mpaka kisiwa kidogo cha Patmo, yu mbali na wauminiwenzake, hana la kufanya ila kuwakumbuka na kuwaombea daima. Wakristowengi walianza kusikia shaka juu ya ukweli wa Kristo kuwa Mwana wa Mungumwenye kutawala mambo yote. Kwa ukali wa mateso yao na uzito wa maudhiwaliyopata ilionekana kwamba ni Kaisari aliye mkuu si Kristo. Kaisari alikuwamkatili, alidai aabudiwe kama mungu, kwa hiyo itakuwaje kwa Kanisa lisilo nanguvu wala sauti? Ndipo Mungu akamjia Yohana kwa mfululizo wa maono nakumwagiza ayaandike mambo atakayoyaona na ujumbe atakaousikia nakutuma „ufunuo‟ huo kwa makanisa saba ya Asia Ndogo.

Pamoja na mateso Kanisa „lilishambuliwa‟ na „uzushi‟ yaani mafundisho namaisha yasiyopatana na Injili ya kweli. Uzushi uliingizwa kutoka nje pamoja nakuzuka ndani ya shirika za Kikristo. Mara nyingi mafundisho ya uongoyalisababisha maisha yasiyowapasa Wakristo. Kwa hiyo kutokana na mzigowake Yohana aligusa mambo hayo katika barua zake kwa makanisa saba,akiwaita watubu na kuyatengeneza mapungufu yao na kuwaonya juu yamatokeo yake wakikosa kutubu. Mitindo ya maisha ya watu walioishi katika Dolailitofautiana sana na mtindo wa maisha ya Kikristo. (Ndivyo ilivyo kila wakati).Yohana alitaka Wakristo wawe tayari kupambana na mazingira yao, wasiogopekuwa tofauti na wengine, wala kwa vyovyote wasiridhiane na hali zilizopo. Kwahiyo alimtukuza Kristo machoni pao ili wamwone kuwa wa thamani kuliko vituvyote vingine na zaidi wawe na uhakika kwamba Yeye ndiye Mshindi,alizishinda nguvu na enzi za uovu pale Msalabani, daima anaendelea kuzitiishachini yake, na mwisho kabisa zisizokubali kutiishwa chini yake zitaangamizwakabisa kabisa. Ni busara sana wasirahisishe maisha yao ya sasa ambayo nimagumu ili waushiriki na Kristo ushindi na utukufu wake wa baadaye.

Page 10: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1380

e. Ujumbe wa KitabuUjumbe hasa ni kwamba mambo hayawi kama yanavyoonekana kuwa. Kwakutazama mambo ya nje ni dhahiri kwamba Dola la Kirumi lina nguvu nyingi,linatawala, linashinda Kanisa. Ila kiroho, sivyo ilivyo hasa. Potelea mbali jinsiinavyoonekana, ni Mungu anayeushika usukani na kuyaongoza matukio yaulimwengu huu. Mungu hujiingiza kwa nguvu katika historia ya wanadamu, naiwapo inaonekana Kaisari anatawala, lakini hasa Yesu ni mtawala kutokana naKufa na Kufufuka kwake. Yeye ameshinda dhambi, maovu, Shetani na enzi zauovu, upinzani wote, na mauti (Kol.2:15) na kwa wote wanaomwamini Kristo,mauti si neno la mwisho. Kwa ushindi wa Msalaba Yesu amestahili kukifunguakitabu na kuzivunja muhuri zake (Ufu.5). Kitabu kina mpango wa Mungu wakuzileta falme na enzi zote za dunia na za ulimwengu wa kiroho ziwe chini yake.Wakristo wapaswa kusimama imara na kukabili udhalimu na maovu, wasiweradhi na mambo jinsi yalivyo, kwa sababu mwisho wa mambo yote ni ushindi waMungu na haki yake. Utu wema utashinda uovu, ukweli utashinda uongo,uaminifu utashinda uasi na upinzani. Kwa hiyo, kwa sababu ya ushindi ambaobaadaye utadhihirika wazi na kwa uhakika, ni busara watu wajihusishe namakusudi ya Mungu wakati huu wa sasa hata ikiwa watateswa kwa kufanyahivyo.

Jambo la „nguvu‟ „uwezo‟ linatawala mawazo ya kitabu hicho. Ziko nguvu zasiasa, za uchumi, za filosofia, za elimu, za sayansi, za teknologia n.k. Kitabukinafunua habari za „nguvu‟ nyingine zilivyo tofauti na zile ambazo wanadamuhuzitumia ili wapate ushindi. Ushindi wao hupatikana kwa kutumia mabavu,kufanya vita, kukandamiza watu, na kuutumia werevu mbalimbali n.k. Ila Munguanatumia nguvu nyingine, „upendo‟, na kwa „nguvu‟ ya upendo ataushinda uasiwote wa wanadamu. Pale Msalabani upendo huo ulidhihirika wazi Yesualipokubali kuwa „Mwana Kondoo‟, dhabihu ya dhambi, na tangu hapo watu„wameshindwa‟ na nguvu hiyo ya upendo nao wameuitikia kwa kujitoa kabisakwake Yesu na kumpa Yeye utii wao wote. Kama Kristo alivyoshinda kwakupitia matesoni vivyo hivyo wafuasi wake wapaswa kuzikanyaga nyayo zilezileza mateso ili wao nao waingie kwenye utukufu wake na kuishi naye milele namilele. Kanisa halitaepa mateso, ila litalindwa na Mungu, na Kristo ameahidikwamba milango ya kuzimu haitalishinda (Mt.16:18).

Kwa hiyo ujumbe wa Kitabu ni ufunuo wa mambo jinsi yalivyo machoni mwaMungu ambayo ni tofauti na jinsi yaonekanavyo kwa macho ya kibinadamu nakwa nje tu. Ni „ufunuo‟ kwa waumini ili „wauone‟ uhalisi na ukweli wa mambo. Niujumbe wa kuwatia moyo wale wote wateswao kwa imani yao na kuwasihiwasikate tamaa wala wasiridhiane na kujisalimisha wakati uaminifu waounapopimwa. Mungu anayaona machozi yao, maombi yao yanasikika nakujibiwa, vifo vyao ni vya thamani, haviwi bure, damu yao italipizwa, na ushindiwa mwisho ni wao. Hawana sababu ya kuona mashaka maana Kristo wao,

Page 11: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1381

baada ya kuuawa, akafufuka, yu hai, anaishi na kumiliki milele na milele nayeAtawakaribisha kwenye Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo, kisha watakuwanaye milele.

Kitabu hicho cha Ufunuo kinalenga kuzikuza tabia za subira na uvumilivu nauaminifu kwa Kristo, si kitabu cha kuuamsha utafiti juu ya matukio yambeleni. Hivyo kama jina lake lilivyo, ni Kitabu cha Ufunuo, si kitabu chakuficha mambo, mafumbo yake yaeleweka kwa waumini wa makanisa saba yaAsia Ndogo, wale wenye masikio ya kusikia Roho asemayo kwao (2:7,11,17,29;3:6,13,22).

f. Mtindo wa KitabuKama jina lake lilivyo, ni Kitabu cha Ufunuo, na ni katika mfuatano wa vitabuvya namna hiyo vilivyoandikwa wakati ule, hasa na Wayahudi. Kimejaa maonoya kimifano na taswira. Yohana aliona maono ya wanyama wenye pembe na tajin.k. Takwimu zimetumiwa kuwa „ishara‟ za wazo au ukweli fulani, nambarikadhaa zina maana fulani, „siku 10‟ „miaka elfu‟ „watu elfu mia na arobaini nanne‟ „siku 7‟ au nusu yake „siku tatu na nusu‟. Kwa hiyo tunatakiwa kutafutamaana ya mambo hayo kwa kujiuliza „hii ni ishara ya nini?‟ wala tusifanye siku10 kuwa siku 10 hasa n.k. Maono ni ya matukio yanayotokea au yatakayotokeabaadaye au matukio ambayo hutokea mara kwa mara katika mwenendo waulimwengu huo. Ni ufunuo juu ya jitahada za Mungu katika kupambana nakuyashinda maovu na hatua kwa hatua kuuleta Ufalme wake. Si vema kusematukio hilo ni tukio fulani hasa, kwa sababu laweza kuwa hilo na tena kuwajingine la baadaye.

Kitabu kinasema juu ya mipango ya Mungu na njia zake za kuuingiza nakuusimamisha Ufalme wake akizidi kuzitiisha falme za dunia hii ziwe chini yake.Hasa twaonyeshwa vita kali kati ya mkuu wa ulimwengu huu, Shetani, na YesuKristo. Shetani anao wasaidizi wake na Yesu anao wasaidizi wake. Shetanianafuliza madai na matakwa yake na Yesu husimamisha haki na utawala wake.Vita huzidi kuwa vikali, na katika vita hiyo watu hujeruhiwa na kuuawa. Ilamwishowe, wakati Mungu atakapoamua, vita yote itakwisha, Shetani na jeshilake lote, na wote waliojiunga naye, wataangamizwa. Kitabu kinafunua hukumuza haki za Mungu zinazotokea wakati wote mpaka hukumu kuu ya mwisho. Piakinafunua njia za utekelezaji wa hukumu hizo, Mungu akitumia uumbaji wakekama balaa na misiba mbalimbali kwa kusudi la kuleta watu kwenye toba.

Mengine katika Kitabu hicho yanafanana na mambo yaliyomo katika Vitabu vyaDanieli, Ezekieli, na Zekaria. Watu na matukio vyaelezwa kwa kutumia mifanoya wanyama, matetemeko n.k. na rangi mbalimbali ni ishara ya mambombalimbali kama vita, njaa, mauti, uzima, n.k.

Page 12: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1382

Kitabu kimeitwa „unabii‟ (1:3; 22:7,10,18,19). Maono yake ni Neno la Mungu. Ilatusifikiri kwamba kinatoa habari za historia yote ya ulimwengu. La, siyo. Hasakinafunua kiini cha mambo halisi yaliyowakabili Wakristo katika yale makanisasaba, wala si wao tu, hata na mambo yanayowakabili Wakristo kizazi baada yakizazi, wanapopambana na mambo na hali zilizo kinyume cha imani yao nakusikia ugumu wa kumfuata Kristo kwa uaminifu. Alitaka wauitikie wito wakujitoa kabisa kwa Kristo wakielewa yanayotokea katika mwenendo wa historiana kuwa na uhakika kwamba yote yataisha katika ushindi wa Kristo na watuwake. Alimaliza kila barua kwa kutoa ahadi kwa washindi, na kuwaonyawalioshindwa juu ya hukumu.

Kitabu kilikuwa msaada mkubwa kwa wakati ule, na si wakati ule tu,kimewasaidia wengi wakati wa kuteswa kwa imani yao. Wala si hivyo tu, kwawote walio na wasiwasi wanapouona uovu unazidi na wabaya hufanikiwa,ujumbe ni kwamba mambo hayawi kama yaonekanavyo, Mungu hutawala nakatika vipingamizi vyote Yeye huzidi kuuingiza Ufalme wake, na mwishoweushindi ni Wake, utu wema utaushinda uovu, ukweli utaushinda uongo, uaminifuutaushinda uasi, na upendo utaishinda chuki. Mungu kamwe hazuiliwi asitimizemapenzi yake ya kuuleta Ufalme wake.

MASWALI Jibu kwa ufupi:1. Mwandishi afikiriwa kuwa nani?2. Alikuwa wapi wakati alipokiandika kitabu hicho?3. Kwa nini alikuwa pale?4. Kabla ya hapa alifikiriwa kuwa wapi?5. Kitabu kizima kilipelekwa kwa akina nani?6. Kiliandikwa kwa sababu gani na kwa shabaha gani? Eleza:7. Ni nini ujumbe mkubwa wa Kitabu?8. Eleza Mtindo wa Kitabu.

UFAFANUZI

SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA

1:1-3 Wito wa Yohana kuandikaKatika vifungu vya kwanza Yohana ameeleza jinsi alivyopata kukiandika hichokitabu. Aliagizwa na Mungu kuyaandika mambo aliyoyaona katika njozi namaono mbalimbali na mambo aliyoyasikia yaliyosemwa na Mungu na malaika.Mungu alimwita ayaone na kuyasikia hayo yote na kuyaandika na kuwapelekea„malaika‟ wa makanisa saba (1:10-11,19; 4:1) (taz. maelezo katika ufafanuzikuhusu neno malaika). Aliagizwa kuandika kabla hajapata kuyaona maono(1:11,19).

Page 13: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1383

k.1 Neno la kwanza kabisa ni „ufunuo‟ kwa hiyo shabaha ya kitabu ni kufunuamambo yaliyofichwa na kuwajulisha watu mambo ambayo hawakuweza kuyajuakwa uwezo wao wenyewe. Hasa kuleta mwanga wa mapenzi ya Mungu katikamambo yaliyokuwa yakitokea mahali pao. Waumini „wauone‟ uhalisi wa mambona kutambua maana yake. Maana ya neno „kufunua‟ ni kuondoa kifuniko iliyaonekane wazi mambo yaliyofichwa. Ni vema tukumbuke jambo hilo, kwasababu watu wameona kitabu hicho ni vigumu sana kueleweka, ni kama fumbosi ufunuo. Lugha yake ni ya ajabu, maono yake ni ya ajabu, takwimu zimetumikakama „ishara‟ kwa hiyo zisimaanishwi zilivyo hasa, kwa mfano, siku 7 si siku 7hasa, miaka elfu miaka elfu kamili. Hata hivyo, bila shaka wale walioandikiwawalielewa yaliyoandikwa. Hasa ufunuo ulionyesha jinsi Mungu alivyohusika nakufanya kazi katika yote yaliyokuwa yakitokea na jinsi atakavyoendelea kuhusikana kufanya kazi ili waumini wapatikanao na maudhi na mateso kwa ajili yakumfuata Kristo kwa uaminifu wajue hakika kwamba mateso yao si bure, bali niya maana kubwa katika mpango mzima wa Mungu kuuleta Ufalme wake.Wameingizwa katika vita kuu kati ya Kristo (Bwana wao) na Shetani (adui waBwana wao) na maisha yao na ushuhuda wao ni wa maana sana katika vita hiyo,ni muhimu wasimame imara upande wa Kristo.

Zilikuwapo hatua tano katika tendo la kufunua: Ufunuo ulitoka kwa Mungu mpakakwa Kristo, yaani Mungu alimpa Kristo, ndipo Kristo akamjulisha malaika ndipomalaika akamjulisha Yohana. Kisha Yohana akawajulisha waumini katikamakanisa saba ya Asia Ndogo kwa njia ya kuwaandikia Kitabu hicho. Kwa hiyo,asili ya yote ambayoYohana aliyaona na kuyasikia na kuyaandika ilikuwaMungu, Mungu alikuwa Mtunzi na Yohana alikuwa mwandishi. Hakuna kitabukingine katika Agano Jipya kinachosema kwa nguvu na kwa wazi zaidi juu ya asiliyake kuwa Mungu. Kwa hiyo Yohana alitazamia kwamba kitabu hichokitapokelewa kama Neno la Mungu na uhushuda wa Yesu Kristo.

„akamwonyesha mtumwa wake Yohana‟ Kama ambavyo tumeona katikautangulizi Yohana hakujiita Mtume, ilitosha ajiite Yohana tu. Ujumbe haukuhitajimwandishi aonyeshe cheo chake kwa sababu kitabu chenyewe kinadai kuwa namamlaka ya Maandiko Matakatifu yaliyotoka moja kwa moja kwa Mungu mpakakwa Kristo mpaka ukamfikia malaika hatimaye Yohana. Ni ufunuo wa YesuKristo, ni mali yake aliyopewa na Mungu, ni Yeye aliyeyafunua mambo kwasababu Yeye ni Mwombezi na Mpatanishi. Zaidi ya kazi ya kufunua, Yeye nimtekelezaji wa mambo yake kwa kuwa Yeye amepewa funguo na Yeyehuzitumia kwa kuitekeleza mipango yote ya Mungu katika historia ya ulimwengu.Malaika aliyemwonyesha Yohana alikuwa chini ya Kristo. Kwa hiyo, zaidi yayote, ni Ufunuo wa Yesu Kristo wa kumdhihirisha alivyo hasa katika adhama nautukufu na mamlaka yake. Kristo amethibitishwa kuwa na cheo

Page 14: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1384

kikuu na kuonekana angali akifanya kazi kwa ajili ya Kanisa lake (ling. naMdo.1:1 „yote aliyoanza Yesu). Haikuwepo nafasi kwa mwingine kuingizamengineyo.

„mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi‟ (4:1; Dan.2:28) Mamboambayo yatatokea hayatokei kwa sababu za siasa tu bali kwa sababu ni mpangowa Mungu ulioelezwa katika Maandiko kabla ya kutokea kwake. Maneno „hayanabudi‟ yaonyesha uhakika wa kufanyika kwa mapenzi ya Mungu. Historia si bahatinasibu, ina shabaha. Mungu anakusudia kuusimamisha Ufalme wake nakuzikomesha tawala na enzi zote zingine. Yesu alipokuja mara ya kwanzaaliuleta Ufalme wa Mungu (Mt.4:17) nao unazidi kusimamishwa. Kuusimamishakutachukua muda ila ukweli ni kwamba umeishafika katika Kristo. Yanayotokeakatika ulimwengu yanahusu kusimamishwa kwa Ufalme wa Mungu mpakautakapotimia katika Kristo kuja kwa mara ya pili. Katika hayo, jambo moja lauhakika ni Kanisa kushambuliwa vikali sana na Dola la Kirumi, na ya kwambamashambulio hayo yatatokea hivi karibuni katika maisha ya yale makanisa sabayaliyoandikiwa.

„kuwako upesi‟ maana yake hakuna kukawia. Neno „upesi‟ lina maana mbili,moja ni kuhusu jambo fulani kutokea hivi karibuni. Maana nyingine ni kuhusujambo kutokea „ghafula‟ wakati utakapotimia, ijapokuwa si lazima wakati uwekaribu. Katika jambo la unabii, mara kwa mara, „wakati‟ umefupishwa. KatikaAgano Jipya „siku za mwisho‟ zilianza Kristo alipokuja nazo zitakwishaatakapokuja tena. Hivyo Wakristo wanaishi katika „siku za mwisho‟. KatikaAgano la Kale Danieli alisema juu ya siku za mwisho akieleza kwambakutakuwapo mfuatano wa Madola mbalimbali, ndipo utasimamishwa ufalmeudumuo, usioweza kuangamizwa, na huo ufalme utaziangamiza kabisa falmezote zinazoinuka juu yake (Dan.2:44). Ndivyo ilivyokuwa pale Asia Ndogo. Dolala Kirumi liliinuka juu ya Wakristo na kuwatesa, hivyo Wakristo waliingizwa katikamashindano kati ya Ufalme wa Mungu na milki za dunia. Mambo hayo hayanabudi kuwako, tena upesi. Yohana aliweka vitisho vya mateso katika mazingira namwanga wa Mungu Muumba (sura ya 4 maono ya Mungu Muumba) na Hukumuya Mwisho na Uumbaji wa Mbingu na Dunia Mpya (Sura 20-22).

k.2 „Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo‟ Yohana alikuwa na uhakikakwamba alikuwa akiwaletea watu Neno la Mungu. Manabii walipowatangaziawatu mapenzi ya Mungu walisema kwa nguvu „Bwana asema hivi..‟ naowaliwasihi watu wayashike maagizo waliyopewa kulingana na mapenzi ya Mungu(Amo.3:7). Mungu anapotoa neno lake anatafuta matokeo kiutendaji, hatoi kamahabari tu. Mungu hufunua mapenzi yake na kuwaita watu washirikiane nayekatika kuyatekeleza (Zab.33:9; Isa.55:11). Ni heshima kubwa kulisikia Neno laMungu pia walisikialo wawiwa wajibu mkubwa. Kwa nini Yohana aliteuliwa kupatamaono hayo na kuleta habari zake kwa

Page 15: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1385

makanisa? Kwa sababu alikuwa „mtumwa wa Yesu Kristo‟. Neno „mtumwa‟lilitumika kuthibitisha mamlaka yake ya kufanya hivyo, si neno la kumshushakama ni mdogo. Tena wale wa kuupokea ufunuo huo pia ni watumwa wenzake.

k.3 Halafu ukubwa na umuhimu wa ujumbe wa Kitabu umedhihirika katikamaneno ya kifungu hicho. Wale wote watakaoyashika mambo yakewatabarikiwa. Wale wote watakaosoma ujumbe huo mbele za waumini katikashirika zao watabarikiwa na wote watakaousikia ujumbe huo pia watabarikiwa,na wote walipaswa wayashike mambo yake. Hivyo, Yohana alikusudia wauminiwote wasomewe kitabu kizima kwa sababu kiliandikwa kwa ajili yao.

Ndani ya Kitabu zimetajwa heri yaani baraka saba (1:3, 14:3, 16:15, 19:9, 20:6,22:7,14). Pamoja na baraka, laana imetajwa kwa yeyote atakayeubadili ujumbehuo, ama kwa kuongeza ama kwa kupunguza maneno yake (22:18-19). Kwahiyo ni dhahiri kwamba unabii huo haukuwa matangazo tu ya habari za matukiofulani kwa kuwa watu wote waliombwa sana wayajali maneno ya Kitabu iliwajiandae kwa saa ya kujaribiwa kwa imani yao. Uheri wao ni katika kuushirikiwokovu kamili wa Mungu utakaotimizwa Yesu atakaporudi. Uheri waounategemea ujumbe wa Kitabu hicho.

1:4-8 Salaam; na Sifa kuu kwa Baba, Roho, Mwanak.4 Kitabu kizima kilipelekwa kwa makanisa saba yaliyokuwemo magharibi yajimbo la Asia Ndogo, jimbo mojawapo katika Dola kubwa la Kirumi (Uturuki yaleo). Ama kila kanisa lilipata nakala ya kitabu kizima au yeye aliyefika kwa kilakanisa aliwasomea Wakristo wa pale, sehemu kwa sehemu kitabu kizima, ndipoakaenda kwa kanisa lingine na kufanya vivyo hivyo. Kisha alipomaliza makanisayote saba akaiacha nakala aliyotumia pale Laodikia au akarudi nayo mpakaEfeso. Hatujui ilikuwaje hasa. Twajua yalikuwapo makanisa mengine katikajimbo hilo, pale Kolosai (Kol.1:2) Hierapoli (Kol.4:13,16) na Troa (Mdo.20:5, 1Kor.2:12) na huenda pale Mileto (Mdo.20:17). Twajua kwamba kama B.K.110Ignatio alipitia sehemu ile njiani kwenda Rumi. Yeye aliziandika barua kwashirika mbalimbali, na Trallas na Magnesia zilikuwa baadhi yake, shirika imaraambazo zilikuwapo kwa muda na hii ilitokea miaka 20 tu baada ya wakati waYohana kuandika (ikiwa tunapokea wazo la wengi kwamba Ufunuo uliandikwakama B.K.95). Ni vigumu kujua sababu ya hayo saba kuchaguliwa. YawezekanaYohana alikuwa na uhusiano wa kipekee nayo. Ni dhahiri aliyafahamu mamboyao na mazingira yao sana. Numbari 7 imetumiwa mara 54 katika Kitabu hicho.Ilikuwa ishara ya ukamilifu na utimilifu. Kwa hiyo huenda Yohana aliyachaguamakanisa hayo saba kuwa niaba ya Kanisa Zima, hivyo ni ujumbe kwa Kanisazima. Tunapotazama zile barua saba twaona kila barua ilifungwa na maneno„yeye aliye na sikio na alisikie neno hilo ambalo Roho ayaambia makanisa(2:7,11,17,19; 3:6,13,22). Tukilinganisha na 1:4 Roho ameelezwa kuwa „robosaba walioko mbele ya Kiti chake cha enzi‟. Roho anatosha kwa maisha ya kilashirika (Zek.4:7).

Page 16: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1386

Kila kanisa lilipokea au kusomewa nakala ya Kitabu kizima. Tukiangalia ramaniya sehemu ile makanisa yalikuwa karibu karibu, rahisi kwa mtu kuyafikia.Yametajwa kwa mzunguko, ilikuwa rahisi kuanzia Efeso ndipo kwenda Smirna,ndipo Pergamo, ndipo Thiatira, ndipo Sardi, halafu Filadelfia, kisha Laodikia.Yawezekana miji hiyo ilijulikana kuwa vituo maalum pengine vya posta katikamzunguko wa sehemu ile. Watu wamewaza kwamba hayo makanisa sabayanatoa picha ya hali mbalimbali zipatikanazo katika Kanisa zima. Mahali fulaniKanisa linaendelea vizuri na mahali pengine lina matatizo yanayohitajikutatuliwa. Wakati fulani Wakristo hupoa katika imani yao; mara nyingine Kanisalasumbuliwa na mafundisho ya uongo, mara nyingine Kanisa la mahali fulanihushambuliwa vikali na serikali au kusumbuliwa na watu wa imani nyingine.Twaona kwamba makanisa mengine yalisifiwa moja kwa moja na makanisamengine yalionywa vikali sana na mengine yalikuwa na mchanganyiko wamambo mazuri na mabaya. Ndivyo ilivyo tukiliangalia Kanisa Zima, hata hivyo, silazima iwe hivyo.

k.4 Yohana aliendelea kwa kutoa salaam kwa makanisa hayo, salaam za neemana amani, sawa na alivyofanya Paulo katika Nyaraka zake. Neemailiwakumbusha upendo wa ajabu wa Mungu kwao wenye dhambi, wasiostahili,katika kuwakirimia baraka nyingi kubwa, hasa kwa kuwapokea na kuwahesabiahaki bila kuwahesabia dhambi zao kutokana na upatanisho alioufanya Kristopale Msalabani. Halafu amani ni matokeo ya neema hii, ni tabasamu ya Mungumioyoni mwao, dalili ya afya njema maishani mwao. Ndipo Yohana alipanuamawazo kuhusu salaam hizo kwa kusema kwamba zilitoka kwa Mungu wa Utatualiye Baba, Roho, Mwana.Alimtaja Baba kwa maneno „yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja‟ nimaneno ya kuukaza Umilele wa Mungu Asiyebadilika. Aliweka „aliyeko‟ kwanzakama Yule anayefanya kazi wakati wa sasa, mhusika wa yale yanayotokeakwao. Mungu ni mtangulizi katika kutenda mambo, halazimishwi kutenda ilaachagua kujiingiza katika mambo kwa shabaha ya kutekeleza makusudi yake.Mungu wao ni wa kutegemewa kabisa. Ni kama jina la sifa na cheo linalotoboawazi hali halisi ya Mungu. Pia ni ukumbusho wa Kutoka 3:13-14 Musaalipomwuliza Mungu aseme nini watu watakapomwuliza ni nani aliyemtuma, jibualilopewa lilikuwa „Mimi niko ambaye Niko‟. Mungu wao ni Mungu yule yule waMusa na Israeli, watu wa Mungu waliotangulia. Yohana alirudia kuyatumiamaneno hayo (1:8, 4:8, 9:17, 16:5) (taz. Ebr.13:8).

Alimtaja Roho kwa maneno „zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chaenzi‟ (3:1; 4:5; 5:6). Kwa sababu maneno hayo yatokea kati ya Baba na Mwanayafikiriwa kwamba yamhusu Roho. Kama ambavyo tumeishaona numbari 7 niishara ya utimilifu na ukamilifu kwa hiyo ina maana kwamba iwapo Roho niMmoja Yohana anapenda wasomaji wake wamtafakari katika utimilifu wautendaji wa kazi zake zote. Kwa neema ya Mungu Yeye ndiye aletaye uzima telemaishani mwa waumini. Alionekana mbele ya Kiti cha Enzi ishara ya

Page 17: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1387

utayari wake wa kuyatekeleza mapenzi ya Mungu. Ni vema kusoma Zekaria4:6-10 na Isaya 11:2ku. Isaya alitaja sifa yaani vipawa saba vya Roho. Rohoanajua mafumbo ya Mungu (1 Kor.2:10ku). Kila Kanisa liliambiwa „alisikieasemalo Roho‟ kwa kuwa Yeye Roho yu kati yao na pamoja nao.

k.5 Yesu Kristo alitajwa baada ya Baba na Roho na Yohana alimweleza kwakirefu sana. Kwanza alimwita „shahidi aliye mwaminifu‟ maana yake Yesu katikamaisha yake yote aliutoa ushuhuda wa kweli kabisa juu ya Mungu kwa kumfunua„Baba yake‟ kwa ukamilifu. Yeye peke yake ndiye mwenye ufahamu kamili waBaba, anamjua kabisa kabisa (Mt.11:27). Mbele ya Pilato alisema kwambaalikuja ili aishuhudie kweli (Yn.18:37). Alipoapizwa na Kuhani Mkuu aseme kwelijuu ya Nafsi yake, alimjibu kwa ujasiri na kukiri kwamba alikuwa Mwana waMungu ingawa alijua hakika kwamba itamgharimia maisha yake akifanya hivyo,akawa shahidi mwaminifu (Mt.26:63). Wakristo wataletwa mbele za liwali waKirumi. Ni vema wakumbuke kwamba wao ni mashahidi wa Kristo wanaofuatanyayo zake na ushuhuda wao utasikika, si katika baraza la duniani tu, hatautasikika katika baraza kuu lenye mamlaka kuu huko mbinguni, na Mhukumu wahilo baraza ni mwenye haki na kweli, ataupindua uamuzi wa duniani kamaalivyofanya kwa Yesu, naye atawafufua kutoka kwa wafu baadaye.

Yohana alichagua sifa za Bwana Yesu kwa uangalifu sana. Neno la ushuhudalimekazwa sana katika Kitabu hicho. Yeye pamoja na Wakristo wenzake katikamakanisa yaliyoandikiwa waliitwa kumshuhudia Kristo. Kuwa waaminifu katikakumshuhudia Kristo kutawagharimu maisha yao, baadhi watauawa, baadhiwatateswa, wengine watafukuzwa makwao, wengine watanyimwa kazi nawengine watalazimishwa kufanya kazi za chini hata za shokoa n.k. Antipa waPergamo ameishauawa, Yohana ameishafukuzwa nchini na muda si mrefuwengine watafanyiwa vivyo hivyo. Shabaha ya Yohana ilikuwa kuwatia moyowasomaji wake ili wawe waaminifu kama Yesu alivyokuwa mwaminifu. Jambokubwa ni uaminifu wao.

„mzaliwa wa kwanza wa waliokufa‟ hayo maneno si jina la heshima tu bali zaidiyanahusu uhusiano wa Yesu na watu wake. Kufufuka kwake ni ishara ya ukweliwa ushuhuda wake juu ya Mungu. Ni ushuhuda wa kutegemewa kabisa. Kwasababu hiyo amekuwa mdhamini wa wengine watakaopitia mautini na kuingiakatika Ufalme wake. Yesu ni kuhani wa kweli aliyejitoa Mwenyewe kuwa dhabihuya dhambi za watu wote. Alikufa kweli, akafufuka kutoka wafu kweli na ameingiakatika utawala wake hali amekirimiwa jina lipitalo kila jina na tangu hapo hatuakwa hatua anawatiisha adui zake wote chini yake. Yeye ni limbuko la wotewatakaozikanyaga nyayo zake (Flp.2:5-11). Maneno hayo yaliwafaa sana walewalioandikiwa ambao walitishwa sana na mambo yaliyokuwa mbele yaowalipotazama „wingu jeusi‟ la mateso watakayopata.

Page 18: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1388

„mkuu wa wafalme wa dunia‟ machoni pa walioandikiwa Kaisari ni mkuu, mkatili,wa kuogopwa sana. Ila Yohana ameonyesha kwamba Yesu amempita, Yesu nimkuu wa wafalme na siku moja hata Kaisari atampigia magoti. Hamna nenolitakalowapata bila kibali chake. Yesu kwa kifo chake na kwa kufufuka kwakeameingia katika utukufu na ufalme wake, hao nao watamfuata, watapitia katikakufa, watafufuka, na watatawala pamoja naye. Zaburi 89:27,37 ina habari yammoja atakayezaliwa kuwa „mzaliwa wangu wa kwanza‟ na „kuwa juu sanakuliko wafalme wa dunia‟. Wayahudi waliamini maneno hayo yalimhusu Masihiatakayekuja. Yesu alijaribiwa na Shetani aliyemwahidi milki zote za ulimwenguna fahari yake ikiwa atamsujudu. Hazikuwa mali yake hasa, ila wanadamuwalipomwasi Mungu walijitia chini yake. Yesu alizipata kwa kumtii Baba yakekwa ukamilifu, si kwa kupatana na Shetani wala si kwa kuridhiana na maovu balikwa kupambana nayo hata kiasi cha kumwaga damu yake ili aishinde dhambi(Ebr.12:3,4) (Taz. Efe:1:20-22; Flp,2:9-11; Kol.1:15-18). Hii ndiyo njia kwawafuasi wake.

Katika kusema juu ya uhusiano wa Yesu na wanadamu Yohana alitaja upendowa Kristo. Ni upendo wa milele uliodhihirika wazi kabisa katika ukombozi waulimwengu. Kwa kifo chake aliwapatia wenye dhambi osho kamili la dhambi zao.Maana ya neno „kuosha‟ ni „kulegezwa‟ yaani kuwekwa huru na kutolewa katikautumwa wa dhambi. Mfano wa jambo hilo katika Agano la Kale ni Waisraelikukombolewa na utumwa wa Misri na kuingia kwenye nchi ya ahadi (Kut.12).Kwa hiyo Yohana alipotoa sifa za Bwana Yesu aliwakumbusha wasomaji wakeupendo wa ajabu wa Yesu. Kristo bado angali akiwapenda sana hata wakati huowa mateso. Wao nao wamrudishie upendo kwa njia ya kuwa waaminifu Kwakehata kufa.

k.6 Maneno hayo ni ukumbusho wa maneno yaliyotumika juu ya taifa la Israelibaada ya Kutoka utumwani (19:6). Matokeo ya kazi ya ukombozi ni kwambawote wamwaminio wafanywa kuwa „ufalme wake‟ (2:26; 3:21; 5:10; 20:6) nakuishi kwa shabaha ya kumtumikia mfalme wao, wakijua kabisa kwamba anahaki zote za kuwatawala katika upendo. Pia watamiliki pamoja naye kwa kuwawao ni wana wa Mfalme wa Wafalme. Pamoja na kuwa „ufalme‟ wamekuwa„makuhani‟. Wakristo wote ni „makuhani‟ si wale tu wenye vyeo katika Kanisa.Heshima ya kuhani ni kumkaribia Mungu moja kwa moja wakati wowote, mahalipopote. Wana heshima ya kujitoa kwa Mungu (Rum.12:1-2) na kumtolea sifa nashukrani zao (1 Pet.2:5,9) na kumwomba kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili yawengine. Pengine maana nyingine ni kwamba wamekuwa makuhani yaanivyombo vya kuwaletea watu baraka za Mungu. Wakristo wameingia katika urithiwa Israeli ya zamani.

„naye ni Baba yake‟ Yohana alitaja uhusiano wa kipekee wa Yesu na Babayake (2:27; 3:4,21; 14:1). Kwa sababu Yesu alimtii Baba yake katika kufa

Page 19: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1389

kwake Msalabani (Flp.2:5ku) amehakikisha kwamba Mungu atazishinda enzizote za uovu na dhambi ya binadamu. Jamii ya waumini wanaendelea kumkiriMungu kuwa „Baba‟ wa Yesu Kristo.

Halafu Yohana alifunga sifa hizo kwa kumsifu Mungu wa Utatu. Utukufu aliotajani utukufu wa Mungu wa Utatu. Aliweka waumini na maisha yao magumu namajaribu yao makali katika mwanga wa Umilele na Ukuu na Utawala wa Mungu.Mambo magumu yatatokea kwa ruhusa ya Mungu, si kwa sababu ameshindwakuyazuia, wala si kwa sababu yupo mwingine mwenye nguvu kuliko Yeye. La!hata kidogo! Yeye yuko wakati wote, MaKaisari huja na kuondoka ila Mungu yukowakati wote. Neno hilo ni amini.

k.7 Faraja kuu kwa waumini ni kwamba Kristo atarudi na kuyahitimisha mamboyote, ndipo taabu zao zote zitakwisha na imani ya Kikristo itathibitishwa kuwa yakweli, waliyoyaamini moyoni kwa imani watayaona kwa wazi. „yuaja na mawingu‟ni maelezo ya jinsi atakavyotokea (Dan.7:13; Zek.12:10; Mt.24:30). Katika Aganola Kale mawingu yalikuwa dalili ya uwezo wa matendo makuu ya Mungu(Hes.11:25; Zab.104:3; Isa.19:1). Yesu ataonekana hali amevikwa Utukufu wakewa asili, tofauti sana na hali ya unyonge wa Kuja kwake mara ya kwanza. Kujakwake kutakuwa wazi, dhahiri machoni pa watu wote, adui kwa rafiki, hakunaatakayeepa kukutana naye, wakipenda, wasipende, watamwona. Itakuwa sikuya maombolezo kwa wengi. Wataomboleza, na Yohana alisema wataombolezakwa ajili yake. Kwani waomboleze kwa ajili yake? Je! ina maana watasikitika kwasababu walimwudhi? Au pengine kwa sababu yule waliyemkataa ametawazwajuu kabisa? Hatujui. Je! watatubu? Mbele Yohana mara kwa mara anatajakwamba watu hawapendi kutubu. Ila katika sehemu nyingine inaonekana watuwatajuta. Hasa hoja ya Yohana ilihusu imani ya Kikristo kuthibitishwa kuwa kwelisi kusema juu ya mambo watakayoyapata wasioamini.

Kwa hiyo, kwa Yohana, Kuja kwa Kristo kwa upande wa waumini ni jambo lakuwatia moyo na kuwafariji. Kuja kwa Kristo ni tukio litakalotokea kweli, si dhanatu. Ni onyo kali kwa adui zake na faraja kwa waumini. Maneno „Naam, Amina‟hayana maana kwamba Yohana aliyafurahia maombolezo ya watu ila alikuwa namzigo sana juu ya wale walioteswa na wale waliomdharau Mungu na kulidhihakiJina la Yesu. Zaidi ya yote alitaka haki ifanyike; wateswao wapate haki yao nawatesi wapate haki yao.

k.8 Mungu alisema maneno hayo (alisema tena 21:5). Alfa ni herufi ya kwanzana Omega ni ya mwisho katika alfabeti ya Kiyunani. Wayahudi walitumia herufiya kwanza na ya mwisho za alfabeti yao kama usemi wa kuonyesha utimilifu naukamilifu wa jambo fulani. Mkazo wa Yohana ni kwamba Mungu ni Mkuu,mwenye uwezo wote, hakuna kitu kabla yake, wala hakuna kitu baada yake, walahakuna kitu nje ya uwezo wake. Yeye yuko wakati wote wala hakuna kitu

Page 20: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1390

kitakachomshinda wakati wowote. Ila tunapouwaza ukuu na uwezo waketukumbuke kwamba Yeye hutawala na kuutumia uwezo wake kwa tabia zaupendo, haki, na rehema. Kamwe hautumii uwezo wake ovyo, bila kujali, kwasababu tabia zake zote huwiana. Ilikuwa faraja kubwa kwa wale walioteswakujua kwamba Mungu wao Yuko wakati wote, naye ni Mwenyezi mwenyekuwapenda upeo.

1:9-11 Yohana aliagizwa kuandikaYohana alijihusisha na wale aliowaandikia kwa kujiweka sawa na wao.Hakujiinua na kudai kuwa na cheo au kuwa bora kuliko wao. Alikuwa mmoja wao,ndugu yao aliyeshiriki pamoja nao mateso ya Kristo. Alikuwa katika kisiwa chaPatmo, si kwa sababu alitaka kuwa pale, bali kwa sababu alikuwa amefukuziwapale kwa ajili ya kumshuhudia Kristo. Hatujui ni kwa jambo gani hasaakufukuzwa, ila twajua kwamba viongozi walikuwa wa kwanza kuwindwa namaadui wa Kanisa ambao walifikiri kwamba kwa kuondolewa viongozi shirika zaKikristo zitadhoofika na waumini watapoa. Pale Patmo aliishi kwa shida, penginealipewa kazi ngumu ya shokoa katika mashimo ya madini. Hasa hali ya kutengwana waumini wenzake ilimwia vigumu sana. Patmo kilikuwa kisiwa kidogo, kamamaili nane kwa nne, katika Bahari ya Aegean maili arobaini mbali na pwani yaAsia Ndogo na kilitumiwa na Warumi kuwa „gereza‟ la kuwapeleka walewaliohesabiwa kuwa hatari kwa serikali. Bandari yake ilikuwa ya mwisho kablaya kufika Efeso katika msafara wa kutoka Rumi kwa bahari. Hivyo Yohanaalikuwa na uzoefu kibinafsi wa yale mashindano yaliyopo kati ya Ufalme waMungu na falme za dunia.

Pamoja na kuwa mshiriki wa mateso, Yohana pamoja na waumini wenzake,alikuwa mshiriki wa ufalme na subira ya Yesu Kristo. Hivyo, mateso, ufalme, nasubira viliwiana. Waliteswa kwa sababu ni washiriki wa ufalme. Bila kuwepo kwaufalme wasingalipingwa na bila kujiunga na Kristo wasingaliteswa (Yn.16:33).Kwa sababu walijua hakika ni washiriki wa ufalme waliweza kuvumilia (Mt.24:13).Bila kujaliwa nguvu za ufalme na kupewa uwezo wa kustahimili wangalishindwa.Kwa hiyo waumini wote huwa na hali moja na ujuzi mmoja wa maisha ya Kikristona hali yao na ujuzi wao ni sawa na Bwana wao Yesu Kristo, mfalme wao,aliyeingia Ufalme wake kwa njia ya dhiki nyingi (Mdo.14:22; 1 The.3:3). Kitabukiliandikwa kwa shabaha ya kuwatia moyo wa kuvumilia. Inabidi wayatafsirimateso yao katika mwanga wa kuwa washiriki wa Kristo na ufalme wake. Matesona subira si utangulizi wa kutawala bali ni sehemu ya maana katika kutawala.Maana yake wanatawala katikati ya dhiki zao kwa kuzivumilia. Kuvumiliakunayavika mateso yao heshima ya kifalme. Ni vema Wakristo watakaoteswahivi karibuni waelewe jambo hilo ili wayakabili mateso kwa tumaini si kwawasiwasi. Katika Injili, Yohana alitilia mkazo wa Yesu kutawala kutokaMsalabani, Msalabani palikuwa mahali pa Kutukuzwa Kwake kwa sababu paletabia zote za Mungu, za upendo, haki, utakatifu, rehema n.k. zilidhihirika wazi(Yn.17:1ku).

Page 21: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1391

Yohana alielewa kwamba maliwali wa Kaisari watakapowalazimisha watuwamfukizie Kaisari uvumba na kumkiri kuwa bwana na Mungu, Wakristowatakuwa mahali finyu wakibanwa kabisa kati ya mawili, ama wamwasi Kristoaliye Bwana wao, au wamwasi Kaisari, ambaye kwa kuzidi mpaka wa haki katikakudai kuabudiwa kama mungu amekuwa si bwana wao halali. Wakidumuwaaminifu kwa Kristo kwa kukataa kumkiri Kaisari kuwa Bwana basi kwavyovyote watateswa.

k.10 (ling. 4:2; 17:3; 21:10) „nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana‟. IwapoYohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo kimwili na kijiografia pia alikuwa „katikaRoho‟. Maana yake alitolewa nje ya mazingira yake, asitawaliwe na wakati namahali, akajaliwa kuwa „katika Roho‟ na katika hali hiyo alipewa maono ya ajabuna kuyasikia mambo ya ajabu. Hivyo alikuwa „katika Patmo‟ pia alikuwa „katikaRoho‟. Mahali pa mawe na miamba paligeuzwa kuwa „mlango wa mbinguni‟kwake. (Twakumbuka Yakobo pale Penueli Mwa.32).

Jambo hilo lilitokea „siku ya Bwana‟ yaani Jumapili. Ni hapo tu katika AganoJipya maneno „siku ya Bwana‟ yametumika. Tangu mwanzo Wakristo walizoeakuiadhimisha siku ya kwanza ya juma kuwa siku ya kumbukumbu ya KufufukaKwake Bwana wao (Yn.20:19; Mdo.20:7; 1 Kor.16:2). Ilikuwa siku yao yakukutana na „kumega Mkate‟ yaani kufanya Ibada ya Ushirika Mtakatifu kamaYesu alivyowaambia ila Yesu hakuwapa amri ya kushika siku fulani ila ilitokea tu.

Bila shaka Yohana katika upweke wake alikuwa akiwakumbuka Wakristowenzake akipiga picha mawazoni mwake ya wale wote katika shirika zao,akiwataja kwa majina katika maombi yake na kukumbuka shida na matatizo yao.

Ndipo hali akiwa katika Roho aliisikia sauti ya nguvu sana nyuma yake, hataalishindwa kuieleza ila kwa kusema ilikuwa kama sauti ya baragumu. KatikaAgano la Kale baragumu imetajwa mara kwa mara, hasa wakati wa matukiomakubwa katika historia ya Israeli, kwa mfano, wakati wa Kutolewa kwa Torati(Kut.19:16ku); katika Sikukuu ya Upatanisho (Law.25:9); wakati wa kuta zaYeriko kuangushwa (Yos.6:5) n.k. Katika Agano Jipya baragumu imetajwakuhusu Kurudi kwa Yesu na wafu kufufuliwa (Mt.24:31; 1 Kor.15:52; 1 The.4:16).Ilikuwa sauti kubwa, na wakati wa Agano la Kale, Mungu aliwakusanya watuwake kwa kutumia baragumu (Kut.19:16,19; Law.25:9; Yos.6:5; Isa.58:1). Ilahaikuwa sauti ya baragumu bali ya Bwana Yesu, maana Yohana alisema „kamasauti...‟

k.11 Lakini mambo ambayo Yohana atayaona na kuyasikia hayakuwa kwa ajiliyake tu bali kwa ajili ya waumini katika makanisa saba ya Asia Ndogo. Aliagizwakuandika katika chuo, hakuandika kwa mapenzi yake bali kwa

Page 22: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1392

kuagizwa. Chuo ni Kitabu hicho cha Ufunuo. Hivyo Yohana alipewa mamlaka yakuandika na andiko lake pia lilipata kuwa na mamlaka. Mambo yake yametokakwa Mungu, ni Neno la Mungu. Pengine Yohana aliandika mambo kadha marabaada ya kuyaona (1:19; 10:4). Kisha akaagizwa akipeleke kitabu kizima kwamakanisa yaliyotajwa. Hayo makanisa yalikuwa karibu karibu, kusini magharibiya Asia Ndogo. Inaonekana kitabu kizima kilipelekwa kwa makanisa yote, na kilakanisa lilikuwa na ujumbe wake ndani yake. Kwa hiyo kitabu hicho kiliandikwakwa kusudi maalum la kuwasaidia Wakristo wafahamu maana ya kweli yamambo yanayowapata ili wayaelewe katika mwanga wa mapenzi ya Mungu nakujua kwamba hayo magumu wanayopata ni sehemu ya maana katika mpangowake. Pengine jambo la Yohana kuambiwa mara mbili kuandika (1:10b 1:19) nikuonyesha umuhimu wa Maono ya Mwana wa Adamu (1:11-18). (TwakumbukaPaulo alipata mamlaka yake alipotokewa na Bwana Yesu njiani kwendaDameski. Ni vema tuone ya kuwa watu wanaopewa mamlaka ni wale wenyemzigo juu ya wokovu wa watu).

1:12-20 Maono ya Mwana wa Adamu katika Utukufuk.12 Baada ya kugeuka ili aione ile sauti iliyosema naye Yohana aliviona vinaravya taa saba vya dhahabu. Zamani Waisraeli waliweka kinara kimoja chenye taasaba katika Maskani (Kut.25:31ku.Hes.8:2) na Zekaria aliona taa saba juu yakinara kimoja (Zek.4:2ku). Ila Yohana aliona vinara saba si kimoja. Vinara vyataa vilikuwa ishara ya yale makanisa saba (k.20). Vilikuwa vya dhahabu, dalili yauthamani wao. Ijapokuwa Wakristo katika shirika hizo walikuwa wachache, nawengi wao walikosa hali nzuri za dunia hii kama elimu, cheo, mali (1 Kor.1:26ku)hata hivyo machoni mwa Mungu wao ni tunu.

Vinara vya taa ni ukumbusho wa wajibu wa makanisa hayo kuwa nuru na kutoanuru ya Kristo mahali walipo (Yn.8:12; Mt.5:14-16; Flp.2:15-16). Ndio wito waona shabaha ya kuwapo kwao. Ikiwa watakosa kuitimiza shabaha hiyo haibakitena sababu ya kuwapo kwao, kinara chaweza kuondolewa, maana hakina kazitena (2:5). Taa hizo zilihitaji mafuta, ishara ya Wakristo kumhitaji Roho Mtakatifuwa kuwawezesha kuutimiza wajibu wao, kama Yesu alivyowaambia nakuwaahidi na kama Nabii Zekaria alivyotangulia kusema (Zek.4:6).

Vinara kuwa saba (si kimoja) ni ishara ya kila kanisa kuwa „kamili‟ katika hali yakuwa na yote yaliyohitajika kwa maisha yake na kazi yake.

Ila jambo kuu na la maana kuliko yote ni lile la Yohana kumwona „mtu, mfano waMwanadamu‟. Zamani, katika njozi, Danieli alimwona „mmoja, mfano wamwanadamu, aliyemjia mzee wa siku na kupewa mamlaka ya milele na ufalmeusioangamizwa...‟ (Dan.7:13) Yesu Mwenyewe alipenda kujiita „mwana waAdamu‟ kama jina la cheo cha Masihi. Huyo ambaye Yohana alimwona alikuwa„mfano‟ wa Mwanadamu ila kwa maelezo yaliyofuata alikuwa zaidi yamwanadamu. Ni dhahiri kwamba alimwona Yesu Kristo (1:18) yule ambaye

Page 23: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1393

Yohana aliandamana naye alipokuwa hapo duniani. Aliegemea kifuani mwakekatika chakula cha mwisho. Iwapo Yohana alikuwa amewahi kumwona Yesu haliamevikwa utukufu kwa muda mfupi wakati alipogeuka sura mlimani (Mt.17:lku.Lk.9:28ku) hata hivyo alishangazwa mno kumwona jinsi alivyoonekana katikamaono hayo.

Huyo Yesu alionekana wapi? Alikuwa katikati ya vile vinara saba. Ishara ya nini?Kila kanisa lilikuwa mahali fulani palipojulikana ila ajabu ni kwamba kiroho Yesuyu pamoja nayo na katikati yao. Yu pamoja na kila Mkristo wa kila shirika. Tenaalikuwa ameyashika makanisa kwa mkono wake wa kuume (k.20). Umoja waoumefichwa ndani yake, na iwapo kila kanisa limesimama peke yake, likiwezakukemewa au kusifiwa, kupewa thawabu au kupewa adhabu (taz. ujumbe kwamakanisa 2:1-3:22) hata hivyo, Kanisa ni moja, wala halitaangamizwa kamwe(Mt.16:18). Kwa hiyo, Bwana wao, iwapo ni Bwana wa Utukufu, ambayeametawazwa juu mbinguni, hawi mbali nao, yu karibu kabisa, hata yu katikatiyao, hali akijua kila jambo wanalolifanya na kufanyiwa, Kwake kila neno na kilatendo ni muhimu, yote ni ya maana, wala hakuna jambo ambalo watawezakuliwaza kwamba hilo si kitu. Walipaswa kuishi „mbele zake‟ kwa kuwa ni Yeyeachunguzaye mioyo na nia zao (Ebr.4:12-13).

k.13b-16 Ni vema tutazame mambo ya vifungu hivyo kwa kushika taswiranzima. Taswira hasa yamhusu mmoja mwenye adhama kuu na utukufu wa ajabukabisa. Vazi, mshipi, kichwa na nywele, macho na miguu na sauti, hizo zotezachochea mawazo ya ukuu, enzi, nguvu, adhama, mamlaka, hekima, utakatifuna ujuzi wake. Tena tabia hizo zapatana na sifa za asili za Mungu Mwenyewe(Yn.14:9). Tunapotazama kila neno tusipoteze taswira nzima za huyo aliyekuwamfano wa Mwanadamu. Jambo muhimu ni maana ya hayo yote na swali lakujiuliza ni „jambo hilo linaashiria nini hasa?‟.

k.13b „amevaa vazi lililofika miguuni‟ Vazi ni ishara ya mtu maarufu, mkuu,mwenye adhama. Katika Israeli Kuhani Mkuu alivaa kwa jinsi hiyo (Kut.28:4;39:29) hata na wakuu wengine, akina Samweli na Sauli walivaa mavazi yakipekee (1 Sam.18.4; 24:5,11) kwa hiyo vazi lake lasema juu ya cheo kikuu namamlaka kuu, hata pengine ni kumwaza kama Kuhani wetu mkuu na Mfalme waWafalme.

k.14 „kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kamatheluji‟. Ni ukumbusho wa yule „mzee wa siku‟ ambaye Danieli alimwona akimpammoja mfano wa Mwanadamu mamlaka na utukufu na ufalme (Dan.7:9,14,18).Ni ishara ya umilele wake na hekima kamili ya kizee, na ya utakatifu halisiusioridhiana na dhambi, maana Kristo hakuwa na dhambi wala hakujua dhambiwala kufanya dhambi.

Page 24: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1394

k.14b „macho yake kama mwali wa moto‟ huleta mawazo ya mwenyekuchunguza na kuona kwa ukamilifu yote yaliyomo nje na ndani ya mtu. Piahuleta wazo la bidii na uwezo, yeye hachoki wala hakati tamaa, ataitekelezamipango yake yote.

k.15a „miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwakatika tanuru‟ ni ishara ya utendaji wa bidii na mbio katika kufanya kazi zake, yuimara, atapambana na maovu na vipingamizi na kuvitiisha chini yake (Eze.1:7).

k.15b „sauti yake kama sauti ya maji mengi‟ ishara ya mamlaka na uwezousiozuilika wa utawala wake (Eze.43:2). Yohana aliishi katika kisiwa kidogo,alikuwa akiisikia ngurumo ya rindimo ya mawimbi ya bahari usiku na mchana.

Kama ambavyo nimesema hapo juu, ijapokuwa mawazo yametolewa kuhusuvazi, nywele n.k. ni vema tusishughulikie hayo zaidi au tutafanana na mtuanayefumua sweta ya rangi nyingi nzuri na kuupoteza uzuri wa sweta yenyewe.Maono hayo yana shabaha ya kuamsha na kuchochea mawazo hadi tutekwe nauzuri na utukufu na adhama ya Yule aliyeonekana hivyo.

k.16 „alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume‟ Katika k.20 Yohanaamesema hizo nyota ni malaika wa yale makanisa saba na tutachunguza maanaya neno „malaika‟ tunapotazama k.20. Hasa jambo kubwa ni kwamba hizo nyotazimo katika mkono wake wa kuume, mkono uliohesabiwa kuwa wa nguvu naheshima, hivyo ni ishara ya kushikwa, kuongozwa na kuwa salama.

k.16b „na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake‟.Upanga ni ishara ya Neno lake la nguvu, kwa Neno lake Yeye huyatekeleza nakuyatimiza mapenzi yake (Isa.11:4; 55:11; 1 The.2:8; Ebr.4:12,13). Ni ishara yauwezo wa Mungu kupenya ndani kabisa na kufunua viini vya moyo na nia(Isa.49:2). Pia upanga ni silaha ya kushambulia, ishara ya Mungu kuchukuahatua za kuhukumu mabaya. Atayatakasa makanisa (2:16) na kuyaadhibumataifa (19:5).

k.16c „uso wake kama jua liking‟aa kwa nguvu zake‟ ishara ya uzuri na utukufuwa Kristo. Mungu hukaa katika nuru isiyokaribiwa. Kristo alijiita nuru yaulimwengu (Yn.8:12; 1 Tim.6:16). Hakuna mmoja atakayeweza kuepa KuwakoKwake, kwa sababu Yeye kama jua huangaza mahali pote.

Kama tutakavyoona tunapotazama barua kwa makanisa sifa hizo zatajwa tena,moja moja kulingana na hali za kila kanisa.

Page 25: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1395

Tukijumlisha hayo yote ni dhahiri kwamba Yohana alimwona Mtu Mtukufu, mtualiye Mungu/mwanadamu, mwenye kuzishiriki tabia zote za Mungu. Ni yulemwenye sifa hizo ambaye anayashika makanisa manyonge ya Asia Ndogo (walasi hayo tu). Wameshikwa naye, wamependelewa naye, na ajabu ni kwamba kwanjia yao atayatekeleza na kuyatimiza makusudi na mapenzi yake.

Maono hayo yalimshangaza Yohana maana yeye alikuwa ametembea pamojana Yesu kwa miaka mitatu alipokuwa mwanadamu hapo duniani. Aliegemeakifuani mwake usiku kabla ya kuuawa. Wakati fulani alijaliwa kuwa miongonimwa wale watatu waliomwona Mlimani alipogeuka sura (Mt.17:1ku). Maonoyaukaza Uungu wa Yesu, na kufanana na yale ya Danieli na Ezekieliwalipomweleza Mungu na utukufu wake. Kama ambavyo Yohana atazidikuonyesha katika Kitabu hicho, Kristo yu katikati ya yote yanayotokea, Yeye niMkuu, ni kama kitovu cha gurudumu ya shughuli. Yeye anatawala historia yote,Yeye ni ufunguo anayefunua maana na shabaha na kila jambo laelezwa kwa jinsilinavyomhusu Yeye.

Yohana alionyeshwa utukufu, adhama kuu, uwezo, na enzi ya Kristo. Ni Kristo,Mtakatifu, anayekuja kuyatakasa makanisa (2:16,18,23). Pia ni Kristo Mhukumuanayekuja kuwaadhibu watesi wao (8:5ku). Anao upanga mkali ukitoka katikakinywa chake, maana yake neno lake lina nguvu ya kutimiza mapenzi yake(Isa.55:11; Ebr. 4:12-13). Taswira ya Yohana ilitangaza utukufu, nguvu, uzuri,adhama na utakatifu wake.

k.17 Yohana aliishiwa nguvu alipomwona Kristo katika utukufu wake, akaangukamiguuni pake kama mtu aliyekufa. Kumwona mmoja aliyefanana na Mungukunaleta hali ya kufa. Ni nani awezaye kumwona Mungu na kuishi? (Kut.33:20)lakini huyo Kristo ndiye anayemfunua Mungu (Yn.1:18) Yeye ni mfano halisi waMungu (Kol.1:15; Flp.2:6ku). Ezekieli alianguka kifudifudi alipouona utukufu waMungu (Eze.1:28; 3:23; 43:3; Ling. na Lk.5:1-11). Yohana alisikia kutishwa sana,hakuanguka kwa desturi ya kumheshimu mkuu tu. Kristo alimfariji na kwaupendo aliweka mkono juu yake na kumwambia „asiogope‟. Yohana alikuwaamelisikia neno hilo mara kwa mara alipotembea na Yesu hapa duniani, maanaYesu alilitumia sana kwa wanafunzi wake. Bila shaka neno hilo lilimhakikishiakwamba ni Yesu kweli. Makusudi ya kumpa maono hayo ni kumtia nguvu nakumfariji si kumtisha.

Mkono ulioshika nyota saba ni ule uliomgusa Yohana na kumfariji na kumtianguvu. Tusijaribu kupatanisha kila jambo, wakati wote tukumbuke ni taswira zakueleza yale yasiyoelezeka kwa njia za kawaida. Tulisoma kwamba Yesualikuwa akizishika nyota saba katika mkono wake wa kuume, na hapa amewekamkono uohuo juu ya Yohana. Ukweli uliopo katika maelezo hayo ni kwambaKristo analishika Kanisa Zima, analiangalia na kulilinda mahali pote, pamoja nakumfahamu kila Mkristo mahali alipo, anajua matatizo yake, naye yu karibukabisa kwa nia ya kumsaidia.

Page 26: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1396

Halafu Yesu alimkumbusha Yohana umilele wake „Mimi ni wa kwanza na wamwisho‟ ni sawa na „mimi ni Alfa na Omega wa k.8 (2:8; 22:13). Kristo sawa naMungu ni wa milele na milele, hakuna aliyemtangulia mwenzake. Alikuwapokabla ya kuja duniani akiwa na uzima ndani yake sawa na Mungu Baba.(Yn.5:26) Ndipo alipokuja duniani akaishi, akauawa, akafufuka, akawa hai tena,wala hafi tena. Yapo maajabu mawili, Yule Mwenye uhai ndani yake (Yn.5:26)akafa; na Huyo aliyekufa yu hai milele na milele. Jambo moja kubwa ni kwambabaada ya Kufa na Kufufuka Kwake Yesu amepatwa na hali tofauti sana na ilealiyokuwa nayo kabla ya kuja duniani. Hakurudia kwenye umilele tu, ila pamojana kurudi alivikwa hali ya ushindi juu ya mauti, mauti tangu hapo imeshindwakabisa. Yesu „alitoroka‟ mauti, akatoka kaburini yu hai, akazichukua funguo zake,Yeye anayo mamlaka juu yake, mfano wa mtu aliye na funguo za kabati anayomamlaka ya kutia au kutoa au kuhifadhi kitu ndani yake.

Kifo cha Kristo kilikuwa kiini cha makusudi ya Mungu ya kuukomboa ulimwengu,na waumini walipaswa kukishuhudia. Wasiwaze mbingu na dunia mpya tu, lamaana sana ni mwenendo wao wa sasa. Katika mashaka na dhiki zao Wakristowalihitaji kujua hakika kwamba Bwana wao ni mshindi wa mauti. Baadhi yao,katika mateso yanayowajia, watauawa, na faraja zao ni katika tumaini lakuishinda mauti, yaani kufufuka kama Bwana wao. Katika 4:10 na 10:6 manenohayo yalitumiwa kumhusu Mungu Baba, Mwana yu sawa na Baba kwa hali zote.Aliye na madaraka juu ya mauti na kuzimu ni Kristo (funguo ni dalili yamadaraka). Kwa hiyo, wale watakaowaua wafanya nini isipokuwa kuwapelekakwa Bwana wao! Mauti kwa Mkristo ni faida si hasara, ni kuwa pamoja na Kristomilele. Kristo baada ya kufa alikwenda Kuzimuni (Mdo.2:27-31). Kristo hutawalawafu baada ya roho zao kutengana na miili yao, wala hakuna kitu, wala mauti,wala kuzimu, kiwezacho kuwatenga na upendo wa Kristo (Rum.8:35-39).

k.19 Katika k.11 aliagizwa kuandika na hapo aliagizwa tena (k.1: 4:1: 22:7)pengine aliendelea kuandika kadiri alivyopata kuyaona maono. Ayaandike yaleambayo yameishapita na ya baadaye na yanayotokea wakati wa sasa. Ilatusifikiri twaweza kugawa Kitabu katika sehemu tatu, mambo yameingiliana.Ilibidi ayaandike yote atakayoyaona bila kujali yahusu wakati gani.

k.20 „siri‟ yahusu mambo yasiyoeleweka kwa watu bila Mungu kuwafunulia.Ndipo Yohana aliambiwa wazi kwamba zile nyota saba ni malaika wa yalemakanisa saba, na vile vinara saba ni makanisa saba. „malaika‟ ni nani hasa?Neno lenyewe lina maana ya „mjumbe‟ ama wa duniani au mbinguni. Ni rahisikuwaza ni kiongozi wa kanisa la palepale, ila wakati wa Yohana haikuwa desturiya kuweka mmoja tu kuwa kiongozi peke yake. Paulo aliwaweka „wazee‟ simzee katika shirika mpya, na katika Nyaraka twaona ni „maaskofu‟/‟wazee‟wanaotajwa. Wazo lingine ni kwamba kila shirika lilikuwa

Page 27: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1397

na „malaika‟ wake huko mbinguni, kama wa pili wake. Wayahudi waliwazakwamba kila taifa lilikuwa na malaika wake (Dan.10:13; 11:1; ling. Mt.18:10;Mdo.12:15). Liko wazo lingine kwamba malaika ni ile hali ya ile shirika kama„roho au nafsi‟ yake, kwa hiyo neno malaika linaashiria shirika lenyewe. Kilabarua ilianza na maneno „kwa malaika wa kanisa lililo..‟ ila yote yaliyoandikwahumo yaliwahusu wote bila kuweka tofauti kati yao.Maono ya Yesu kuwa katikati ya vinara saba ni fundisho kubwa na la maanasana. Liliwafundisha Wakristo (na hata sisi wa leo) kwamba Kristo si „hayupo‟ eti!aliondoka duniani alipopaa na kurudi mbinguni (Efe.4:10). Majaliwa ya Kanisayalifungamana na Kristo si Kaisari wa Kirumi. Ndivyo ilivyo wakati wote.

MASWALI1. Yohana alipataje kukiandika Kitabu cha Ufunuo?2. Neno „Ufunuo‟ linatueleza nini kuhusu mambo yaliyomo?3. Eleza maana ya Maono ya vinara saba na mtu mfano wa Mwanadamu

kuwa katikati yake.4. Onyesha jinsi Maono hayo yalivyowahusu na kuwasaidia walioandikiwa.5. Taswira nzima ya huyo aliyekuwa mfano wa Mwanadamu iliashiria nini juu

yake?6. Ina maana gani kusoma kwamba Yesu anazo funguo za mauti na za

kuzimu?

SURA 2 - 3 UJUMBE KWA MAKANISA SABAKatika sura hizo mbili tunazo barua saba kwa makanisa saba yaliyokuwamokatika eneo la Asia Ndogo. Barua hizo ni sehemu katika Kitabu kizima, tusiwazekwamba kila barua ilitumwa peke yake kwa Kanisa la mahali palipotajwa. Mambokadha yaliyotajwa katika barua hizo yametajwa katika sehemu nyingine zaKitabu. Kwa mfano Mti wa Uzima 2:7 ling. na 22:2,14; Jina Jipya 2:17, 3:12/14:1:22:4; Nyota ya Asubuhi 2:28/22:16; Mauti ya Pili 2:11/20:14; Mamlaka juu yaMataifa 2:2/12:5, 20:4.

Barua zafanana kimpango:a) Mahali kanisa lilipo:b) Sifa mojawapo ya Kristo: (sifa hizo zilitajwa katika Maono ya Kristo

yaliyotangulia (1:12ku)c) Sifa kwa hali au jambo fulani katika Kanisa lile:d) Kemeo kwa hali au jambo fulani katika Kanisa lile:e) Onyo:f) Wito wa Kutubu na Kutengeneza:g) Ahadi kwa yeye ashindaye:

Kanisa la Laodikia halikusifiwa kwa hali au jambo lolote. Kanisala Smirna na la Filadelfia: haukutajwa upungufu wowote.

Page 28: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1398

Katika barua tatu za kwanza maneno „yeye aliye na sikio, na alisikie‟ yalitanguliamaneno „yeye ashindaye‟ na katika barua nne za mwisho maneno hayo yalifuatamaneno „yeye ashindaye‟.

Wakati wote katika historia yake Kanisa limekuwa na hali mbalimbali kama hizo,kwa hiyo, ijapokuwa ni wazi kwamba hayo yalikuwa makanisa kweli yenyemambo hayo, hivyo ujumbe huo wafaa hata leo.

Ni vema tujiulize, Kwa nini Kristo ameonekana kama ni mpelelezi wa makanisahayo kana kwamba anawatayarisha kwa jambo fulani? Kama ni hivyo, alikuwaakiwatayarisha kwa ajili ya nini? Kwa Kurudi Kwake? au pengine Kwa matesowatakayopata kwa ajili yake? Inaonekana ni kwa ajili ya mateso, maana ni YeyeKristo anayewatayarisha, tena hali zinazosifiwa ni subira, uvumilivu, uaminifu,kudumu n.k. Hali hizo hasa zahusu wakati wa sasa, wakati wa kushindana nawapinzani na kuyakabili mateso. Wakristo waitwa kuyashinda majaribu yao yaimani ndipo baadaye wazirithi ahadi walizopewa (3:21).

2:1-7 Barua kwa Kanisa la Efeso (Mdo.18:19-28; 19:1-41)Huenda Yohana alishtuka aliposikia Kanisa la Efeso linatajwa kwanza. Kanisahilo, likiwa katika Jiji Kuu la maana sana, lilikuwa muhimu kwa kueneza Ukristokatika sehemu zile. Kanisa lilipandwa na Paulo na wenzake wakati wa safarikubwa ya tatu ya Uinjilisti B.K.52-54. Alikaa muda mrefu na Injili ilienea sana(Mdo.18-21). Huduma yake ilibarikiwa sana hata biashara ya visanamuilipungua. Baadaye alimtuma Timotheo kutengeneza mambo wakati wa kuingiakwa mafundisho ya uongo (1 Tim.1:3). Kwa ushuhuda wa maandishi mbalimbaliMtume Yohana aliishi na kufanya huduma pale Efeso kuanzia B.K.66. Hivyohakuwa mgeni kwao. Wakati alipoandika Kitabu hicho Kanisa limekuwapo palekwa miaka kama arobaini na ndani yake walikuwemo waongofu wa kwanzapamoja na waumini waliopatikana baadaye.

Kwa miaka mingi Wayunani walitawala sehemu zile hadi zilipowekwa chini yautawala wa Dola la Kirumi. Lilikuwa jiji kuu la kwanza katika Jimbo la Asia. Makaomakuu ya serikali yalikuwapo Pergamo, hata hivyo, kila liwali mpya alipaswaapitie Efeso kwanza ndipo aende Pergamo. Lilikuwa Jiji Huru, maana yakeWarumi hawakuweka kikosi cha Jeshi pale. Kwa hali zote, uzuri, utajiri,mafanikio n.k. Efeso ulikuwa mbele, na hasa kwa sababu ya mahali pakekijiografia. Ulisimama kwenye mdomo wa Mto Cayster, kwenye pwani ya Bahariya Aegean. Bandari yake ilikuwa kubwa yenye uwezo wa kupokea merikebukubwa. Zingine zilitoka mbali zikishusha na kupandisha bidhaa aina nyingi. HivyoJiji lilitajirika na kuwa na maendeleo mengi. Wengi walitoka magharibi mpakamashariki na kutoka mashariki mpaka magharibi na kupitia pale. Barabara kuuzilikutana pale, ile iliyotoka mbali kwa Mesopatamia na ile ya kutoka Galatia nazile zilizotoka kwa miji ya ndani. Liliitwa „Soko la Asia‟ „Mwanga wa Asia‟ „Langola kuingia Asia‟.

Page 29: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1399

Jambo moja lililoongeza umaarufu wake lilikuwa Hekalu la mungu mke Artemi(Kwa KiLatini Diana). Ibada ya Artemi iliingizwa zamani na Wayunani, huendaibada nyingine ilikuwepo na Wayunani waliibadili jina na kuisisitiza zaidi. Hekalulake lilijengwa kwa marimari safi, la kwanza katika ulimwengu kujengwa hivyo,nalo lilihesabiwa kuwa moja katika maajabu saba ya ulimwengu. Katika mwakaK.K.29 sehemu ya jengo la hekalu iliwekwa wakfu kwa mungu-mke Roma namungu Julius, hivyo ulitokea mwungano kati ya Ibada ya Artemi na Ibada yaKumwabudu Kaisari. Katika Matendo 19:23ku. twapata habari ya shida iliyotokeabaina ya Paulo na wafuasi wa Artemi, ila shida ilisababishwa na kupungua kwabiashara ya visanamu vya Artemi wakati wengi walipomgeukia Kristo nakuvitupilia mbali visanamu vyao ingawa Paulo hakumlaumu Artemi. Neno hilolatuonyesha jinsi wengi walivyopata kazi kwa njia ya Ibada ya Artemi na kwawatalii wengi waliovutwa kufika Efeso na kuliona hekalu lake la ajabu.Katika eneo la jengo la Hekalu la Artemi paliwekwa Maktaba na Jumba laHazina na Jumba la Tamthilia. Pamoja na hayo yote Michezo Mikubwailifanyika Efeso pia zilikuwapo Baraza za Hakimu. Hata mahekalu mengineyalikuwapo.

Baadaye Jiji hilo lilipoa, mdomo wa Mto Caystor ulizidi kujaa mchanga na melizilishindwa kufika kwa ukaribu. Siku hizo Efeso umeitwa Ayasaluk. HamnaKanisa pale.

2.1 „Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika‟.... Yohana aliagizwa kuandikabarua hiyo yenye ujumbe kutoka kwa Bwana Yesu. Hatuna uhakika wa maanaya „malaika‟ kwa kawaida maana yake ni „mjumbe‟. Hapo nyuma katika maelezoya 1:16,20 mawazo mbalimbali yametolewa. Haidhuru maana yake ni nini nidhahiri kwamba ujumbe ni kwa shirika zima na kwa kila mmoja katika shirika kwasababu kila mmoja aliitwa kuujali huo ujumbe. Ujumbe ulihusu makanisamengine pia (2:7).

Halafu inatajwa sifa moja ya Bwana Yesu ambayo pia ilitajwa katika maono yakwanza aliyopata Yohana (1:12,16). „azishikaye hizo nyota saba.. yeye aendayekatikati ya vile vinara saba..‟ maneno hayo yana nguvu kuliko yale ya maono.Iwapo Kanisa la pale ni muhimu kwa kuwa ni katika Mji mkuu wa maana hatahivyo wao ni shirika moja tu (nyota ni 7 na vinara ni 7). Walikumbushwa kwambakila shirika ni wa maana katika mpango wa Mungu, na wao, pamoja na wengine,budi Kristo awachunguze na kutoa maoni yake. „aendaye‟ ujumbe watoka kwaYule anayefanya kazi kwa nguvu na bidii kati yao, Yule aliye imara, tayarikuwaongoza, kuwakemea, na kuwaokoa.

k.2 Tena ujumbe ni kutoka kwa Yule anayeyajua mambo yao. Anajua nini?Anajua matendo yao, taabu yao, subira yao, na hali yao ya kutokuchukulianana wabaya. Waliyapenda na kuyathamini mafundisho ya kweli hata

Page 30: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1400

waliwachunguza wale waliojiita mitume na kuwapima kama walikuwa wa kweliau sio. Walikuwa wameendelea vizuri, walifanya matendo mazuri na kuvumiliashida kwa ajili ya imani yao. Pia waliwakemea wale ambao hawakuishi maishayaliyowapasa kama wafuasi wa Kristo. Tena waliilinda Imani na wale waliojaribukuipotosha. Waliendelea bila kuchoka ijapokuwa haikuwa rahisi kumfuata Kristo.Hivyo Kristo aliwasifu kwa mengi. Matendo mema ni muhimu katika kuwawaaminifu kwa Kristo maana yamshuhudia vizuri.

k.4 Hata hivyo Kristo alikuwa na neno juu yao. Hilo ni neno gani? Alisema„umeacha upendo wako wa kwanza‟. Maana yake nini? kama walikuwa na halihizo njema wamekosea wapi? Ni kama walifanya hayo mazuri yaliyotajwa bilamoyo, kama mazoea tu. Mfano wa mume na mke katika ndoa ambao katika sikuza kwanza wapendana kwa moyo ndipo baadaye waendelea kama kawaida,mke akipika chakula na kufua nguo n.k. kwa uaminifu ila ule moyo wa kwanzaumepoa, hawasikii „joto‟ la moyo kama walivyosikia siku za kuchumbiana. Munguhutaka ule moyo wa kwanza uendelee katika uhusiano kati yake na wafuasiwake. Yeye habadiliki, hapoi kwa watu wake. Bila upendo yote mengine mazurini bure (1 Kor.13:2). Walipataje kupoa? Bila shaka hali hiyo iliingia polepole.Yawezekana katika kuwa na mzigo juu ya kweli na kuwapinga waongo kwa bidiiwamekuwa watu wa kuhukumuhukumu na kwa sababu hiyo wamepatwa namoyo baridi. Wameishikilia kweli na kuipigania huku wamepoa katika upendo.Paulo aliwaandikia WaEfeso „tuishike kweli katika upendo‟ (Efe.4:15).Wamesifiwa kwa kutokuchukuliana na wabaya na wamekemewa kwa kuuachaupendo wao wa kwanza. Tuwe na tahadhari juu ya „nguvu‟ yetu kwa kuwainaweza kusababisha tunaswe katika hali isiyoruhusiwa. Katika Ukristo upendona kweli vyaungana, vyote viwili vinatakiwa.

k.5 Yesu aliwashauri mambo matatu: „kumbuka ni wapi ulikoanguka‟ „ukatubu‟„ukayafanye matendo ya kwanza‟. Ni rahisi kuteleza bila kutambua. Waliitwawatazame nyuma na kulinganisha jinsi walivyo sasa na jinsi walivyokuwa siku zakwanza za kuamini kwao ili watambue ni nini upungufu au kosa lao. Halafuwatakapotambua wamepaswa kufanya nini ndipo wakate shauri la kulifanya,kisha walifanye.

k.5b Ndipo Yesu aliwaonya kwamba atakiondoa „kinara‟ chao. Aliwapa nafasi yakutubu na aliweka mbele yao hatua tatu za kufuata. Ila wasipokubali mashauriyake watakoma kuwa Kanisa, mwanga wao utazimika nao watakosa kuitoa nuruya Injili na shabaha ya kuwako kwao itakwisha. Yawezekana maneno hayoyahusu wakati wa mwisho na kama ni hivyo maana yake ni kwambahawatazishiriki baraka za baadaye.

k.6 Hata hivyo Yesu alitaja jambo jingine la sifa, waliyachukia matendo yaWanikolai ambayo Yesu pia aliyachukia. Hivyo walifanana na Kristo katika

Page 31: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1401

kutokuchukuliana na hao Wanikolai. Imesemekana kwamba hao Wanikolai niwafuasi wa Nikolai, mmoja wa wale saba waliochaguliwa kufanya hudumu yamezani kwa wajane, ila jambo hilo halijahakikishwa, wengine wafikiri kwambahakukosa ila shida iliingia kwa sababu watu hawakumwelewa vizuri. (Mdo.6:5).Yafikiriwa alipoa baadaye na kulegea katika maisha ya Kikristo kwa sababualijaribu kujihusisha na watu kupita kiasi hata ilitokea kwamba haikuonekanatofauti sana kati ya Imani ya Kikristo na dini za kipagani. Iwapo hatuna uhakikajuu yake, jambo tunalolijua ni kwamba hao Wanikolai waliotajwa hapowaliridhiana na mambo kadha, huenda walihudhuria karamu za kipagani na kulachakula kilichotolewa kwa sanamu. Paulo alitoa mafundisho juu ya mambo kamahayo (1 Kor.8 na 10: 14ku). Wakristo walijaribiwa sana kwa upande wakujihusisha na wengine wasio Wakristo. Iliwawia vigumu kushirikiana na wenzaokwa sababu karibu kila jambo la maisha lilifungamana na ibada na kutoa dhabihukwa mungu fulani. Hata Wakristo wengi wa siku hizi katika nchi za Afrikawametatizwa na mambo ya matambiko kwa ndugu zao waliokufa na desturizinazowaunganisha na jamaa zao. Swala kubwa limekuwa „Ni kwa kiasi ganiwaweza kushirikiana na ndugu zao katika desturi za kikabila bila kuuharibuushuhuda wao kwa Kristo?‟. Twajifunza tusiridhiane na mafundisho ya uongo namaovu katika Kanisa. Yesu aliwasifu WaEfeso kwa kutokuridhiana hukualiwakemea kwa ukosefu wa upendo. Hivyo twaona ya kuwa si upendokuyaachilia mabovu yaendelee bila kuyakemea, ila kukemea kuwe katika hali yakupenda watu na kuchukia dhambi zao. Yafikiriwa mafundisho ya „Balaamu‟(2:24) na ya „Yezebeli‟ (2:20) yalifanana na ya hao Wanikolai.

Kwa hiyo tumeona kwamba Kristo anayewashika na kuwaongoza na kutembeakati yao ni Kristo mwenye uwezo wa kuwatia nguvu kwa maisha yao ya kiroho,pia anao uwezo wa kuwahukumu hata kuwaondoa. Ni makanisa mawiliyaliyopewa onyo la kuondolewa, Efeso na Laodikia, na yote mawili kwa sababuya ukosefu wa upendo. Hivyo Kanisa lisilo na upendo lijihadhari sana,halitadumu likikosa kuwa na upendo (1 Kor.13:2).

k.7 Halafu, mwishowe, Yesu alimwita kila mmoja aujali ujumbe wake kwasababu Roho Mtakatifu ndiye wa kuwaelimisha juu ya hayo aliyoyasema. Kishaahadi ilitolewa kwa „ashindaye‟ yaani kwa yule atakayedumu kuwa mwaminifuhadi mwisho. Aliahidiwa „kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani yaMungu‟. Chakula bora kuliko kile kilichotolewa katika karamu za miungu.Mwenye kushinda atashirikishwa baraka za uzima wa milele na kurudishiwa uleushirikiano mwema na wa ukaribu na Mungu ambao hapo mwanzo Adamualikuwa nao katika Bustani ya Adeni (Mwa.3:22). Laana za Anguko zitageuzwakuwa baraka na hali njema zote zilizopotezwa zitarudishiwa tele.

2:8-11 Barua kwa Kanisa la SmirnaSmirna lilikuwa jiji kubwa lililoshindana na Efeso juu ya kuitwa jiji la kwanza laJimbo la Asia na baadaye lilichukua mahali pa Efso na kuitwa la kwanza. Leo

Page 32: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1402

pale Smirna liko Jiji kubwa, la pili katika Uturuki ya KiAsia, nalo laitwa Izmir.Palikuwepo mji uliotangulia huo uliokuwapo wakati wa Yohana. UliangamizwaK.K.580 na kulala chini kwa miaka kama mia mbili tatu hivi halafu ulijengwa upyaK.K.290 ng‟ambo ya pili ya ghuba kwa mpango maalumu, mpango mzuri sanawa kupendeza na waandishi wengi waliusifu uzuri wake hata liliitwa „Uzuri waAsia‟. Lilishindana na Jiji la Efeso lililokuwa kama maili arobaini kuelekea kusini.Lilikuwa na bandari, si kubwa, ila kwa sababu ya jiografia yake ilikuwa vigumukushambuliwa. Jiji lilisitawi. Liliwahi kujiunga na Dola la Kirumi, hata kabla ya mijimingine na hata kabla ya Dola kuwa kubwa, na kwa sababu hiyo uhusiano katiyao ulikuwa mzuri sana. Mwaka K.K.195 hekalu la mungu mke Roma lilijengwa,yawezekana la kwanza kujengwa. Mwaka B.K.26 hekalu lilijengwa kwa KaisariTiberia, hayo yote dalili ya uaminifu wake kwa Dola. Yalikuwepo mahekalu kwamiungu mingine, Zeus, Cybele, Apollo, Nemeseis, Aphrodite na Asclepios. Piaulikuwepo Uwanja wa Michezo na Michezo mikubwa ilifanyika kila mwaka.Maktaba, Jumba la Tamthilia, na Ukumbi wa Muziki ulikuwepo. Hayo yoteyalifanya Jiji la Smirna kuwa na sifa ya kuwa „hai‟.

Wayahudi wengi waliishi pale, huenda walivutwa na nafasi za kufanya biasharana uchumi. Walikuwa na nguvu na inaonekana ni hao walioamsha fitina juu yaWakristo wa pale. Wayahudi waliachiliwa katika jambo la kuabudu miungu yaKirumi, hawakutakiwa kufukizia uvumba kwenye sanamu ya Kaisari na kumkirikuwa bwana na mungu. Mwanzoni ilidhaniwa Ukristo ni madhehebu ya Kiyahudikwa sababu Wakristo wote wa kwanza walikuwa Wayahudi. Ndipo baada yamuda Injili ilizidi kuhubiriwa kati ya WaMataifa na wengi wao walimpokea Kristo.Hivyo mwisho wa karne ya kwanza waumini wengi zaidi walikuwa WaMataifa siWayahudi ndipo ilikuwa dhahiri kwamba dini ya Kikristo ni tofauti na dini yaKiyahudi. Kwa hiyo Wakristo hawakuachiwa kama Wayahudi walivyoachiliwa.Pamoja na hayo Wayahudi walioishi katika nchi za WaMataifa waliwaoneaWakristo wivu kwa jinsi walivyovuta watu kwa Ukristo na mara nyingi waliamshafitina juu yao. Baadhi ya Wakristo walipoa na wengine kwa sababu ya dhiki zaowalirudi nyuma. Katika barua hizo ni wazi kwamba Kristo alitaka kuwatia moyowa kuvumilia na kuendelea potelea mbali wapatwe na shida gani kwa sababumwisho wa safari yao ni raha katika uzima wa milele.

Hatuna habari kamili juu ya chanzo cha Kanisa la Smirna. Yafikiriwa Kanisalilipandwa pale wakati uleule wa uinjilisti wa Paulo na mwenzake katika maeneoya Efeso na Troa (Mdo.19:10). Tuna habari ya Askofu Polikarpo aliyekuwamwanafunzi wa Yohana. Yeye alikuwa Askofu wa Smirna B.K.115- 155 mudamfupi baada ya Kitabu hicho kuandikwa. Aliuawa kwa imani yake B.K.155.Ignatio wa Antiokia alipitia pale njiani kwenda Rumi kama B.K.110. Yeyealiandika barua mbili, moja kwa Kanisa hilo na moja kwa Askofu Polikarpo miakamichache baada ya Kitabu hicho kuandikwa.

Page 33: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1403

k.8 Yesu alianza ujumbe wake kwa kujitaja kuwa „wa kwanza na wa mwisho,aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai‟ kulingana na historia ya kuwa mji uliokufana kufufuka. Sifa hiyo ilikuwa baadhi ya sifa za „mtu mfano wa Mwanadamu‟(Kristo) katika maono ya Yohana (1:17-18). Hivyo Yesu alijihusisha nao kamayule wa kujua historia yao. Yesu alikuwa amekufa na kufufuka.

k.9 Alijua nini zaidi juu yao? Alijua kwamba Wakristo wa Smirna waliteswa kwaajili ya imani yao, nao walikuwa katika dhiki, kama watu waliokandamizwa chinikwa sababu ya kumwamini Kristo. Pia walikuwa maskini sana hali wamefilisikakabisa, ndiyo maana ya neno lililotumika hapo. Mara nyingi Wakristo walinyimwakazi, mahitaji, na mara nyingine walinyang‟anywa mali zao (Ebr.10:34). Kwasababu ya imani yao walihesabiwa kuwa watu wasio na haki zozote mbele yaSheria. Ila Yesu hakutaka wajihurumie kwa sababu ya hali hizo bali waufikirieutajiri wao kiroho, hazina yao ni kuwa na Kristo na baraka zote zilizomo ndaniyake.

Walitukanwa na Wayahudi ambao Yesu hakukubali kuwaita „watu wa Mungu‟bali watu wa Shetani, watu waliotumiwa na Shetani kuwashtaki Wakristo nakusababisha wapate shida na serikali. Kitaifa walikuwa Wayahudi ila hawakuwaWayahudi wa kweli, baba yao si Ibrahimu, maana hawafuati kielelezo chake, baliShetani (Yn.8:33-34; 16:2; Rum.2:28).

k.10 Yesu alijua kwamba mateso yao hayajaisha bado. Mbele yao ni kipindi chamateso makali na baadhi yao watatupwa gerezani, mahali pa kungojea hukumuya kuuawa. Kristo aliwaambia wasiyaogope yale yatakayowapata, akawaombawawe waaminifu hata kufa, yaani potelea mbali wapatwe na nini waendeleekuwa watiifu Kwake. „nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi‟ Tusiwaze kwamba nisiku kumi hasa, ila ni lugha ya kueleza ya kuwa mateso yao hayataendelea bilakikomo, watateswa kwa muda wa kutosha, si muda usio na kikomo. Neno lamwisho si kwa watesi wao. Mateso yatoka kwa Shetani kwa njia ya kuwatumiawatu kama Wayahudi, ila Mungu huyatumia kwa kuipima na kuiimarisha imaniyao. Ni makusudi ya Mungu wauingie Ufalme wake ijapokuwa itakuwa kwa njiaya dhiki nyingi (Mdo.14:22).

Yesu alitoa ahadi ya „taji ya uzima‟. Taji ni dalili ya ushindi, ila taji yao si ya mauaau majani kama waliyopata washindi wa michezo (pale Smirna michezomikubwa ilifanyika). Taji yao ni bora sana, ni ya uzima, ni ya kuishi na Kristomilele na milele, ni kuushiriki uzima wa Yule Aliyekufa na Kufufuka.Hawatapatikana na mauti ya pili, watesi waweza kuiua miili yao ila hawawezikuzigusa roho zao (20:6,14;21:8; Mt.10:28). Mauti ya pili ni kuharimishwa nauzima wa milele.

Kristo hakuwa na neno juu ya Makanisa mawili, Kanisa hilo la Smirna na Kanisala Filadelfia.

Page 34: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1404

2:12-17 Barua kwa Kanisa la PergamoMwaka K.K.133 Mfalme wa Pergamo alilikabidhi Jiji lake kwa Dola nalo liliwekwakuwa Jiji kuu la Jimbo la Asia na makao makuu ya Jimbo la Kirumiyalisimamishwa pale. Hekalu lilijengwa mapema sana kwa ibada za kumwabuduKaisari, huenda ndiyo sababu Yesu alisema „najua ukaapo, ndipo penye kiti chaenzi cha Shetani‟. Kijiografia mji ulijengwa juu ya mlima mkubwa wa miamba,ulikuwa rahisi kulindwa ila shida ilikuwa ukosefu wa maji. Pergamo (unaitwaBergama leo) ulikuwa maili kama 55 kaskazini mashariki ya Smirna. Haukufaakwa uchumi kwa sababu ulikuwa maili 15 ndani ya nchi, mbali na mto na bahari.Lilikuwa na majengo mazuri; maktaba yake ilikuwa na vitabu vingi kama lakimbili. Neno la Kiingereza „parchment‟ latoka kwa jina la Pergamo. Pia lilijulikanasana kuwa mahali pa uponyaji na ibada zilifanyika kwa mungu Asclepius, munguwa uponyaji, na makuhani wengi walihudumia katika ibada hizo. Ishara yamungu Asclepius ilikuwa nyoka, ambayo kwa Wakristo ni ishara ya Shetani.Wengi walitoka mbali wakiutafuta uponyaji. Pamoja na mambo hayo Jiji lilijaamahekalu na madhabahu nyingi za kipagani, mojawapo kubwa lilikuwa kwaZeus. Kwa jumla Pergamo ulitoa nafasi ya maisha ya shibe ya kimwili, ya kiakili,na ya kiroho, mwundo wa jamii iliyo tofauti na jamii ya Kikristo, na wengiwalishawishiwa na mivuto yake. Pamoja na hayo haikosi Wakristo pia walivutwana mambo hayo na baadhi yao walijaribiwa kujihusisha nayo na kuishi nusukwenye Pergamo na nusu kwenye Ukristo.

k.12b Kristo alianza ujumbe wake kwa kujitaja kuwa na „huo upanga mkali,wenye makali kuwili‟ (1:16). Katika k.16b aliwaonya atautumia wasipotubu.Maana yake nini? Bila shaka upanga ni Neno lake (Ebr.4:12) Yeye ndiye „kweli‟(Yn.14:6) Mwenye ukweli wote, naye ataushambulia uongo na uovu popoteutakapoonekana. Tena upanga uliwakumbusha waumini kwamba yukomwingine aliye na upanga mkononi, liwali wa Jiji, mwenye uwezo na mamlaka yakuutumia kwa kuwatiisha watu wamwabudu Kaisari.

k.13 Kristo alijua mahali walipoishi, alijua ni kituo kikuu cha serikali, na alifahamumagumu waliyoyapata. Upanga huo wa serikali umekwisha kutumika, Wakristowameishateswa na mmoja wao Antipa aliuawa, pengine alikataa kumkiri Kaisarikuwa Bwana na kumfukizia uvumba. Hata hivyo wengine walidumu kuwawaaminifu kwa Kristo. Kwa hiyo Yesu alikuwa akisema na Wakristo ambaobaadhi yao wamesimama imara wakati mgumu.

k.14 Ila Kristo alikuwa na machache ya kuwakemea. Kanisa halikuwa tayarikuwatenga wale walioridhiana na mambo fulani, hasa wale waliokula vituvilivyotolewa kwa sanamu. Tatizo hilo lilitokea mapema katika Kanisa, Pauloaliligusa katika Waraka kwa Wakorintho (1 Kor.8-9). Kwa hiyo twaona jinsiilivyokuwa vigumu kufanya iliyo sahihi, maana Kanisa la Efeso liliwatengawakosaji na kusifiwa kwa ajili hiyo, ila walipatwa na moyo baridi wa kuukosaupendo na walikemewa kwa ajili hiyo. Hapo Kanisa la Pergamo limeelekea

Page 35: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1405

kuwahurumia na kuwaachilia wakosaji, bila kuwatenga. Kristo aliwakemea kwasababu hawakuwatenga, kwa kuwa Yeye huchukia hali za kuridhiana. Piawalikuwa walegevu katika mambo ya jinsia, walizini. Kuna „kuzini‟ kimwili nakuna „kuzini‟ kiroho yaani kumwacha Mungu wa kweli na kumfuata mungumwingine. Hapo si wazi ni kuzini kupi kunakotajwa, yawezekana ni aina zote.

Kwa hiyo Wakristo wa Pergamo walikuwa thabiti katika kuyakabili mateso,hawakuridhiana na serikali na madai yake, lakini walikuwa wameridhiana nawenzao walioshiriki katika karamu za kipagani na kula vitu vilivyotolewa kwasanamu.

k.16 Kristo alitoa mwito wa kutubu na kutengeneza hali hizo. Aliwaita wote siwale wakosaji tu. Jambo kubwa lilihusu hali yao ya kuchukuliana na watuwaliofanya mambo hayo ingawa wao wenyewe hawakuyafanya. Yesu ni „mkali‟anao upanga kinywani mwake, neno lake lina nguvu ya kupenya ndani yao nakuifunua dhambi yao ya kuridhiana, nao wapaswa waitubu. Neno lake lina uwezowa kuokoa na lina uwezo wa kuangamiza.

k.17 Kama ambavyo tumeona katika ujumbe kwa makanisa mengine Yesu alitoaahadi kwa washindi, wale ambao watadumu waaminifu Kwake potelea mbaliwapatwe na maudhi na mateso gani. Kristo aliwaahidi nini? „baadhi ya manailiyofichwa‟ na „jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtuila yeye anayelipokea‟? Nini maana yake? Wale wanaokataa kuhudhuriakaramu za kipagani watakaribishwa kwenye karamu ya Masihi wa kweli,watasikia „shibe‟ ya kweli (Yn.6:33ku). Jiwe jeupe litakuwa nini? huenda ni isharaya „tiketi/kiingilio‟ iliyotakiwa na mtu ili aingie sherehe fulani. Ama ni jiwe jeupealilotumia hakimu mahakamani alipotaka kuuonyesha uamuzi wa „huna hatia‟.Yasemekana jiwe lilitumiwa kama tiketi, pia, lilitumiwa barazani. Ni vigumu kujuakwa uhakika kama hayo ndiyo maana yake. Labda ni njia ya kusema ni yule mtumwenyewe ndiye atakayeingia. Si wazi kama jina jipya ni la mtu au la Mungu.Laweza kuwa ishara ya utu mpya na tabia mpya ya muumini na ya kusisitizakwamba yule mtu mwenyewe, mwenye nafsi yake kipekee ndiyeatakayeshirikishwa mambo mema ya baadaye. Jina jipya huenda ni ishara yamtu aliyebadilishwa na Kristo ambaye mwenyewe anayafahamu mabadilikoyaliyotokea ndani yake. Kwa vyovyote maneno hayo yaashiria maisha mapya yabaadaye ambayo hayaelezeki kwa kulingana na wakati huo(1 Kor.1:9ku).

2:18-29 Barua kwa Kanisa la Thiatira(Leo Thiatira ni Akhisar, mji wa kisasa, mji wa maendeleo, kwenye njia kuu yakutoka Izmir mpaka Bursa).Mji huo ulikuwa maili kama 40 kusini mashariki ya Pergamo, mji mdogo kulikomiji mingine ambayo makanisa yao yaliandikiwa barua ila barua yake ni ndefukuliko zao. Mji ulijengwa katika nchi tambarare, mahali rahisi pa kushambuliwa

Page 36: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1406

na Warumi waliweka kikosi cha askari pale kuilinda njia ya kwenda Pergamo, jijikubwa la jimbo. Palikuwepo hekalu kwa Tyrimnos na inaonekana ibada yakeiliungana na ibada ya Apollo mungu wa jua. Katika sarafu za pesa upande mmojaulikuwa na sura ya Kaisari na wa pili sura ya Apollo. Mji ulijulikana kwa biasharana vikundi vingi vya ufundi vilivyokuwapo.

k.18 Yesu alijiita „Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wamoto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana‟ (1:14b,15). Ni hapo tukatika Kitabu kizima Yesu ameitwa Mwana wa Mungu. Anayaona yote (machokama mwali wa moto) naye atakuwa mwepesi wa kuyafuatia maovu nakuyakandamiza (miguu iliyosuguliwa sana) (Dan.10:6). Yesu ni Mungu hakimuachunguzaye ndani na kuzitambua hila za Yezebeli. Hasira yake yawaka juu yawote waipingao kweli na kuwapotosha watu wake.

k.19 Yesu alijua nini kuhusu Kanisa hilo la Thiatira? Alifahamu kwamba Wakristowa pale ni wenye upendo na imani, walimtumikia Mungu na kuhudumiana waokwa wao katika maisha ya kila siku. Walikuwa wavumilivu, tena walikuwa namaendeleo katika maisha ya kiroho wakifanya vizuri zaidi ya hapo nyuma. Yesualiwasifu kwa mengi mazuri.

k.20 Lakini Yesu alikuwa na neno juu yao kwa sababu walimkubali mwanamkemmoja jina lake Yezebeli (huenda si jina lake hasa ila ni jina la kuashiria dhambiyake iliyofanana na ile ya Yezebeli, Mfoinike, mwabudu wa Baali,aliyewakosesha Israeli zamani za Mfalme Ahabu na Nabii Eliya (1Waf.16:31; 2Waf.9:22). Alijidai kuwa nabii mke naye aliipotosha imani ya baadhi ya wauminikwa kuwashawishi kwamba si kosa kula chakula kilichotolewa kwa sanamu n.k.Yawezekana aliwaambia kwamba sanamu si kitu kwa hiyo hawawezi kudhuriwana chakula kilichotolewa kwake na ya kuwa ubatizo wao ni kinga, wameokolewakwa neema, Kristo ni nguvu yao kwa hiyo waweza kuhudhuria mahekalu yakipagani na kushiriki katika karamu zilizofanyika humo (1 Kor.8:4). Alijidai kuwanabii mke, labda alidai kwamba amefunuliwa fumbo za Shetani (k.24: labda niYesu aliyeyaeleza mafundisho yake kuwa fumbo za Shetani). Pengine alikuwana uwezo wa kufanya maajabu fulani (1 Yoh.4:1; 2 Tim.3:1). Kwa kifupi twawezakusema kwamba aliwaambia waweza kucheza na moto bila kuunguzwa nao!!Iliyopo ni kwamba alikuwa miongoni mwa waumini na mama mwenye nguvu yakuwashawishi watu. Kwa njia yake ushuhuda wa Kikristo ulipozwa na Shetanialipata njia ya kupenya ndani ya shirika na kuwavuruga. Ni vigumu kujua „kuzini‟kulikuwa jambo la kimwili au la kiroho au aina zote mbili. Katika Israeli jambo lakumwasi Mungu na kufuata mabaali au miungu migeni lilihesabiwa „kuzini‟ kwakuwa ilifikiriwa kwamba Mungu wa Israeli ni „mume‟ wao wa kweli na kumwachakwa „wapenzi wengine‟ (miungu mingine) ni „kuzini‟ (kiroho). Mara nyingi katikamahekalu nafasi za kuzini (kimwili) ziliwekwa, makahaba waliwekwa na upeo wakuabudu ulifikiwa katika kuzini nao.

Page 37: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1407

Jambo hilo liliwawia vigumu Wakristo wengi maana pale Thiatira palikuwepovyama vingi vya wafanyakazi, kama vya wafua shaba, wafinyanzi, wapishi,watia rangi, washonaji n.k. Lidia ametajwa kama mwongofu wa kwanza wa Ulayanaye alitoka Thiatira (Mdo. 16:14). Kila chama kilikuwa na mungu wake, nailikuwa vigumu mtu apate kazi bila kujiunga na chama na kuzihudhuria karamuna sherehe zilizohusika na mungu wa chama chake. Karamu na sherehe hizozilianza na tendo la kutoa dhabihu au kutoa sehemu ya nyama itakayoliwakwenye sanamu ya mungu fulani. Ilikuwa vigumu kwa Wakristo kupata kazi bilakushirikiana na wafanyakazi wenzao katika mambo hayo. Tena mambo hayoyalikuwa kama kawaida ya maisha ya kila siku, kila jambo lilifanyika kwakutambua mungu mhusika kwa kufanya matambiko. Kwa hiyo Mkristo aliyekataakufuata desturi hizo alisikia kama ametengwa na wenzake na mengi ya maishaya kila siku. Ila Kristo, kama Eliya zamani, aliwapa changamoto ya kukata shaurijuu ya yupi watakayemtumikia, Yeye au huyo mama.

k.21-23 Inaonekana wameishapewa changamoto ya kutengeneza jambo hilolakini bado hawajafanya lolote. Hatujui changamoto hiyo ilikuwa kwa njia gani ilaonyo ni kwamba wasipomchukulia hatua huyo mama na wale waliojiunga nayehakika huyo mama na wenzake watapatwa na hukumu. Kwa manenoyaliyotumiwa inaonekana ataugua au kufa ghafula. Ila Kristo awapa nafasi yatoba. Wasipotubu shida itawapata, na kwa shida hiyo watu watafahamu kwambaYesu anajua yatendekayo kati yao naye hatayaachia mambo yaendelea jinsiyalivyo. Kristo ni mpelelezi wa makanisa mwenye kuwaadhibu wakosaji na kutoathawabu kwa waaminifu.

k.24-25 Ila ni wazi kwamba si wote walioshawishiwa na Yezebeli na hila zake.Wapo waliokuwa thabiti ambao walikataa kuridhiana na desturi zilizo kinyumecha imani yao. Bila shaka haikuwa rahisi kuwa Mkristo, walionja shida zakunyimwa kazi, kudhihakiwa n.k. hata hivyo walidumu kuwa waaminifu kwaKristo. Kristo aliwasihi washike sana walicho nacho mpaka mwisho.

k.26-28 Halafu Yesu alitoa ahadi kwa washindi. Ahadi ya mamlaka juu yamataifa. Watamiliki pamoja na Kristo na kuushiriki ushindi wake juu yaulimwengu na nguvu zote zilizokuwa kinyume chake. Kristo alipewa mamlaka juuya mataifa, nao kwa njia ya kuihubiri Injili wamepewa kazi ya kuutangaza Ufalmewake na Ushindi wake. Wote watakaomkataa watapotea na wotewatakaomkubali wataishi (Zab.2). Kristo, peke yake, ni Mwokozi, hakunamwingine, yeye si mmoja kati ya waokozi, wala yeye si mkuu kati yao, bali Yeyepeke yake ndiye Mwokozi (Mdo.4:12). Kwa hiyo wapaswa kumpa Yeye utiifu waowote bila kuridhiana na mengine, wampinge Yezebeli, mdanganyifu, ambayeawafundisha kwamba hamna hatari katika kuridhiana. Wawe na utambuzi juu yahila zake.

Page 38: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1408

Pia walipewa ahadi ya nyota ya asubuhi, dalili ya ushindi. Nyota ya asubuhi niKristo Mwenyewe (22:16). Watazidi kumjua na kushirikiana naye kwa ukaribusana. Wakimwondoa yule Yezebeli wataweza kuwa Kanisa lenye nguvu yakuieneza Injili na kuvuta wengi kwa Kristo.

3:1-6 Barua kwa Kanisa la SardiMji wa Sardi ulikuwa mji wa mafanikio, wa biashara na kujulikana kwautengenezaji wa nguo na vitambaa. Twaona Yesu alijihusisha nao kwa kutajanguo na kwa kugusa historia yao ya kukosa kukesha. Zamani Sardi ulikuwa mjimkuu wa nchi ya Lidia. Ulijengwa juu ya mlima mrefu na wenyeji walipoongezekamji ulienea kwenye eneo la chini kama mji wa pili. Barabara tano zilikutanakaribu yake. Wenyeji walidhani kwamba wako salama kwa sababu mpando mkaliwa mlima uliwatisha maadui wasiweze wakawashambulia. Hata hivyo, katikakustarehe na kujivuna kwamba hawawezi kutekwa, waliacha kuweka walinzikulinda sehemu za mpando mkali na kwa mara mbili adui walifaulu wakija usikukwa njia iliyodhaniwa haipandiki. Mji ulipatwa na tetemeko kubwa la nchi B.K.17lililoharibu mazingira yake na tangu hapo mji haukufanikiwa kama hapo nyuma.Hekalu la Cybele lilijengwa kati ya mji na mto na hilo lilipoangamizwa (K.K.498)lingine la Artemi likajengwa (K.K.334).

Kristo alijitaja kuwa na Robo saba za Mungu na zile nyota saba (1:4,16). Yesualisema nao kama Yule wa kuongoza huduma ya Roho Mtakatifu aliyeiona halihalisi ya ndani, mwenye uwezo wa kuwahuisha waumini au kuleta hukumuisiyotazamiwa.Kristo alianza na neno la hukumu tofauti na kawaida yake ya kutoa sifa kwanza.Alisemaje juu ya Wakristo wa Sardi? Aliwafananisha na mji wao. Kama wenyeji,walikuwa wamelala usingizi, wamekufa ganzi kiroho, hata hali zozote za uhaizilitaka kufa. Ila sivyo walivyoonekana kwa nje, maana walikuwa na „jina la kuwahai‟. Hatusikii habari za uzushi, wala mafundisho ya uongo, wala mateso, walamatatizo fulani, waliishi kwa utulivu ila ulikuwa utulivu wa makaburi. Waliepashida, waliridhiana na hali za pale. Ni Wakristo wasio na moyo wa kutekelezaimani yao, wamekuwa hivi hivi tu, wakiishi kwa mradi tu. Walikuwa na sifa „lakuwa hai‟ lakini hawakuistahili sifa hiyo, wamerudi nyuma na baadhi wamenajisimavazi yao, maana yake wameridhiana na desturi za kipagani na kuuharibuushuhuda wao wa KiKristo. Kanisa la Sardi lilitofautiana na Kanisa la Pergamona la Thiatira, maana Kanisa la Sardi lilikuwa na wengi waliokuwa wameridhikana hali yao na wachache waliokuwa waaminifu lakini katika makanisa yaPergamo na Thiatira wengi walikuwa waaminifu na wachache sio. Kristo aliye naRoho saba aliwafunulia hali yao halisi.

Aliwashauri mambo matano: kukesha, kuimarisha, kukumbuka, kushika, nakutubu. Kwanza aliwasihi wawe tofauti na wenyeji waliokosa kukesha, waowakeshe, waujali mwenendo wao, wautie maanani na kujihadhari na hatari

Page 39: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1409

mbalimbali. Ndipo aliwaita wayaimarishe mambo yaliyosalia, yaliyotaka kufa.Halafu wakumbuke hali yao ya zamani na hasa mafundisho waliyopewa nawalinganishe hali yao ya sasa na mafundisho waliyopewa, ndipo watakapoonawapaswa kurekebisha mambo gani ndipo wayatengeneze na kuyashika yalewaliyofundishwa hapo mwanzo. Kisha wayashike hayo. Haitoshi watambue niwapi wamelegea, wamewajibika kuyashika. Neno la mwisho ni kutubu, yaaniwamrudie Bwana wao Yesu Kristo, waache kuutegemea uzuri wa maishayanayopatikana kwa kuishi katika Sardi. Vema wakumbuke kwamba maishahayo si ya kutegemewa, mji wao umetekwa mara mbili, umepatwa na tetemekola nchi, si mji wa kutegemewa. Adui walikuja usiku „kama wevi‟ na kuuteka.Bwana wao Kristo, Yeye naye atakuja „kama mwivi‟ Yeye ni Bwana wa mabwana.Ni busara wakeshe. Pamoja na kuwa ahadi, Kuja Kwake ni onyo ili watuwajiandae. Wala tusifikiri Yohana alikuwa akisemea Kuja Kwake mwisho wamambo yote, Kristo „huja‟ (naja kwako) mara kwa mara katika hukumu mbalimbali.

Si wote katika Sardi ambao walikaa hali wameridhika na Ukristo wao. Wachachewalikuwa na moyo wa uaminifu na wa kujitoa. Kristo aliwaahidi nini? Kristoaliwaahidi atawavika mavazi meupe (mji ulijulikana kwa vitambaa vyake). Maanayake nini? Watavikwa haki yake na kuwa safi, watatakaswa, watatukuzwa,wataushiriki utukufu wa Kristo Mwenyewe. Wataurithi uzima wa milele, na Kristoatayakiri majina yao mbele za Babake na za malaika wake (Mt.10:32). Kristohatawaonea haya kwa kuwa wao hawakumwonea Yeye haya. Mamlaka ya Kristojuu ya Kanisa yaonekana katika Kitabu cha uzima chenye majina ya warithi wauzima wa milele. Ni Yeye aliye na mamlaka juu ya Kitabu hicho. Walioandikwahumo ni wale tu „waliostahili‟ kwa sababu wamedumu kuwa waaminifu Kwake.Wameokolewa kwa neema na kudumu kwao ni thibitisho la uteule wao. (Kila mjiulikuwa na kitabu chenye majina ya raia wake). Twafunuliwa mawazo ya Kristojuu ya Wakristo wasio na msimamo, wale wanaoridhiana na mazingira yao,wanaotafuta kuishi bila shida na mateso. Kanisa hilo halikusifiwa ila baadhi yaowachache walitajwa kwa uzuri.

3:7-13 Barua kwa Kanisa la FiladelfiaSiku hizi mji huu unaitwa Akhisar, ni kama maili 27 kusini mashariki ya Sardi, mjiwa kisasa wenye maendeleo mazuri. Wakristo wapo.Wakati wa Yohana mji ulikuwa na historia fupi, ulianzishwa kama mwaka K.K.140na watu kutoka Pergamo. Mipaka ya Frigia, Lidia na Misia ilikutana karibu nashabaha ilikuwa kuufanya kuwa kituo cha kuueneza utamaduni, lugha, na desturiza Kiyunani ili zipate nguvu katika nchi zilizopakana. Shabaha hiyo ilifaulu maanawenyeji waliacha kuitumia lugha yao na kuitumia lugha ya Kiyunani. Barabarakuu ya kwenda ndani ya Asia Ndogo mpaka mashariki ilipitia Filadelfia. Mara kwamara matetemeko ya nchi yalitokea hata ilifanya watu wahofu kuishi pale kwahiyo wakazi hawakuwa wengi maana hawakusikia usalama na hata walioishipale walizoea kutoka nje usiku kwa ajili ya

Page 40: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1410

matetemeko mengi. Ardhi ilifaa ulimaji wa mizabibu na mji ulijulikana kwamizabibu yake mizuri. Mara mbili mji ulijengwa kwa upya baada ya kulazwa chinina matetemeko. Ulipewa jina jipya mara mbili au zaidi kufuatana na Kaisarialiyetoa msaada kwa ujenzi wake, lakini watu walirudia kulitumia jina lake lakwanza la Filadelfia. Palikuwapo hekalu la Dionysus pamoja na mahekalu mengiya miungu mbalimbali. Wayahudi waliishi pale na kuwa na sinagogi lao. Kwa jinsibarua inavyotaja Wayahudi inaonekana Wakristo walipata shida kutoka kwaWayahudi, pengine walitolewa sinagogini. Yesu alijihusisha na Kanisa hilo kwakusema alikuwa na „ufunguo wa Daudi‟.

k.7 Kristo aliwasalimu kwa kujiita Mtakatifu, sifa ya Mungu Mwenyewe (Isa.6:3;40:5; 43:15). Neno hilo linaonyesha kwamba Yeye hushiriki hali na tabia zaUungu (6:10). „aliye wa kweli‟ maana yake Yeye ni wa kutegemewa kabisa, wakuaminika kama Masihi wa kweli. „aliye na ufunguo wa Daudi....‟ Ufunguo niishara ya Yeye kuwa na mamlaka yote mikononi mwake, mwenye uwezo wakuyatekeleza mapenzi yake (Isa.22:22).

k.8 Kristo alitoa sifa gani? Alisema „unazo nguvu kidogo‟ kwa maneno hayotwaelekezwa kufikiri kwamba huenda waumini walikuwa wachache ambao kwahali za kimwili walikuwa wanyonge, watu wasio na sauti katika jamii. Hata hivyoKristo aliwasifu kwa uaminifu wao, inaonekana kwamba miongoni mwaohawakuwa na mtu au watu waliowasumbua kwa mafundisho ya uongo aumaisha mabovu. Inaonekana wameishapitia kwenye majaribio ya imani yao naowakadumu kuwa waaminifu kwa Kristo. Hatuambiwi ni nini iliyowapata.

k.9 Yesu alitaka wafahamu kwamba vipingimizi vyao ni nafasi yao ya kuwavutawatu kwa Kristo. Mlango u wazi, nafasi zipo, na Kristo atawawezesha kufaulu,hata adui zao hawataweza kuwazuia, na adui watatambua kwamba ni watuwaliopendwa na Kristo. Kwa hiyo wajipe moyo. Wao ni Israeli ya kweli wenyekuzirithi ahadi zilizotolewa katika Agano la Kale. Kristo alisema hao Wayahudiwaliowapinga ni wa sinagogi la Shetani kwa sababu waliwalaani Wakristo nakumkataa Masihi wao wa kweli. Mambo yamepinduliwa, maana Wayahudiwaliamini kabisa kwamba wao wamechaguliwa na Mungu kuwatiisha WaMataifachini yao, kumbe! wao watawekwa chini ya yule Masihi waliyemkataa na chini yaWakristo, wafuasi wake. Katika Agano la Kale, baada ya Kurudi kutoka Babelimanabii walilitumainisha taifa la Israeli kwamba wao watazidi kuwaongozaWaMataifa na kuwa mwanga kwao (Isa.45:14; 60:14; Eze.36:23; 37:27-28).Kumbe! ni Kanisa, Israeli Mpya, litakalofanya hivi. Yesu aliwaita Wayahudi „wasinagogi la Shetani‟ maana yake hawawi wateule tena. Pengine Wayahudiwaliwatoa Wakristo katika masinagogi yao. Pamoja na hayo maneno „mlango uwazi‟ yaweka mbele za Wakristo nafasi za uinjilisti katika Frigia na Lidia n.k.Kama utamaduni wa Kiyunani ulifaulu kupenya maisha ya wenyeji hao, vivyohivyo, na Injili ina uwezo wa kuenezwa na kupokelewa kwao. Wainue macho yaokwa nafasi zilizo mbele yao, kwa Wayahudi, na kwa

Page 41: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1411

wenyeji mipakani mwao. Kweli, wao wenyewe wana nguvu kidogo, ila KristoBwana wao anao uwezo wa kutosha wa kuwawezesha kuutimiza wajibu huo.

k.10 „umelishika neno la subira yangu‟ Kristo alivumilia mengi alipoishi hapaduniani, naye aliwaachia kielelezo chema, cha kuwatia moyo. Aliwahakikishiakwamba Yeye alielewa jinsi walivyojisikia. Kwa sababu wamevumilia Kristoaliwaahidi kwamba atazidi kuwasaidia watakapopatwa na mashambulio makalizaidi siku za usoni. „utoke katika saa ya kujaribiwa‟ maneno hayo yawezakumaanisha kwamba Yesu atawapitisha salama au atawaepusha na shida. Kwaupande wao iliyotakiwa ni uaminifu. Hatujui ni mateso gani yaliyokuwa mbeleyao, huenda yalihusu Ibada ya Kaisari.

k.11 „Naja upesi‟ maneno hayo hayahusu Kuja Kwake mara ya pili bali KujaKwake kwao na kuwasaidia wakati wa mahitaji yao. Ndipo Yesu aliwashauriwashike walicho nacho wasije wakaipoteza taji yao. Taji ni dalili ya ushindi.

k.12 Halafu Yesu alitoa ahadi kwa kila ashindaye. Ahadi ya kuwa nguzo katikahekalu la Mungu na kukaa humo bila kutoka tena. Ahadi ya kuingizwa katikahekalu la Mungu na kuishi humo milele, yaani kuishi katika Kuwako kwa Munguna mbele zake. Neno hilo la kuwa „nguzo katika hekalu‟ lilifaa sana kwa watuwalioishi mahali pasipokuwa imara, mahali palipotikiswa na matetemeko marakwa mara. Wawe na uhakika juu ya sasa na ya baadaye. Wao ni mali ya Mungu,raia wa Ufalme wa Mungu, washiriki wa Mji Mkuu, Yerusalemu Mpya, na waMwana wake, ndiyo maana ya kuandikwa majina hayo yote, ishara na muhuri yauheri wao katika uzima wa milele. Pengine kutaja majina kuliwakumbusha jinsimji wao ulivyobadilishwa jina mara kwa mara. Kristo hakuwakemea kwa jambololote.

3:14-22 Barua kwa Kanisa la LaodikiaJiji la Laodikia lilikuwa maili 6 kutoka Hierapoli, na miji hiyo miwili ilitajwa katikaWaraka wa Paulo kwa Wakolosai (Kol.4:13). Jiji lilijengwa B.K.261 penye Bondela kukutana kwa Mto Lycus na Mto Meander. Njia tatu zilipitia pale, njia kuukutoka Efeso kuelekea mashariki mpaka Shamu na Ufrata, njia kutoka Pergamokwenda Pisidia na Pamfilia mpaka Perge na nyingine iliyokwenda mpaka Frigiaya kati na ya magharibi. Kwa hiyo jiji hilo lilitawala njia za kuingia Lidia na nchiza mbele yake. Maili sita mbali na mji zilikuwepo chemchemi za maji ya moto,na maji yake yaliletwa kwa bomba mpaka mjini. Yalipofika mjini yalikuwa nauvuguvugu, si mazuri. Jiji lilijulikana sana kwa Chuo cha Uganga na dawa mojaiitwayo „unga wa Phrygia‟ iliyosifiwa sana na kutumiwa kwa kutibu macho. Piadawa ya masikio ilitengezwa pale. Sifa nyingine ilikuwa sufu nzuri za kondoowaliochungwa bondeni, sufu ya rangi nyeusi, laini sana iliyotumika kwakutengeneza mikeka na nguo. Pia jiji lilikuwa kituo kikubwa cha kuendelezauchumi na shughuli za fedha, benki nyingi zilikuwapo. Hivyo Jiji

Page 42: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1412

lilikuwa tajiri sana na wakazi wengi walikuwa matajiri. Palikuwepo ukumbi wakufanyia michezo, tamthilia, michezo ya kuzoeza viungo vya mwili pamoja nauwanja wa michezo. Wayahudi kama elfu saba waliishi humo nao waliruhusiwakufuata desturi zao. Kwa hali nyingi Jiji la Laodikia lilikuwa na sifa nyingi, lilikuwana uwezo wa kujitegemea na kujengwa upya bila msaada wa kutoka nje, wakatiwa kuangushwa na tetemeko la nchi.

Kanisa la pale lilikuwaje? Lilianzishwa nyakati za Paulo, pengine Epafra alihubiriInjili pale (Kol.1:7; 4:12) na Paulo aliwaandikia Waraka ambao hauonekani katikaAgano Jipya (Kol.4:16). Kanisa la Laodikia lilikuwa Kanisa katika Jamiiiliyositawi, watu wakiwa na mali na mafanikio, watu waliokuwa na shibe nautoshelevu wa maisha ya kila siku.

k.14 Kristo alijiita „aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzowa kuumba kwa Mungu‟ (1:5). Amina ni ishara ya uimara wake wa kuwamwaminifu kwa ahadi zake na kuwa thabiti wa kuyatimiza makusudi yake. Yeyeni yule wa kuutoa ushuhuda wa kweli juu ya hali halisi ya Kanisa hilo. Yeye ni wamilele, Mwenyewe hana asili ila Yeye ndiye asili ya vitu vyote, ana mamlaka juuya uumbaji mzima (Yn.1:3; Kol.1:15ku). Sifa hizo hazikutajwa katika maono yasura ya kwanza, ni barua hiyo tu ambayo haikuingiza sifa kadhaa za yale maono.

k.15ku Kristo alijua nini kuhusu Wakristo wa Laodikia? Alijua kwambawamefanana kabisa na mji wao. Hawawi baridi wala moto sawa na maji yachemchemi zao. Hawakuwa na „moto‟ wa kutaka kumshuhudia Kristo na kuletawatu Kwake, wala hawakuwa na „ubaridi‟ wa kuiacha imani yao. Hali hiyoilimchukiza Kristo, afadhali wangalikuwa moto au baridi (Rum.12:11) kwa sababuni vigumu kumwamsha mtu ambaye hasikii ana shida. Wamekaa tu,wameridhika tu, hawana nia yoyote ya kukazana katika mwenendo wao. NiKanisa lililo maskini kiroho ambalo hata benki zote, na farmasia zote za dawa,na viwanda vyote vya ufumaji haviwezi kutibu shida zao. Ni Kristo tu aliye asili yautajiri wa kweli. Sikitiko ni kwamba hawakuitambua hali yao, kinyume chake,walijiona kuwa hawana haja ya kitu chochote. Kristo hakutaja matendo aumakosa fulani ila alijumlisha hali yao jinsi ilivyo machoni mwake.

Kristo alitaka kuivunja hali hiyo ya kutokujali na kuridhika na kujidanganya.Aliwaambia wazi hali halisi waliyo nayo. Machoni mwake ni wanyonge, wenyemashaka, maskini, vipofu, na uchi. Hali za ajabu sana na kinyume kabisa chajinsi wao wenyewe walivyojiona. Tena Kristo alitoboa wazi jinsi alivyosikia kwasababu ya hali hizo. Alisema kwamba amewakinai, amesikia kuwatapika watokekatika kinywa chake. Hakusema amekasirika, wala ya kuwa amehuzunika ilaamewachoka. Ni wa kuhurumiwa sana. Kristo hakuona neno lolote la kuwasifu.

Page 43: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1413

k.18 Lakini Kristo alikuwa na uwezo wa kuzitibu shida zao za umaskini na uchina upofu wa kiroho. Aliwashauri kwa upole sana, hasa tukikumbuka jinsi shidazao zilivyopita zote zilizoonekana katika makanisa mengine. Aliwashauri wajeKwake na kupata mali ya kweli si mali ya dunia hii, kwa sababu katika utajiri waowote hawakumwekea Mungu nafasi ya kuyatawala maisha yao. Pia waje Kwakeili wavikwe haki yake wasijisifie kwa sababu ya sufu yao nzuri bali wavae mavaziya matendo mema na tabia safi. Kristo anayo dawa nzuri kwa roho zao, dawaitakayowasaidia kuyaona yaliyo ya maana katika maisha hayo ili wasidanganywena kushawishiwa na mambo ya dunia hiyo inayopita. Kristo aliwashauri kwaupole na sauti nyororo, kwa upendo wa kuwavuta wafanye bidii na kutubu.Alishuhudia kwamba Yeye huwakemea wale anaowapenda, ni sehemu katikaupendo wa kweli, sawa na upendo wa wazazi walio tayari kusema „la‟ kwa mtotoasije akajiumiza. Kristo alichukua jukumu la kumjia kila mmoja wao. Alitangulia,akaja na kusimama penye mlango wa moyo na kubisha. Hatamlazimisha mtu,amngojea mtu amruhusu aingie maishani mwake kwa shabaha ya kumsaidia.Tangu hapo yeyote atakayeitika vema na kumfungulia atashirikiana vema naBwana wake na uhusiano wao utarudi kuwa mzuri.

Yesu alitoa ahadi gani kwa kila aliyeshinda? Aliwaahidi kwamba wataishi katikauhusiano mwema na wa ukaribu naye katika uzima wa milele, wataketi pamojanaye katika Ufalme wa Mungu. Kristo ameketi kwenye Kiti cha Enzi kwa sababuya ushindi wake pale Msalabani alipopambana na enzi za uovu na kuzishinda(Kol.2:15). Wao nao wapaswa washindane na hali zozote zinazompinga Mungundipo wataushiriki ushindi wa Kristo.

Ujumbe huo ulikwenda kwa Kanisa tajiri katika jamii tajiri na ni onyo kwa wotewaishio katika jamii za namna hii, hasa Wakristo wa nchi zilizoendelea zamagharibi na penginepo. Ni hatari sana kufikiri yote ni sawa na kuridhika na haliya kawaida bila kutia maanani mambo ya kiroho. Twaona Kristo akisema naKanisa hilo kulingana na mazingira yake, kama alivyofanya na makanisa yote.Hivyo twajifunza kwamba Kristo atafuta kusema na Wakristo kulingana na hali namazingira yao. Kwa sababu anawapenda yuko tayari kuugusa udhaifu wao nakuweka wazi shida zao, kuwakemea na kuwafunulia hali yao halisi kusudiwatubu na kuutengeneza mwenendo wao.

MASWALI Jibukwa ufupi:

1. Makanisa hayo saba yalikuwa katika eneo gani?2. Yalikabiliwa na hatari gani?3. Sifa zilizotajwa katika kila barua zilimhusu nani? nazo zilikuwa

zimeishatajwa wapi?4. Orodhesha mambo yaliyosifiwa katika makanisa kwa jumla.

Page 44: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1414

5. Orodhesha mambo yaliyokemewa katika makanisa kwa jumla.6. Nini tofauti kati ya „upanga wa Kristo‟ na „upanga‟ wa utawala wa

Pergamo.7. Waumini wa Laodikia waliishi katika jamii wa hali gani?

Walikosea wapi? Kristo aliwaonaje? Alitoa wito gani?8. Kwa barua hizo saba twajifunza nini juu ya Kristo na jinsi

anavyojihusisha na watu wake?9. Ni matatizo gani yanayowakumba Wakristo wa leo?10. Tunga barua fupi ambayo unafikiri Kristo angewaandikia Kanisa la

mahali pako leo ukikumbuka mazingira yake:a) angesifia mambo gani?b) angekemea mambo gani?c) angetoa maonyo gani?d) angetoa ahadi gani?

SURA 4 - 5: MAONO YA MBINGUNI

Baada ya kupewa ujumbe kwa makanisa saba Yohana Saliitwa na Yesukupanda juu na kuona maono mengine.

Maono ya sura hizo ni ya Mbinguni na ya Mungu katika Kiti cha Enzi akiabudiwana uumbaji wake wote na ya Mwana Kondoo aliyestahili kukifungua kitabuchenye muhuri saba, pamoja na maono juu ya muhuri hizo saba.

Habari njema ni kwamba Kiti cha Enzi kimekaliwa na Yeye aliye kati ya yoteyanayotokea, yote yakiwa katika utawala wake. Kwa macho ya kibinadamuilikuwa rahisi kufikiri kwamba Kaisari ni mkuu mwenye kutawala mambo, lakinisivyo ilivyo. Mambo hayawi kama yaonekanavyo. Wakristo waliobanwa na dhikina mateso inabidi wamkazie macho Mungu wao na Kristo Bwana wao ili wauoneuhalisi wa Yesu kuwa Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Mambo yoteyamo mikononi mwake na mwisho wa ulimwengu na ushindi wa Munguumeamriwa na Mungu peke yake, nao unatambuliwa kwa kutazama mambo jinsiyalivyo machoni pake. Bila maono kutoka Kwake haiwezekani kuutambua ukweliwa mambo jinsi yalivyo hasa. Wakristo wa vizazi vyote wapaswa kuutambuaukweli huo, na hasa zaidi wakati wa kuteswa. Wawe na uhakika kwamba Mungundiye Muumba wa milele na katika Yeye kila kiumbe hupata maana yake naumuhimu wake.

4:1-11 Maono ya Mbinguni: Mungu aabudiwa na Uumbaji Mzima4:1 „Baada ya hayo‟ Yohana alizoea kuyatumia maneno hayo alipoanza habariya maono mapya (7:1,9; 15:5; 18:1; 19:1). Yohana aliona mlango ukifungukambinguni, maana yake, njia ilikuwa wazi; akaisikia ile sauti ambayo aliisikia haponyuma (1:10) sauti ya Bwana Yesu nayo ilimwambia apande juu ndipo

Page 45: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1415

ataonyeshwa „mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo‟. Yohanaaliingia „mbinguni‟ kwa kuitwa na kwa kutawaliwa na Roho. Maneno „hayanabudi‟ huonyesha kwamba mambo hayatokei hivi hivi tu, kama kwa bahati nasibu,bali kwa shabaha ya kutekeleza mapenzi ya Mungu. Matukio ya duniani huwasehemu katika mpango mzima wa Mungu. Yohana aliitwa kwa Makao Makuuyanayotawala na kuongoza ile vita iliyoko daima kati ya Ufalme wa nuru na falmena enzi za giza.

„mbinguni‟ Yohana alitumia neno hilo kwa maana mbalimbali. Hapo ni mahali paMungu kujifunua na kuudhihirisha ukweli wa jinsi mambo yalivyo hasa.

4:2 „mara nalikuwa katika Roho‟ (1:10) maana yake Yohana hakutawaliwa namazingira na hali za dunia bali alikuwa katika hali iliyomwezesha kuyapokeamaono.„na tazama‟ Kitu cha kwanza kilichokamata usikivu wake kilikuwa kiti cha enzi.Alitaja kiti hicho mara 17 katika sura za 4 na 5 na kwa mara 47 katika kitabukizima. Kimetajwa mara 62 katika Agano Jipya lote. Ndipo Yohana alitumiamaneno „kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu yake‟. Neno „kimewekwa‟linatilia mkazo kwamba hakiwi pale kwa bahati nasibu, bali kimewekwa kwamakusudi na Mungu. Tukumbuke kwamba hayo yote si picha ya mbinguni bali nimaono, tusifikiri kwamba kuna kiti pale. Halafu Yohana alitaja ya kuwa mmojaalikuwa ameketi juu yake. Habari njema na faraja kwa Wakristo ni kwamba kitihiki cha enzi kimekaliwa na Mungu Mwenyewe, Mungu wao. Wao wanaogopa kitikingine cha enzi, kile cha Kaisari, lakini ujumbe watakaopata kutoka katika kitabuhicho cha Yohana na kwa maono aliyoyapata kwa Mungu ni kwamba hakika kipoKiti kimoja kikuu cha enzi, kipitacho vingine vyote, nacho kimekaliwa na Munguwao. Hicho kiti cha enzi kinaashiria Makao Makuu ya Mungu. Kutoka Kiti hichomipango ya kuyatekeleza mapenzi yake hufanyika. Iwapo watu wana hiari yakufanya kinyume chake hawawezi kuyazuia mapenzi yake yasitendeke. Munguaweza kuyachukua yote hata maovu na kuyageuza yatimize makusudi yakeambayo mwishoni ni kuleta mambo ya duniani kulingana na ya mbinguni („ufalmewa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, nayeatamiliki hata milele na milele‟ 11:15).

k.3 Tukumbuke ya kuwa Yohana alikuwa amekolewa sana mambo ya Agano laKale na mengi katika Kitabu hicho yafanana na mambo yaliyomo katika Vitabuvya Kutoka, Ezekieli, na Danieli.

Kama desturi yake ilivyokuwa Yohana alijizuiazuia katika kumwelezea Yulealiyeketi juu ya kiti cha enzi, hasa kwa sababu Mungu amezidi maelezo yoteyawezayo kutumika kwa kumwelezea. Yohana alijaribu kuonyesha utukufu wakewa ajabu sana na fahari yake isiyoelezeka kwa kutumia neno „mithili ya‟. Kito„yaspi‟ chaleta wazo la mwanga mkubwa mweupe sana, wa nuru

Page 46: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1416

isiyokaribiwa (21:11; 1 Tim.6:16). „Akiki‟ kilikuwa kito chekundu kama damu,pengine kuashiria hukumu kali za Mungu.

Katika taswira hiyo ya kustaajabisha sana kilionekana kitu cha kuleta faraja„upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi‟(Eze.1:28). Upinde ni dalili ya rehema na neema zinazotoka na kukizunguka kilekiti cha enzi. Ni ukumbusho wa Agano alilolifanya Mungu na viumbe vyake wotewakati wa Nuhu baada ya Gharika kuwaangamiza waasi wote (Mwa.9:8- 17). Kiticha enzi, dalili ya nguvu na uwezo na utawala, kimezungukwa na neema narehema. Agano la Mungu ni la milele kama Yeye alivyo wa milele, hawezikulikana, ni agano la kuizuia ghadhabu yake kwa wote watakaojificha ndani yaKristo, aliye mfano wa safina. Kwao dhoruba imekwisha, Yesu amekufa kwa ajiliya dhambi zao. Mungu Mtakatifu hawezi kuchukuliana na dhambi naameidhihirisha chuki yake kwa dhambi katika hukumu zake. Kwa hiyo olezinazokuja zina shabaha ya kuwaonya na kuwaokoa wenye dhambi, nakuwatakasa waumini. Maono na misiba na maafa yatakayofuata yasitafsiriwekana kwamba Mungu ameisahau ahadi yake kwa Nuhu. Rehema zake ni nyingisawa na utukufu wake ulio mwingi, Yeye hautumii uwezo wake mkuu nje yaupendo wake wa kuwarehemu watu na kuwapatia nafasi za toba. Kwa sababutabia yake ni kuwavuta watu si kuwashurutisha ni wazi kwamba nia yake nikumbadili mtu kuliko kumwangamiza.

k.4 Halafu Yohana aliviona viti vingine vya enzi, ishirini na vinne, ambavyovilizunguka kile kiti cha enzi. Viti hivi vilikaliwa na wazee ishirini na wanne,ambao wameketi juu yake hali wamevikwa mavazi meupe na vichwani wamevaataji za dhahabu. Mavazi meupe ishara ya utakatifu na ushindi na taji za dhahabuishara ya heshima ya kifalme. Neno kwa viti vya enzi ni lilelile lililotumika kwa kiticha enzi cha Mungu. Hao ni akina nani, ni wajumbe au wawakilishi wa nini?

Kwa maelezo ya Yohana ni wazi kwamba wamepewa heshima kubwa, maanawako karibu kabisa na kiti cha enzi, tena wamevaa mavazi meupe dalili ya usafina ushindi, tena wamevaa taji ya dhahabu, taji ya kifalme. Wazo moja ni kwambawapo tu kwa shabaha ya kuuongeza utukufu na fahari na ukuu wa Kiti cha enzina hasa kwa Yule aliyeketi juu yake. Kazi yao ilikuwa kuzitupa taji zao mbele yakiti cha enzi na kumsujudia Yule aliyekaa juu yake na kumpa sifa za ustahili wake(k.10-11).

Wataalamu wameshindwa kupatana kuhusu hao wazee ishirini na wanne kuwani akina nani. Mawazo mbalimbali yametolewa na kuandikwa hapo. Moja nikwamba ni malaika maarufu kuliko malaika wengine wote. Katika Isaya wazeewametajwa (Isa.24:23). Viti vya enzi vimetajwa katika WaKolosai 1:16. Wazolingine ni kwamba ni malaika walio mabalozi wa jumuiya nzima ya waumini. Likowazo la kufikiri wahusika na ahadi ya Yesu kwa Mitume kabla ya kuuawa

Page 47: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1417

kwake. Yesu aliwapa ahadi ya kuketi katika viti vya enzi (Lk.22:28-30) kwa hiyoiwapo haifikiriwi hao ni wale Mitume 12 hasa, hata hivyo wanawakilisha jamii yawote walio waaminifu kwa Yesu na kwa mafundisho aliyowakabidhi Mitume.Wazo hilo lapatana na shabaha ya barua kwa makanisa katika kuwasihi Wakristowawe waaminifu kwa Kristo katika kuyafuata mafundisho ya KiMitume. Tenawazo lingine ni kwamba ni wawakilishi wa waliokombolewa kwa kuwa hesabu ya24 ni ishara ya watu wa Mungu wa Agano la Kale na wa Agano Jipya. Katika21:12 milango ya Yerusalemu Mpya ina majina ya kabila 12 za Israeli na misingiina majina 12 ya Mitume. Ila wengine wameona shida ya kupokea wazo hilowakisema waliokombolewa hawatajwi mpaka 7:9-10 nao hawaketi katika viti vyaenzi mpaka mwisho wa mambo yote kutimia. Potelea mbali ni akina nani auwajumbe gani, neno kuu ni kwamba wako mbele ya Kiti cha Enzi katika hali yakuabudu. Kwa vyovyote hao huuongeza utukufu na fahari na ukuu wa Kiti chaEnzi na wa Yule aketiye juu yake.

k.5 Ndipo Yohana aliuona umeme na kuzisikia sauti na ngurumo zikitoka katikakile kiti cha enzi. Ni ukumbusho wa wakati wa Kutolewa Torati penye Mlima waSinai (Kut.19:16). Mungu hutawala kwa haki ambayo imejumlishwa katika sheriaalizotoa kwa wanadamu. Mara kwa mara umeme na ngurumo zimekuwa isharaya ghadhabu ya Mungu juu ya uasi wa wanadamu. Ulimwengu hauruhusiwikukana Kuwapo Kwake (8:5; 11:19; 16:18; Rum. 1:28ku). Pia umeme nangurumo zinaushuhududia ushindi wa Mungu kama zilivyofanya wakati wa YesuKufa na Kufufuka (Mt.27:51-54; 28:2-3; Ebr.12:22- 29). Ni kama mshindo wamatarumbeta yakisherehekea na kuadhimisha uwezo mkuu wa Mungu Muumba.

Halafu Yohana alitaja habari ya taa saba za moto zilizowaka mbele ya kiti chaenzi nazo ni Roho saba za Mungu. Ni dhihirisho la Roho Mtakatifu katika utimilifuwa kutenda kwake. Yeye huchunguza mambo yote na kufanya kazi za kutakasana kuhukumu. Amejaa hekima halisi na ufahamu kamili. Katika salaam zaYohana kwa makanisa alieleza Roho Mtakatifu kwa lugha hiyo (1:4). Taa hizoziliwaka, ishara ya „moto‟ dalili ya uwezo wake (Mdo.1:6-8; 2:1-4; 1 Kor.4:20-21;Yn.14:16-17). Yesu aliwaahidi wanafunzi wake kwamba Roho atawafundisha natena atawafariji (Yn.14:26-27). Mungu yu pamoja na wafuasi wake kwa shabahaya kuwawezesha ili udhaifu wao ugeuzwe kuwa nguvu ya kuyashinda majaribuyao na kutimiza wajibu wao. Ni neno la kuwafaa Wakristo katika makanisa sabapia lafaa sisi wa leo tunapopambana na dunia iliyo kinyume cha Kristo.

k.6-8 Ndipo Yohana alisema aliona kama bahari ya kioo, kama bilauri, hakusemaaliona bahari ila kama bahari. Ni wazi kwamba ameshindwa kupata lugha yakueleza taswira hiyo. Yasemekana kwamba zamani zile kioo cha kawaidakilikuwa cheusi si wazi, na kioo safi kilikuwa ghali sana. Shabaha ya Yohana nikuukuza ukuu na uzuri na utukufu wa Mungu. Pengine ni

Page 48: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1418

ukumbusho juu ya utakatifu halisi wa Mungu na jinsi alivyo tofauti sana nawanadamu. Kwa hali zote Yeye huwa mbali nasi katika utukufu na utakatifu.Pana pengo kubwa mno kati yake na sisi. Hawezi kukaribiwa ovyo, hata Yohanaaliyeruhusiwa kupita katika mlango uliofunguka alitishwa alipouona utukufu wayule aliyeketi katika kiti cha enzi. Vyote vilivyozunguka kile kiti vilimsujudia,vilikuwako kwa ajili yake tu. Neno hilo ni kitisho sana kwa wale wanaouharibuuumbaji wake na kuwatesa watu wake. Twakumbuka Bahari ya Shamu ilikuwakati ya Waisraeli na Nchi ya Ahadi, Mungu akayasimamisha maji ili Waisraeliwaingie Kanaani ndipo maji yakarudi na kuwameza Wamisri waliothubutukuwafuatia.

Katika mawazo ya Yohana mbingu na dunia zimefungamana, ni za utaratibu wasasa na wa wakati huu. Mungu aliziumba mbingu na dunia za sasa (Mwa.1:1)nazo zitapita, moja haitapita bila ya pili (Isa.65:17; 66:22; Mk.13:31; 2 Pet.3:13).Yohana aliposema juu ya mbingu mpya na dunia mpya jambo la kwanzaalilolitaja ni „hamna bahari tena‟. Bahari pia ni ya utaratibu wa kwanza. Katika13:1 bahari imetajwa kuwa mahali atokapo Mnyama wa kwanza, kama mahalipa maovu. Katika 15:2 waliokombolewa hawana budi waivuke bahari wakitakakuingia mbinguni. Katika 21:1 tumeishaona kwamba hamna bahari tena, penginemaana yake ni kwamba maovu hayatazuka tena kamwe.

Halafu Yohana aliona wenye uhai wanne katikati na pande zote za kile kiti chaenzi. Hapo tena Yohana hana lugha ya kueleza mambo aliyoyaona. Hao wenyeuhai wanne walikuwa mahali pa heshima kuu karibu kabisa na kile kiti cha enzi(5:6; 14:3) nao wamsifu Mungu daima wakiongoza ibada ya mbinguni (5:6; 14:3).Walikuwa tayari kutumika popote duniani (4:6, 5:8,14; 7:11; 14:4; 19:4). Twaonawalihusika na kutokea kwa ghadhabu ya Mungu (6:1-7;15:7). Hao pia wakuzafahari na utukufu wa Mungu aliyeketi katika Kiti cha Enzi.

Hao ni akina nani au wajumbe gani? wanawakilisha nini? Wataalamu wengihufikiri ni makerubi na maserafi, wakuu katika malaika, ambao katika Agano laKale waonekana kuwa walinzi wa mambo matakatifu (Mwa.3:24; Kut.25:20; 1Sam.4:4; 2 Sam.6:2; Zab.80:1; 99:1). Ezekieli alitaja Makerubi na Isaya Maserafiila ziko tofauti katika mambo kadha na hao wa Ufunuo (Isa.6:1-3; Eze.1:5ku.10:19-20).

Haidhuru walikuwa akina nani twaelekezwa kufikiri kwamba wanawakilisha ainaya viumbe vilivyo hai. Simba – wanyama wa mwitu; ndama – wanyama wakufuga; tai – ndege; uso wa wanadamu – wamadamu. Wengine waona kwambahao huashiria hali mbalimbali kama nguvu (simba), utumishi (ndama), wepesi(tai), akili (mwanadamu). Maumbile yanawakilishwa mbele ya kiti cha enzikatika hali ya kumwabudu Muumba wake na kuwa tayari kufanya mapenzi yake.

Page 49: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1419

„kila mmoja alikuwa na mabawa sita na pande zote na ndani wamejaa macho‟huenda mabawa ni ishara ya utii na utayari wao wa kufanya mapenzi ya Mungu.Macho ni dalili ya kukesha daima.

k.8b-11 Wimbo wao ulitangaza Utakatifu wa Mungu wa Utatu, Mungu Mtakatifundiye kiini cha wimbo huo (Isa.6:1ku). Kwa sababu Mungu ni Mtakatifu na waMilele viumbe wanawajibika kufanya mapenzi yake na kumsifu na kumwabudu(Rum.1:19-20). Pamoja na Utakatifu wake jambo lingine la maana ni Umilele waMungu Muumba (1:4; Kut.3:14). Mungu ni mwema na wa kweli na alikusudiamema kwa uumbaji wake (Mwa.1:31) kwa hiyo, kwa vyovyote atauongozauumbaji utimize lengo lake, atatekeleza ukombozi wa viumbe vyake, ukomboziwa kuumbwa upya baada ya anguko (Ling.Mwa.3:1ku. na Ufu.5 inayofuata surahiyo).

k.9-11 Wenye uhai wanne walimsifu Mungu kwa sababu alistahili kusifiwa nakupewa utukufu, heshima, na shukrani. Ndipo wale wazee ishirini na wannewaliitika kwa kujiunga nao; walianguka mbele zake yeye aketiye juu ya kiti chaenzi na kumsujudia na kuzitupa taji zao mbele yake. Neno „wanapompa‟linaonyesha kwamba hao wenye uhai wanne walizoea kumsifu Mungu kilawalipomwona ameudhihirisha ukuu wake (5:8,14; 11:16; 19:4). Hao wazeeishirini na wanne pia walimpa sifa za ustahili wake, utukufu, heshima na uweza.Ni kwa sababu gani walifanya hivyo „kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vituvyote na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa‟. Hivyowalimsifu Mungu mwenye kuviumba vitu vyote, Mungu hai, Mungu mwenyeuwezo. Ni Yeye tu aliyestahili kuupokea utiifu wa wanadamu na kuabudiwa.Maovu yamesababishwa na wanadamu kuvipotosha vilivyofanyika vyema sanana Mungu (Mwa.1:31). Utakatifu wa Mungu ndio msingi wa maovu yotekuondolewa na mwishoni kufutwa kabisa, ndipo hapatakuwepo nafasi tena kwakitu chochote kilicho kichafu au kisicho cha kweli (21:27).

Kwa asili ulimwengu ni mali ya Mungu nao ni mwema. Wakristo walihitaji kujuanjia zitakazotumiwa na Mungu katika kuutiisha chini yake ulimwengu uliomwasi.Mungu awezaje kuutawala ulimwengu wa uasi? Katika sura zifuatazo Yohanaalipewa maono juu ya njia hizo za kuukomboa ulimwengu wa uasi, nafasi za tobazitakazotolewa, na hukumu zitakazowapata wasiotubu. Wakristo watashindakwa njia ya kuwa waaminifu hadi kufa katika majaribu yao yote.

Ni vema tusikwame katika kutafuta maana ya kila neno, tukumbuke kwamba nimaono na ni wazi kwamba neno kuu la kushikilia ni kiti cha enzi na yulealiyekikalia. Yote mengine yaliongeza fahari wa kile kiti na yule aliyeketi juu yake.Kila kitu kingine hakina maana yoyote nje ya kile kiti cha enzi. Ni taswira juu yaMungu Muumba hali akiabudiwa mchana na usiku na viumbe vyake

Page 50: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1420

vyote. Kiti cha enzi ni ishara ya utawala wake juu ya mambo yote. Mungualiviumba vitu vyote kwa ajili yake Mwenyewe, si kwa ajili ya watawala waulimwengu huu wala kwa Kanisa na wakuu wake. Mwisho wa uumbaji ni juu yake.

MASWALI1. Yohana alipata maono hayo ili Wakristo waelewe nini?2. Maneno yafuatayo yana maana gani:

„nalikuwa katika Roho‟„kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi....‟„upinde wa mvua ulikizunguka katika kiti cha enzi‟

3. Toa mawazo kuhusu wale „wazee ishirini na wanne‟e) „Roho saba za Mungu‟ Roho Mtakatifu ni mmoja, mbona basi twasoma

Roho saba? Eleza maana ya maneno hayo.f) Toa mawazo kuhusu wale „wenye uhai wanne‟.g) Mungu alipewa sifa gani na hao wamwabuduo mchana na usiku?h) Taswira nzima iliashiria nini na vitu vingi vimetajwa kwa shabaha gani

hasa?

5:1-14 Maono Ya Mbinguni: Mwana-kondoo Wa MunguKatika sura ya nne tulipewa habari ya maono ya Yohana juu ya Mungu Muumbakatika Kiti cha Enzi akiabudiwa na uumbaji mzima. Katika sura hii tuna habari yamaono ya Mungu Mwana, Mkombozi wa ulimwengu, akishirikishwa Kiti cha Enzina kuabudiwa na uumbaji wote, sawa na Mungu.

k.1 Jambo la kwanza katika maono ni Yohana kuona kitabu kilichotiwa muhurisaba. Kilikuwa katika mkono wa kuume wa Mungu (mkono wa kuume ulikuwaishara ya heshima). Kilitiwa muhuri saba, inaonekana kitabu kilikuwa na sehemusaba, kila sehemu ilitiwa muhuri, na kila muhuri ilihitajiwa kuvunjwa. Kitabu kilijaamaandishi ndani na nje, ishara ya utimilifu na ukamilifu wa mambo yaliyomo, yoteyamo. Muhuri zilionyesha kwamba mambo ya kitabu hayatajulikana wala mamboyake hayatatekelezwa mpaka muhuri zake zitakapovunjwa. Mungu ayajua yote,ameyapanga yote tangu mwanzo, ila hayatatokea bila Kristo. Mambo yaliyomoni yale yatakapotokea muhuri zitakapovunjwa, mpango wa Mungu wa kukomboaulimwengu.

Wazo ni kwamba kitabu kina habari za mipango ya Mungu ya ukomboziuliotabiriwa katika Agano la Kale. Kwa njia ya Ukombozi Mungu ataweka utawalawake juu ya ulimwengu uliomwasi na hatua kwa hatua ulimwengu utarudishwana kulifikia lengo la kuumbwa kwake. Hivyo mambo yaliyomo yahusu mamboyatakayotokea tangu Kristo alipokufa Msalabani hadi Atakaporudi, ndipo„Yerusalemu Mpya‟ utatokea. Bila ufunuo wa njia atakazozitumia Mungu kwakuuleta Ufalme wake yote ni fumbo na giza.

Page 51: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1421

Makusudi ya Mungu katika Ukombozi yalianza kufaulu Kristo alipozishinda enziza uovu pale Msalabani (Kol.2:15) na yaendelezwa katika kushinda kwa wafuasiwake, wale mashahidi wa kweli, ambao kwa uaminifu wao wanapiga vita vyaimani. Ndipo utatokea ushindi wa mwisho Kristo atakaporudi kama Bwana waMabwana na Mfalme wa Wafalme.

Kile kitabu kilibaki bila muhuri zake kuvunjwa mpaka Kuja kwa Kristo. Mungualikuwa ameweka mpaka katika Uwezo wake. Wanadamu pamoja na uumbajimzima watalitimiza lengo la kuumbwa kwake kwa njia ya yule Mwanadamualiyestahili kwa sababu alikuwa tayari kujitoa kabisa kufanya mapenzi yake.Huyo ni Yesu Kristo. Kwa hiyo kuzivunja muhuri ni zaidi ya kuyafunua mapenziya Mungu ni ya kuyatekeleza pia.

(Mawazo juu ya muhuri 7, tarumbeta 7, na vitasa 7 - Je! ni mambo tofauti nayanayofuatana, mambo ya vitasa yakifuata baragumu, na mambo ya baragumuyakitanguliwa na muhuri? Labda siyo. Pengine ni vema kuwaza kwamba nimambo mamoja, yakitazamwa kwa upande mmoja, halafu kwa upandemwingine, pia kwa mikazo ya tofauti, pamoja na kuingiza mambo mapya katikamambo yaleyale. Ni mfano wa mpiga picha ambaye apiga picha ya mtu, halafumazingira yake, mara ampige kwa karibu, mara kwa mbali, mara kutoka upandefulani halafu upande mwingine n.k.

k.2 Baada ya kukiona kitabu cha muhuri saba Yohana alimwona malaikamwenye nguvu. Ilihitaji malaika wa nguvu kutoa wito mkubwa kwa uumbaji wote.Kwa sauti kuu aliuliza „N‟nani astahiliye kukifungua kitabu na kuzivunja muhurizake?‟ Mkazo ni juu ya ustahili (si nguvu) wa yule aliyetakiwa. Kitabu kinahukumu za haki ya Mungu juu ya ulimwengu wa uasi kwa hiyo yule wa kuzivunjamuhuri, yaani, kuzitekeleza hukumu hizo apaswa kuwa mwema, mwenye haki,mwadilifu wa hali ya juu, ambaye kiroho amestahili kufanya kazi hiyo.

k.3 Hakuna aliyepatikana wa kuuitikia wito wa malaika. Hamna malaika, walakerubi, wala mtakatifu, wala nabii, wala kuhani, aliyekuwa amestahili kukitazamalicha ya kukifungua kitabu. Yohana alisikitika mno, akalia sana. Alihuzunishwasana kwa sababu alitamani sana sana kuona makusudi ya Mungu yatimizwekumbe! yamesimama; matumaini yamekwisha. Aliambiwa ataona mambo yajayo(4:1) kumbe mambo yameshindikana. Makusudi ya Mungu hayatafunuliwa walahayatatekelezwa asipopatikana mtu aliyestahili. Amekosekana mtu wa kuletahaki na kulipiza kisasi watesi wa watu wa Mungu (6:9).

Bila shaka mambo yalitokea hivyo ili iwe dhahiri kwamba katika wanadamuhakuna hata mmoja aliyestahili. Hamna mmoja awezaye kuzivunja pingu zadhambi, wala kufanya fidia ya dhambi, wala kuziharibu enzi za maovu nakuzifutilia mbali.

Page 52: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1422

Kwa malezi yake ya Kiyahudi Yohana alikuwa amekolewa tumaini la Masihi nakuamini kwamba siku moja Mungu ataushika utawala wa kifalme hapa dunianina kuwaadhibu wahalifu na kutengeneza yote yaliyopotoka. Wakati wa matesowatu wa Mungu walitamani sana kufikia kikomo cha mateso yao na kupataushindi wa imani yao. Kama haki haitashinda, imani katika Mungu mwenye hakini bure. Mungu Mtakatifu na wa haki budi alipize kisasi (Lk.18:7)

k.4 Kama kitabu hakitafunguliwa watu wa Mungu hawana ulinzi wakati wa dhikizao, wala hakuna hukumu kwa ulimwengu unaowatesa, wala hakuna matumainiya ushindi mwishoni, wala hakuna mbingu mpya na dunia mpya na urithi wauzima wa milele.

k.5 Ndipo mzee mmoja (mara nyingi malaika alisema na Yohana) wa walewazee ishirini na wanne akamtuliza Yohana na kumwambia asilie kwa sababuamepatikana mmoja aliyestahili kukifungua kitabu. Alimtumainisha kwa kutaja„Simba wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi‟ lugha aliyoifahamu Yohana kutokaAgano la Kale (Mwa.49:9; Isa.11:1,10). Kwa hiyo, atakayetokea kukifunguakitabu ni yule Masihi aliyeahidiwa. Kwa hiyo matumaini na matazamio yoteyanakaribia kutimizwa.

k.6 Hivyo alitazamishwa atamwona „simba‟ lakini alipotazama kumbe! alimwonaMwana Kondoo (si simba) hali amesimama, tena alionekana kana kwambaamechinjwa. „kana kwamba‟ kwa sababu yu hai, amefufuka katika wafu. Kifochake chadumu kuwa cha thamani. Naye alikuwa katikati kabisa ya kiti cha enzina ya wale wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Alikuwa napembe saba, ishara ya nguvu na mamlaka yake, mwenye uwezo wa kulikabilikila jambo. Macho saba, ishara ya ukamilifu wa kuona kwake na uwezo wakupenya ndani ya kila kitu. Sifa hizo ni za Mungu na Kristo huzishiriki(1 Kor.1:24). Roho Mtakatifu alitumwa ulimwenguni kama pembe na macho yaMwana Kondoo (Yn.15:26; 16:7; Mdo.2:33). Roho saba ni maneno ya kuashiriautimilifu wa kutenda kazi zake kwa uwezo na bidii. Kwa hiyo kudura ya Mungu sikukandamiza (kama simba) bali ni kusihi bila kukoma, kusubiri na kuvumilia.Kudura aina hiyo ndiyo msingi na kiini cha Kiti cha Enzi, kwa kuwa MwanaKondoo ametawazwa baada ya Kudhiliwa kwake na Kuuawa kwake. Kwawengine ni kikwazo na upuzi, bali kwa wengine kama Wakristo katika makanisasaba ni „uwezo wa Mungu‟ kuwaokoa (1 Kor.1:22-24). Yesu alizishinda enzi zauovu na nguvu za dhambi na mauti kwa kifo chake, vivyo hivyo, Wakristowatazishinda nguvu za uovu zilizolishambulia Kanisa kwa kujitoa kwa Kristo. Kilabarua ilimalizika na ahadi kwa „ashindaye‟. Hayo maono yalikuwa ya ajabu sanayenye maana kubwa sana kwa historia ya ulimwengu na ya wanadamu.

Mwana-Kondoo aliyeonekana kana kwamba amechinjwa ni ishara ya KristoMkombozi aliyesulibiwa Msalabani. Kwa nini Kristo amestahili? Amestahili kwasababu alijitoa mpaka kufa kwa ajili ya kulitatua tatizo kuu la wanadamu

Page 53: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1423

ambalo ni dhambi. Upendo ndio kitu cha nguvu, upendo wa kujitoa, na kwaupendo wa namna hiyo Mungu ataushinda ulimwengu. Msalaba ni kiini chamakusudi yote ya Mungu. Kristo yu hai baada ya kufa naye amepewa heshimaya hali ya juu kwa kukirimiwa jina lipitalo kila jina na kwa jina lake kila gotilitapigwa na kila ulimi utakiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana kwa utukufu waMungu Baba. Wakristo walioandikiwa katika yale makanisa saba wataitwa kukiri„Kaisari ni Bwana‟ ila itawapasa kuwa waaminifu kwa Kristo na kukiri „Kristo niBwana‟. Hivyo ni maono ya kuwafunulia Wakristo uhalisi wa kimsingi, ukweli wauwezo mkuu wa Kristo kuwa umefungamana na kujitoa upeo. Mwana kondooalionekana dhaifu mwenye jeraha za mauti ila ni Yeye ambaye atayatimizamakusudi ya Mungu na kuitekeleza mipango yake. Mamlaka aliyopewa ilikuwathawabu kwa Kujitoa Kwake na ni faraja kuu kwa watu wake.(Watu wa dunia wanazo ishara zao za nguvu, mara nyingi huwa wanyama aundege wakali, tazama ishara ya mataifa „makubwa‟ Urusi - dubu; Uingereza -simba; Ufaransa - chui; Amerika - tai. Kwa ishara hizo picha ni ya „nguvu‟ kamazana za vita, teknologia, utawala wa dikteta, sayansi n.k.)

Pembe saba ni dalili ya uwezo na mamlaka yake ya kifalme na macho saba niishara ya utimilifu wa ujuzi na ufahamu wake. Macho saba ni picha ya RohoMtakatifu hali akifanya kazi kwa uwezo na bidii katika dunia yote. Yeye ni pembena macho ya Mwana Kondoo, maana ni Yeye asemaye mioyoni mwa watu nakuzigusa dhamiri zao, akiwashtaki dhambi na kuwatafsiria Kristo na maana yakazi yake (Yn.16:13ku.) Tukitazama Injili ya Yohana kuanzia sura 14 - 16 twaonaya kuwa Yesu alitoa mafundisho mengi juu ya Roho Mtakatifu hata alisema ilifaaYeye aondoke ili Roho aje (Yn.16:7). Yesu atakufa kwa ukombozi na Rohoatawafahamisha watu mioyoni mwao maana ya Kifo chake na kuzileta barakazake nafsini mwao. Kwa hiyo Mungu ataitekeleza mipango yake ya kuutiishaulimwengu wa uasi chini yake kwa kuutumia uwezo mkuu uliofungamana naupendo wa ajabu.

k.7 Ndipo Yohana alimwona Mwana-Kondoo akija na kukichukua kitabu natendo hilo lilisababisha wale wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wannekuanguka mbele zake (hata kabla hajazivunja muhuri zake). Kila mmoja waoalikuwa na kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, wakimwabudusawa na Mungu. Kwa tendo la upatanisho ambalo limeishafanyika paleMsalabani Kristo ameupokea Ufalme na mamlaka ya kutawala yote, ndiyomaana ya kukichukua kitabu. Baba hakuacha kiti cha enzi ila Kristo alikaribishwaawe pamoja naye (22:1) hivyo Mungu hutawala kwa njia ya Mwana Wake.(Mt.28:18; Flp.2:9; Ebr.2:8-9; Zab.2 na 110; Dan.7: 9-14). Kwa hiyo wakati mpyaumetokea mbinguni na duniani (20:1-4) Agano Jipya limetengenezwa. Shetaniamefungwa (Ling. Mt.12:28ku), mbinguni roho za wafu zamiliki pamoja na Kristo.Yesu ni ufunguo wa historia na kwa njia yake Mungu atayatimiza makusudi yakeya kuushinda uovu.

Page 54: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1424

k.8 Mara alipokichukua kitabu furaha kuu na sifa kuu zilitokea, wale wenye uhaiwanne, na wale wazee ishirini na wanne, wote walianguka mbele zaMwana-Kondoo na kumwabudu. Alishangiliwa kwa ushindi wa Msalaba,akatawazwa juu (Flp.2:7-11 hasa k.9 „kwa sababu hiyo‟..) akapewa haki yakukichukua kitabu na kuzivunja muhuri zake. Hivyo mambo yalifikia upeo naUumbaji mzima ulimsifu, kwa kuwa kama uumbaji uliingizwa katika laana yaAnguko vivyo hivyo uumbaji unashirikishwa baraka za ukombozi wa Kristo(Kol.1:20; Rum.8:18ku). Kila mmoja wao alikuwa na kinubi na vitasa vyadhahabu vilivyojaa manukato na tumeambiwa kwamba manukato ni maombi yawatakatifu. Maombi ya watu wa Mungu yaliletwa mbele za Mungu katika vyombovya dhahabu, dalili ya thamani yake. Hapo duniani wamedharauliwa,wamehesabiwa kuwa si kitu, lakini kwa Mungu ni wapenzi, mboni ya jicho lake,wa thamani sana. Yeye huyajali maombi yao na kuyajibu. Kwa hiyo, si kazi burekudumu katika maombi, si bure kutamani sana Ufalme wake uje, maombi nisehemu ya maana katika mpango wa Mungu wa kuuleta Ufalme.

k.9 Waliimba wimbo mpya, ni mpya kwa sababu Agano ni Jipya na limetokezahali mpya katika uhusiano baina ya Mungu na uumbaji ambao umesababisha nakuhitaji itikio jipya. Waliimba nini? Waliimba „wastahili wewe kukitwaakitabu......kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako, watu wakila kabila... ukawafanya kuwa ufalme na makuhani...nao wanamiliki juu ya nchi‟.Mwana Kondoo amestahili kwa sababu ya mambo matatu (i) „alichinjwa‟ yaaniKristo alijitoa mpaka kufa, akavumilia kifo cha ukatili sana. (ii) „akamnunuliaMungu watu‟ kutoka aina zote za wanadamu. (iii) „akawafanya kuwa ufalme namakuhani kwa Mungu wetu‟ (1:6). Kuwa Mkristo ni kuwa mfalme na kuhani kwanjia ya Kristo. Kwa njia yao Kristo anaendelea kufanya kazi zake za kifalme nakikuhani. Watu wake wamekuwa shirika ya makuhani, watu wa kumtumikiaMungu pia wamekuwa „ufalme‟ hali wanatawala duniani kwa kutumia silahazilezile alizotumia Kristo, silaha za upendo, uvumilivu, amani n.k. tunda la Rohomioyoni mwao (Gal.5:22; Efe.2:6; 1 Pet.2:9). Utawala wao si wa nguvu za duniawala si kwa taratibu za siasa bali ni utawala wa kiroho kwa kutumia „nguvu‟ yaupendo wa kujitoa. „kwa damu yake‟ ni ukumbusho wa gharama kubwa mno yaukombozi wao. Waliokombolewa ni mali ya Mungu.

k.11-12 Halafu malaika wengi wasiohesabika kwa wingi wao, pamoja na walewenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne walijiunga pamoja nakuzipaza sauti zao katika sifa kuu kwa Mwana-Kondoo. Sifa zao zilitaja uweza,utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu na baraka zake (ni sifa saba kuashiriakwamba Yesu amezistahili sifa zote nazo zimetajwa mahali mbalimbali katikaAgano Jipya). Yesu amestahili kabisa kupewa sifa hizo zote, kwa sababualichinjwa.

Page 55: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1425

k.13 Ndipo viumbe wote walijiunga katika sifa hizo wakitaja mambo mannekuhusu Mungu na Mwana Kondoo. Sifa hizo zadumu milele na milele kwasababu Mungu na Mwana Kondoo ni wa milele na milele. Usawa wa Mungu naMwana Kondoo umedhihirika. Katika kitabu hicho wako pamoja katika ghadhabu(6:16) wako pamoja na waumini katika kuwafariji (7:9,10,17; 14:1,4) Mungu naMwana Kondoo ni „hekalu‟ na „nuru‟ na „maburudiko‟ na „watawala‟ katikaYerusalemu mpya (21:22,23, 22:1,3). Mungu na Mwana huwa umoja (Yn.10:30).Kisha wale wenye uhai wanne wakatia sahihi zao kwenye sifa hizo naowakasema „Amina‟ (hao walianza sifa 4:8). Wale wazee wakaanguka nakusujudu. Maono hayo yanaudhihirisha uhalisi wa mambo jinsi yalivyo hasa.Kwa macho ya kibinadamu na kwa kutazama mambo ya hapa duniani,inaonekana kwamba maovu yana nguvu, wabaya huwasumbua na kuwatishawatu wema, wadanganyifu na waongo huzidi kupotosha mambo. Hata hivyo,Mungu amepata dawa ya kutibu ugonjwa wa dhambi, na kwa Yesu Kristo, Munguatazidi kuyahukumu na kuyaondoa maovu na siku moja wapinzani wake wotewasiokubali kutubu wataangamizwa.

Ulimwengu unatawaliwa kutoka Kiti cha Enzi kwa hiyo walioandikiwa hawanahaja ya kumwogopa Kaisari, hata ikiwa watauawa, kifo chao si neno lamwisho, roho zao zitalindwa salama hadi siku ya ufufuo ndipo na miili yao piaitafufuka nao wataishi milele na milele sawa na Bwana wao na pamoja naye.Mungu ndiye mwenye neno la mwisho. Kutawazwa kwa Kristo ni mwanzo wahukumu (sura ya 6 na kuendelea). Kufa na Kufufuka kwa Kristo ni jibu la Mungukwa dhambi, na dhambi imepigwa marufuku katika maisha ya wanadamu, tanguhapo watu hupewa nafasi ya kutubu au kupatwa na hukumu.

MASWALI1. Eleza mambo kuhusu kitabu alichokiona Yohana, kilikuwa wapi na

kilikuwa na hali gani?1. Ni mambo gani yaliyomo kitabuni?2. Kitabu kilitiwa muhuri, jambo hili linaonyesha nini?3. Kwa nini Yohana alilia? alifikirije?4. Yohana aliambiwa atamwona nani? ila alipotazama alimwona nani?

Jambo hilo liliashiria nini?5. Ni nini iliyomfanya huyo Mwana Kondoo awe amestahili kukichukua

kitabu na kuzifungua muhuri zake?6. Mwishoni mwa maono ya sura ya tano Mwana Kondoo alionekana

katika hali gani?7. Wakristo walipata msaada gani kwa maono hayo?

6:1 - 8:5 MUHURI YA SABA: MAONO YA HUKUMU ZA MUNGUKinapofunguliwa kitabu kilichotiwa muhuri mambo hutendeka. Sura zilizotanguliazilikuwa za utangulizi. Katika sura ya tano tumeona Mwana Kondoo aliyechinjwaameadhimishwa, ameishashinda na ushindi wa Msalaba

Page 56: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1426

ndio msingi wa ushindi wa mwisho utakaotokea baadaye atakaporudi kamaBwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme (19:11-22:5). Kabla ya ushindi huowa mwisho Kanisa litapita katika misukosuko na vipingamizi vingi.

Hapo twaanza habari za muhuri saba zinazovunjwa na Mwana Kondoo namambo yaliyomo yafunuliwa na kutekelezwa. Ni vema tusijaribu kuunganishahukumu hizo na matukio fulani ya historia, kwa sababu mambo yaliyotajwahutokea mara kwa mara katika maisha ya kibinadamu. Ila ni hukumu za Mungujuu ya ulimwengu uliomwasi, ni itikio lake kwa ushindi wa Kristo (sura ya 5). Walatusitafute kuchora mpango wa mfuatano wa matukio. Mambo yahusu upana wawakati. Ni matukio ya kawaida katika maisha ya wanadamu wanaomwasiMungu, Yeye amewaruhusu watu wapigane vita, wapate shida za uchumi namipango yao ya fedha kuharibika n.k. Hayo yote yanatokea, si kwa sababuMungu ameziandaa, la, sivyo, zatokea kwa sababu ya uovu na uasi wakibinadamu, ila uhalisi ni kwamba Kristo awaita wapanda farasi waje kusudi watuwatambue ya kuwa hamna wokovu wala amani nje ya Kristo na tiba yake yadhambi. Mungu hawezi kushindwa na lolote litakalotokea, kwa sababu Kristohakushindwa na ubaya uliompata Yeye, aliyachukua yote yaliyotupwa Kwake nakuyageuza kuwa wokovu wa wanadamu.

Muhuri zinapovunjwa kilichoandikwa hakisomwi bali maono yafuata na mamboyatendeka.

Muhuri nne za kwanza hufanana katika mengi; zote zafunguliwa na Mwana-Kondoo; na kila moja hutaja farasi wa rangi fulani, na mpanda farasi (Zek.1:8;6:1ku). Kila mmoja hutokea kwa kuitwa na mmoja wa wale wenye uhai wannekwa mfuatano. Hao wenye uhai wanne walimwabudu Mungu (5:8) wakaonekanakama wawakilishi wa viumbe hai (4:7). Inaonekana wapanda farasi ni wa maanakuliko farasi na kila mmoja ni ishara ya shida na shida hizo zatumiwa na Mungukuleta hukumu yake. Shida za aina hizo zilitajwa na Bwana Yesu (Mt.24).

Ni Mwana-Kondoo anayezivunja muhuri na kuyatekeleza yaliyomo. Iwapo kaziyake kubwa ilikuwa kuokoa, ndani yake ilikuwamo hukumu ya dhambi, na mtuasipomkubali Yesu amwokoe na dhambi zake, imebakia ahukumiwe kwa dhambizake. Dhambi ina mbegu za uharibifu ndani yake.

Kila mmoja wa wale wenye uhai wanne aliita „njoo‟. Alimwita nani? Si Yohana,maana yeye ameisha kuwapo, pengine ni mpanda farasi. Potelea mbali ni nanihasa fundisho ni kwamba shida na misiba haitokei hivi hivi tu, zimeruhusiwa naMungu nazo ni sehemu katika mpango wake wa kuyatekeleza makusudi yake.

Page 57: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1427

6:1-2 Muhuri Ya Kwanza: Farasi mweupeBaada ya kuisikia sauti kuu kama ya ngurumo ya mmoja wa wenye uhai wannendipo Yohana akamwona farasi mweupe, na juu yake mtu mwenye uta, piaakapewa taji. Neno alilotumia Yohana kwa taji ni ile ya ushindi katika michezon.k. si taji ya kifalme. Uta ulitumiwa na Waparthi ambao wakati Yohanaalipoandika waliishi mashariki ya Dola la Kirumi. Mara kwa mara walishambuliaDola la Kirumi mipakani mwake. Wapanda farasi walikuwa mabingwa wa vita,wakitumia uta na mishale kwa ustadi sana. Neno „akapewa‟ linaonyeshaamepewa ruhusa na Mungu kwa kufanya mambo yake. Kwa maneno „alipewataji‟ ni kusema kwamba ushindi anaoupata si kwa uwezo wake mwenyewe tu,bali ni kwa sababu ameruhusiwa na Mungu kushinda. Apata tu kile Mungualichomruhusu awe nacho. Shabaha ya mpanda farasi ilikuwa kushinda, hasaalitaka sana kushinda, nia yake yote ilikuwa kushinda. Huenda ni ishara ya vitaya kuishambulia nchi nyingine, kuvuka mipaka na kuchukua maeneo ya nchi ile.Ijapokuwa vita ni vibaya sana, kwa wengine vita ya namna hiyo ina kivutioambacho rangi nyeupe inaashiria „utukufu‟ wake. Ajabu ni kwamba, hadi leowatu hutumia fedha nyingi katika kujipatia zana za vita, na kuandaa vita yakushambulia nchi za jirani zao. Hawajali kama vita hiyo ni ya haki, wala hawajalihali ya wananchi wao na hali ya maisha yao na mahitaji yao ya lazima. Kupiganakuna mvuto, watu hupenda sana kuwashinda wengine. Fundisho kubwa nikwamba Mungu ameweka nafasi kwa hayo kutokea. Watu hutamani sanaamani lakini wakuta nini? vita!! Amani wataipata wapi?

Liko wazo lingine lipendwalo na baadhi ya wataalamu. Hao hufikiri kwambampanda farasi mweupe ni Kristo na ushindi ni ushindi wa Injili. Wamelinganishana 19:11ku. ambapo Kristo amepanda farasi mweupe, ila katika 19:11 silaha niupanga, Neno la Mungu. Maana yake ni kwamba Kristo ametoka kufanya vita yaInjili, vita inayoendeshwa na mashahidi wake kama wale waumini katikaMakanisa saba. Kwa tangazo la Injili na kwa ushuhuda wao Shetanihughadhabika na kufanya vita kali nao (Mt.10:34ku).

Baadhi ya watu wanaona shida katika kupokea wazo hilo. Hao wanaona muhurinne za kwanza zimefungamana na ni vigumu kumweka Yesu na Injili katikamuhuri za vita, njaa, n.k. Tena wanaona Kristo yuko mbinguni akifungua kilamuhuri, hivyo imekuwaje awe mmoja wa wapanda farasi ambaye tumeambiwa„akapewa‟. Amepewaje? na ni Yeye anayeifungua muhuri? yawezekana, ila sirahisi kufikiri hivyo.Kwa Yohana hakuna jambo lolote, hata likiwa baya sana ambalo Mungu hawezikulitumia katika kuuleta Ufalme wake. Jinsi alivyougeuza ule ubaya mkubwauliofanyika katika kumshtaki na kumwua Kristo, mwenye haki, akamfufua kutokawafu, vivyo hivyo aweza kuugeuza ubaya wote kuwa njia ya kuuhukumu uasi wawanadamu wasiotubu na kuuthibitisha utawala wake juu ya yote mbinguni naduniani.

Page 58: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1428

6:3-4 Muhuri Ya Pili: Farasi MwekunduHalafu Yohana alimwona farasi mwekundu na juu yake amepanda yulealiyepewa kuiondoa amani katika nchi. Akapewa upanga mkubwa, ndipo watuwakauana. Ni wanadamu wanaouana si mpanda farasi. Hapo tena ni ishara yavita, pengine ni vita ya ndani na misukosuko na mafarakano nchini. Ranginyekundu ni ishara ya ubaya wa vita. Iwapo kwa upande mmoja vita ina mvutona utukufu kwa upande wa pili ni chukizo. Fundisho la muhuri ya pili hufananana ile ya kwanza, Mungu ameiwekea nafasi vita akijua hali ya wanadamu nikushindana. Ni njia mojawapo ya kufanya hukumu juu ya ulimwengu wa uasiakiitumia historia ya wanadamu kuwa njia ya kuwahukumu wanadamu. Munguhuruhusu mambo yatokee kulingana na tabia na dhambi ya wanadamu. Hakunajambo linalotokea lililo kinyume chake litakalomshinda.

6:5-6 Muhuri Ya Tatu: Farasi MweusiYohana alipotazama alimwona farasi mweusi na aliyepanda juu yake alikuwa namizani mkononi mwake. Halafu alisikia sauti ikisema „kibaba cha ngano.... navibaba vitatu vya shayiri.. wala usiyadhuru mafuta wala divai‟. Ni ishara ya uhabawa chakula, mshahara wa kutwa ukitumika kwa kununua chakula kwa mtummoja kula kwa kutwa. Walio na mapato madogo wawe radhi na shayiri tu. Ilakupatikana kwa mafuta na divai ni ishara ama ya matajiri kupata chakula chao,au kuona kwamba mimea yenye mizizi mirefu haitaguswa. Hivyo, ijapokuwauhaba wa chakula upo, si njaa, mpaka umewekwa. Wakati wa Kaisari Domitianingano ilipungua sana hata alitoa amri watu wapunguze mashamba ya mizabibukwa nusu na kulima ngano badala yake, lakini wakulima hawakukubali na amriiliondolewa. Mara kwa mara uhaba wa mahitaji ya lazima hutokea kwa sababuya udhalimu wa wakubwa na watu kukosa kufanyiwa kwa haki. Katika hayo yotetwaona ruhusa ya Mungu maana sauti ilitoka katikati ya wale wenye uhai wanne.Tena kwa huruma zake aliweka mipaka katika shida watakazozipata watu.

6:7-8 Muhuri Ya Nne: Farasi wa KujivujivuYohana alipotazama alimwona farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyekuwajuu yake aliitwa Mauti na Kuzimu akafuatana naye. Kwa sababu ni lugha yataswira, ya maono, hatuna haja ya kutafuta farasi mwingine au mpanda farasimwingine kwa Kuzimu. Hao walitokea bila kuwa na nembo au ishara kama nta,upanga, mizani. Baada ya kufa watu waenda kuzimuni. Walipewa mamlaka juuya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawaniwa nchi. Muhuri hiyo hujumlisha matokeo ya ile muhuri tatu zingine. Yahusu vifovitokeavyo kwa vita, njaa, tauni n.k. si vifo vyote. Kila mwanadamu, akipendaasipende, hana budi afe, ila baadhi huwahi kufa kwa sababu zisizo halali. Hatahivyo Mungu ni juu ya hayo yote, Mauti iliingia ulimwenguni baada ya wanadamukumwasi Mungu (Rum.5:12-14). Kuzimu ni mahali pa roho za watu kuingojeahukumu ya mwisho. Tena twaona madaraka ya Mungu katika

Page 59: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1429

kuweka mpaka, yaani ni robo tu ya watu watakaokufa hivyo. Hizo hukumu sihukumu za mwisho, hizo zinatokeatokea katika historia ya wanadamu, zinashabaha ya kuvuta watu wajihoji na kutubu.

KUPEWA ni kuonyesha kwamba hata nguvu za uovu haziwezi kufanya maovuyao bila ruksa ya Mungu. Maovu hayatoki moja kwa moja kwa Mungu, ilaanayavumilia. Anayatumia kuwa chombo cha hukumu na njia ya kuwafahamishawatu juu ya kushindwa kwao ili wamgeukee Kristo kwa wokovu, hivyo ubayawowote unaotokea waweza kutumiwa na Mungu katika kuyatekeleza makusudiyake mema ya kuwaokoa wanadamu.

Iwapo inaonekana Kitabu cha Ufunuo kinafunua hukumu za Mungu kulikorehema zake, ni ujumbe ambao ulimwengu wa uasi unahitaji kuusikia. Ni lazima,kwa sababu hamna dalili za toba. Pia twaona jinsi tabia ya dhambi ni kujiharibu,na Mungu akiiachia nafasi kwa mambo kuharibika. Kifo cha Yesu Msalabanikimezivunja nguvu za uovu (Mdo.2:22ku. Kol.2:15). Mungu huleta mema kutokakatika mabaya, hivyo Shetani hushindwa na silaha zake mwenyewe. Kwasababu, Mungu akiachilia nafasi kwa dhambi, basi wenye dhambi wataumizwana mambo wanayoyafanya, na maumivu hayo ni hukumu yao. Vyote ni mikononimwa yule aliyekichukua kitabu cha muhuri saba na kuzifungua muhuri zake.

MASWALI1. Kwa jumla, muhuri zinatoa habari za nini?2. Ni nani aliyeifungua kila muhuri? dalili ya nini?3. Walipotokea farasi na wapanda wake walisababisha nini kutokea?4. Maneno „njoo‟ „kupewa‟ „robo ya..‟ huonyesha nini?5. Mungu amewekea nafasi kwa shida gani kutokea katika maisha ya

wanadamu? Shida hizo huwa ni njia za Mungu kufanya nini?

6:9-11 Muhudri Ya Tano: Maono katika ulimwengu wa kiroho6:9-17 Hapo mambo ni tofauti sana na yale ya muhuri nne zilizotangulia. Maonoyahusu mashahidi, wale waliokuwa waaminifu mpaka kufa kwa ajili ya Kristo. Bilashaka shabaha ilikuwa kuleta faraja na tumaini kwa wale katika makanisa sabaarnbao walipingwa sana na karibuni hivi walitazamia watateswa kwa imani yao,maana kitabu kinawalenga hao (1:2,9; 2:13).

Muhuri hiyo ya tano haitaji rnmoja wa wale wenye uhai wanne kusema Njookama ilivyokuwa katika mihuri minne ya kwanza. Yohana aliona nini? Aliona rohoza wale waliochinjwa kwa ajili ya Neno la Mungu na kwa ushuhuda wao. Hizoroho zilikuwa wapi? Zilikuwa chini ya madhabahu, mahali pa heshima kuu nausalama sana. Zilikuwa hai, adui zao waliiua miili yao ila hawakuweza kuzigusaroho zao (Mt.10:28). Walikuwa mbali na mashambulio na uharibifu wa ainayoyote. Kwa hiyo, walipokufa duniani, jambo la maana sana lilitokea

Page 60: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1430

mbinguni, vifo vyao vilihesabiwa kuwa dhabihu na ibada na utumishi kwa Mungu(Rum.12:1-2; Flp.2:17) sawa na jinsi kifo cha ukatili cha Yesu kilivyogeuzwakuwa dhabihu ya dhambi.

k.10 Hao mashahidi walimlilia Mungu ili haki yao idhihirike, na Mungu waoaonekana kuwa Mungu wa haki, maana waliuawa isivyo halali, hawakuwa nakosa ila tu walithubutu kumkiri Kristo. Hivyo hukumu yao ilihitaji kubadilishwakwa njia ya Mungu kuwahukumu watesi wao. Mungu aligeuza hukumu ya mautiya Yesu kwa Kumfufua kutoka wafu. Pilato alikata shauri kumtoa kwa adui zakenao wakamwua, watu waliamua kwamba Yesu hakufaa kuwa Masihi wao naowakamwunga mkono Pilato kwa uamuzi wake. Lakini Mungu alifanya nini,akawaachia wafanye yale yote waliyotaka, yaliyokuwemo katika uwezo waokufanya, ndipo siku ya tatu akamfufua kutoka wafu, akaupindua uamuzi wao.Ndivyo itakavyokuwa kwa wote watakaoteswa isiyo halali. Kweli hapa dunianiwatauawa, ila mbinguni mashtaka juu yao hayasimami, Mungu huwatunzasalama salimini, ndipo Siku ya Ufufuo watafufuka mwili na roho pamoja.Walimlilia nani? Walimwita „Mola‟ „Mtakatlfu‟ „Mwenye kweli‟ yule wakutegemewa. Mzigo wao ulikuwa juu ya haki, si kulipiza kisasi kibinafsi. Walitakakujua ni lini ambapo Mungu ataidhihirisha haki yake na kuwapatia haki.Ijapokuwa inaonekana Yohana anataja wale waliokwisha kuuawa, hasa lengolake ni wale ambao karibuni hivi wataitwa kukanyaga nyayo zilezile. Neno hilolahusu wote ambao katika kila kizazi watateswa kwa njia rnbalimbali kwa ajili yakumkiri Kristo. Wote wajitoao kuwa waaminifu kwa Kristo wamehesabiwa harufuya manukato ya Kristo na maisha yao kuwa dhabihu ya kujitoa Kwake. Kilio chaokina maana sana katika mwanga wa kufahamu kwamba Mungu anao uwezomkuu katika ulimwengu huu na uwezo huo unaongozwa na kanuni za haki.

Bila shaka wengine watafikiri kwamba kilio chao ni tofauti na vilio vya BwanaYesu na Stefano ambao walipouawa waliwaombea wauaji wao wasamehewe.Neno linalotawala mawazo ya Yohana lahusu haki, Mungu asiposawazishamambo haitakuwa wazi kwamba Mungu ni mtawala wa haki (Mwa.4:10; Ebr.11:4).

Itikio la Mungu kwa vilio vyao lilikuwaje? Walipewa kila mmoja nguo ndefu,nyeupe. Jambo hilo laukanusha uamuzi wa wale waliowashtaki hapo duniani.Nguo hiyo ilithibitisha haki na ushindi wao. Hawajafika bado kwenye upeo wauheri na baraka ila wamewekewa mbali na uwezekano wa kuchafuka. Wamepataushindi, wamepumzika, na Mungu ameona wapaswa waendelee kupumzikampaka na wenzao wengine watakapoishi na kushinda kama wao walivyofanyaili itimie hesabu yao. Je! ina maana kwamba hesabu hii imeshawekwa, hamnanafasi nyingine huko mbinguni? Tukitazama sura ya saba twaona tumeambiwahesabu ya 144,000, kama hesabu kamili, ila Yohana alipotazama aliona umatiwa watu usiohesabika (7:9) . Huenda maana yake ni

Page 61: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1431

kwamba vifo vya mashahidi ndiyo njia ambayo kwayo Mungu atapata ushindi.Kwa upande wa Mungu Yeye hana mashaka yoyote juu yao. Ila wakati wahukumu ya mwisho ni bado. Katika mwenendo wa historia mateso na dhikizitatokea kwa sababu tabia ya watu ni kuichukia nuru. Paulo aliwafundishawaamini kwamba wamewekewa dhiki kama fungu la imani yao (Mdo.14:22; 1The.3:3).

Twaona umuhimu wa „ushuhuda‟ ili watu wote wapewa nafasi ya kuisikia Injili nakuitika kwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Pia twaona jinsi wanadamuwanavyokazana kuwachukia wale wanaowapa changamoto ya kuamini.k.10 watesi wao waitwa „hao wakaao juu ya nchi‟ wametajwa tena katika 3:10,8:13; 11:10; 13:8,14, 17:8, 13:12, 17:2. Ni usemi wa kueleza wale wanadamuwasioamini, ambao wamestarehe hapo duniani, wakijisikia raha kama wako„nyumbani‟ bila maelekeo yoyote ya kumjali Mungu. „muda mchache‟ ni mudatangu Kupaa kwa Kristo hadi Kurudi Kwake. Urneitwa muda mfupi kwa sababuni muda ulio na mwisho, historia si mzunguko, ni kama mstari unaoanzia wakatifulani na kuisha wakati fulani. Historia ina lengo. Mwisho kabisa utaleta rnwishowa maovu yote na watendao maovu. Msalaba ni thibitisho la kuwa Mungukamwe haridhiani na dhambi.

6:12-7:17 Muhuri Ya Sita: Tetemeko kubwa na kutikiswa kwa vitu vyote(Ling. Mt.24; Ebr.12:26)

Muhuri nne za kwanza zilisema juu ya misiba na shida zitokeazo mara kwa marakatika historia ya ulimwengu. Je! Kanisa linahusikaje na hayo yote? Jibu latolewakwa njia ya Muhuri ya tano. Wakristo washiriki katika taabu za ulimwengu kamawengine wote na zaidi ya hizo wapatwa na magumu na mateso yasiyowapatawengine kwa sababu ya utiifu wao kwa Kristo. Halafu Muhuri ya sita yatupelekakwa Sikukuu ya Mwisho, Siku ya Hasira ya Mwana- Kondoo, Siku ya Mungukusema „Basi! yatosha‟. Itatokea nini katika Sikukuu hiyo?

Yohana aliona mabadiliko katika viumbe vya asili - tetemeko kuu la nchi; na jua,mwezi na nyota kubadilishwa hali, na vyote vilivyodhaniwa kuwa imara vilitegukana taratibu zake zilichafuka. Yohana alitumia lugha ya taswira kueleza habarihiyo „jua kuwa jeusi kama gunia la singa‟ „mwezi wote ukawa kama damu‟ „nyotakuanguka kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake‟ „mbingu kuondolewakama ukurasa ulivyokunjwa‟ „kila mlima na kisiwa kuhamishwa kutoka mahalipake‟. Mara nyingi alisema „kama‟ akitafuta lugha ya kueleza jinsi viumbe hivivilivyoshindwa kuufuata utaratibu wake. Ni mwisho wa uumbaji kwa jinsiulivyokuwa. Twaweza kutokujali lugha iliyotumiwa ila kwa vyovyote tujali jamboambalo linaashiriwa na lugha hiyo ambayo ni hukumu kali ya Mungu.

Page 62: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1432

Wanadamu waliguswa sana sana na matukio hayo, walibaki hali wameishiwanguvu, hawana la kufanya, wala hakuna aliyeweza kuyaepa au kuyatoroka.Wametaja katika mfuatano wa ukubwa na uwezo wao; wafalme, wakuu,majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mtumwa na mwungwana, haidhuruwalikuwa akina nani hawakuweza kujisalimisha katika Sikukuu hiyo. Walipotezamamlaka waliyokuwa nayo, mali waliyokuwa nayo, heshima waliyokuwa nayo,chochote kile walichothamini na kukitegemea. Wa kwanza katika jamii walisikiakuishiwa nguvu sawa na wale ambao hawakuwa na nguvu kama watumwa.Ujasiri wa kumwasi Mungu walipata kwa kudhani kwamba ulimwenguWanamoishi utaendelea tu katika hali ilivyo na vitu vya asili kama jua na mwezina milima n.k. havibadiliki wala havitaondoka. Kumbe, vitu hivi vitakapotikiswandipo hata waasi waliojaa viburi watautambua ujinga na utupu wao. Walitakakufa, waliona afadhali wafe badala ya kukutana na Yule aliyeketi kwenye Kiti chaEnzi na yule Mwana-Kondoo. Hawakuogopa kufa kama walivyowaogopa hao.Hawakutaka kukutana na Mungu aliye Mtakatifu, Mwenye haki, wala hawakutakakuuona uso wa Mwokozi waliyemkataa. Ajabu ni kwamba hawakukubali kutubu.Ni wao waliotumia maneno „hasira ya Mwana-Kondoo‟. Kama ambavyotunasoma katika Rum.1:18ku. watu wamemkataa Mungu, wameukandamizaukweli wa Kuwepo Kwake. Wamegeuza kweli kuwa uongo na kwa sababu hiyoufahamu wao umetiwa giza na dhamiri zao zimekufa ganzi. Wamwona Mungukama jitu la kutisha, mnyama mkali sana na Kristo kuwa Mwana-Kondoo aliyejaaghadhabu, si kama Mpenzi wao aliyejaa upendo na msamaha. Jitu kali hasa niShetani, mungu wao, mdanganyifu, ambaye tangu mwanzo amewaambukizawanadamu uongo wake. Uongo mkubwa ni kwamba Mungu hana haki ya kuwajuu yao wala wao hawana haja ya kumtegea. Sikitiko ni kwamba wamepofushwamacho wayatambue hayo yote. Potelea mbali wawaze nini, ni Mungu na Kristowalio katika Kiti cha Enzi. Ghadhabu ya Mungu ni itikio la utakatifu wake kwamaovu ya wanadamu wakaidi wanaokazana kuongoza maisha yao bila kumjaliMungu. Siku hiyo imeitwa Siku iliyo kuu kwa sababu yatakayotokea katika Sikuhiyo yagusa kila kitu. Ni siku ya mapinduzi, ya viburi na majivuno ya wanadamukutetemeshwa na kuondolewa (Isa.2:12ku. Ebr.12:27).

Ni vema tufahamu kwamba upinzani una sura nyingi, hasa kwa jumla ni mipangoyote ya wanadamu wasiomwekea Mungu nafasi katika mambo ya ujamii, yauchumi, ya siasa, ya elimu n.k. Hasira ya Mwana-Kondoo inatisha sana, kwasababu ni hasira ya yule mpole sana, aliyejaa upendo na rehema na neema,aliye mwema kupita wote, aliyekufa kwa ajili ya wenye dhambi. Kama hukumu yaMungu ilimpatia Yesu alipojitwisha dhambi itakuwaje kwa wale wasiokubali Kifochake kwa ajili yao? Ni vigumu kufikiri kwamba wataachiliwa bila kuhukumiwakwa dhambi zao. Maono hayo hayakulenga kuwatisha waumini balikuwahakikishia kwamba Mungu yu juu ya yote (Isa.44:10).

Page 63: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1433

7:1-17 Watumishi wa Mungu watiwa mihuriSura hii ni tofauti sana na ya sita. Katika sura ya sita tuliona hofu kuu ya waasiwalipofikiwa na hukumu kali ya mwisho. Hapo twaona uheri wa waliokombolewa.Kwanza wakiwa hapa duniani walitiwa mihuri na baadaye twawaona katika haliya kutukuzwa huko mbinguni.

Tuko kati ya muhuri ya sita na kabla ya kuanza kwa muhuri ya saba. Maneno yamwisho katika 6:17 ni swali „naye ni nani awezaye kusimama?‟. Hapo katika suraya saba twapewa jibu.

Katika Kitabu hicho tusifikiri kwamba mfuatano wa mambo ni sawa na sura zake.Mara kwa mara Yohana anaturudisha kwa yale yaliyotangulia na kuyatazamakutoka upande mwingine na kufunua jambo jingine lililomo.

k.1 Hapo inaonekana tumerudi kwa maono ya mihuri minne ya farasi wanne wasura ya sita na shida zilizotokea farasi waliporuhusiwa kutokea, kwa kuutumiamfano wa pepo nne si farasi. (Eze.6:5; 9:1-4). Yohana aliona malaika wannewamesimama katika pembe nne za nchi (ishara ya dunia nzima) nao walizizuiapepo nne zisivume juu ya nchi, wala bahari, wala mti wowote. Pepo ni dalili yauharibifu na nguvu za upepo zilizohitaji kushikwa na kutawaliwa. Hivyo, maanayake ni kwamba Mungu ndiye mwenye uwezo juu ya uharibifu unaotokeatokea.Hoja mojawapo ya maana ya Kitabu hicho yahusu utawala wa nguvu za maovuna kuonyesha kwamba matokeo ya uovu yageuzwa ili yasaidie makusudi memaya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Kwa hiyo maneno „baada ya hayo‟ (k.1)hayana maana kwamba „pepo nne‟ ni baada ya „farasi wanne‟, ni mambo mamoja.

k.2-3 Halafu Yohana alimwona malaika mwingine akipanda kutoka mawio ya jua(mahali pa baraka) na malaika huyo alikuwa na muhuri ya Mungu aliye hai nayeakawaagiza wale malaika wanne kwa sauti kuu na kuwaambia wasifanye lolotempaka watumishi wa Mungu wametiwa mihuri katika vipaji vya nyuso zao. Kwahiyo watumishi wa Mungu watiwa muhuri hata kabla ya hukumu za walewapanda farasi na zile pepo nne. Muhuri ni alama ya kuwa mali ya Mungu naishara ya kulindwa naye. Wamenunuliwa na damu ya Kristo ili wawe milki yake.Kanisa halitaangamizwa, milango ya kuzimu haitalishinda (Eze.9:l- 4; Mt.l6:18;Efe.4.30; 2 Tim. 2:19). Haina maana kwamba watu wa Mungu hawatapatwa nashida, la, watazipata, ila hakika watapitia katika dhiki zao na kufika salamasalimini kwao mbinguni.Muhuri unathibitisha ukweli wa kiti, na ukweli wa Uana wao unahakikishwa naRoho aliye ndani yao (Rum.8:15), ni alama ya kuthaminiwa sana, watalindwakiimani na kiroho, iwapo baadhi yao watateswa hata kuuawa kimwili.

k.4-8 Ndipo Yohana alisikia hesabu yao walioitiwa muhuri katika kila kabila yaWaisraeli, na hesabu hiyo ilikuwa mia na arobaini na nne elfu. Ni hesabu au

Page 64: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1434

takwimu ya „ishara‟. Ijapokuwa inaonekana hesabu hiyo ilihusu watu wa Munguwa Agano la Kale, kwa kuwa Yohana aliendelea kwa kutaja kila kabila, hatahivyo yafikiriwa kuwa ni hesabu ya Kanisa Zima, maana Kanisa limerithi ahadizote zilizotolewa katika Agano la Kale (2:9; 3:9; Rum.2:29; Gal.3:29; 6:16). Nivigumu kufikiri ni Israeli ya zamani, maana kabila ya Dani iliachwa, na mmoja wawana wa Yusufu aliingizwa na mmoja hakuingizwa na orodha ni tofauti na orodhanyingine zote. Tena ni ajabu kila kabila ina watu kumi na mbili elfu na tunajuakwamba kabila nyingine zilikuwa na watu wengi na nyingine watu wachache.Kwa hiyo si hesabu ya kawaida, ila ya ishara, ya utimilifu wa idadi ya watu waMungu wa vizazi vyote, Mungu anawajua kwa jumla pia anamfahamu kila mmojarnmoja, naye atamtunza kila rnmoja na kumfikisha Kwake (2 Tim.2:19). Idaditimilifu isiyo na mpaka.

k.9-10 Katika k.4 Yohana alisikia hesabu ya waliotiwa muhuri, ila alipotazamaaliona (kwa unga‟vu) umati mkubwa sana wa watu, umati usiohesabika kwawingi wake. Tena ni watu wa aina zote waliotoka pande zote za dunia.Inaonekana hao ni walewale 144,000 wa k.4. Kwa wanadamu hawahesabiki, ilakwa Mungu kila mmoja amefahamika.

Wako wapi? Wamesimama mbele ya Kiti cha Enzi na mbele za Mwana- Kondoo(Baba na Mwana yu pamoja) hali wamevikwa mavazi meupe (wamehesabiwahaki kwa imani) wana matawi ya mitende mikononi mwao (ishara ya ushindiwalioupata, kwa kuwa walipita salama katika vita ya kuupima uaminifu wao kwaKristo) nao wamsifu Mungu sana na kukiri ya kuwa wokovu wao umetoka kwamapenzi ya Mungu na kwa kujitoa kwa Mwana-Kondoo (Mungu na MwanaKondoo watajwa pamoja tena).

k.11-12 Halafu Yohana aliwaona malaika wote na wale wenye uhai wanne nawale wazee ishirini na wanne nao wote walikuwa karibu kabisa na Kile kiti chaEnzi nao wakaanguka kifudifudi na kumsujudu Mungu na kusema Amina. Aminalilikuwa itikio lao kwa hayo yote, kwa kutiwa muhuri watumishi wa Mungu na kwaumati mkubwa wa watu walio mbele ya Kiti cha Enzi, wakitoa sifa zao nyingi kwaMungu wao. Twaona itikio la watu na itikio la malaika na la enzi za juu nikumwabudu Mungu na kutangaza sifa zake kuu. Kwa mara ya pili walisemaAmina, kama thibitisho lao kwa sifa zote zilizotolewa, ni kusema Ndiyo, Ni kweli,thibitisho la sifa zote zilizotolewa. Zile sifa saba zilifanana na zile za 5:12 ilatofauti moja ilikuwa shukrani kuwekwa badala ya utajiri.

k.13 Ndipo mmoja wa wale wazee akamwuliza Yohana kuhusu wale waliovikwamavazi meupe kwamba hao wametoka wapi? Bila shaka shabaha yake ilikuwakuuvuta usikivu wa Yohana ili afikiri sana juu ya huo umati wa watu. Wamewezajekusimama mbele za Kiti cha Enzi, penye heshima kuu, karibu na Mungu. Yohanaakajibu kwa kukiri ya kwamba yule aliyemwuliza alijua jibu si yeye. Kisha Yohanaakapewa sababu mbili za huo umati wa watu

Page 65: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1435

kuwa mbele ya Kiti cha Enzi. Sababu moja ni kwamba wanapita katika „dhiki ileiliyo kuu‟ na pili „wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo‟. Tazamaneno „wanapita, si kana kwamba hao wote wamernaliza safari yao, baadhiwangali hapa duniani na baadhi wataishi na kuwafuata baadaye. Hao wotewanashindana na maovu, wanasimama imara wakati wa imani yao kupingwa, nawanapoitwa kumkiri Kaisari kuwa Bwana wathubutu kumtetea Kristo si Kaisari.Hao wote wako salama katikati ya shida zao hali wakimtegemea Mungu kwamsaada, maana Mungu amewatia muhuri. Tukumbuke shabaha ya Yohana nikuwatia moyo Wakristo katika makanisa saba waliokabiliwa na mateso makali.Faida ya Kitabu ni kwa wote wanaoplta katika dhiki kwa ajili ya imani yao. Katikakila kizazi wako Wakristo wanaojaribiwa, sana juu ya uaminifu wao kwa Kristo.

„wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe...‟ sababu ya pili ya hao watu kuwambele ya Kiti cha Enzi yahusu itikio lao kwa wito wa Injili. Hao wamemjiaMwokozi wao Yesu Kristo na kumpokea na kumruhusu awaoshe dhambi zao.Kifo cha Kristo kimetosha kabisa. (Ajabu ni kwamba mavazi meupe yametokanana damu nyekundu ya Kristo - mwujiza kwelikweli (Isa.l:18). Wamehesabukwamba dhabihu aliyoitoa Msalabani kwa ajili ya dhambi zao imetosha kabisakuzifidia dhambi zao na kuwapatia msamaha? na uzima. Kwa hiyo hao watu niwenye dhambi waliookolewa kwa neema, na kwa shukrani wamempa Yeye utiifuwao, nao wamtegemee kabisa na kumtumikia kwa weupe wa moyo. Wakosalama katikati ya shida. „dhiki ile kuu‟ ni maneno ya kujumlisha magumu yote,si jambo au tukio fulani hasa. Maana ni umati mkubwa wa watu ambaowametoka katika dhiki hiyo pamoja na kusafishwa na damu ya Kristo, kwa hiyosi baadhi ya waumini, ni waumini wote wa kweli.

k.15-17 Kiti cha Enzi ni mahali pa utumishi udumuo mchana na usiku, pia nimahali pa utunzaji mzuri. Kwake watapata raha wala hawatasikia hamu yoyoteisiyoridhishwa. Watachungwa na Mwana-Kondoo Mwenyewe, kumbe Mwana-Kondoo ni Mchungaji pia (Yn.lO:ll ku) naye atawapatia „shibe‟ ya maisha nakushirikiana nao kwa ukaribu kabisa. Mambo yote ya nyuma yatasawazishwa,„machozi yao yote yatafutwa‟. Bila shaka maneno hayo yalisikika kama muzikimasikioni mwa Wakristo wa makanisa saba

8:1-5 Muhuri Wa Saba: Uhusiano kati ya. maombi kwenda juu kwa Munguna hukumu kushuka kutoka kwa Mungu

Muhuri ya sita mnatuleta kwenye ukingo wa „mambo ya mwisho‟ na kwa rnuhuriwa saba. Muhuri ya sita ilifunua habari za Sikukuu ya mwisho ya hukumu kali yaMungu (6:12-17). Ndipo katika sura ya saba tulipewa habari ya watumishi waMungu kutiwa muhuri hata kabla ya muhuri kufunguliwa. Hivyo tungetazamiakwamba tutamwona Mwana Kondoo akishikilia utawala baada ya ushindi mkuu.Lakini sivyo. Ajabu ni kwamba Baada ya sifa na nyimbo na muziki ya (7:10ku)twasoma habari ya ukimya wa nusu saa mbinguni.

Page 66: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1436

Inaonekana tumerudishwa nyuma tena na baragumu zahusu wakati uleule wamuhuri, mambo yakitazamwa kwa upande mwingine na katika mwanga wamambo yasiyotajwa hapo nyuma. Hasa twapata habari za hukumuzitakazowapata waasi wanaokataa kutubu.

k.1 Muhuri ya saba ilipofunguliwa, kukawa kimya,mbinguni kama muda wanusu saa (Hab.2:20; Zek.2:13) . Kwanini kuwepo kimya mbinguni? maana vakenini? Huenda ina maana kwamba mambo ya muhuri ya saba hayajafunuliwabado. Au pengine, lazima iwepo nafasi na ukimya baada yasauti za sifa iliMaombi yasikike. Au pengine ni mshangao wa kuona hukumu za Munguzitakazotokea baragumu saba zitakapopigwa.

k.2 Mungu anasikia kilio na maombi ya watu wake kama ambavyo tulionakatika 6:9ku.Ndipo Yohana aliwaona wale malaika saba wasimamao rnbele za Mungu, naowakapewa baragumu saba. (Katika Kitabu cha kwanza cha Enoki 20:2-8majina ya malaika wa „Kuwako kwa Mungu‟ yametajwa kuwa: Urieli, Rafaeli,Ragueli, Mikaeli, Sarieli, Gabrieli, na Remieli). Wameonekana kama kundi rasmi.Wakati wa vitasa malaika saba wametajwa, kama ni walewale au kundi linginehatujui (15:1,6; 16:1; 17:1; 21:9).

k.3 Halafu malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenyechetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi yawatakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya Kiti cha Enzi.Moshi wa ule uvumba ukapanda kwa Mungu pamoja na maombi ya watakatifu,kutoka mkononi mwa malaika. Huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijazamoto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme natetemeko la nchi. Maana yake nini hayo yote? Tunaona maombi ya watu waMungu yanaletwa mbele za Mungu hali yakichanganywa na uvumba mwingi.Uvumba ni dalili ya nini? Pengine ni maombi ya Kristo. Pengine ni kuonyeshamwungano wa ibada ya duniani na ibada ya mbinguni. Chetezo cha dhahabu namadhabahu ya dhahahu ni ishara ya uthamani, umuhimu, na nguvu yamaombi, maombi yafaa sana. Itikio la Mungu kwa maombi ya watu wake nikumwaga hukumu zake. Katika 6:10 tuliona watakatifu walimlilia Munguawapatie haki kwa kuwaadhibu watesi wao. Chetezo kilekile kilichopelekamaombi juu kwa Mungu kilijazwa moto wa madhabahu nao ulitupwa juu ya nchina hukumu za Mungu zilitokea. Kwa hiyo upo uhusiano mkubwa kati yamaombi ya watu na hukumu za Mungu. Watu wa Mungu wanayo silaha kalisana ya kuwasaidia katika mashindano yao na maovu, maombi yao yamvutaMungu atende kazi za hukumu. Pia madhabahu ni ishara ya hali ya kidhabihuya maombi ya kweli. Kuomba si kazi rahisi, inahitaji mtu ajitoe na kukazana nakudumu katika kuomba. Watu wa Mungu wanao uwezo, uwezo wa maombi.Iwapo wanateswa isivyo halali siyo kusema wayapokee mateso yao bila kujali,budi wamlilie Mungu awapatie haki.

Page 67: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1437

Tusiwaze kwamba malaika nl wapatanishi kati yetu na Mungu, waitwa wajoliwenzetu (19:10; 22:9).

Tukiuliza „uwezo na nguvu za kweli zina nani?‟ Je! zina Kaisari? Je! zina enzi zaulimwengu huu? Je! zina „enzi za uovu?‟. Jibu ni: Nguvu na uwezo zina maombiya watu wa Mungu, maombi yao yaungana na „moto‟ wa Mungu.

Mihuri saba yafuatwa na baragumu saba, ila tusiziweka katika mfuatano wawakati wa mambo kutokea, kwa sababu tutaona ya kuwa mengi ya baragumuyafanana na mambo ya mihuri.

8:6 - 11:19 BARAGUMU SABA ZA MAONYO YA HUKUMU

8:6 Tulipotazama habari ya muhuri ya saba tuliambiwa juu ya malaika sabawasimamao mbele za Mungu nao wakapewa baragumu saba ndipo wakajifanyatayari kuzipiga tarumbeta zao (k.6).

Muhuri nne za kwanza zilifanana na ndivyo ilivyo kwa baragumu nne za kwanza.

Baragumu zimetajwa mara kwa mara katika Agano la Kale. Zilitumika wakatimbalimbali. Kwa kutangaza „ushindi‟ kama ule uliotokea wakati wa kuta zaYeriko kuanguka baada ya watu kuuzunguka mji na kupiga baragumu. Kwawakati wa „Kutawazwa Mfalme‟ (1 Waf.1:34,39; 2 Waf.11:13). Zilihusika na ibadaza Kiyahudi kwa kukiri kwamba Mungu ni Mfalme wao (Zab.47:5; 98:6) ling. na11:15. Zilitumika wakati wa kuliita Taifa litubu ili Mungu asilete hukumu (Yer.4:5;6:18; Ufu.9:20). Katika Sikukuu za shangwe na Siku ya mwezi kuandama naWakati wa kutoa dhabibu (Hes.10:10). Ilikuwepo Sikukuu ya ukumbusho wakupiga baragumu katika Sikukuu ya Mwaka Mpya iliyofanyika siku 10 kabla yaSikukuu ya Upatanisho (Law. 23:24).

Baragumu zatoa maonyo. Muhuri zilitoa habari juu ya misiba inayofuata dhambiza wanadamu hasa dhambi ya kuwapinga watu wa Mungu. Baragumu zatoahabari juu ya misiba itakayowapata watu wa dunia wanaokazana kutokumjaliMungu wala kutubu. Katika kuwahukumu Mungu atumia vitu vya asili, nchi namimea; bahari; mito na chemchemi; jua, mwezi na nyota. Hivyo wanadamuwaguswa katika maisha ya kimwili kwa njia ya vile vitu vya asili wanavyotegemeabila kumjali Yeye aliyeviumba na kuwaruhusu kuvitumia. Mapigo hayo niukumbusho wa mapigo yaliyopata nchi ya Misri wakati wa Farao na Musa, Faraoalipokataa kuwaruhusu Waisraeli kurudi makwao. Badala ya kutubu Faraoaliufanya moyo wake kuwa mgumu (Kut.9:20-21). Twaona kwamba maovu yawanadamu hayaachiliwi, Mungu huyatia maanani na kuyahukumu. Misiba,maafa, madhara nk. hayatokei kwa bahati nasibu kwa sababu ulimwenguunatawaliwa na Mungu.

Page 68: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1438

8:7 Baragumu ya Kwanza (Ling. Kut.9:23-26; Eze.38:22)Baragumu ilipigwa halafu ikatokea mvua ya mawe na moto vilivyotangamana nadamu vikatupwa juu ya nchi na theluthi ya miti ikateketea na majani mabichi yotepia. Maana yake ni nini? Ni ishara ya maafa yanayotokea mara kwa mara,yanayogusa nchi, miti, na majani. „Theluthi‟ iliguswa, sehemu isiyo kubwa walandogo, wanadamu waliweza kustahimili shida hiyo ila ilitosha kuwafanyawajihoji, waitie maanani, waonywe, ili watubu.8:8-9 Baragumu ya Pili (Ling. Kut.7:20-21)Ilipopigwa baragumu ya pili, kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao motokikatupwa katika bahari ndipo theluthi ya bahari ikawa damu. Theluthi ya viumbehai waliomo baharini wakafa, na theluthi ya merikebu zikaharibiwa. Ni ishara yamaafa yanayotokea mara kwa mara kwa viumbe waishio baharini na kwamerikebu zipitazo juu yake. Kwa sababu bidhaa nyingi husafirishwa na merikebuliko wazo la uchumi kuguswa. Siku hizi tunasikia habari za bahari kuchafuka kwauchafu unaotupwa ovyo kutoka katika viwanda na kwa mafuta kumwagika nakusababisha uharibifu kutokana na ajali za meli kugonga mwamba nk. „kitu,mfano wa mlima mkubwa....‟ maneno hayo yaonyesha kwamba Munguanaruhusu hayo yote yatokee akitumia hasara za namna hii kuwa njia yakuwaonya wanadamu hata kuwaadhibu kwa kiasi, ili watu wajihoji. Theluthiimetajwa; hizo si hukumu za mwisho, bado ingaliko nafasi kwa watu kutubu nakumrudia Mungu.

8:10-11 Baragumu ya Tatu (Ling. Yer.9:15)Ilipopigwa baragumu ya tatu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ilikuwaikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi zamaji. Jina la nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ya nchi ikawa pakanga, nawanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu. Hapotwaona maji ya mito na chemchemi yalitiwa uchungu na wanadamu wengiwakafa kwa sababu hiyo. Kwa maneno ya „nyota kubwa kutoka mbinguni‟Yohana alitaka kukaza asili yake kuwa nje ya wanadamu. Pia „theluthi‟ ya mitonk. iliguswa. Twaona vitu asili kama maji yanayohifadhi maisha ya watuyalitumiwa na Mungu kuwa chombo cha hukumu zake. Yohana hakutaka watuwawaze kwamba mambo hayo hutokea tu kama vitu vilivyo nje ya madaraka yaMungu. Kwa hukumu ya baragumu hiyo wanadamu walipoteza maisha yao.Kama ilivyokuwa katika Mapigo Kumi ya Misri, mapigo yalizidi kwa uzito kadiriFarao alivyozidi kumpinga Mungu na kulikataa ombi lililoletwa na Musa. Katikamapigo ya kwanza wanadamu hawakuguswa.

8:12 Baragumu ya Nne (Ling. Kut.10:21-23)Ilipopigwa baragumu ya nne, jua, mwezi, na nyota ziliguswa ndipo theluthi yamchana haikuwa ya kawaida na vivyo hivyo kwa usiku. Tukumbuke Yohanaanatumia lugha ya taswira hafuati elimu ya falaki. Katika Isaya 13:9ku. nabiialitabiri kwamba giza litatangulia hukumu ya Mungu juu ya waasi. Pia

Page 69: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1439

twakumbuka pigo la 9 juu ya WaMisri kabla ya Waisraeli kupewa ruksa yakuondoka. Mapigo yalikuwa na shabaha ya kuwafanya wanadamu wamkiriMungu na kazi zake (Kut.8:7,18). Yohana alitaka kuelekeza mawazo ya watuwamfikirie Yule aletaye mambo hayo na kuizingatia shabaha yake. Kwa lughaaliyoitumia ni wazi kwamba Yohana hakutaka watu wayatafiti mambo yenyewe.Wanadamu tangu wakati wote wamevutwa na mambo ya buruji na maaguzi kwanyota (taz. magazeti ya siku hizi). Yohana alitaka watu wafahamu kwambaMungu ni mtawala wa mfumo wa jua na sayari zake na viumbe vya asili kamamwezi na nyota. Yeye huvitumia katika kuhukumu wanadamu.

Baragumu hizo ni Maonyo, hasara zaletwa katika mazingara ya kibinadamu,katika vitu asili kama maji na mwanga, na katika uchumi nk. Hasara hizozaonyesha ghadhabu ya Mungu juu ya dhambi, pia zawapatia watu nafasi yatoba. Tukichunguza kwa ndani, ni kazi za REHEMA, wanadamu wanapewanafasi ya toba kabla ya hukumu ya mwisho. Ni fadhili za Mungu, Mungu akifanyajuu chini kuwaamsha wanadamu hata kuwashtusha juu ya hatari iliyo mbele yaowanapoendelea kutokumjali na kumwasi. Fundisho kubwa ni kwamba maovu yawanadamu hayaachiliwi na Mungu, hukumu zake ni matokeo ya dhambi, kwasababu dhambi yenyewe inazalisha shida na uharibifu. „theluthi‟ inatuonyeshakwamba hayo yote yamo katika utawala wa Mungu. Mungu anakabili dhambi nauasi wa wanadamu.

Ni vema tukumbuke ya kwamba Kitabu ni barua iliyoandikwa na mchungajialiyetaka kuwatia nguvu watu wake waliopambana na magumu na shidawalizozipata katika kumfuata Kristo, ambao pia walitazamia kwamba hivi karibuniwatapata mateso makali, haikuwa kama matangazo ya hukumu za kuwaogofyawapagani. Wakristo walitaka kujua Mungu anafanya nini kuhusu hayoyanayowapata? Je! Mungu anashindwa na maovu ya watu? anachukua hatuagani juu yake? Jibu la Kitabu hicho ni kwamba maafa na misiba ya sasa niutangulizi wa wokovu mkuu wa Mungu. Kanisa (Israeli mpya) lafanana na Israeliya zamani, lina „Kutoka Kupya‟ na kama Mapigo yalitangulia Waisraeli kuondokaMisri na kusafiri mpaka Kanaani, nchi ya ahadi, vivyo hivyo, Wakristo wanaKutoka Kupya, lazima washindane na vipingamizi vyote vya wale wanaotakakuwazuia wasifike nchi ya ahadi (11:8; 15:2-3). Kila baragumu lafanana na ombila Musa kwa Farao alipomsihi awaruhusu watu waondoke nchini. Yesu alitajamaafa kuwa mwanzo wa „utungu‟ utungu wa kuzaa Dahari Mpya (Mt.24:8-9;Lk.21:28).

8:13 Ole TatuKabla ya kueleza Baragumu tatu za mwisho Yohana aliona na kusikia taimmoja akiruka katikati ya mbingu akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole waowakaao juu ya nchi! kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaikawatatu walio tayari kupiga. Desturi ya tai ni kuzungukazunguka angani nakurukia mzoga kutoka juu (Lk.17:37). Yohana alitaka kutilia mkazo uzito wa

Page 70: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1440

hukumu ya Mungu inayokuja. Kwa nini uzito unazidi? ni kwa sababu watuhawawi tayari kutubu. Ijapokuwa kazi za Mungu ni dhahiri kwao hawawi tayarikuzikiri kuwa zake.

9:1-12 Baragumu ya Tano ambayo ni Ole wa KwanzaKwa muhuri tatu za mwisho tuliingia katika ulimwengu wa kiroho na vivyo hivyokwa baragumu za mwisho, ila kwa muhuri mambo yalihusu mbinguni lakini kwabaragumu yahusu shimo la kuzimu. Hizo baragumu za mwisho zaitwa „ole‟ kwasababu hukumu zake zagusa sana maisha ya wanadamu kuliko mazingira yake.

Baragumu ilipopigwa Yohana aliona nyota iliyotoka mbinguni imeanguka juu yanchi, naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Nyota ilionekana kuwa yenyenafsi, yawezekana ni malaika aliyeanguka (Isa.14:12; Lk.10:18). Katika 1:20malaika aliitwa nyota. Pengine ni Shetani. Ni mjumbe wa uovu anayefanya kazizake kwa ruhusa ya Mungu. Katika 20:1 tuna malaika mwingine, mjumbe wakufanya kazi njema ya Mungu, yeye alilifunga shimo kwa mapenzi ya Mungu.Mungu huwaruhusu wanadamu na malaika nafasi za kutokumtii, hivyo uovuutajiharibu wenyewe.

k.1b Hiyo nyota, kama ni Shetani au kama ni malaika fulani, alipewa ufunguowa shimo la kuzimu, naye akalifungua. Jambo kubwa ni kuona ya kwambaALIPEWA UFUNGUO, na mle ndani ya shimo la kuzimu kuna mashetani namapepo wabaya. (Lk.8:31 mapepo wabaya walimwomba Yesu asiwapelekeshimoni).

k.2ku (Kuhusu nzige ling. na Kut.10:1-20 na Yoe.1:2:11).Kwa taswira hii Yohana alikuwa akitoa habari za enzi hizo za uovu, akitaja moshiwa tanuru kubwa na jua na anga kutiwa giza, ndipo nzige wakatoka katika huomoshi na kwenda juu ya nchi hali wamepewa nguvu kama ile ya nge. Giza hiloJe! liliashiria nini? pengine ni ishara ya ufahamu na akili za watu kutiwa giza namaovu yanayoenea duniani hata wasiweze kuutambua vizuri. Hasa watuwanapohubiriwa Injili na kuitika vibaya kwa kumkataa Kristo aliye Nuru ndipowanapofushwa macho yao ya kiroho (Yn.3:19ku. 2 Kor.4:4). Pia ni dalili yamaovu kuenea kote.

k.4ku „Nzige‟ (ambao kawaida yao ni kula majani) waliambiwa wazi kwambawasiyadhuru majani, wala miti, ila watu, wale wote wasio na muhuri ya Mungukatika vipaji vyao. Tena walipewa mipaka ya kiasi cha kuwadhuru,hawakuruhusiwa kuwaua bali kuwatesa kwa miezi mitano. Maumivu yaoyalifanana na kuumwa na nge, maumivu makali hata watu walitamani kufa ilawalinyimwa kufa maana tumeambiwa mauti itawakimbia. Maana yake nini? Inamaana kwamba enzi za uovu zinaruhusiwa na Mungu kufanya kazi zao mbaya,ila zenyewe hazina uwezo au nafasi kufanya zaidi ya mipaka iliyowekwa na

Page 71: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1441

Mungu. Mipaka ilihusu muda, uzito, kiasi, na wa akina nani kushambuliwa.Hawakuweza kuwadhuru wenye muhuri ya Mungu, maana yake hawakuwezakuyagusa maisha yao ya kiroho na kuuharibu uhusiano wao na Mungu.Tukumbuke ni mambo ya kiroho yanayozungumzwa si mambo ya kimwili.Twakumbushwa jinsi ambavyo Waisraeli hawakuguswa na mapigo yaliyoletwajuu ya WaMisri. Uovu hausimami peke yake wala hauna mamlaka yakeyenyewe. Shetani si „mungu wa pili‟ ijapokuwa alitaka kuwa hivyo, nayealiwaambukiza wanadamu tabia iyohiyo ya kutamani kuwa kama Mungu(Mwa.3:5). Ni Shetani anayechochea nia kaidi za watu Kumpinga Mungu nakumkataa Kristo. Nzige walionekana kuwa na afya na nguvu, ishara ya „afya‟ na„nguvu‟ ya maovu.

k.7-11 Hao nzige walifanya kazi kwa utaratibu wakiongozwa na kiongoziambaye tumepewa jina lake la Kiebrania kuwa Abadoni na kwa KiyunaniApolioni, yaani Mharibu. Huyo ametajwa kuwa mfalme na malaika wa kuzimu.Yohana amewaeleza hao nzige kwa taswira ya ajabu. Vema tukumbuke nitaswira, tazama jinsi alivyorudia kusema „kama‟ „kama‟. Maumbo yao yalikuwakama farasi walio tayari kwa vita, na vichwani walivaa taji kama ya dhahabu, nanyuso zao zilifanana na nyuso za wanadamu. Nywele zilikuwa kama zawanawake. Meno yao yalikuwa kama ya simba, makali sana. Vifuani walivaa diriiza chuma. Sauti ya mabawa ilikuwa kama sauti ya magari ya farasi wengiwaendao kasi vitani. Mikia yao ilifanana na ya nge na miiba; na nguvu yakuwadhuru wanadamu ilikuwa katika mikia. Maana yake nini hayo yote?Tukijumlisha twapata picha ya uharibifu, chuki, mamlaka, akili, utongozi, uvutiko,nguvu, ukali, nk. zinazotumiwa na roho mbaya, kiongozi wa upinzani juu yaMungu na Kristo, upinzani unaosababisha hukumu za Mungu zinazowaumizawanadamu.

Dhambi na Shetani huharibu maisha ya wanadamu na kuyafanya yasiwe yamaana wala thamani. Watu wanapoisikia Injili na kuikataa, wasimkubali Kristoawe kiongozi wa maisha yao, wanajiweka mbali na Mungu na kuwa kinyumechake, na Shetani huwateka na kuwanasa katika dhambi zao. Tuukumbukemfano aliosema Bwana Yesu katika Mathayo 12:43-45. Hata hivyo, Munguangali ni Mtawala na Mwenye madaraka, akiyatekeleza mapenzi yake kwakumpatia kila mmoja matunda ya uchaguzi wake. Mungu huyatumia maovu kuwaadhabu na kwa njia ya adhabu awaita watu watubu. Shabaha njema ya Munguni kuwashtusha ili wachunguze maisha yao. Ni Yeye tu aliye na uwezo wakuziongoza nia kaidi za wanadamu. Mungu hadhihakiwi, mtu huvuna kulinganana kupanda kwake na katika muda huo wote wa kuishi ipo nafasi ya toba.

k.12 Ole wa kwanza umeishapita, na zimebaki ole mbili, baragumu ya sita nasaba. Kwa kutumia neno ole badala ya baragumu mkazo ni juu ya uzito wahukumu hizo.

Page 72: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1442

9:13-21 Baragumu ya Sita ambayo ni Ole wa PiliOnyo hilo ni la mwisho kwa watu kupewa nafasi ya toba kwa kuwa onyo la tatuhalitatoa nafasi hiyo maana mambo ya mwisho yatakuwa yamefika itakapoliabaragumu ya saba. Baragumu ya sita ilipopigwa Yohana alisikia sauti mojailiyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,mahali pa ibada na maombi. Neno „ole‟ linaonyesha uzito uzidio wa hukumu zaMungu. Maana yake nini sauti iliyotoka katika zile pembe za madhabahu?Inaonekana hukumu hiyo ni itikio la Mungu kwa maombi ya watakatifu waketukikumbuka kwamba chetezo kilichopeleka maombi kwa Mungu kilijazwa motowa madhabahu (hukumu) ndipo ukatupwa duniani (6:9-10; 8:3-5).

k.13-15 Ndipo Yohana akataja habari za malaika wanne waliofungwa kwenyemto mkubwa Frati, na malaika wa sita aliyekuwa na baragumu aliambiwa na ilesauti awafungue hao malaika wanne waliofungwa. Kazi yao ilikuwa kuua theluthiya wanadamu, ila hatusomi kwamba ni hao waliowaua. Hao malaika waonekanakuwa malaika wabaya ambao wamezuiliwa wasifanye lolote mpaka wakatiulioamriwa na Mungu, ndipo Mungu akawaruhusu. Katika k.15 twasoma kwambahao walikuwa wamewekwa tayari kwa wakati rasmi hata saa pamoja na siku namwezi na mwaka vimepangwa. Walifunguliwa kwa saa rasmi. Maneno hayoyaonyesha madaraka ya Mungu juu ya mambo yote.

k.16ku Zamani zile watu waliogopa sana wenyeji walioishi mashariki yao upandewa Mto Frati. Waparthi wa sehemu zile walikuwa mabingwa wa vita ya wapandafarasi, waliweza kupiga mishale mbele hata nyuma yao, nao walikuwawamewashinda Warumi mara mbili katika vita. Tena watu walisikia hofu juu ya„mashariki‟ maana hawakujua kuna nini huko. Katika historia yao Waisraeliwalishambuliwa na Wababeli na Waashuru ambao Mungu aliwatumia kufanyamapenzi yake ya kuwaadhibu watu wake (Isa.7:20; 8:7). Twasoma kwamba watuwalikufa kwa moto, moshi, na kiberiti vilivyotoka kwa majeshi hayo (19:20; 20:14;21:8) vitu hivi vinaashiria ukali wa hukumu hiyo. Yohana ametaja milioni mia mbilikuwa hesabu ya wapanda farasi, hesabu isiyohesabika, ishara ya enzi za uovuzilizoko wakati wote tayari kumsaidia Shetani katika vita ya kumpinga Kristo. Haowapanda farasi walikuwa wakali na hali ya kuonekana kwao ni ishara yaghadhabu ya Shetani kuzidi na jeshi lake lote kufanya juu chini kuwashambuliawanadamu hasa watu wa Mungu. Huenda siyo vita ya kimwili bali ya kiroho, na„mashariki‟ huenda si mashariki hasa, ila Yohana ametumia hali ya hewa yawakati ule kwa kueleza uhalisi wa kiroho na vifo vinavyotokea kwa sababu yachuki ya Shetani. Ni vifo vya wanadamu wanaokufa kabla ya wakati wao kwa njiazisizo halali. Dalili ya uzito yaonekana katika kulinganisha baragumu ya tano naile ya sita. Katika baragumu ya tano watu hawakuweza kufa, walinyimwa kufa,waliumizwa tu, ila katika baragumu ya sita watu walikufa.

Page 73: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1443

Je! Mungu alikuwa na kusudi gani? Nyuma ya hukumu hizo ni upendo wa Mungu.Atafuta njia ya kuwashtusha wanadamu na kuwaonya wasifuate njia iendayoJehanamu akiwaonjesha taabu zake, angalau kwa kidogo tu. Shabaha ilikuwakuwafanya theluthi mbili zilizosalia waje kwenye toba, wakubali kuacha miunguya uongo, imani na ibada za uongo, na maisha yao mabovu. Ujinga wa sanamuwanazoziabudu unaonekana katika maneno „zisizoweza kuona, wala kusikia,wala kuenenda‟. Lakini watu hawakutaka kutubu, hawatatubu potelea mbaliwapatwe na shida gani. Shetani haachi kushikilia nia yake ya kumpingaMungu na kukazana katika kuwashika na kuwadanganya na kuwapotoshawatu. Uasi una hali ya kujiangamiza na ni Mungu peke yake aliye na uwezo wakuwaponya wanadamu. Yeye hutamani sana sana kuwaokoa wanadamu nakuwarudisha kwenye uheri wao. Kumkataa ni kuukataa ule uwezo ambao pekeyake unaweza kuwabadili ili waache dhambi zao. Wanadamu waliumbwa iliwamwabudu Muumba wao na wasipofanya hivi kwa vyovyote watajitengenezeamiungu yao (Rum.1:22-25) ndipo hutokea imani na dini za uongo, maishamabovu, udhalimu katika jamii, na ukosefu wa haki katika siasa na taasisi zawatu. Dhambi ni tokeo la kujipatia miungu badala ya Mungu. Halafu swali lazuka;Watu wa Mungu wafanye nini? Kama jibu la Mungu kwa maombi yao nikumruhusu Shetani alete uharibifu juu ya uharibifu, wafanye nini zaidi? Wakristowapaswa waendelee kuwa waaminifu kwa Kristo haidhuru wateswe hata kuuawakwa ajili ya ushuhuda wao. Tukumbuke kwamba Kitabu kiliandikwa kwa ajili yaWakristo katika Makanisa Saba na Yohana alitaka wafahamu kwamba hawanabudi kuishi katika ulimwengu huu wa uasi, daima watazungukwa na umati wawatu wanaompinga Mungu kwa njia mbalimbali. Katika sura ifuatayo Yohanaanatoa jibu lingine.

Katika ole hiyo twathibitisha ya kuwa Mungu alikuwa juu ya hayo yote, malaikawanne walifungwa ndipo wakafunguliwa kwa saa maalumu, kabla ya hapowalizuiliwa. Hata kiasi cha watu watakaoguswa kiliwekwa na Mungu. Shabahaya Mungu ilikuwa njema. Kwa vyovyote alitaka watu watubu ili waujue wokovuwake ila twadokezewa kwamba hawatatubu (2 Pet.3:9).

MASWALI1. Kwa jumla, baragumu zinatofautiana na muhuri kwa njia zipi?2. Baragumu nne za kwanza zinaeleza nini hasa?3. Kwa nini baragumu tatu za mwisho zimeitwa Ole? ni ishara ya nini?4. Baragumu ya sita haikuonekana kutoa nafasi ya nini tofauti na

baragumu zilizotangulia?5. Maneno yafuatayo ni ishara ya kuonyesha nini? (Usieleze kila jambo

kwa kirefu, ila jumlisha yote)„sauti moja iliyotoka katika zile pembe ya madhabahu..... ....wafunguehao malaika .............‟„wamewekwa tayari kwa ..........‟„ili kwamba waue theluthi ya .......‟

Page 74: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1444

10: 1-11 Malaika mwenye nguvu na Kitabu kidogoHatupati habari ya baragumu ya saba ambayo ni ole wa tatu mpaka 11:15, kwahiyo, mambo yanayotajwa hapa ama ni mambo yahusuyo baragumu ya sita auni kipengele kati ya baragumu ya sita na ya saba. Katika habari za muhuri tulionakipengele kati ya muhuri ya 6 na ya 7. Kipengele kilihusu watu wa Mungu natulipewa habari ya watu mia na arobaini na nne elfu kutiwa muhuri na maono yaumati mkubwa wa watu waliokombolewa wakionekana mbinguni. Hapo tenainaonekana mambo yahusu watu wa Mungu, yaani Kanisa na wajibu wake katikamuda wote wa baragumu kulia. Liko wazo la kuwa Mungu amesimama katikakuleta hukumu (Mk.13:20) ili mzunguko wa dhambi na hukumu, dhambi nahukumu, .....uvunjwe.

k.1ku Yohana aliona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutokambinguni. Iwapo Yohana ametaja malaika mara nyingi ametaja malaika mwenyenguvu mara tatu tu. Hapo nyuma alipohitajika mtu kuvunja muhuri saba za Kitabuchenye Muhuri (5:1ku) ni malaika wa nguvu aliyetoa mwito „ni nani astahiliye....‟(5:2). Huenda Yohana alitaka tuone uhusiano wa Kitabu kile na kitabu hichokidogo. Wengine wamemwaza huyo malaika kuwa Kristo kwa jinsi alivyoelezwaila ni vigumu kukubali kwamba Yohana angalimweleza Kristo kama ni malaika,wala hatuoni malaika kuabudiwa au kupewa heshima zimhusuzo Mungu na Yesutu. Yohana alitaka kutilia mkazo juu ya huyo malaika kuwa mjumbe aliyetoka nakutumwa na Mungu akiuleta ujumbe wa Mungu, na kwa sababu hiyo, anayosemayana mamlaka ya Mungu.

Tumeambiwa nini juu ya malaika? alishuka kutoka mbinguni; amevikwa wingu;upinde wa mvua (ishara ya agano la Mungu na uaminifu wake) ulikuwa juu yakichwa chake; uso wake ulikuwa kama jua; miguu yake kama nguzo za moto(ishara za utukufu wa Mungu). Mkononi alikuwa na kitabu kidogo ambachokimefunguliwa. Mguu wa kuume ulikuwa juu ya bahari na mguu wa kushotoulikuwa juu ya nchi. Akalia kwa sauti kuu kama simba angurumavyo. Alipolia, zilengurumo saba zilitoa sauti zao, ndipo Yohana alisema kwamba zilipotoa sautizao yeye alikuwa tayari kuandika. Halafu akaisikia sauti kutoka mbinguniikisema, Yatie muhuri maneno yaliyonenwa na ngurumo saba, usiyaandike.Taswira ni ya malaika aliyetoka kwa Mungu mwenye mamlaka yake. Kitabu„kimefunguliwa‟ ni ishara ya mambo yaliyo tayari kufunuliwa. Miguu kuwa juu yanchi na bahari inaashiria ujumbe wake unaowahusu wanadamu wote (k.11).Iwapo Yohana hakuruhusiwa kuandika mambo aliyoyasikia yaliyonenwa nangurumo saba inaonekana aliyafahamu yaliyonenwa. Tungependa kujua mambohayo ila ni kazi bure kuyahisi maana hatuwezi kujua kwa uhakika. (wazo moja nikwamba Mungu aliamua kufikisha mwisho wa mambo yote ili wanadamuwasiendelee katika dhambi zao zilizosababisha wazidi kupata shida, shidaambazo Mungu alizitumia kama chombo chake cha hukumu (Mk.13:20).

Page 75: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1445

k.5ku Halafu huyo malaika akauinua mkono wake wa kuume kuelekea mbingunina kuapa kwa Yeye aliye hai milele na milele, Muumba wa mbingu na nchi nabahari na vyote vilivyomo.Kwa sababu Mungu ni wa milele hakika atayatimiza mapenzi yake na kwasababu ni Muumba wa vitu vyote atayatimiza makusudi yake ya tangu mwanzoya kuwapatia mema watu wake mwishoni na Yeye atukuzwe na viumbe vyakevyote (4:11; Rum.8:28).

Malaika aliapa nini? Aliapa kwamba „hakuna kukawia isipokuwa katika siku zabaragumu ya saba‟. Neno la Kiyunani lina maana ya kukawia, si vizuri kulitafsiri„hakuna wakati tena‟. Katika kalenda ya Mungu bado liko tukio moja ambalo nila mwisho. Hilo ni mambo ya baragumu ya saba, baragumu hiyo itakapolia ndipomwisho utakuwa umefika. Mungu amekwisha kutoa nafasi za kutosha kwawanadamu kutubu, kwa hiyo hakuna maana wala sababu ya kuendelea katikamzunguko wa dhambi na hukumu. Si kana kwamba kwa ghafula Munguamesikia kuchoka, la, Yeye hajachoka kutoa nafasi kwa watu kutubu ila watuwamezikinai nafasi hizo, wao wamechoka, hawataki kutubu. Kukawiakumekuwepo, kwa sababu, katika 6:10 tulipewa habari za mashahidi waliolia„mpaka lini‟ na Mungu aliwatuliza na kuwaambia wastarehe muda mfupi (2Pet.3:9). Katika utawala wa Mungu juu ya uumbaji Yeye ayaongoza mambo yotempaka mwisho ili watu wake wapatiwe mema na mapenzi yake ya tangumwanzo yatimizwe (Rum.8:28). Ila katika muda huo wote Kanisa linawajibikakuitangaza Injili.

k.7 „siri ya Mungu‟ ni nini? Ni Injili ambayo ni chombo chake cha kuyatimizamakusudi yake ya milele. Kwa Injili wenye kuiamini wapata wokovu kamili naowatazishiriki baraka za uzima wa milele. Wale wenye kuikataa Injili wanaishi sasachini ya hukumu ya Mungu (Yn.3:36) nao wataishiriki hukumu kali ya mwisho juuya waasi wote. Yohana alikiita Kitabu chake unabii (1:3) mambo hayo manabiiwaliyafahamu (Amo.3:7).

k.8ku Hapo mambo yanafanana na yale yaliyompata Ezekieli. Yohana naEzekieli, wote wawili walikuwa manabii, wote walikuwa katika nchi ya kigeni, nawote wawili waliambiwa wakile kitabu ambacho kitakuwa kitamu mdomoni nakusababisha wausikie uchungu (Eze.3:1-3;14). Ezekieli aliwaletea watu ujumbekuhusu mwenendo wao. Mwenye haki akiacha kufanya haki na kutenda maovuatapatwa na mauti; ila mwenye haki akiujali ujumbe wa nabii na kufanya memabasi huyo ataishi (Eze.3:20-21). Ndipo Yohana aliambiwa amwendee malaikaakitwae kile kitabu kilichofunguliwa (inaonekana kimeendelea kufunguliwa). Kwamara ya tatu twaambiwa huyo malaika alikuwa na mguu mmoja juu ya nchi nammoja juu ya bahari, ishara ya ujumbe wa kitabu kuwa kwa ajili ya wanadamupopote walipo. Yohana akakitwaa kile kitabu, kisha malaika akamwambia akile,akimwonya kwamba kiwapo kinywani kitakuwa kitamu lakini tumboni atausikiauchungu. Ilitokea kama alivyoambiwa kisha aliambiwa

Page 76: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1446

itampasa atoe unabii tena juu ya watu, taifa, lugha na wafalme wengi, ujumbe nikwa watu wote. Yana maana gani mambo hayo? Kukila ni ishara ya Yohanakukolewa kabisa nafsini mwake na ujumbe wa kitabu, ujumbe ambao iwapo kwasehemu utamfurahisha, ni „mtamu‟, ila kwa ndani utamtia huzuni, atausikiauchungu. Injili ni habari njema, ila inaondoa visingizio vyote kwa wale wotewasioipokea. Si rahisi kuwaonya watu juu ya hukumu kali za Mungu, ila ni furahakubwa kuwatangazia wokovu wa msamaha wa dhambi na kipawa cha uzima wamilele. Hii ndiyo kazi ya Kanisa (Rum.11:22: 2 Kor.2:15-16)

Wazo juu ya kitabu kidogo mkononi mwa malaika mwenye nguvu. Kanisalaonekana kuwa kitu hafifu katika ulimwengu huu, waumini wengi hawana nguvuwala uwezo wala elimu za hali ya juu. Hata hivyo kile kitabu kidogo katika mkonowa malaika mwenye nguvu ni ishara ya Nguvu ya Neno la Mungu. Neno hilo nila maana sana, latawala mambo yote, yaliyomo ni muhimu kwa kilamwanadamu, yahusu kuishi au kuangamizwa milele. Injili itahubiriwa kotekotendipo ule mwisho utakuja (Mk.13:10).

MASWALI1. Kile kitabu kidogo ni nini?2. Maneno yafuatayo yana maana gani?

(a) „mguu mmoja juu ya nchi na mmoja juu ya bahari‟(b) „kitakutia uchungu tumboni mwako bali katika kinywa chako

kitakuwa kitamu kama asali‟

11:1-14 Mashahidi WawiliMambo ya sura hii yasema juu ya wajibu wa Kanisa uliodokezwa katika sura yakumi, wajibu wa kumshuhudia Kristo na kutangaza Injili yake. Twaonyeshwanguvu ya Neno la Mungu pamoja na nguvu ya upinzani wa ulimwengu.

k.1-2 Mara nyingi Yohana alikuwa mtazamaji wa mambo ila hapo ameingizwakatika mambo na kuwa mtendaji. Alipewa mwanzi kama fimbo na kuambiwaalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. Piaalikatazwa asilipime behewa la nje ya hekalu, kwa kuwa Mataifa wamepewa hilo,nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.

Tukumbuke ni taswira na takwimu si hesabu ya kawaida bali ni „ishara‟.

Hekalu lenyewe lilipimwa, ishara ya kuonyesha kwamba lililindwa kipekee nawasujuduo humo walihifadhiwa wasipatwe na madhara ya kiroho, iwapo kimwiliwatateswa. Wakati wa Agano la Kale ni makuhani tu walioruhusiwa kuingia mlendani ya hekalu ila sasa, kutokana na ukombozi wa Kristo, kila muumini ni kuhani(1:6) naye aweza kumkaribia Mungu wakati wowote bila kizuizi. Kanisa ni HekaluJipya la Mungu (1 Kor.3:16; Efe.2:19-22). Habari hii inafanana na ile ya wale miana arobaini na nne elfu waliohesabiwa na kutiwa muhuri (7:3ku).

Page 77: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1447

Neno „hekalu‟ linatuongoza kuwaza watu wa Mungu katika hali ya kuwa watu wa„ibada‟ wanaomwambudu Mungu na Kristo. Neno „madhabahu‟ laleta wazo la„dhabihu‟. Wakristo humtumikia Mungu kwa hali ya kujitoa Kwake. Piamadhabahu ni ukumbusho wa mahali ambapo maombi ya watu wa Munguyasikika (8:2). Katika hekalu madhabahu ilikuwa ya maana. Waliokuwamo mlendani ya hekalu walilindwa kipekee.

k.2 Halafu Yohana alikatazwa asiipime behewa iliyo nje ya hekalu, na sababualiyopewa ilikuwa „kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mjimtakatifu miezi 42‟. Hivyo behewa haikuwa na ulinzi maalumu. Twaona tenaneno la ruhusa, Mataifa „wamepewa‟. Maana yake nini? Inaonekana kwambawasioamini waruhusiwa kuwatesa Wakristo. Tena katika ruhusa hiyo mudaumewekwa, miezi kadhaa imetajwa na mahali pamewekwa, ni behewa ya nje, sihekalu na ndani yake.

Kabla ya kuendelea ni vema tuone ya kuwa „miezi 42‟ ni sawa na „siku 1260‟ (k.3)na ya „wakati na nyakati na nusu ya wakati‟ (12:14). Kwa hiyo muda wa mambokadhaa umelinganishwa, pamoja na kulinganishwa na jambo mojawapo kubwakatika historia ya Waisraeli. Kwa muda wa miaka mitatu u nusu tangu mwezi wasita mwaka K.K.168 hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka K.K.165 Hekalu paleYerusalemu lilitiwa unajisi na Mtawala Antiochus

Hekalu laYerusalemu

Page 78: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1448

Epiphanes aliyesimamisha sanamu ya kipagani mle ndani, pamoja na kufanyavitendo vya ukatili na kuushambulia vikali sana Mji Mtakatifu. Watu wa Munguwalifadhaika sana, ila WaMakabayo walisimama imara na kupigana vita nao,kisha wakawashinda. (Habari hii yapatikana katika Vitabu vya WaMakabayokatika Apokrifa).

k.3 Halafu twaona mashahidi wawili wa Mungu waliruhusiwa kutoa unabii kwasiku 1260, hali wamevikwa magunia, ishara ya uzito wa ujumbe wao wa kuwaitawatu kutubu na wa uaminifu wao. Ujumbe laini hautauamsha ulimwengu wa uasi.Muda uliotajwa ni uleule wa Mataifa kuukanyaga mji mtakatifu. Hao wawili siwatu fulani hasa ila wanamithilisha watu wa Mungu wa nyakati zote. Katikasheria ya Kiyahudi mashahidi wawili walitakiwa kwa kulithibitisha shtaka juu yamtu. Kwa hiyo ina maana kwamba ushuhuda wa hao wawili unauhalilishaujumbe wao (Kum.17:6; 19:5; Yn.8:17; 15:26-27; Mdo.1:8). Kwa hiyo Kanisalinapaswa liendelee kumshuhudia Kristo potelea mbali mashahidi waudhiwehata kuuawa kwa ajili yake. Tusifikiri mji mtakatifu ni Yerusalemu hasa, ila nipopote ulimwenguni ambapo Kanisa lautimiza wajibu wake wa kumshuhudiaKristo. Yohana alipokuwa akiandika hicho Kitabu Yerusalemu ulikuwaumeishaanguka. Injili ni kwa ulimwengu wote (10:11). Bila shaka maana yakekwa wale walioandikiwa ni kwamba wameitwa kuendelea kutoa ushuhuda waokatika ulimwengu ulio kinyume cha Kristo, potelea mbali watakavyofanyiwa. Witowa Kanisa ni kuitangaza Injili, na lina nguvu linapokazana kuutekeleza wajibuwake, tena lina nguvu linapokuwa Kanisa la toba, hali limevikwa „magunia‟.Mwanzoni mwa Kitabu makanisa saba yalifananishwa na vinara vya taa (1:12,20).

k.4 Hao mashahidi wamefananishwa na Mizeituni miwili. Katika Kitabu chaZekaria Mizeituni miwili iliwakilisha Kuhani na Mfalme (Zek.4:3-6,11). Wakristowamefanywa kuwa ukuhani wa kifalme (Ufu.1:5; 5:10). Pia Roho Mtakatifuametajwa. Daima Roho Mtakatifu huliwezesha Kanisa zima ili wauminiwasimame imara kama Yoshua na Zerubabeli walivyofanya zamani, kusudiushuhuda wake usizimishwe na watu waovu. Pia wamefananishwa na Vinara 2,ishara ya Kanisa kuwa mwanga na nuru (Mt.5:14).

k.5-6 Wapinzani wa ujumbe wa wale mashahidi wanajivutia shida nyingi,watavuna kulingana na walivyofanya. Ujumbe wa mashahidi si maneno matupu,bali ndani yake zimo hukumu mfano wa moto. Hao mashahidi wanao uwezo nanguvu kama Musa aliokuwa nao alipopambana na Farao na kama Eliyaalipopambana na Mfalme Ahabu (Kut.7:20-25; 1 Waf.17:1ku). Watumishi waMungu hujaliwa uwezo kwa kazi zao.k.7ku Hapa mabadiliko makubwa yalitokea, tumepelekwa mpaka mwisho wanyakati za Kuhubiri Injili. Kwa mara ya kwanza mnyama atokaye katika kuzimuanatajwa. Yeye aliamsha vita kali juu ya wale mashahidi wawili hata wakauawa.Taswira ni ya enzi za uovu zinazoongozwa na Shetani zikiinuka

Page 79: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1449

kwa nguvu sana juu ya Kanisa na kulipinga kiasi cha kuukomesha ushuhudawake. Wale mashahidi wataendelea na kazi yao ya kutoa ushuhuda mpakamuda utakapotimia ndipo mashambulio makali sana yatatokea juu ya Kanisa.Jambo hilo limeonekana katika 2 The.2:3ku. Ndipo itaonekana kwamba enzi zauovu zimelishinda Kanisa na kuukomesha kabisa ushuhuda wake. Dunia ilifurahisana sana kwa sababu ya kunyamazishwa kwa sauti za mashahidizilizowasumbua kwa ushuhuda wao. Waliona vema hata wakapelekeanazawadi. Twaona adui wa Injili wameitwa „wakaao juu ya nchi‟ ambao walitajwahapa nyuma (3:10; 8:13; 11:10). Walionyesha dharau kubwa kwa hao mashahidi,walitaka kuwaaibisha kabisa hata hawakuzizika maiti zao. Hao mashahidihawatauawa mpaka wameitimiza kazi yao na watu wamepata nafasi tele zakutubu.

k.8 „uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, Misri, tena ni hapo Bwana wao (Yesu)aliposulibiwa‟. Miji iliyotajwa ni ishara ya jumuiya ya wanadamu ambaowamejiunga pamoja na kuendesha shughuli zao bila kumjali wala kumchaMungu. Kwa hiyo ni majina yanayoashiria uasi wa ulimwengu, katika siku zaYohana ulikuwa Rumi. Sodoma ulijulikana kwa uasherati wake, Misri kwa ukatiliwa kutesa na kukandamizi watu wa Mungu, na Yerusalemu kwa kosa kubwalipitalo kila kosa, kosa la kumkataa Kristo na wokovu wake. Kila mji ulipatwa nahukumu ya Mungu. Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mji na kila kundi la watu nakila mtu asiyemkubali Kristo na wokovu wake.

k.11-13a Lakini furaha yao ilikuwa ya muda mfupi „siku tatu u nusu‟ ukilinganishana miaka mitatu u nusu ya ushuhuda wao. Ndipo mashahidi wawili walifufuliwa,wakawa hai tena na watesi wao waliogopa sana. Walifanana na Bwana waoambaye alipouawa alionekana kana kwamba ameshindwa, lakini siku ya tatuakafufuka na baada ya siku 40 akapaa mbinguni. Mashahidi pia waliitwawapande huku juu, nao wakapanda machoni pa adui zao na katika saa iletetemeko kuu la nchi lilitokea na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka na wanadamuelfu saba wakauawa na tetemeko hilo. Kuwa mwaminifu mpaka kufa ni kipimocha uaminifu kwa Mungu. Fundisho ni kwamba Mungu ataidhihirisha haki yamashahidi machoni pa wote (1 The.4:17). Kupaa kwa Yesu kumethibitisha KujaKwake kwa mara ya pili kama mashahidi wawili walivyosema (Mdo.1:11)

k.13b „waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu‟.Waliitika tofauti na hapo nyuma, „wakamtukuza Mungu‟. Saa ya ushindi waKanisa ni saa ya hukumu ya ulimwengu. Watu wakamtukuza Mungu baada yanafasi ya kutubu kuwa imepita, ni kama wamelazimishwa kufanya hivyo baadaya kuziona kazi zake. Watu hawawezi kuletwa kwenye toba bila ushuhuda waKanisa. Wataalamu kadhaa wanafikiri kwamba Yohana anadokezea wokovu wawatu wengi na kufa kwa mashahidi wawili ni kusema juu ya mambo yanayolipataKanisa mahali mahali mara kwa mara. Uhakika wa hayo kutokea

Page 80: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1450

umeonekana katika mambo hayo kuandikwa kana kwamba yameishatokea. Kaziya ushuhuda ni muhimu sana katika mpango wa Mungu. Tusifikiri mnyamaatokaye shimoni atoka mara moja tu, ni hali na tabia yake ya daima (17:8).

Ni dhahiri kwamba Yohana anataka kufundisha kwamba Mungu amewekampaka nguvu za uovu nazo zitatumiwa na Mungu katika kuyatimiza makusudiyake. Yuko Mungu mmoja tu, atawalaye Yeye peke yake tu, hamna wawili wamilele walio na uwezo unaolingana. Shetani si mungu wa pili, wala si wa milele,wala si mwenye uwezo sawa na Mungu.

k.14 Yohana alisema ole wa pili umeishapita na ole wa tatu unakuja upesi. Olewa tatu Je! ni baragumu ya saba.

11:15-19 Baragumu ya saba: Tangazo la kufika kwa „mwisho‟Muhuri ya saba ilipovunjwa kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa(8:1). Lakini baragumu ya saba ni tofauti sana, badala ya kimya Yohana alizisikiasauti kuu mbinguni zikimtukuza Mungu na kuutangaza ushindi wake katika Kujakwa Ufalme wake na wa Kristo, na katika kufika kwa mwisho wa „ufalme wadunia‟. Yohana hakutoa maelezo ya huo mwisho ila alitoa habari jinsi mamboyalivyokuwa mbinguni baada ya hukumu ya mwisho. Mpaka hapo iwapo Munguametawala, ametawala katika hali ya kupingwa, Shetani naye alikuwa amedaiapewe utiifu wa wanadamu, madai ya uongo yaliyokosa haki na uhalali. Alipewanafasi ya kuwatiisha wanadamu, alifanya vita kali, ila mwishowe, iwapoamefanya juu chini, hata kuwaua mashahidi wa kweli, Mungu amemshinda.„ufalme wa dunia‟ ni lugha ya kujumlisha tawala zote za dunia na jamii nzima yawanadamu waliomwasi Mungu katika vizazi vyote. Yohana ameandika kamahayo yote yamekwisha kutokea ingawa bado hayajatokea, alijua hakika Munguatashinda, hata alimtaja Mungu kwa kusema „uliyeko na uliyekuwako‟ (k.17) si„utakayekuja‟ (ling. na 1:8) maana amemwona kama ameisha kuja na kumshindaShetani na enzi zake zote katika mashindano makuu ya mwisho yaliyotajwakatika 11:7ku. Jambo hilo lilimfanya Mungu ayafunge mambo yote na kuletahukumu ya mwisho na kuwalipiza wale walioharibu nchi kwa kuwaharibu waowenyewe. Ndipo waliodumu waaminifu Kwake watapewa thawabu yao. Wakatiwote hukumu za Mungu zafuata kanuni moja, jinsi alivyofanya mtu ndivyoatakavyofanyiwa, ama mema, ama mabaya, taz. k.18 mataifa walikasirika, hasiraya Mungu ikaja. Walioharibu wataharibiwa. Baadhi ya wataalamu wafikiri „Ufalmewa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake....‟ nimaneno kuhusu Ushindi wa Kristo katika Kufa na Kufufuka Kwake kwa kuwaalitawazwa juu na kupewa jina lipitalo kila jina....(Flp.2:5ku). Kutokea hapoalianza kutawala (k.17) na hukumu za Mungu juu ya waiharibuo nchi pia zilianza(k.18). Hii ni uhalisi mmoja ambao Yohana alitaka kuukaza katika Kitabu chake.

Page 81: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1451

k.16-17 Yohana aliwaona wale wazee ishirini na wanne, waliotajwa katika 7:11waliziitikia sauti za mbinguni zilizotangaza ushindi wa Mungu kwa kuangukachini na kumsujudia, na kumshukuru. Walimshukuru kwa sababu ameshinda,ameutwaa uweza wake mkuu na kumiliki. Tangu hapo upinzani wote utakwisha,wala hautazuka tena kamwe. Ni neno la shukrani kubwa, kwa sababu bilakutoweka kabisa kwa enzi za uovu na upinzani wote watu wa Mungu hawanausalama, hawataweza kutulia na kuufurahia wokovu wao. Yesu aliwafundishawafuasi wake kuomba „ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa dunianikama huko mbinguni‟. Katika Mungu kuutwaa uweza wake mkuu na kumilikindipo maombi ya Wakristo wote wa vizazi vyote yatatimizwa.Haidhuru habari hiyo yahusu mwisho ama yahusu ushindi alioupata KristoMsalabani, jambo la hakika ni kwamba Mungu anatawala juu ya ulimwengu wauasi.

k.18 Kwa nini mataifa walikasirika? Walikasirika kwa sababu walijua kwa hakikakwamba hawana nafasi tena. Mungu ameendelea kuwapa nafasi ili awaletekwenye toba, muhuri ziliwaita, tarumbeta ziliwaita, hata baadaye vitasa vitawaita,hata hivyo watadumu kuwa wakaidi. „hasira yako nayo ikaja‟ hasira ya Munguina utaratibu, haiji ovyoovyo bila sababu. Ni itikio lake linalolingana na kosa (1Kor.3:17). Mungu hana la kufanya zaidi isipokuwa kuzileta hukumu zake zamwisho (Dan.7:14; Zab.2:7ku. Lk.1:33; Mt.25: 31ku). Katika hukumu hizoatawaharibu hao waiharibuo nchi, yaani ataangamiza enzi za uovuzilizosababisha watu kumwasi Mungu (Babeli, Mnyama wa kwanza, nabii wauongo nk) ndipo watu watawekwa huru ili wawe waaminifu kwa Mungu nakumwabudu jinsi ilivyowapasa. Hukumu za Mungu hazina vitisho kwa wamchaoMungu. Uovu utafuata mwenendo wake na kukusanya majeshi yake wawapingewatu wa Mungu, nao utashindwa kwa njia ya imani na uaminifu wao kwa Bwanawao. Kwa njia hiyo Yohana anawasihi waumini katika makanisa wadumu kuwawaaminifu kwa Kristo kati ya vipingamizi vingi na majaribu makali.

k.19 Halafu Yohana aliona Hekalu la Mungu liko wazi mbinguni na sanduku laagano lilionekana ndani yake. Kabla ya Kuja kwa Kristo Waisraelihawakuruhusiwa kuingia mle ndani ya Hekalu mahali pa sanduku la agano.Sanduku la agano lilikuwa mahali ambapo Mungu aliahidi atakutana na watuwake (Kut.25:22). Ni kuhani mkuu peke yake aliyeweza kuingia mle ndani, tenamara moja tu kwa mwaka, pia ilimbidi aende na damu ya mwanakondooaliyechinjwa. Yesu alipokufa Pazia lililozuia watu wasione mle ndani lilipasuliwa,ishara ya njia kuwa wazi kwa watu kumwendea Mungu kwa njia ya imani katikaYesu Kristo na Kifo chake (Ebr.10:19). Maana yake ni kwamba watu wa Munguwaweza kuwa na ushirikiano mwema kabisa, wa uhuru, na Mungu wao. Sandukula Agano ni ishara ya uaminifu wa Mungu kwa Agano lake. Katika vizazi vyoteamezitimiza ahadi zake kwa watu wake. Tena msingi wa utawala wake ni hakina uadilifu. Ndipo umeme, radi, tetemeko la nchi

Page 82: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1452

ziliashiria uwezo mkuu na utukufu wa Mungu. Yeye aweza kutimiza yotealiyoahidi.

MASWALIJibu kwa kifupi:

1. Kupimwa kwa hekalu la nje ni ishara ya nini?2. Miezi 42 ni sawa na siku?

Ni muda wa tangu lini mpaka lini?3. Mashahidi wawili ni wawakilishi wa?

Walipewa ruhusa gani?Kwa kazi yao watajaliwa nini? nao walifanana na akina nani?

4. Baadaye sana mabadiliko makubwa yalitokea katika hali yao.Ilitokea nini?Ni ishara ya wakati gani?Wapinzani wao walifurahi sana, kwa nini?Furaha yao iliendelea kwa muda gani?Iliwapata nini hao mashahidi wawili?Kazi muhimu ya Kanisa ni ipi?

5. Baragumu ya saba inatupeleka kwa wakati gani?Mwisho wa makusudi ya Mungu ni nini?Mpaka hapa Mungu ametawala katika hali ya ku..........?Baada ya hapa Mungu atatawala bila ..............?

6. Katika hukumu ya mwisho watumishi wa Mungu watapewa nini?na wapinzani wa Mungu watapewa nini?

7. Wakati wote hukumu za Mungu zinalingana na ..........?8. Hekalu la Mungu kuwa wazi na sanduku la agano lake kuonekana

ndani yake ni ishara ya tabia zipi za Mungu?

SURA 12-14 SHIDA KWA KANISA: UPINZANI JUU YA KRISTO NAKANISA:Fungu kubwa la kwanza la Kitabu, sura za 1-11, lina sehemu tatu hasa: Baruasaba, muhuri saba, na baragumu saba. Kwa muhuri na baragumu tulionyeshwahukumu za Mungu juu ya adui za Kristo na watu wake. Pia tulionyeshwausalama wa wafuasi wa Kristo, na kudokezwa habari za ushindi mkuu wa Kristona wafuasi wake Mungu atakapoleta „ule mwisho‟.

Fungu la pili la Kitabu, sura za 12-14, katikati ya Kitabu, lina habari za aduiWakuu wa Kristo; Joka Kubwa, Mnyama atokaye baharini, na Mnyama atokayenchini.

Fungu kubwa la Kitabu, sura za 15-22, lina sehemu tatu. Vitasa 7, sura za 15-16; Ushindi wa Kristo, sura za 17-20; na habari za Yerusalemu Mpya, sura za21-22.

Page 83: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1453

Katika sehemu hiyo ya kati kuna ishara saba. Twakumbushwa ule uaduimkubwa ulio kati ya Kristo na Shetani ambao unaendelea katika Kanisakupingwa vikali sana. Mkazo ni juu ya ushindi mkuu wa Mungu juu ya Shetanina enzi zake, ushindi uliodhihirika hasa katika Kristo na Msalaba wake(Kol.2:15). Tukumbuke kwamba shabaha ya Kitabu ilikuwa kuwasaidiaWakristo waliopatwa na shida kwa ajili ya Imani yao. Wakati wa Yohanailitazamiwa watateswa vikali hivi karibuni. Mkazo ni kwamba ushindi unaMungu, maovu yote na yule mwovu aliye asili yake havitakuwa na neno lamwisho. Iwapo kwa wakati huo inaonekana uovu una nguvu, sivyo ilivyo. Kamailivyokuwa kwa Kristo. Alipouawa ilionekana ameshindwa, kumbe siku ya tatuakafufuka kutoka kwa wafu kisha akapaa. Ndivyo itakavyokuwa kwa wafuasiwake wanaozikanyaga nyayo zake, watateswa na kuuawa na baada ya kufawatapokelewa na kutawazwa juu pamoja na Kristo katika uzima wa milele.

12:1-6 Maono ya Mwanamke aliyevikwa juaKatika sehemu hiyo Yohana anatumia lugha mpya katika kueleza uadui mkuu navita kali juu ya Mungu na Kristo. Analeta mbele yetu Joka Kubwa na Wanyamawawili. Ni hao wanaotoa changamoto kwa utawala wa Mungu na haki ya Kristokutawala pamoja naye.

k.1-2 Hapo Yohana aliona ishara kuu mbinguni. Alimwona mwanamkealiyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake na juu ya kichwa chake tajiya nyota kumi na mbili. Ni dhahiri kwamba huyo alikuwa maarufu sana. Kwa hiyo,huyo ni nani? Anaashiria nini? Ni ishara ya Israeli, Watu wa Mungu, ambaokutoka kwao Masihi alikuja. Huenda jua na mwezi na nyota kumi na mbili niishara ya „ufunuo‟ „mwanga‟ wa kweli za Mungu katika Maandiko yaliyotabiriKuja kwa Masihi na kuwafunulia watu juu ya wokovu wake (Ling.na ndoto yaYusufu Mwa.37:9).

k.2 Huyo mwanamke alikuwa na mimba akiwa na utungu wa kuzaa, dalili yawatu wa Mungu wa kale wakitamani sana wapate Masihi waliyeahidiwa. Ahadiilitolewa mapema sana, mara baada ya Anguko (Mwa.3:15; Isa.26:17;Mik.4:9,10; 5.2,3). Ingekuwa rahisi kufikiri mwanamke ni Mariamu, mamayeYesu, ila kwa sababu anaendelea katika jamii ya watu wa Mungu, Kanisa, nivema kumwaza kuwa jamii ya watu wa Mungu wa kale (12.17).

k.3 Ndipo Yohana aliona ishara nyingine mbinguni. Aliona joka kubwa jekundu,ishara ya chuki kali sana iliyojaa tamaa ya kuua (Yn.8:44). Alikuwa na vichwasaba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Hii ni ishara yamamlaka aliyojitwalia bila haki (Lk.4:6; Yn.14:30). Pembe ni dalili ya „afya‟ na„uhai‟ wa uovu. Kwa hiyo Joka anazo nguvu, anadai mamlaka juu ya ulimwenguwote, ni mkali sana, akitamani sana kumaliza adui zake. Yohana alitoboa wazihuyo ni Shetani (k.9). Ni adui mkuu wa Kristo na wafuasi wake.

Page 84: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1454

k.4a Alipomwasi Mungu alivuta „theluthi ya nyota‟ nyuma yake. Shetani anaowasaidizi wake, pepo wabaya, mashetani, enzi za uovu, mamlaka za giza. Wotewanaunga mkono na wanamtii Shetani katika vita kali kati yake na Kristo nawafuasi wake. Hawachoki katika vita yao (Efe.6:12). „theluthi‟ ni kuonyeshakwamba iwapo Joka ni Kubwa hata hivyo amewekewa mpaka katika nafasi namatokeo ya jitahada zake. Yeye si mkuu mwenye madaraka yote mikononimwake, afanya kwa kiasi kile anachoruhusiwa na Mungu. Ni mpinzani mkuu.

k.4b Vita kati ya Mungu na Shetani iliendelea katika historia yote ya Watu waMungu. Aliwashambulia Watu wa Mungu wa zamani, kwa mfano, wakati waMusa Shetani alimtumia Farao ili awapinge watu wa Mungu wasirudi makwao(Farao ameitwa Joka Eze.29:3; 32:2) wakati wa Yeremia alimtumiaNebukadreza (Yer.51:34).

k.5 Iwapo Shetani alisimama mbele za yule mwanamke alipotaka kuzaa,akashindwa kumpata mtoto wake. Mtoto ni Kristo (Zab.2:2ku; Mwa.3:15; Gal.4:4;Isa.26:17-18). Herode alifanya mpango wa kumwua akashindwa (Mt.2:13ku).Yohana hakutaja mambo mengine ya maisha ya Yesu, majaribu yake na hatarimbalimbali zilizompata, ingawa tunajua kwamba aliwindwawindwa. Walahakuweza kutia ufa kati yake na Baba yake, Yesu alidumu mwaminifu kwaBabake, (Mt.3:1-11) hata katika kumtii na kuzivumilia taabu za Msalaba(Zab.2:2-7; Mwa.3:15; Gal.4:4; Rum.1:4). Shetani alifanya juu chini iliamwangamize Kristo kabla hajatimiza lengo la Kuja Kwake na kuufanyaukombozi wa ulimwengu. Yohana hakutaja jambo lolote kati ya kuingia kwakeulimwenguni, yaani kuzaliwa kwake, na „kutoroka‟ ulimwenguni kabisa, kwaKupaa Kwake, hata hakusema lolote juu ya Kufa na Kufufuka Kwake. Kwamaneno „akanyakuliwa hata kwa Mungu na kwa kiti chake cha enzi‟ Yohanaalitaka kuonyesha ushindi mkuu wa Yesu. Twakumbushwa habari za Yesukupewa jina lipitalo kila jina, na mamlaka yote mbinguni na duniani (Mt.28:18-20:Flp.2:9-11). Aliyeshinda ni Kristo si Shetani, vivyo hivyo wafuasi wa Kristo katikamakanisa yaliyoandikiwa watamshinda Shetani wakiwa waaminifu Kwake mpakakufa.

(Liko wazo la kufikiri kwamba „alinyakuliwa‟ si wakati wa Kupaa Kwake baliwakati wa Kufa Kwake, alipofufuliwa kutoka kwa wafu (Rum.1:4) akawekwambali na adui zake wote, wasiweze kumpata tena, haidhuru wafanye nini.Maadamu alipoishi ilikuwapo nafasi avutwe kumwasi Babaye, ndiyo sababu hatapale Gethsemane Shetani alifanya juu chini kumtisha ili asiende Msalabani,maana alijua hakika kwamba akifa atafaulu kukomboa wanadamu na kuwatoachini ya utawala wa dhambi).

Aliyezaliwa ni yule atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma.Amepewa mamlaka juu ya mataifa yote kuwachunga kwa fimbo ya chuma.Kazi yake ni kuchunga si kutawala. Fimbo hiyo si dalili ya ukali bali inaashiria

Page 85: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1455

uthabiti na uimara wa utawala wake, hana wasiwasi wowote (Mt.9:36;Yn.10:11ku). Zaburi 2 ilitabiri mambo hayo. Utawala wa Mungu umejengwa juuya Kristo na ukombozi wake. Kifungu hicho chatafsiri maono ya Sura ya 5 Kristoalipoadhimishwa na kushirikishwa Kiti cha Enzi cha Babake.

k.6 Mwanamke alikimbilia jangwani alipotambua kwamba yeye atapatikana nahasira za Shetani zilizowaka sana aliposhindwa kumpata Masihi Mwenyewe.Twaona mwanamke anaendelea katika watu wa Mungu wa Agano Jipya(Rum.9:5). Jangwani palikuwa mahali palipotengenezwa kumpokea, paleatakuwa salama, atalindwa na Mungu. Jangwa iwapo ni mahali pagumu nimahali pa kuhifadhiwa, mahali pa kutunzwa na Mungu. Muda wa kukaa jangwanini muda uleule wa mashahidi wawili kutoa ushuhuda wao (11:3). Kwa hiyoKanisa (Watu wa Mungu/Israeli Mpya) litalindwa wakati wote wa kutoa„ushuhuda wake‟ yaani wakati wa Injili kuhubiriwa. Neno hilo ni la faraja sanakwa wale watakaoishuhudia Injili, ingawa baadhi yao watagharimiwa maishayao. Ni ukumbusho wa Waisraeli kutunzwa jangwani wakati wote wa safari yaotangu walipotoka Misri mpaka walipoingia nchi ya ahadi, Kanaani. Waisraeliwalipiga makambi 42 jangwani (Hes.33:5ku). Miezi 42 ni sawa na siku 1260.

12:7-12 Vita mbingunik.7 Inafikiriwa vifungu hivi vyarudia mambo ya k.4 na k.5. Ndipo Yohana alionavita mbinguni kati ya Mikaeli na malaika zake na joka na malaika zake. Ushindimkuu ulipatikana, Mikaeli na malaika zake walishinda hata Shetani pamoja namalaika zake wakatupwa chini wasionekane tena mbinguni. Yohana alitajamajina yote ya joka ili iwe dhahiri ni nani aliyeshindwa na kutupwa chini duniani.Joka ni yule mkubwa, Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote. Katikak.10 ameitwa „mshtaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu,mchana na usiku‟. Zamani za Agano la Kale alimshtaki Ayubu (Ayu.1:6ku) naYoshua Kuhani Mkuu wakati wa Nabii Zekaria (Zek.3:1-2). Alimdanganya Hawa(Mwa.3:1-7) Yesu alimwita mwongo na mwuaji (Yn.8:44). Inaonekana tumerudiasehemu ya kwanza na mambo yale yameelezwa tena. Kwa hiyo wauminiwameingizwa katika mashindano makubwa baina ya utu wema na uovu, katikavita kali kati ya Kristo na Shetani. Vita kuu ilitokeawakati gani? Ilitokea pale Msalabani Kristo alipokufa na kulipa fidia ya dhambi(k.11; Yn.12:31; Lk.10:18; Kol.2:15) na ushindi wake ulithibitishwa kwa Kufufukana Kupaa na Kutawazwa Kwake. Waumini wajue hakika kwamba ushindi ni waokutokana na ushindi wa Kristo.

Mikaeli, malaika mkuu (Yud.9) aonekana kuwa malaika wa ki-vita (Dan.10:13,21;12:1). Yeye ana malaika wanaomsaidia, na Shetani pia anao malaika wa kwake.Maana ya malaika ni mjumbe.

Shetani alipoteza kazi yake maalumu ya kuwashtaki watu kwa Mungu. Hakuwezakumwendea Mungu kwa uhuru kama hapo nyuma. Kwa upande wa

Page 86: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1456

waumini hakuna shitaka litakalosimama mbele za Mungu kwa sababu Kristoamelipa madeni yao yote ya dhambi, wamehesabiwa haki bure kwa neema(Rum.8:1,34). Twajua wanadamu walifaulu kumshitaki Yesu barazani kuwamhalifu wa hali ya juu, hata wakamwua. Hata hivyo kwenye baraza la mbinguni,kwa Mungu, Mungu hakuukubali uamuzi wao, akaupindua, akamfufua Yesukutoka kwa wafu na kufutilia mbali shitaka juu yake. Tangu hapo hakuna kesiyoyote itakayofaulu juu ya mwenye dhambi mradi yule mwenye dhambiamempokea Kristo kuwa Mwokozi wake na kuamini kwamba alikufa kwa ajili yadhambi zake.

k.10 Furaha kubwa sana ilitokea mbinguni kwa sababu ya ushindi wa Kristo.Walifurahi kwa sababu wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu na mamlaka yaKristo zimedhihirika kabisa. Wimbo ulikaza ushindi wa Mungu na kushindwa kwaIbilisi. Tena kwa sababu mshtaki Ibilisi amenyimwa kazi yake mbaya yakuwashtaki wateule wa Mungu. Hamna kitu chochote kiwezacho kuwazuiawaumini wasiushiriki ushindi wa Mungu (Rum.8:33-34).

Kwa nini Mikaeli aliweza kufanya vita hiyo, ni kwa sababu ya ushindi wa Kristohapo duniani, Mikaeli alikuwa „nakala‟ ya Kristo. Aliondoa „bendera‟ ya Shetaniisipepee tena pale mbinguni, mfano wa Jemadari akaaye katika Makao yaKuangalia vita, na kuondoa bendera ya adui kwenye ramani ya vita mara vita yamahali pale inapofaulu. Twaona waumini wanashinda kwa „damu ya Mwana-Kondoo‟ si kwa uwezo wa Mikaeli. Ingawa wamewajibika kumshuhudia Kristompaka kufa, hata hivyo, msingi wa ushindi wao ni Kifo cha Kristo.

k.11 Imeandikwa kana kwamba wamekwishateswa na kushinda kwa sababundivyo itakayokuwa. Wataushiriki ushindi wa Kristo. Ni kama Yohana anawasihiwaumini wawe waaminifu mpaka kufa wala wasiogope kumshuhudia Kristo hasawatakapoitwa kusema Kaisari ni Bwana na kufukiza uvumba kwenye sanamuyake. Hakuna la kuwazuia wasishinde, mradi wawe waaminifu.

k.12 Iwapo mambo hayo yalisababisha shangwe mbinguni, duniani ni tofautisana. Shetani hakuwa tayari kukubali kushindwa, hivyo akaamua aendelee navita yake. Shetani alijaa ghadhabu nyingi aliposhindwa kumwangusha Kristo naalipotolewa mbinguni hali akijua ya kwamba sasa upo uwezekano wa wanadamukusamehewa dhambi zao. Basi, alibaki na shabaha moja ya kuwaangushawafuasi wa Kristo popote walipo, hasa kwa sababu alijua kwamba anao mudamfupi tu wa kufanya hivyo kwa sababu Mungu hatamruhusu aendelee kuharibukwa muda mrefu. Ni adui wa hatari sana, mfano wa nyoka aliyebanwa pembeni,anajua hawezi kutoka salama, hivyo atikisatikisa mkia wake vikali sana nakuharibu chochote kilicho njiani. Kwa hiyo ni ole kwa nchi na bahari. Taabuzatokea si kwa sababu Shetani ana nguvu nyingi bali kwa sababu ameshindwa,hana nguvu juu ya Kristo, ila kwa muda uliombakia ajikaza kisabuni ili aharibuchochote awezacho. Mwisho wake

Page 87: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1457

umeishaamriwa na Mungu (20:10). Haiwezekani amani iwepo ila ile inayojengwajuu ya haki na utakatifu wa Mungu (Rum.3:26).

12: 13-17 Vita kati ya Shetani na Mwanamkek.13 Inaonekana vifungu hivi vyaeleza zaidi jambo la k.6. pia inaonekanaYohana ametumia mambo yaliyotokea Waisraeli walipokimbilia jangwaniwalipoondoka Misri. Yohana aliona kwamba vita kati ya Shetani na Mwanamkealiyemzaa mtoto mwanamume iliendelea. Shetani aliposhindwa kumpata mtotowake, Kristo, alikazana kuwafuatia wafuasi wake, jamii ya waliokombolewa.Hawezi kumpata Kristo Mwenyewe ila aweza kumwudhi kwa njia ya kumwudhi„mama‟ jamii ya watu wa Mungu ambao alitoka kwao.

k.14 Ila mwanamke alipewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aendezake nyikani hata mahali pake. Mabawa ni dalili ya urahisi na wepesi wakukimbia kwake. Ni ukumbusho wa jinsi Waisraeli walivyotoroka kutoka Misrizamani. Farao alikazana kuwafuatia (Kut.14:8) na Mungu aliwabeba juu yamabawa ya tai (Kut.19:4; Kum.32:10-11; Isa.40:31). Nyikani pameitwa mahalipake, pale atakuwa salama na kulishwa. Iwapo Yohana hakusema ni naniatakayemlisha bila shaka ni Mungu. Ukumbusho wa jinsi Mungu alivyowalishaWaisraeli muda wote wa kusafiri jangwani. Muda wa usalama wake umetajwakuwa „wakati na nyakati na nusu ya wakati‟ ambao ni sawa na siku 1260 na miezi42, muda wa mashahidi wawili kutoa ushuhuda wao. Pia twakumbushwaWaisraeli walipiga kambi mara 42 jangwani (Hes.33:5ku). Maana yake nini?Waumini wanaishi humo duniani ila hawaishiriki tabia yake (Yn.17:11,14). Kwasababu hawawi wa ulimwengu huu waweza kutambua vizuri ukweli wa mambojinsi yalivyo hasa na kutambua utongozaji na ubatili wa dunia hii. Wao ni wasafirina wapitaji tu (1 Pet.2:11). Kama mashahidi wawili walivyoweza kutoa ushuhudawao muda wa siku 1260 (11:3ku) ndivyo na hao wa mwanamke watakavyoishisalama nyikani muda ulio sawa na muda wa mashahidi. Ina maana kwambaKanisa litaendelea na kuutimiza wajibu wake kwa muda wote ulioamriwa naMungu.

k.15-16 Iwapo Shetani alijitahidi kuwapata kwa njia ya kuwachukua na „mto‟yaani kuwadanganya na uongo wake haiwezekani wadanganyike kwa kuwa niwatu wa kweli kama Bwana wao, wamejitoa kabisa kuishikilia Injili ya kweli.Kama tulivyoona katika barua kwa makanisa Wakristo walishambuliwa namafundisho ya uongo yaliyolenga kuipotosha imani yao ya kweli. Mto wa Munguni mto wa uzima (21:1). Twakumbushwa tena habari za Waisraeli wakati wakutoka Misri (Kut.15:12).

k.17 Waumini wameelezwa kuwa watu wazishikao amri za Mungu na kuwa naushuhuda wa Yesu. Shetani hulishambulia Kanisa kwa jumla na Mkristo mmojammoja na katika vita hiyo ni hatari kuridhiana na kujisalimisha. Mungu ni Mwenyehaki na mwenye kuwahesabia haki wote wampokeao Kristo. Msalaba

Page 88: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1458

ni tiba ya kuiponya dhambi na kuzivunja pingu zake na kuondoa hatia yake. PaleMsalabani mwenye dhambi ametangazwa na Mhukumu wa watu wote kuwa„hana hatia‟. Kwa tangazo hilo mwenye dhambi awekwa huru na kutiwa moyo wakutokufanya dhambi na badala yake ajaliwa nia ya kutenda haki.

k.18 Ndipo Yohana alimwona Joka hali amesimama juu ya mchanga wa bahari.Alikuwa akikusanya majeshi ya kufanya vita juu ya Watu wa Mungu. Shetanihachoki, hasikii aibu, hata kama ameshindwa vibaya sana hakati tamaa.Twajifunza kwamba Shetani amenyang‟anywa haki yake ya kuwashitaki watu waMungu, hawezi kuleta ufa kati yao na Mungu wao, katika Kristo wamepatanishwana dhambi zao zimesamehewa. Ila ule uadui alio nao bado ungali unaendeleana uharibifu unaoletwa na dhambi ungalipo. Kwa hiyo mateso ya Kanisayanasababishwa na kuchochewa na Shetani. Vita hiyo si ya kawaida, ni yakipekee, ilianza mbinguni, kisha ikaletwa kwetu duniani. Paulo aliwaambiaWaEfeso habari hiyo alipowaandikia „kwa maana kushindanakwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu yawakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho‟(Efe.6:10ku).

MASWALI1. Taswira ya sura 12 ni habari ya nini?2. Mwanamke aliyevikwa jua na kuwa na mimba ni ishara ya nini?3. Ni nani aliye adui mkubwa wa Kristo na Kanisa lake?4. Shetani alipoteza kazi gani alipotupwa chini mpaka duniani?5. Shetani anajikaza kwa sababu anadhani kwamba atamshinda Kristo au

vipi? Eleza.6. Mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai...aende zake nyikani, hapo

alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati‟ Maneno hayoyanatufundisha nini kuhusu Kanisa?

SURA 13 MAONO YA WANYAMA WAWILIKatika sura iliyotangulia tuliona ya kwamba Shetani hakukubali kushindwa,alipotolewa mbinguni kuja duniani alikazana kufanya uharibifu mkubwa nakufanya juu chini kuwapinga wale wamfuatao Kristo. Yohana anatufunulia nikwa njia gani anaendeleza shabaha yake. Katika sura hiyo tumepewa habari zamaono aliyoyapata Yohana ya Wanyama wawili, mmoja aliyetoka baharini nammoja aliyetoka nchini. Hao ni wasaidizi wa Joka, yaani Shetani, katikajitahada zake za kuharibu kazi ya Mungu na kuwaondoa waumini kwenye utiifuwao kwa Kristo.

13:1-10 Mnyama atokaye bahariniShetani alimwita mnyama kutoka baharini. Shetani ni ishara ya uovu na nguvuzake. Yeye huhitaji „vyombo‟ vya kumsaidia ili afaulu kuzitimiza shabaha zake.

Page 89: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1459

Vyombo ni watu hasa katika taasisi na jamii na shirika za aina mbalimbali. KatikaIsaya 17:12 na Ufu.17:15 mataifa yamefananishwa na bahari. Misukosuko yabahari ni mfano wa fujo na hali mbaya katika jamii na katika siasa na mara nyingizinatokeza tawala za uonevu na udhalimu ama wa mtu mmoja kama dikteta amawa kundi la watu. Zamani za kale watu walidhani „bahari‟ ni mahali pa kuinukakwa „maovu‟ maana walishindwa kujua yaliyomo mle ndani, misukosuko yake nakutokutulia kwake, pamoja na kina chake kirefu vilisababisha mawazo hayo hatawatu wengine walifikiri kwamba mienendo mikubwa ya historia huongozwa nayo.Wakristo wa Asia Ndogo walipotazama magharibi-kaskazini ya Bahari yaAegean walikumbushwa Dola kubwa la Kirumi na vitisho vyake.

k.1-2 Yohana alimwona mnyama mkali sana, wa kutisha, wa kuogofya. Alikuwana pembe kumi, vichwa saba (sawa na joka kubwa) na vilemba kumi kwenyepembe zake na majina ya makufuru juu ya vichwa vyake. Kwa sura alionekanakama chui, dalili ya wepesi wa kukamata mateka, alikuwa na miguu kama dubudalili ya nguvu ya kuponda na kukandamiza vibaya, na mdomo kama simba daliliya nguvu ya kuraruararua mawindo. Katika Danieli 7 twapata habari za wanyamawanne wenye nguvu nao walikuwa ishara ya madola makubwa manne, ila huyomnyama aliyeelezwa na Yohana ni mmoja tu, mwenye tabia zote za wanyamawanne, wa kutisha zaidi sana. Katika Danieli hao wanyama waliashiria madolamakubwa katika mfuatano wa kutokea kwao.

Vichwa na pembe ni dalili za uwezo na mamlaka ambaye Shetaniamemshirikisha. Ni ishara ya uwezo wa kutisha wa tawala za dunia hii. Maovuyanayofanywa na tawala za hapo duniani yana asili katika Joka kubwa, Shetani.

Huyo mnyama ni ishara ya nini hasa? Anafikiriwa kuwa ishara ya nguvu zakudhuru za mamlaka za ulimwengu huu. Serikali na tawala mbalimbali zinatumianguvu zao katika kuendeleza mambo yasiyo haki na kweli, kwa kuwakandamizawatu na kuwanyima haki zao, na hasa kama ilivyokuwa wakati wa Kitabukuandikwa, mkuu wa Dola alijiinua na kudai kuabudiwa kama Mungu. Serikalizina hatari ya kujiingiza katika maisha ya raia na kutaka kuyatawala maeneoyasiyo haki yao kutawala. Mapenzi ya Mungu ni kwamba waongoze mambo kwasheria za haki na kwa utaratibu mzuri. Shetani amefaulu mara kwa mara kufanyaviongozi waziweke sheria mbaya na kuongoza kwa mabavu. Shetani (ni mwigowa kubeza wa Mungu) anamwonea Mungu wivu akitamani sana kuwa na Uwezona Utawala kama Mungu. Ila hana haki yoyote. Mungu anayo haki kabisa juu yamaisha yetu kwa kuwa ni Yeye aliyetuumba na kutukomboa kwa njia ya Kristo.

Hoja mojawapo kubwa ya Kitabu ni „uwezo/nguvu‟. Ni uwezo gani utakaoshinda?Injili imeudhihirisha upendo kuwa kitu cha nguvu sana. Upendo

Page 90: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1460

wa kujitoa ulioonekana katika Kristo kuukomboa ulimwengu na kuwaokoa wenyedhambi. Wote wanaowaongoza watu hujaribiwa sana kutumia nguvu mbalimbalibadala ya upendo.

Twatumia lugha ya „mataifa makubwa‟ kueleza mataifa yenye nguvu ya uchumi,zana za vita, teknologia nk. Hao huwa na maelekeo ya kujiinua juu ya mataifamengine. Tuone „ishara‟ zao - Marekani ni tai, Urusi ni dubu, Ufransa ni chui,Uingereza ni simba nk. Ila tusifikiri ni mataifa hayo tu, hata katika nchi zilizopatauhuru karibuni hivi wameinuka watawala wa kuwakandamiza watu wao. Maovuyaliyopo duniani hutokana na kumwiga Yule Mwovu, ni zaidi ya maovu yawanadamu, hata hivyo ni uovu unaoendelezwa na matendo maovu yawanadamu. Huyo mnyama ni kama „mikono‟ ya Shetani, mikono anayoitumiaShetani kwa kufanya kazi zake mbovu za kuharibu kazi njema ya Mungu.Ulimwengu unakaliwa na adui mkubwa, amchukiaye Kristo zaidi ya yote.Twaona huyu mnyama alivaa majina ya makufuru, maana yake, alimdharausana Mungu. Madai yake kuwa „mfalme wa wafalme‟ ni madai ya uongo.

(Paulo alifundisha kwamba Serikali zimewekwa kwa mpango wa Mungu. Kwahiyo, swali lililopo ni kwamba, imekuwaje hiyo mamlaka iliyotoka kwa Munguiitwe ya Shetani na kufanana naye? Katika Warumi 13:1ku. Pauloamezungumzia jambo hilo. Alianza kwa kusema kwamba „hakuna mamlakaisipokuwa ile inayotoka kwa Mungu‟ yaani ni Mungu aliyeamua na kuidhinishaziwepo serikali na tawala mbalimbali na kuruhusu ziwe na mamlaka ya kuongozamambo nchini. Pia, Paulo alitaja shabaha ya Mungu katika kuziidhinisha,ambayo ni kuutunza usalama wa watu kwa kuwaadhibu waovu na kuuendelezautu wema. Shetani hakuunda mpango huo wala hakuzianzisha tawala hizo, ilayeye hujitahidi kuzipotosha ili zisitimize lile lengo lililowekwa na Mungu. Yeyehujiingiza katika mamlaka mbalimbali na kuzigeuza ziwakandamize watu kwakuziweka sheria na taratibu na uongozi mbovu. Halafu katika serikali nyinginewakuu hujiinua na kuudai utiifu uzidio, ule ambao ni wa Mungu peke yake.Mkristo hawezi kumwita Kaisari ni Bwana wala kufukiza uvumba kwenye sanamuyake. Serikali halali hutumia mamlaka chini ya Mungu na kwa shabahailiyowekwa na Mungu na serikali isiyo halali hutumia mamlaka kama ni yake tuna kwa shabaha zake tu. Kwa kujumlisha twaweza kusema kwamba serikali niulinzi mmoja uliowekwa na Mungu kwa kuziwekea mipaka enzi za uovu.

Mambo yaliyotokea wakati wa Kaisari Domitiani yalikuwa malimbuko ya mamboyatakayotokea mbeleni hasa nyakati za mwisho. Katika Agano Jipya MpingaKristo, mtu wa kuasi ametajwa, katika wakati wake maovu yatazidi (atatokeamara kabla ya Kuja kwa Kristo tena 2 The.2:3; 1 Yoh.2:18). Ni Joka anayempamnyama nguvu na kiti chake cha enzi na mamlaka kuu. Yohana alitaka Wakristowafahamu kwamba adui zao ni wa nguvu sana hata hivyo

Page 91: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1461

hawawezi kupita mpaka ulioruhusiwa na Mungu. Ila tusiwaze matukio fulanihasa kwa sababu hali hii hutokea mara kwa mara katika mwenendo wa historia.

k.3 Huyo mnyama alitiwa jeraha la mauti katika kimoja cha vichwa vyake, ilaajabu ilitokea, jeraha lake likapona, watu wakastaajabu, wakaona ya kuwa nikazi bure kumpinga huyo mnyama, wakawa tayari kumwabudu mnyama pamojana Joka. Anaigiza na kubeza Kufa na Kufufuka Kwa Kristo. Jambo hilolashuhudia udhaifu wa ubinadamu kukabili udhalimu katika jamii na siasa.Mawazo mbalimbali yametolewa kuhusu jeraha la mauti na kupona kwake. Wazomoja ni kwamba uovu ambao asili yake ni Shetani, umeonekana katika moyo wawanadamu na katika jumuiya ya watu, ni uovu usioweza kuangamizwa, unatokeatena na tena na tena nao utaendelea kutokea hadi mwisho hata watu hushangaa„uhai wake‟. Katika „kumwabudu mnyama‟ watu humpa Shetani sifa ambazo niza Mungu peke yake kwa sababu hawana utambuzi wala uwezo wa kirohokumpinga. Hivyo hali ya kibinadamu yageuzwa kuwa ya kinyama. Wakati waYohana ilikuwa rahisi watu wawe na shukrani kwa Dola la Kirumi. Dola lililetaamani mahali pengi na usalama na mafanikio ambayo watu hawakuwa nayohapo nyuma. Walikuwa wameomba kwa miungu yao, hawakupata kitu, ila Dolaliliwapatia, basi hawakusikia shida kumwabudu mkuu wa Dola na kuhudhuriaibada katika mahekalu yaliyojengwa kwa ajili hiyo.Kwa upande wa siasa za zamani zile lilikuwapo wazo la nguvu sana lililosemakwamba Kaisari Nero atakuwa hai tena. Baadhi ya watu walifikiri kwamba hakufaila alikuwa amekwenda mpaka nchi ya Waparthi na kutoka huko ataongozamajeshi yao na kulishambulia Dola. Wazo lingine lilihusu Dola la Kirumi ambalomara kwa mara lilififia halafu likapata nguvu tena. Hata wengine wameonakwamba aina moja ya siasa ikitoweka mahali fulani itatokea na kufaulu mahalipengine, na kwa sababu hiyo watu hudhani kwamba „siasa‟ haifi, ni ya kudumu,kwa hiyo watu huweka matumaini yao ya „wokovu‟ katika siasa. Watuwasiomwamini Mwana Kondoo, Kristo, hawana njia isipokuwa kuweka tumainilao la wokovu katika imani/dini fulani au mpango fulani wa kibinadamu. Wakatiwowote Kanisa litakapouliza maswali au kutoa changamoto juu ya uhalali waserikali kufanya jambo fulani litateswa. Twakumbuka Eliya, nabii wa kweli,aliyefukuzwa na Mfalme, na wakati uleule manabii wa Baali waliosema mamboya kumfurahisha Mfalme walikaa salama, hata wakala mezani pake. Kuikuzaserikali zaidi ya vitu vyote ni kukufuru sana, ni jambo lisilo halali, hata ikiwaserikali imeleta amani na mafanikio, kama Dola la Rumi lilivyofanya. Ni vema tuitiiserikali katika mambo ya halali ila kamwe hatuwezi kuiabudu.

k.5 Sasa tutazame mambo ambayo Joka alimpa Mnyama aliyetoka baharini.Kwanza alipewa „kinywa cha kunena maneno makuu ya makufuru. Pili alipewa„uwezo wa kufanya kazi miezi 42‟. Tatu alipewa „kufanya vita na watakatifu na

Page 92: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1462

kuwashinda..(k.7). Ni Joka aliyempa mnayama uwezo, hata hivyo, hayo yoteyalikuwa chini ya utawala wa Mungu. Uovu umewekwa mipaka, hauna nguvuinayoweza kutumiwa nje ya ruhusa ya Mungu. Waumini wawe na uhakikakwamba Mungu anao uwezo hata juu ya Shetani na jeshi lake lote na nguvu zakezote. Tena wajue kwamba wapinzani wamewekewa muda na Mungu, muda wakufanya kazi muda wa „miezi arobaini na miwili‟. Muda huo ni sawa na muda waMashahidi wawili kutoa ushuhuda wao, yaani muda wa Kanisa kufanya kaziyake. Kwa hiyo katika muda wote wa Kanisa kuutimiza wajibu wake wakumshuhudia Kristo, Shetani naye hufanya kazi yake ya kuuzuia ushuhuda huona kuwaudhi mashahidi (11:2; Dan.7:25). Ndivyo ilivyokuwa wakati wa Yohanaalipowaandikia waumini wa Asia Ndogo na ndivyo itakavyokuwa hadi mwisho.Mwishoni hayo yote yatatokea kwa wema wao (Rum.8:28).

k.6 Mungu huhesabu kwamba kuwatesa watu wake ni sawa na kumkufuru Yeye.„nao wakaao mbinguni‟ hao ni akina nani? huenda ni Kanisa na waumini walioduniani ambao wamewazwa kama wameketi pamoja na Kristo mbinguni(Efe.2:6) maana tayari ni raia wa mbinguni (Flp.3:20). Upo uhusiano mkubwakati ya Mungu na watu wake, jambo kubwa ni uhusiano wao si mahali kamatutakavyoona mbele katika Yerusalemu Mpya.k.7 Mnyama aliruhusiwa kuwadhuru waumini hata kuwaua baadhi yao, lakiniingawa kwa macho ya kibinadamu imeonekana wameshindwa, badohawajashindwa. Aweza kuiua miili yao lakini hawezi kuifisha imani yao walakuziua roho zao (Mt.10:28). Kwa sababu ya imani katika Mungu wataishi milelepamoja na Bwana wao (12:11). Mnyama hufanya kazi duniani kote, popote Injiliinapotangazwa.

k.8 Wengi sana watamsujudu mnyama, huenda Yohana alitazama mbele sanakwa nyakati zilizotajwa na Paulo katika 2 The.2:4ku Hata ikiwa wengi wamsujudumnyama baadhi ya watu sio, hao wanakataa kumkiri Kaisari kuwa ni Bwana nakufukiza uvumba kwenye sanamu yake. Hao wamejitoa kabisa kwa Yesu Kristoyule ambaye alijitoa kuwa sadaka kwa dhambi zao hata kabla ya misingi yadunia kuwekwa. Yohana alitaka waumini wajue hakika kwamba wokovu wao sibahati nasibu, wala si wazo la baadaye ambalo Mungu aliliamua alipoona jinsimambo yalivyokuwa yakienda, bali ni mpango wake tangu mwanzo (1 Pet.1:20).Haidhuru watapatwa na shida gani wafuasi wa Kristo hulindwa na Mungu, naowatapita salama katika hatari zote mpaka wafike salama salimini kwa Bwanawao. Kitabu ni cha MwanaKondoo, mali ya Yule aliyewafia. Maneno„MwanaKondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia‟ yanatoboa wazikwamba Mungu alikusudia Kifo cha Kristo tangu milele. Majina yaliyoandikwahumo ni ya wale waliokubali kwamba aliwafia. Mungu ni mwaminifu kwa ahadizake za wokovu.

Page 93: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1463

k.9 Maneno „mtu akiwa na sikio na asikie‟ yanatukumbusha maneno ya Yesukwa makanisa saba, alifunga kila barua na maneno hayo. Pia ni manenoaliyoyatumia Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani. Ni vema tuwe watu wa„kusikia‟ asemayo Yesu.

k.10 Wakristo wawe tayari kupokea lolote litakalowapata. Wasiridhiane na halina hewa ya mazingira yao. Wasirudishe ovu kwa ovu, wala baya kwa baya, baliwafuate kielelezo cha Bwana Yesu. Ndipo uovu utabakia palepale kwake bilakuendelezwa mbele zaidi. Wauzime ovu kwa mema. Ufalme wa Munguhauendelezwi na vita na mbinu za kimwili wala kweli zake hazilindwi na upanga.Silaha za Mkristo ni za kiroho, ni subira na uvumilivu, uaminifu na upendo.

13:11-18 Mnyama atokaye nchiniNdipo Yohana alimwona mnyama mwingine aliyetoka nchini, mahali pa „mazoea‟ya wanadamu, mahali pao pa kuishi. Kwa hiyo huyu mnyama hasababishimashaka kama yule wa kwanza. Pia alikuwa na pembe mbili tu, na kuonekanakama Mwana-Kondoo, hakuwa wa kutisha na kuogofya kama mnyama wakwanza, ni igizo la kumbeza Bwana Yesu aliye Mwana Kondoo halisi. Aitwanabii wa uongo katika 16:13; 19:20; 20:10; jina la kuonyesha tabia yake nanamna ya kazi yake. Iwapo alionekana mpole, sivyo alivyo, maana hunena kamajoka (Mt.7:15). Alijiunga na mnyama wa kwanza akijitahidi kuwaondoa watukwenye utiifu wao kwa Kristo, hasa kwa kuwashawishi na kuwadanganya.„Anavaa‟ Shetani na uongo wake katika mavazi ya „kweli‟ ili awapotoshe watu.Shabaha yake ilikuwa kuvuta watu ili wamsujudie mnyama wa kwanza. Yeyeanazo nguvu zote za mnyama wa kwanza, anafanya kazi bega kwa bega naye,wala hafanyi lolote lililo kinyume chake. Huyo mnyama ni tofauti sana na Yesu.Autumia uwezo wote wa mnyama wa kwanza. Yesu alikataa kuupokea uwezowa Shetani (Lk.4:6).

Huyo ni ishara ya nini hasa? Wakati wa Yohana katika Dola la Kirumi kundi la„wazee‟ katika miji mikubwa walikuwa na mamlaka ya kuidhinisha na kuongozausimamizi wa ibada kwa Kaisari. Hivyo walisaidia kujenga „ufalme wa upinzani‟juu ya Kristo na kutoa uhalali kwa ibada hizo ambazo kimsingi ziliendeleza ibadaya sanamu na kutoa nafasi kwa watu kuifuata badala ya kumwabudu Mungu wakweli na Kristo wake. Walikuwepo makuhani wengi waliotumika katikakuzisimamisha Ibada za Kaisari. Kazi yao ilikuwa kuwapa watu nafasi ya kufukizauvumba au kumimina mafuta kwenye sanamu ya Kaisari na kusikia ukiri wa watuwa kusema kuwa Kaisari ni Bwana. Ila ishara haiishii hapo tu. Pamoja na hayohuyo mnyama kwa upande fulani si mgeni (Mk.13:22; 2 The.2:9; 2 Pet.2:1-3)aweza kuwa ndani ya shirika za Kikristo. Watu huonekana wapole na wazuri ilahushauri mipango inayoendeleza elimu ya binadamu kuliko Neno la Mungu naushuhuda wa Kristo. Hali hiyo ipo katika ulimwengu wetu wa sasa. Wala si hivyotu, mnyama aliyetoka nchini ni ishara ya itikadi za

Page 94: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1464

watu, dini na filosofia mbalimbali, hekima ya dunia hiyo nk. hizo zaonekana kuwamsaada kwa watu ila zinadanganya watu wasiitambue hali yao halisi ya kuwawenye dhambi na haja yao kubwa ya kumpokea Yesu Kristo aliye pekee niMwokozi wa kweli. Wako manabii wa uongo, dini za uongo, imani za uongo,filosofia za uongo, zimejaa hekima, ila hekima ni ya dunia hii, hazimfikishi mtukwa Mungu wa kweli. Huyo mnyama alisimama mbele ya mnyama wa kwanzatayari kufuata amri yake na kunena kwa mamlaka yake.

Inaonekana Yohana anawashauri wasomaji wake wachunguze zaidi iliwasidanganyike kwa sura ya nje na kwa hila za yule mwovu. Ziko falme mbili,Ufalme wa Mungu na ufalme wa Shetani (ijapokuwa si falme zilizo sawa ila zotezinatafuta utiifu wa wanadamu) na ziko „Utatu‟ wa aina mbili, Utatu wa Mungu(Baba, Mwana, Roho) na utatu wa Shetani (Shetani, Mnyama wa kwanza, igizola kumbeza Kristo na Mnyama wa pili aitwaye pia Nabii wa Uongo, igizo lakumbeza Roho Mtakatifu). Mitume walikuwa wafuasi wa Kristo katika huduma namamlaka waliyopewa (Mdo.1:1-11). Mahubiri ya Mitume yalikuwa na mamlakakwa sababu yalijengwa juu ya Ufufuo wa Yesu na wao kuwa mashahidi wake(Mdo.2:22-36). Mnyama wa pili „alinena‟ kama joka (13:11b; 12b) na kamaMitume walivyoendeleza mamlaka ya Kristo ndivyo alivyofanya mnyama wa pilikwa bwana wake (13:12). Pia mitume walifanya miujiza na ishara (Mdo.2:14-25;5:12; 15:4) kama ishara za Ufalme wa Mungu. Mnyama wa pili naye alifanyamiujiza ya kuleta moto na uhai (ling. 13:12-13 na vifungu vya Matendo). Kwa hiyomnyama wa pili aweza kuwa ndani ya shirika za Kikristo na kujifanya kuwa Mkristo.

k.16ku Kazi yake ni katika dunia nzima naye hufanikiwa sana. Afanya ishara zamaajabu za kuwadanganya „wakaao juu ya nchi‟ yaani wasiomcha Mungu (kamaYesu alivyosema Mt.24:24). Kama maajabu yalikuwa ya kweli au siyo si neno ilashabaha ilikuwa kuwadanganya watu. Katika siku za Yohana ushirikina mwingiulikuwepo (Mdo.13:6ku. 16:16ku; 19:13ku). Makuhani katika hekalu za kipaganizilitumia uchawi na ulozi katika kuvuta watu. Kwa mfano, sanamu ilisimamishwa,wakaifanya inene, na hapa Yohana ametaja jambo la namna hii. Mambo kamahayo yavuta usikivu wa watu na kuimarisha enzi ya Shetani. Watu waliagizwakutengeneza sanamu ya yule mnyama wa kwanza ndipo mnyama wa pili„akapewa‟ kuitia pumzi hata sanamu ikanena. Wote waliokataa kumsujudumnyama waliuawa. Madai ya kutoa uhai ni kufuru kuu kwa sababu kutoa uhai nikazi ya Mungu peke yake (Mt.7:15; 2 Kor.11:14). Yohana hachoki katikakuwakumbusha wasomaji wake kwamba uwezo wa wanyama hao ni uwezo uliona mpaka na nafasi wanazozipata ni zile tu wanazoachiwa na Mungu.

k.15 Ila mnyama hawezi kuwadanganya waumini wa kweli, hao wakubalikuuawa kuliko kumsujudu (Kum.13:1-3). Yawezekana si Wakristo wotewatakaouawa ila kwa sheria zilizokuwapo nafasi ilikuwapo kuwashtaki wakatiwowote.

Page 95: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1465

k.16-17 Halafu twaona kwamba wafuasi wa mnyama watiwa alama kwenyevipaji vya nyuso au katika mkono wa kuume. Ni igizo la kubeza wafuasi wa Kristowaliotiwa muhuri (7:3). Tusiwaze kwamba chapa ilionekana wazi, ila iliashiriakujitoa kwa mwenye mamlaka kama huyo mnyama, dalili ya kuwa mali yake, kwakuwa wameambukizwa tabia yake. Wale waliokataa kuipokea chapa ya mnyamawalipatwa na shida za kuishi pengine walishindwa kupata riziki. „Chapa‟ ilikuwanini hasa, huenda ilikuwa „cheti‟ alichopata mtu baada ya kumtolea Kaisari ibada.Bila cheti mtu hakuruhusiwa kununua chakula nk. Wakristo wa kwelihawakuweza kumtolea Kaisari ibada na kusema kuwa yeye ni bwana kwa kuwaKristo ni Bwana wao. Potelea mbali „chapa‟ iliashiria nini ina maana kwambawenye chapa waliishiriki tabia za mnyama. Tena twapewa kuona upana wautawala wake. Yohana alitaja aina za watu waloihusika kwa kutumia maneno„wadogo kwa wakubwa, maskini kwa matajiri, na walio huru na watumwa‟.

k.18 Kifungu hicho chaanza na mwito wa kuwa na hekima kuhusu hesabu yamnyama aliyetoka nchini. Herufi za Alfabeti zilitumiwa kwa takwimu, kwa hiyo,tumepewa hesabu kwa mnyama. Hesabu yenyewe ni 666, tena Yohana alisemani „ya kibinadamu‟. Ni hesabu ya „ishara‟. Watu wametoa mawazo mengi juu yahesabu hiyo. Wazo moja ambalo lafikiriwa kuwa la kufaa ni kulinganisha nahesabu „777‟ takwimu ya 7 ilikuwa ishara ya ukamilifu na utimilifu, kwa hiyonumbari 7 mara 3 inasisitiza ukamilifu na utimilifu. Hivyo hesabu „666‟ ni isharaya kusisitiza upungufu juu ya upungufu juu ya upungufu. Tofauti kati yaupungufu wa mnyama na utimilifu wa Kristo haitengenezeki. Ipo tofauti mno katiya uongo (wa mnyama) na ukweli (wa Mwana Kondoo). Nje ya Kristo na wokovuwake hakuna tiba kwa dhambi na upungufu wa wanadamu (Rum.3:23). Hamnauponyaji katika itikadi, filosofia, dini, katika kukuza elimu ya binadamu(humanism) nk. Haidhuru wanadamu wafanye nini, bila Kristo, daima upungufuupo. Shetani hufanya juu chini ili watu waendelee kudanganyika na kujidanganyakatika fikira zao. Twajifunza kwamba dini, itikadi, imani, mawazo makuu, filosofiank. za uongo zina nguvu ya kuwapotosha watu na kuwadanganya na ndiyosababu kuzitegemea kwa wokovu ni sawa na kuabudu sanamu, ni kumkuzaShetani si Mungu. Ni vigumu watu kutambua jambo hilo.

MASWALI1. Shetani anasaidiwa na nini na kutumia mambo gani katika kumpinga Mungu?

(a) Mwelezea mnyama atokaye baharini kuwa ishara ya nini?(b) Mwelezea mnyama atokaye nchini kuwa ishara ya nini?

2. Kwa mazingira ya walioandikiwa habari hii ilisema juu ya nini? 3.Toa mawazo kuhusu hesabu „666‟

Page 96: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1466

SURA 14 MAONO MBALIMBALI

14:1-5 Maono ya Mwana Kondoo na WaliokombolewaKama ambavyo tumeona mara kwa mara kwa ghafula badiliko latokea katikamaono ya Yohana. Kuanzia 12:13 mpaka 13:18 tulijulishwa habari za Utatu waWaovu Watatu. Walidhihirishwa kuwa maadui wakuu wa Watu wa Mungu hapaduniani. Walipewa mamlaka ya kuwashinda (13:7) na kuwatongoza watuwengine wote na kuwashawishi kumwabudu Yule Mwovu badala ya Mungu(13:16-17). Kwa hiyo mwisho wa sura 13, kutokana na mbinu za Mnyama wa pili,maoni ya kuwa, kwa upande wa elimu na maadili, hakuna haja ya kuweka msingiwa kumwabudu Mungu yaliingizwa katika mawazo na maisha ya wanadamu.Ndivyo ilivyo hadi leo na vita ipo kati ya Mungu na Yule mwovu hapa duniani. Ilakama ambavyo tumeona tangu mwanzo matokeo ya vita hiyo yameishaamriwahata sifa kuu zilizosikika mara kwa mara zimethibitisha habari hiyo (5:9; 7:10;Zab.98:1-3). Joka ameishafukuzwa mbinguni kutokana na Kufa na Kutukuzwakwa Kristo. Ndiyo sababu Yohana aweza kuleta habari za maono ya tofauti sanakatika sura ya 14. Badala ya picha ya ulimwengu hali umekubali kujiunga na YuleMwovu na kuwa chini yake katika kumpinga Kristo, maono ni ya matokeo yamwisho yatakayotimizwa hapa duniani, kwa sababu yaliyotokea mbinguniyaongoza matokeo ya hapa duniani. Kila wakati Yohana ametuonyesha yambinguni ndipo ya duniani.

Baada ya kuyaona mambo ya kutisha sana, maono ya enzi na nguvu za uovuzikishambulia Kanisa hapo Yohana aona mambo ya kutia moyo yahusuyo enziza utu wema. Alipata maono ya Mwana Kondoo na wafuasi wake juu ya mlimaSayuni, tofauti na mnyama aliyetoka baharini na mnyama aliyetoka nchini.Mwana Kondoo amesimama juu ya Mlima Sayuni, mlima wa Mungu. Vifungu hivivinatukumbusha habari za Zaburi 2. Zaburi hiyo inaanza kwa kusema juu yawaasi wanaojitahidi sana kumzuia Mungu na madaraka yake katika maisha yaobinafsi na katika jamii. Halafu inaendelea katika k.6 kusema juu ya Mungu„Nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu‟. Katika Yoeli2:32 Mlima Sayuni umehusika na wokovu. Neno la faraja ni kuona uheri wawafuasi wa Mwana Kondoo, wakiwa pamoja na Bwana wao, watu mia naarobaini na nne elfu. Hesabu ni ileile ya wale waliotiwa muhuri (7:3). Katika vipajivya nyuso zao jina la Yesu na jina la Baba yake liliandikwa, tofauti na umati wawatu waliokuwa na jina la mnyama (13:16). Jina ni la Baba na Mwana kwasababu hakuna awezaye kumjia Baba isipokuwa kwa Yesu (Yn.14:6-7). Wotewaliotiwa muhuri walifika kwenye Mlima Sayuni, ijapokuwa walishambuliwa vikalisana na maovu ya mnyama wa kwanza na hila za mnyama wa pili, hakuna hatammoja aliyepotea. Tusifikiri hao 144,000 ni baadhi ya Wakristo ambao walikuwawazuri zaidi ya wenzao, la, hesabu hiyo inaashiria Kanisa Zima. Ushindi wa adui(13:7) ulikuwa wa muda mfupi.

Page 97: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1467

k.2-3 Ndipo Yohana aliisikia sauti kutoka mbinguni. Hiyo sauti ilimshangaza hataalipoieleza alitumia tashibihi tatu. Ilikuwa kama „ya maji mengi‟ na kama „ya radikuu‟ dalili za nguvu na mamlaka, tena ilikuwa sauti tamu kama ya muziki „yawapiga vinubi‟ dalili ya furaha. Waliokombolewa waliuimba wimbo mpya mbeleza kiti cha enzi, yaani mbele za Mungu na wenye uhai wanne, na wale wazee.Ni wimbo mpya kwa sababu ya hali zao mpya za furaha na ushindi. Wimbo huoni wimbo wa ukombozi na ni wale tu waliokombolewa wanaoujua kibinafsi.Mungu anawajua na wao wamjua Mungu na Mwokozi wao (2 Tim.2:19; Mt.11;27;Yn.17:20ku). „wamenunuliwa katika nchi‟ ushindi wao watokana na ukombozi waBwana Yesu pale Msalabani.

k.4 Tusifikiri neno „bikira‟ lina maana kwamba hao ni waseja, ambaohawakuoa/hawakuolewa (2 Kor.11:2). Kanisa limefananishwa na Bibi Arusi waKristo aliye mwaminifu kwa Bwana Arusi wake. Neno „bikira‟ ni ishara ya walewaliokuwa waaminifu kabisa kwa Mungu, walikuwa wamejitunza wasijewakanajisika na ibada na desturi za kipagani. Hawakujisalimisha kwa kuridhianana mambo kinyume cha imani yao. Hawakuvutwa na tamaa za dunia hii.Walikataa kumwabudu mnyama na kukiri kwamba Kaisari ni Bwana na kufukizauvumba kwenye sanamu yake. Walikuwa wamejitoa kabisa kwa Kristo nakumfuata kila aendako, maana yake walimtii bila kujali shida walizozipata (13:13;17:2).

„malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo‟ Kwa kawaida neno „malimbuko‟lina maana ya mavuno ya kwanza ambayo yatafuatwa na mavuno menginebaadaye. Kama ni hivyo ina maana kwamba idadi yao itaongezeka ilatumekwishaona kwamba hao 144,000 ni wote waliotiwa muhuri. Ila hasa inamaana kwamba hao ni „toleo‟ kwa Mungu, ni lugha ya kidhabihu kuonyeshakwamba walimtumikia Bwana wao kwa kujitoa kama dhabihu (Rum.12:1-2;Yak.1:18). Hasa walijihesabu kuwa mali ya Mungu. Yawezekana Yohanaaliwaza mashahidi ambao watasababisha mavuno makubwa, kama Tertulianoalivyosema zamani „damu ya mashahidi ni mbegu ya Kanisa‟. Vilevile BwanaYesu alisema „chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyohiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi‟ (Yn.12:24).

Mkazo ni juu ya usafi wao, uhusiano wao na Mungu, watu waliompenda Munguna kumfuata Yesu sawasawa (Yer.18:13-15; Hos.5:4; Ebr.12:2; Yoh.14:26).Walikuwa watu wa kweli, zaidi ya kusema kweli, walikataa kabisa kulogwa nahila za Shetani na kudanganywa na uongo wake na kutongozwa na dunia.Hawakuwa na hatia, kazi njema iliyoanza ndani yao hapa duniani itaendelezwana kutimilika (1 The.5:23-24; Flp.1:6). Tusiwaze kwamba Sayuni ni mahali, nineno la kueleza „uhalisi wa kiroho‟ (Ebr.12:22; Efe.2:6; Yn.4:20-24).

Page 98: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1468

14:6-13 Maono ya Malaika watatuKatika sehemu hiyo Yohana aliwaona malaika watatu, kila mmoja alikuwa natangazo, moja la neema, moja la hukumu ya Babeli, na moja la onyo juu yamatokeo makali ya kuikataa Injili. Budi matangazo hayo yazingatiwe. Hamnahaja kwa malaika kuruka kati ya anga katika siku za mbele, kwa sababu maonyoyaliyomo ulimwenguni kutokana na ujumbe wa malaika hao yafaa wakati wotehata mpaka mwisho wa nyakati.

k.6-7 Malaika wa kwanza alikuwa na Injili ya milele ya kuhubiriwa ulimwengunikwa „hao wakaao juu ya nchi‟ yaani kwa wale ambao wamestarehe na kutuliahapa duniani hali wamelogwa na mivuto yake tofauti na wale 144,000waliokombolewa (k.3) Mnyama alidai kuwa na madaraka juu ya ulimwengumzima, madai ya uongo, madai matupu, ila watu walishangazwa na jinsialivyoonekana kuwa na uwezo. Ila yupo aliye na uwezo wa kweli, Muumba wakweli, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. Yeye ndiyemwenye madaraka ya milele juu ya ulimwengu mzima. Hii ni habari njema kwawamchao Mungu hata kwa adui za Mungu, kwa sababu Mungu ni wa milele siDola la Kirumi na Kaisari wake ambaye ni wa muda tu. Wale wakaao juu ya nchiwapaswa wautambue ukweli huo kabla ya saa ya hukumu. Hii ni Injili kimsingi(Mdo.14:15) ni Injili ya milele kwa sababu ni Injili kwa kila wakati na kila mahalina imesimama katika tabia na makusudi ya Mungu yasiyobadilika. Mungu niMuumba na Mhifadhi wa ulimwengu. Joka na wanyama wasaidizi wake niwaharibu na hukumu yao italingana na jinsi walivyofanya (Rum. 1:24,26,28).Jambo moja kubwa la maana sana ni kwamba hukumu itawaondoa waharibuwote ili makusudi mema ya Muumba yasimame. Malaika aliwaita watu waujaliukweli wa Mungu kuwa Muumba na Mhukumu kwa kumwabudu na kumcha.Kama hawatamtukuza kwa hiari watalazamika kufanya wakipenda, wasipende.Ni habari njema kwa waumini walioteswa kujua kwamba watesi wao wataitwakutoa hesabu ya ukatili wao na ya kuwa muda wao umeishaamriwa,hawataruhusiwa kuendeleaendelea.

k.8 Habari njema iliendelea katika tangazo la malaika wa pili aliyetangazakuanguka kwa Babeli, ule mji mkubwa. Kila mara Babeli umetajwa kuwamkubwa. Malaika alitangaza anguko lake kana kwamba limekwisha kutokea, naalifanya hivi kwa sababu ya uhakika wake. Yohana anayo mengi zaidi kusemajuu yake katika sura ya 18. Twakumbushwa habari za Mnara wa Babeli katikaMwanzo 11. Babeli ni ishara ya kiburi na uasi wa kibinadamu, watu wakijiungapamoja na kupanga na kuendesha maisha yao bila kumjali Mungu na amri zake,wakifanya mapenzi yao si mapenzi ya Mungu. WaMataifa wote wamelogwa naBabeli, yaani na dunia, wamevutwa na uzuri na anasa zake, wamedanganywana kumetameta kwake na umalidadi wake. Kwa sababu hiyo ama kwa sababuwameshindwa kutoka kwake au kwa sababu hawataki kuachana naye hawauitikiiwito wa Injili na kumwamini Kristo. Ila Mungu anao watu wengine, jamii iliyo heriya wale wote ambao wamejitoa

Page 99: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1469

kumpenda, kumcha na kumtii Kristo. Tusiwaze Babeli kuwa mji fulani, bali nitamathali ya watu kujiunga pamoja na katika kiburi cha kumwasi Mungu. Babelihutongoza na kuwashurutisha watu kwa kuwapa „mvinyo‟ na mvinyo hiyohuwafanya wasiwe waaminifu kwa Mungu Muumba wao. Ni mfano wa mleviambaye hatapona ulevi wake mpaka mvinyo unaomlevya utakapokosekana.Wakati wa Yohana Babeli ulikuwa Rumi, lakini wakati wote Babeli upo na wakatiwote Babeli huhukumiwa (Yn.3:19). Utakapoanguka ndipo watu watawekwahuru mbali na mivuto yake. Hasa hukumu ni juu ya „Babeli‟ ila wale waliokazanakumpenda Babeli wataishiriki hukumu yake ambayo italingana na hali yao, waowalikunywa mvinyo ya Babeli nao watakunywa „mvinyo ya ghadhabu yauasherati wake‟ yaani hukumu kali ya Mungu. Ila kama Waisraeli waliokuwautumwani huko Babeli waliwekwa huru na kurudi makwao vivyo hivyo „wa Babeli‟watawekwa huru Babeli utakapoanguka nao wataweza kumrudia Mungu wakweli na kumwabudu jinsi iwapasavyo na kwa jinsi imstahilivyo.

k.9:12 Malaika wa tatu alifuata na kwa sauti alitoa onyo kali kwa yeyoteamsujudiaye mnyama na kuipokea chapa yake. Alisema kila mmoja waoatakunywa katika „mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipokuchanganywa na maji....atateswa kwa moto na kiberiti mbele za malaikawatakatifu na mbele za Mwana Kondoo‟. Lugha hii inatukumbusha hukumuiliyowapata watu wa Sodoma na Gomora zamani za kale. Hapo dunianighadhabu ya Mungu imechanganywa na neema, jinsi Bwana Yesu alivyosema„Mungu huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye hakina wasio haki Mt.5:45). Ila katika jehanum ni ghadhabu tupu. Hamna usalamawowote kwa wale wanaompa mnyama utiifu wao, ambao wakataa kabisa kutubuiwapo mara kwa mara wameitwa kutubu kwa njia ya Injili kuhubiriwa na kwamaonyo waliyopata kwa njia ya hukumu zilizotangulia, maana hizo zililengakuwaleta watu kwenye toba. Iwapo lugha iliyotumika ni lugha ya tamathali, niishara ya jambo la kweli ambalo hali yake halisi itazidi kwa ukali hata ukali walugha iliyotumika. Ni dalili ya hukumu nzito, watavuna matokeo ya dhambi zao(walizozifurahia hapa duniani) milele na milele, wala hawatapata nafasi za tobatena zitakapopita siku za neema. Mambo hayo yatatokea mbele za MwanaKondoo na malaika zake watakatifu, yaani hayo yatawapata wakiwa katika haliya kujua vizuri kwamba Kristo alikufa Msalabani kwa ajili yao, naye angaliwezana alitaka sana sana kuwaokoa. Mvinyo itakuwa bila kuchanganywa na maji,yaani bila kupunguziwa nguvu yake, kwa sababu hukumu zilizotangulia zilikuwa„fadhili za Mungu‟ kwao, zilitoa nafasi ya toba, ila hukumu ya mwisho haitakuwana nafasi ya toba. Ni hukumu za haki, zafanyika machoni mwa Mwana Kondoona malaika zake watakatifu wasio na wasiwasi wowote juu yake. Wapatwao nahukumu hiyo wataumia zaidi watakapomwona adui yao Mwana Kondoo katikautukufu wa ajabu pamoja na wafuasi wake waaminifu. Ingawa hiyo hukumuinaonekana kama bado, hata hivyo, ipo tayari.

Page 100: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1470

Ni vema tukumbuke ya kuwa hukumu hiyo itawapata kwa sababu wamekazanakumsujudia mnyama na kumsukumia mbali Kristo aliyewafia kwa upendo waajabu. Kwa Yohana mbinguni ni pazuri mno hata hapaelezeki kwa uzuri na rahana furaha yake. Vilevile kunyimwa kufika mbinguni ni hasara kubwa isiyoelezeka.Ghadhabu ya Mungu ni hasira yake takatifu iliyokazwa daima juu ya dhambi.Neno hilo litawatia Wakristo moyo wa kudumu kuwa waaminifu kwa Kristo nakufanya uinjilisti wa kuwavuta watu iwapo kwa kufanya hivi watavuta chuki nahasira ya Shetani.

k.12 Bila shaka Yohana alikuwa akiwaza Wakristo katika makanisa sabawaliojaribiwa kuridhiana na kumfuata Kristo nusunusu ili wasiteswe kwa imaniyao. Upendo na uaminifu wao kwa Kristo ulimkasirisha Shetani na bila shakawengine walijaribiwa wanyamaze na waifiche nuru yao. Yohana aliwaza kwambani vema waumini wapime mambo kwa sababu ni afadhali sana kumtii Kristokikamilifu, hata ikiwa tokeo lake ni maudhi na kifo kuliko kujisalimisha nakutokutia maanani hukumu ya mwisho. Twaweza kufumba macho kwa habari yajehanum ila kwa kufumba macho hakuondoi uhalisi wake. Wakristo walihitajisubira hali wakiendelea kuzitii amri za Mungu na kumshuhudia Kristo. Hamnahasara katika kumtumikia Bwana (1 Kor.3:14; 15:58). Kila kundi la watu lapatahaki yake; „wa Babeli waishiriki hukumu yake‟ na „wa Kristo waushiriki ushindi nautukufu wake‟.

k.13 Katika Kitabu hicho zipo heri saba, na hapa tunayo mojawapo. „heri wafuwafao katika Bwana tangu sasa‟. Ni neno la faraja kwa wale waliokabili kifo kwaajili ya imani yao, wala si kwa hao tu, ni kwa wote watakaokuwa waaminifu hatakufa kwa ajili ya Bwana wao. Heri hiyo inahusu „wafao katika Bwana‟. Kifokitawaletea pumziko na raha mbali na maumivu na majaribu yao. Matendo yaomema yatawafuata. Twaokolewa kwa neema si matendo mema ila shabaha yakuokolewa ni kutenda matendo mema (Efe.2:8-10). Roho anatia muhuri manenoya Yohana, ni hapa tu na katika 22:7 Roho ametajwa isipokuwa katika zile baruasaba.

14:14-20 Mavuno - Hukumu ya mwisho

Inaonekana habari hii inahusu hukumu ya mwisho ikielezwa kwa mfano wakuvuna. Mavuno mawili yametajwa, na ni vigumu kujua kama ni hukumu mbili,moja ya wenye haki na moja ya wasio haki, au ni hukumu moja ikirudiwakuelezwa zaidi katika mavuno ya pili.

Yohana aliona wingu jeupe na juu ya wingu ameketi mmoja mfano waMwanadamu, mwenye taji ya dhahabu kichwani, na katika mkono wake alishikamundu mkali. Alikuwa ameketi juu ya wingu jeupe.

Ndipo Yohana alimwona malaika aliyetoka katika hekalu, naye alimlilia kwa sautikuu yule aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu. Malaika akamwambia autie munduwake na kuvuna kwa sababu mavuno yamekomaa, naye akafanya hivyo.

Page 101: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1471

Huyo aliyekuwa mfano wa Mwanadamu juu ya wingu jeupe alikuwa nani? Kwajinsi alivyoelezwa anaonekana kuwa Kristo (Dan.7:13). Ila kwa upande mmojani tatizo kukubali kuwa ni Kristo kwa sababu imesema aliagizwa na malaika nani vigumu kufikiri kwamba Kristo aweza kuagizwa na malaika. Twaona malaikaalitoka hekaluni, ishara ya Kuwako kwa Mungu, na alileta ujumbe wa mapenziya Mungu wa kusema kwamba wakati wa kuvuna umefika. Kwa hiyo ni Munguhasa anayemwagiza Kristo kwa njia ya huyo malaika. Kama Kristo ni mvunajitwakumbushwa maneno yake aliposema kwamba hakujua saa ya Kurudi Kwake(Mk.13:32; Mdo.1:7) ila wengine wanasema maneno hayo yalimhusu alipokuwahapa duniani, hayamhusu kama Mwana Kondoo aliyeketi na Baba katika Kiti chaEnzi. Kwa hiyo ni vigumu kusema kwa uhakika, ila neno tunalojua kwa hakika nikwamba Kristo anahusika kabisa na hukumu ya mwisho (Mt.24:32; Mk.13:27).Pengine mavuno hayo ya kwanza ni mavuno ya wenye haki, Kristo akijakuwachukua Kwake watu wake (1 The.4:15-17). Kuvuna kutawaokoa na aduizao Joka, mnyama wa kwanza, mnyama wa pili, na Babeli/Kahaba mkuu.

k.17 Ndipo malaika mwingine alitoka katika hekalu lililoko mbinguni. Huyoalikuwa na mamlaka ya Mungu ya kuitekeleza hukumu yake maana alikuwa namundu mkali (Yoe.3:13). Ndipo malaika mwingine mwenye mamlaka juu ya motoakatoka katika ile madhabahu akamlilia yule malaika mwenye mundu nakumwambia autie mundu wake mkali na kuvichuma vichala vya mzabibu kwasababu zimeiva sana. Ni mavuno ya mizabibu. Madhabahu ni ukumbusho wa8:3-5 jinsi Mungu alivyoyajibu maombi ya waaminifu wake kwa kumiminahukumu zake juu ya nchi. Kwa hiyo hukumu kali ya mwisho ni jibu lake la mwishokwa maombi yao.Zabibu zilitupwa katika shinikizo kubwa la ghadhabu ya Mungu, ukali waghadhabu ya Mungu waonekana katika kuimithilisha na desturi ya zamani zileya kukanyaga zabibu ili maji/damu yake itoke. Kwa mavuno yote mawili twasomamavuno yalikuwa tayari, kwa hiyo, ina maana kwamba hukumu ilifanyika wakatiwa kufaa, wakati uliotimia, wakati ulioamriwa na Mungu, wakati wa dhambi zawanadamu kuufikia upeo. „mwendo wa maili mia mbili‟ ni hesabu ya kuashiriautimilifu wa hukumu juu ya ulimwengu mzima, haitakuwa ya nusunusu, walahakuna atakayeiepa. Neno „mavuno‟ latufundisha kwamba hukumu zote zaMungu zinafuata kanuni moja, zinalingana na „upandaji‟ wa mtu yaani kwa jinsialivyoishi. Hukumu zinauthibitisha ushindi kamili wa mwisho wa Mungu juu yaadui zake wote na upinzani wote ambavyo alikuwa ameishashinda paleMsalabani. Enzi zote za uovu na waovu wote wataangamizwa kabisa kabisa.

MASWALI1. Katika sura 14 Yohana aliona maono ya kuwahusu watu gani na hali yao?2. Malaika watatu walileta matangazo matatu. Yalikuwa nini?3. Mavuno ni mavuno gani na ya wakati gani?

Page 102: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1472

SURA 15 MAONO YA VITASA SABA VYA MAPIGO

15:1 Yohana alitangaza kwamba aliona ishara nyingine katika mbingu iliyokubwa na ya ajabu. Aliona nini? Aliona malaika saba wenye mapigo saba yamwisho. Katika hayo mapigo ghadhabu ya Mungu imetimilika. Vitasa hivivyafuata baragumu zilizolia kwa kuwaonya watu watubu. Haikubaki nafasi yatoba kwa watu ambao hawakuyajali maonyo makali yaliyotoka kwa Mungu.Kama ni mapigo saba ya mwisho ni vema kufikiri kwamba muda wa mapigohayo ni uleule wa muhuri saba na baragumu saba, maana vitasa vina hukumunzito zaidi kwa sababu watu hawakutubu. Hivyo, katika mwenendo wa historiaMungu huleta hukumu zake na uzito wao huzidi kulingana na ugumu wawanadamu wanaokataa kutubu. Muhuri na baragumu na vitasa ni mambomamoja. Mpiga picha apiga picha kutoka upande fulani ndipo upande mwingine,kwa ukaribu na kwa mbali, kwa kuingiza mazingira au siyo. Ndivyo ilivyo namuhuri na baragumu na vitasa, jambo la hukumu latazamwa kutoka upande huuhalafu kwa upande mwingine.

Yohana alisema ishara ilikuwa kubwa na ya ajabu kama matendo ya Munguyalivyoelezwa kuwa (k.3) kwa sababu ghadhabu yake hufikia lengo lake katikahukumu ya mwisho. Mkazo ni juu ya mwisho. Wakati wote tukumbuke Kitabukimeandikwa kwa waumini katika makanisa si kuwataarifu waasi juu ya mamboyatakayowapata. Shabaha ilikuwa kuwafariji na kuwatia moyo ili wadumuwaaminifu wakati wa kujaribiwa kwao.

15:2-4 Kipengele: Picha ya Washindi hali wamefika salamaMara baada ya kutayarisha njia kwa hukumu za vitasa, ambazo zitaelezwa mojamoja baadaye, Yohana ameweka kipengele kama tulivyoona katika sura ya sabana tena katika 10:1-11,13. Katika nafasi hiyo twapewa picha ya washindi, watuwa Mungu, ambao wamepitia katika magumu mengi, wamehitimu mtihani waowa majaribu makali na kufika salama salimini kwa Mungu. Aliona kitu kamamfano (hakusema ilikuwa) wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto. Iliashirianini? pengine ni ishara ya hali ya Mungu na jinsi anavyozidi mno kwa uzuri nausafi wake. Pia yawezekana ni ishara ya hukumu, na maneno „iliyochangamanana moto‟ huenda yanadokezea damu ya mashahidi iliyomwagika. Kandokandoya bahari ya kioo washindi walikuwa wamesimama. Walikuwa upande waMwana Kondoo na kinyume cha Joka na wanyama na vitisho vyao namashawishi yao. Ni ukumbusho wa Wana wa Israeli wakati wa kuivuka Bahari yaShamu wakifuatwa na Wamisri. Ndipo walipofika salama ng‟ambo ya bahariwaliuimba wimbo wa kumsifu Mungu kwa wokovu wao wa kimwili (Kut.15;Kum.32). Kwa njia ya uaminifu wao kwa Kristo waumini katika makanisa saba„wamemtoroka‟ mnyama. Kwa vinubi walivyopewa na Mungu (waliokolewa kwaneema si kwa ustahili wao) waliuimba wimbo wa Musa na wa Mwana Kondoo.Yesu alikuwa amewaokoa kweli na kuwaweka huru mbali na dhambi zao.Waliyafurahia sana matendo

Page 103: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1473

makuu ya Mungu na kuzikiri njia za Mungu kuwa za haki na kweli. Yeye ndiyeMfalme juu ya mataifa. Twaambiwa jinsi waumini wa kweli walivyomwaza Munguwalipoziona hukumu zake. Hawakusita wala hawakuona wasiwasi juu yake,waliunga mkono na yote yaliyotendeka na kuyafikiria kuwa sawa kabisa(Kum.32:4). Mungu huendelea kuwaokoa watu wake kizazi baada ya kizazi.

k.4 Ndipo changamoto ilitolewa. Swali liliulizwa. „Ni nani asiyekucha, Ee Bwanana kulitukuza jina lako?‟ (Yer.10:7). Sababu tatu zilitolewa katika kulijibu swalihilo. Sababu ya kwanza ni kwamba Mungu ni Mtakatifu. Yeye ni wa pekee, walahakuna mwingine aliye kama Yeye, hakuna anayemkaribia hata kidogo(Zab.99:3). Sababu ya pili ni kuwa Yeye asujudiwe na mataifa yote kwa sababuni Yeye peke yake aliye na madaraka juu yao (Zab.86:9). Sababu ya tatu nikwamba matendo yake ya haki yamefunuliwa, kazi zake zinamthibitisha kuwamwenye haki katika njia zake zote (Zab.98:2). Washindi walimpa Mungu sifazote, hawakusema lolote juu yao wenyewe, hawakutaja uzuri wala uaminifu wao.

15:5-8 Malaika saba kupewa vitasa vya mapigoBaada ya kuivuka Bahari ya Shamu, Waisraeli wakaja mpaka Mlima Sinai mahaliwalipopewa mbao mbili zenye amri kumi. Hiyo Torati ilishuhudia haki na utakatifuwa Mungu. Kama ambavyo tumeishaona Yohana alivutwa sana na jambo la„ushuhuda‟ na hapo aliona hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa(11:19). Maana yake nini? Jangwani Hema ilishuhudia Kuwako Kwa Mungu katiyao, na Mbao mbili zilishuhudia jinsi Mungu alivyo kinyume cha dhambi. Nidhambi peke yake ivutayo ghadhabu ya Mungu. Ina maana kwamba watuwasipoiitikia neema ya Mungu katika Injili, basi, watakutana na Torati na madaiyake, wala hakuna atakayeponyoka, maana hakuna mwenye haki hata mmoja,hakuna awezaye kuyatimiza madai ya Torati (Rum.3:10.23). Wakati wa rehemautakuwa umepita.

k.6 Yohana ametilia mkazo jambo la hao malaika saba kuwa wametoka kwaMungu aliye Mtakatifu. Kwanza walitoka hekaluni (ishara ya Kuwako kwaMungu), wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung‟aa, mavazi ya ukuhani,wamefungwa vifuani mishipi ya dhahabu, dalili ya utakatifu na ya ushirikiano waona Mungu Mtakatifu, wakapewa vitasa saba vya dhahabu na mmoja wa walewenye uhai wanne, hao walikuwa karibu sana na Mungu. Vitasa vilijaa ghadhabuya Mungu ambaye ameelezwa kuwa „hai hata milele na milele‟. Ghadhabu yaMungu haina hali yoyote ya dhambi, haiji kwa haraka bali kwa utaratibu; hainatamaa ya kibinafsi ndani yake; inatoka kwa utakatifu wake na mzigo wake ni kwausawa, uadilifu na haki kufanyika. Agano lake ni msingi wa kuwapatia wale waliowaaminifu kwake haki na watesi wao hukumu. Maonyo hayo si maonyo yamaneno tu, yatoka kwa Yeye aliye hai milele na milele (Ebr.10: 31; Lk.12:4,5;Isa.33:14).

Page 104: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1474

k.8 Hapo tena Yohana ameukaza utukufu na uweza wa Mungu, alisema hekalulikajazwa moshi. Ndipo akataja kwamba hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia mlendani mpaka mapigo saba yamepigwa na malaika saba. Musa hakuruhusiwakupaingia Patakatifu wakati wa kupaweka wakfu (Kut.40:34) wala Sulemaniwakati wa hekalu kuwekwa wakfu (1 Waf.6:10; ling. Isa.6:4; Eze.44:4). Huendaina maana kwamba mapigo hayazuiliki, au pengine maana yake ni kwambahukumu zi karibu kabisa na mpaka zimepita hakuna awezaye kustahimiliKuwako kwa Mungu au pengine ina maana kwamba kwa sababu ni siku zahukumu, hamna nafasi kwa maombi wala toba wala upatanisho (Zab.77:9).

Yawezekana vitasa ni ukumbusho wa chetezo cha kushusha hukumu kama jibula Mungu kwa maombi ya watu wake (8:2-5). Ni mmoja wa wale wenye uhaiwanne aliyewapa malaika vitasa. Ikiwa yeye anawakilisha maumbile ni isharakwamba Mungu atayatumia maumbile kuwa chombo cha kuzitekeleza hukumuzake. Hakuonyesha wasiwasi kwa sababu alijua hukumu za Mungu ni kweli nahaki.

MASWALI1. Kabla ya maono ya vitasa saba Yohana alipewa maono gani?2. Maono hayo yalikuwa kwa ajili ya nani? na kwa shabaha gani?3. Waumini walionaje hukumu za Mungu?

SURA 16 VITASA SABA VYA GHADHABU YA MUNGU

Hayo tunayosoma juu ya vitasa yatukumbusha mapigo juu ya Misri. Piayatukumbusha habari za baragumu za maonyo (8-11). Hata hivyo vitasavyatofautiana na mapigo ya Misri na hukumu za baragumu. Katika mapigomatano ya kwanza juu ya Misri watu hawakuguswa; vilevile katika baragumunne za kwanza watu hawakuguswa. Katika hukumu za vitasa, tangu mwanzowatu wameguswa. Pia katika baragumu nne za kwanza mpaka uliwekwa,theluthi moja ya nchi, bahari, maji, mwanga, iliguswa, lakini kwa vitasa mpakahaukuwekwa. Kwa hiyo, hukumu hizo zaonekana kuwa za baadaye si zakwanza, ni hukumu za adhabu za mwisho. Ni hukumu juu ya ulimwengu mzimaishara ya ushindi mkuu wa Mungu juu ya maovu yote. Iwapo hukumu hizo ninzito hata hivyo inaonekana nafasi ilikuwapo kwa toba, kwa sababu mara kwamara Yohana alitaja kwamba wanadamu hawakutubu (k.9,11,21).

k.1 Sauti kuu ilitoka hekaluni, Yohana hakusema ilikuwa sauti ya nani.Yaonekana ni ya Mungu Mwenyewe, maana katika 15:8 tulisoma kwambahakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia mle ndani. „ilitoka hekaluni‟ ishara ya kuwahukumu hizo zilitoka kwa Mungu. Ni tangazo maalumu la kuja kwa hukumunzito za mwisho. Katika 15:7 malaika walipewa vitasa ila hawakuvimiminampaka walipoamriwa.

Page 105: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1475

16:2 Kitasa cha kwanzaMalaika wa kwanza alikimimina kitasa chake juu ya nchi. Watu walipatwa namajipu mabaya. Ni watu gani walioguswa? Ni wale wenye chapa ya mnyama nawale walioisujudia sanamu yake, yaani wale waliojitoa kufanya maovu. Ni isharakwamba wale wafanyao maovu wataadhibiwa. Wengine hawakuguswa. Niukumbusho wa majipu yaliyowapata Wamisri (Kut.9:9-11).

16:3 Kitasa cha piliMalaika wa pili alikimimina kitasa chake juu ya bahari, ndipo ikawa damu kamadamu ya mfu na vitu vyote (si theluthi 8:8) vyenye uhai katika bahari vikafa.

16:4-7 Kitasa cha tatuMalaika wa tatu alikimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji,zikawa damu (Ling.Kut.7:17-21). Hapo hatuambiwi juu ya kufa kwa watu auviumbe. Labda ni kwa sababu hukumu nyingine zilifuata kwa haraka. Bila majihakuna kiumbe awezaye kuishi. Ila Yohana ametaja jambo jingine la maana.Malaika wa maji hakusikia uchungu bali alimwunga mkono Mungu na hukumuzake na kushuhudia haki, utakatifu na umilele wake. Hukumu zilikuwa za hakikwa sababu zililingana na udhalimu wa watu waliowaua watumishi wa Mungu.Walivuna walichopanda, nao waliistahili adhabu yao. Pengine liko wazo lakudokezea kwamba waovu wamefitinika wao kwa wao nao wameanzakumegana na kuuana. Hata madhabahu „ilisema‟ na kuunga mkono maoni yamalaika wa maji juu ya hukumu hizo. Madhabahu ni ishara ya uhusiano kati yamaombi ya watakatifu na moto wa Mungu (8:3: 14:18). Hayo yote yatilia mkazojuu ya njia za Mungu kuwa za haki na kweli (15:3). Uumbaji ulioguswa nakuumizwa huunga mkono Mungu na hukumu zake, umekuwa radhi kuwachombo cha hukumu hizo. Kwa hiyo ni Vitu vya asili pamoja na watu wa Munguwaliokubali kwa moyo hukumu zake.

16:8-9 Kitasa cha nneMalaika wa nne alikimimina kitasa chake juu ya jua na tokeo lake lilikuwawanadamu kuunguzwa vibaya sana hata wakalitukana jina la Mungu. Twaonaneno „likapewa kuwaunguza‟ ukumbusho wa Mungu kuwa juu ya vitu hivi. Juahalina mamlaka lenyewe ya kufanya neno. Hapo nyuma watu hawakujali kwakuwa hawakusikia maumivu kutokana na mipaka iliyowekwa (6:12; 8:12; 9:2).Katika tarumbeta ya nne nguvu ya jua ilipunguzwa kwa theluthi moja (8:12) lakinikwa vitasa nguvu ya jua imezidi mno kiasi cha watu kuunguzwa. Ingawa watuwaliweza kuona mkono wa Mungu katika jambo hilo, hata hivyo, walikataakutubu, na badala ya kutubu na kumtumkuza Mungu wakamtukana. Kamawangalitubu wangalimtukuza Mungu. „wakalitukana jina la Mungu aliye namamlaka juu ya mapigo hayo‟ kwa maneno hayo Yohana amekaza uhusiano katiya Mungu na mapigo na mamlaka yake katika matukio hayo yote. Mpaka haponi mnyama tu aliyekufuru (13:1,5,6; 17:3) ila tangu sasa wale

Page 106: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1476

wamtumikiao mnyama pia wamkufuru Mungu (k.9,11,21). Wameambukizwatabia zake. Neno hilo latuonyesha kwamba shabaha ya hukumu za Munguilikuwa kuleta watu kwenye toba.

16:10-11 Kitasa cha tanoMalaika wa tano alikimimina kitasa chake „juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama‟na giza lilitokea katika ufalme wake, wakatafuna ndimi zao kwa sababu yamaumivu nao walimtukana Mungu kwa sababu hiyo na kwa sababu ya majipu.Hata hivyo, hawakuyatubia maovu yao. Hayo yote ni ishara ya nini? Kwa maraya kwanza „mnyama‟ mwenyewe ameshambuliwa na ufalme wake umeguswa.Hapo nyuma wafuasi wake waliguswa nao wataendelea kuguswa. Yawezekanani ishara ya fitina na kutoafikiana kutokea katika jamii za watu, ufa ukitokeakatika uhusiano wa wao kwa wao na watu watengana kwa kuwa ndoto zao zaraha na mafanikio zatoweka, maana bila kumkubali Mungu na sheria zakehamna mafanikio ya kweli, haiwezekani kujenga „paradiso‟ kwa kumpa Mungukisogo. Watu wanaolichagua giza badala ya nuru watakuta kwamba uchaguziwao unatiliwa muhuri na Mungu, watapatwa na giza la ghadhabu ya Mungu(Yn.3:19-21). Pengine giza ni ishara ya nguvu kupungua na udhaifu kuonekanakatika „ufalme wa yule mwovu‟ kwa kuwa taratibu za kuishi kijamii zinaharibika.Itakapotokea hivi watu watausikia uchungu sana mioyoni mwao. Sikitiko kubwani kwamba badala ya kutubu kwa kumgeukia Mungu na kuyaacha maovu yaowalizidi kumtukana. Hayo yote huthibitisha kwamba mfumo wa Jamii wasiomjaliMungu hauwezi kufaulu. Mungu anaunda mfumo mwingine wa Jamii ya watuambao wamemkubali Kristo na kumpa Yeye utiifu wao kwa kuishi kwa kanuni yaKumpenda Mungu na kumpenda jirani kama nafsi yao. Mfumo huo utafaulu kwasababu tabia zao zitakuwa kama mafuta ya „kuendesha‟ Jamii hiyo. Yohanaamekaza giza na maumivu yao makali (ling. na Baragumu ya 5 9:lku.5ku). Hatamaumivu makali hayawaamshi watu waitambue hali halisi iliyopo na hatari yahukumu ya Mungu.

„kiti cha enzi cha yule mnyama‟ ni ishara ya mpango maalum wa Shetanikujiingiza katika muundo wa Jamii ulioundwa na Mungu na kwa nia mbayakuupotosha kama njia mojawapo ya kulitimiza lengo lake la kumpinga Mungu.Katika Kitabu cha Danieli kuna mengi yanayoonyesha upinzani kati ya „mnyama‟(falme na tawala za dunia hii) na Mungu na Ufalme wake. Kuna habari ya mtimkubwa na sanamu kubwa ya falme kubwa kuangushwa. Ufalme wa Belshazzaulihesabiwa na kukomeshwa. Wanyama wakubwa wenye uwezowalinyang‟anywa utawala (Dan.2:35ku. 4:14ku. 7:12ku) na hayo yote yalitokeaili watu wajue ya kuwa Mungu Mwenyewe anatawala katika falme za dunia. Kwasababu watu hawakubali kwamba Mungu anayo haki kabisa ya kuwaongozawatu walikosa kuzionja rehema zake. Wale wanaopotea wameshindwakuyahuzunikia kwa dhati makosa yao, wamezidi kulichukia neno la haki, ambalohaki mojawapo kubwa ni haki ya Mungu kuwahukumu.

Page 107: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1477

16:12-16 Kitasa cha sitaMalaika wa sita alikimimina kitasa chake. Yohana amesema mengi zaidi juu yakitasa hicho cha sita kuliko vile vilivyotangulia. Ni matayarisho kwa mambo yamwisho. Kitasa kilimiminwa juu ya mto mkubwa Frati. Mto huo ulitajwa katikahabari ya tarumbeta ya sita (9:13-15). Maji yake yakakauka, ili njia itengenezwekwa wafalme watokao katika maawio ya jua. Ni vigumu kusema kama habarihii inahusu wafalme wa kweli watakaotokea kihistoria au ni kutaja habariinayotokeatokea katika historia. Hatuambiwi kama walikuja au siyo, maanahawatajwi tena. Wengi waliamini kwamba Nero atatokea tena na kuwaongozaWaparthi walioishi mashariki nao watalishambulia Dola la Kirumi. Kwa jinsiYohana alivyoandika inaonekana jambo hilo litatokea, ila haitakuwa Nero balimtawala mwingine wa kutisha sana na Wakristo watateswa sana kwa mara yamwisho. Ni kama timizo la mwenendo wa historia yote, Shetani daima humpingaKristo, Shetani ni nyuma ya watawala wanaotokeatokea wakishambulia Kanisana wafuasi wa Kristo, na hali hii itaendelea mpaka atakapotokea yule mtawalaau kundi la watawala watakaojiunga na kufanya hivyo kwa mara ya mwisho.

k.13 Halafu Yohana aliona roho tatu za uchafu mfano wa vyura (Kut.8:3) na hizoroho zilitoka katika kinywa (kinywa - ishara ya usemi wa kuwashawishi nakuwadanganya watu) cha yule joka (Shetani 12:3,9) na katika kinywa cha yulemnyama atokaye baharini (ishara ya enzi za ulimwengu huu 13:1,7) na katikakinywa cha yule nabii wa uongo (mnyama atokaye nchini, ishara ya dini nafilosofia za uongo 13:11). Hao ndio maadui wakubwa wa Kristo na Kanisa. Vyurani ishara ya uovu, hawana uvuto, ni chukizo, ni wachafu, nao wafanya kelele bilakutimiza lolote. Roho hizo zilitoka katika kinywa, ishara ya aina ya kazi yao,kutumia maneno ya kuwashawishi na kuwadanganya watu (Ling. na 1Waf.22:21-23; Zab.2:2). Ni ishara ya kuwa iwapo uovu waonekana kuwa nanguvu, na wa kutisha sana, hata hivyo, mwishowe hautatimiza lolote, hautafaulu.Halafu Yohana alisema kwamba hizo roho ni za mashetani zifanyazo ishara nazoziliwaendea wafalme ambao waweza kuwa wale wafalme kumi wa 17:12ku.Katika Agano la Kale matendo makuu ya Mungu yalihusika na kukaushwa kwamaji, Bahari ya Shamu (Kut.14:21) Mto Yordani (Yos.3:16ku) pia yalitajwa katikaunabii (Isa.11:15; Yer.51:36; Zek.10:11). Hofu zote za watu zitatimizwa.Haidhuru ni za nini hasa, ni wazi kwamba ni ishara ya nguvu za uharibifuzimpingazo Mungu. Ila tusifikiri Yohana anataja hofu za watu wa wakati ule tu.Utakapokaribia mwisho wa mambo yote, nguvu za uovu, hata ikiwa zimefitinika(17:16) zitasababisha mashindano makubwa kati ya enzi za uovu na enzi za utuwema. Hizo roho zawashawishi watawala wa ulimwengu waje na kufanya vita (1Waf.22:21). Roho hizo ni za Shetani ambazo zina uwezo juu ya watawala wadunia hii. Mpaka wakati huo amani imeendelea kwa sababu ya uwepo wa uwianowa uwezo kati ya mataifa. Hivyo, iwapo vita imetokea hapa na pale si mahalipote. Shetani baada ya kuona hakufaulu kuyapotosha mambo, aliamuakuchukua hatua za kuleta

Page 108: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1478

maangamizi makubwa. Ila tukumbuke mfano ni wa vyura!! Hayo yote yafikawapi? Yafika kwenye siku kuu ya nani? Yafika kwenye siku kuu ya MunguMwenyezi. Yaitwa „siku ile kuu‟, ni siku ya Mungu (2 Pet.3:12) si ya wanadamu,wala ya mpinga-Kristo. Ni siku ya kutimia kwa makusudi mema ya Mungu.Mungu atabaki peke yake Mkuu kabisa juu ya yote, dunia yote itamsujudu Yeye.k.15 Ndipo Kristo Mwenyewe atajiingiza na kutangaza Kuja Kwake na kutoa Herikwa wote watakaokuwa tayari kumpokea katika hali ya usafi wa maisha na haliya kuvikwa haki yake (Flp.3:9). Itakuwa aibu kubwa kwa Mkristo yeyote ambayeatakutwa katika hali ya kupoa au kukosa uaminifu Bwana atakaporudi maanaatakuja siku asiyotazamiwa (Ufu.3:3; Mt.24:42; 2 Pet.3:19; 1 The.5:2). Haowaitwa „heri‟ (ziko heri 7 katika Kitabu hiki).

k.16 Neno „Har-Magedoni‟ lina maana ya Mlima wa Megido, ila tatizo ni kwambapale Megido hakuna Mlima ila mwinuko tu. Katika historia ya Waisraeli ni mahalipa vita na mahali pa adui za Israeli kushindwa (Amu.5:19,31). Zamani zaWaamuzi watu wa Mungu hawakuwa na tumaini lolote la kushinda, Siseraalikuwa na magari ya chuma 900 na Waisraeli walikosa silaha (Amu.4:15) lakiniBwana alimtorosha Sisera ndipo Waisraeli wakashinda. Ndivyo itakavyokuwa juuya enzi za uovu, zinaonekana kuwa na nguvu, huku enzi za utu wemazinaonekana kuwa dhaifu sana. Hata hivyo utu wema utaushinda uovu, kwakuwa Mungu yu upande wake na Mungu yu kinyume kabisa cha uovu. Kwa hiyoni vema kuwaza jina la Magedoni kuwa „jina la ishara‟ linaloashiria tukio simahali, hivyo ni jina la ishara kwa vita kuu ya mwisho itakayotokea kati yaMpinga-Kristo na Kristo Mwenyewe na kati ya enzi za uovu na Kanisa inayotajwakatika 19:11-21. Hukumu zimekuwa kubwa na nzito kwa sababu ya uzito naugumu wa mioyo ya watu.

16:17-21 Kitasa cha sabaMalaika wa saba alikimimina kitasa chake juu ya anga. Anga ilifikiriwa kuwamakao makuu ya uovu, ya pepo wabaya nk. kwa hiyo, ni ishara ya uovukushambuliwa mahali pake. Wazo lingine ni kwamba kila kiumbe hai kinahitajihewa kwa kuishi. Ndipo Yohana alisema sauti kuu ilitoka katika hekalu na kile kiticha enzi na kusema „imekwisha kuwa‟. Yote yanayofuata yameidhinishwa naMungu. Maneno „imekwisha kuwa‟ yaonyesha kwamba upeo umefika, upeo wahukumu za Mungu na upeo wa makusudi yake kutimia. Huo upeo ulishuhudiwana vitisho vikali vya umeme, radi, sauti, na tetemeko kubwa ambalo mfano wakehaukuonekana hapo nyuma. Katika muhuri ya saba na tarumbeta ya saba vitishohivi vilitajwa (8:5; 11:19). Katika sehemu ile ya Asia Ndogo matetemeko ya nchiyalitokea mara nyingi ila Yohana alitaka wasomaji wake waelewe kwamba hilolitakalotokea litakuwa kali mno. (Taz. Hagai 2:6 na ling. na Ebr.12:26-27).

Page 109: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1479

k.19 Ndipo ulitokea ugawanyiko katika mji ule mkubwa na miji ya mataifaikaanguka. Huo mwanguko ni ishara ya nini? Ni ishara ya fitina na kudhoofikakatika mfumo wa jamii, kiburi cha wanadamu kushushwa chini, mawazo marefuya wanadamu kufupishwa na utupu na ubatili wa wanadamu kudhihirishwaambao kwa kiburi chao walithubutu kujitegemea na kupanga maisha bila kumjaliMungu. Babeli, ule mji mkuu ulikumbukwa mbele za Mungu na kupewa kikombecha mvinyo ya ghadhabu na hasira za Mungu. Jamii ya wanadamu huendeleakatika kudhani kwamba Mungu ama ameusahau uasi wao ama haujali, lakini,sivyo ilivyo, bali Mungu anaukumbuka naye ataitekeleza hukumu juu ya Babeliuliowatongoza watu na anasa zake. Mungu anauangusha Babeli kabisa kabisausipate kuinuka tena. Jambo la „Wakati‟ na „historia‟ vitafutwa kabisa na badalayake umilele na Ufalme wa Mungu utakuwapo. Kwa lugha aliyotumia Yohanaalitaka kuyaonyesha maangamizi kabisa ya mfumo wa jamii walioishi bila kumjaliMungu. Hakusema kwamba waliuawa.

k.20-21 „kila kisiwa kikakimbia wala milima haikuonekana tena, na mvua yamawe makubwa...ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu‟ Yohana alipotajamilima bila shaka wasomaji wake walikumbuka ya kuwa Jiji la Rumi lilijengwa juuya milima saba. Pia mvua ya mawe ni ukumbusho wa mapigo ya Misri. Katikahistoria ya Waisraeli waasi walizoea kuabudu Mabaali na Maashtorethi kwenyemilima. Kwa kutaja milima, visiwa nk. Yohana alikuwa akisema juu ya mwisho wamfumo wa jamii kwa jinsi ilivyokuwa. Ila sikitiko ni kwamba hata lile pigo la mvuaya mawe halikuvuta watu kwa toba bali wakaendelea kumtukana Mungu wakatiwalikuwa wangali wanayasikia maumivu makali. Kwa hiyo inaonyesha kwambahadi kumiminwa kwa kitasa hicho nafasi zilikuwapo kwa toba. Tusifikiri kwambani mahali fulani ambapo palishambuliwa ila ni lugha ya kuashiria kuangushwakabisa kwa enzi na nguvu zote za upinzani hata kuanguka kwa makao makuu yaUovu.

MASWALIg. Ipo tofauti zipi kati ya vitasa na baragumu kwa upande wa

hukumu?h. „mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu; na miji ya

mataifa ikaanguka...‟ Hayo maneno yanaeleza nini?

SURA 17 MAONO YA KAHABA NA MNYAMA

Kuanzia sura hii twaambiwa habari za anguko kuu la Mji Mkuu, uitwao Kahaba.Jumuiya ya sasa ya wanadamu itatoweka na badala yake jamii mpya ya watuwa Mungu itatokea. Yerusalemu Mpya utakuwa badala ya Babeli na Bibi Arusibadala ya Kahaba.

17:1-18 Maelezo ya Babeli na Tangazo la Kuanguka KwakeBabeli umekwisha kutajwa hapo nyuma 14:8 na 16:19 na hapa tena umetajwa

Page 110: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1480

ila habari za Kuanguka Kwake zimeandikwa katika sura ya 18. Katika sura hii ya17 Yohana amepewa maono ya Kahaba ambaye kwa lugha nyingine aitwaBabeli Mkuu. Yohana aliitwa na mmoja wa wale malaika saba wa vitasa aje hukuili amwonyeshe hukumu ya kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi. (Baadayeataitwa na malaika huyo na kuonyeshwa Bibi Arusi wa Mwana Kondoo 21:9).Malaika alisema kwamba wafalme wa nchi wamezini na huyo kahaba. Pia haowakaao katika nchi, waliotajwa hapa nyuma, wamezini naye. Hao ni watuwaliokuwa wamestarehe hapo duniani wakihesabu hapa ni kwao maana waliishikwa mambo ya kimwili tu. Habari moja ya maana sana katika historia ya Israeliilitokea wakati wa mashindano makali kati ya Nabii Eliya na mwanamkeYezebeli, mke wa Mfalme Ahabu (2 Waf.9:22). Yezebeli alitajwa katika baruakwa Kanisa la Thiatira (2:20). Shabaha ya Yohana ilikuwa kuwafunulia wasomajiwake ukweli juu ya „mungu mke Roma‟ aliyekuwa na hekalu katika mahali patatuanbapo makanisa yalipelekewa barua. Mahekalu yake yalipambwa vizuri sana,hata hivyo yeye ni kahaba mkuu mwenye uvuto mkubwa wa kushawishi watuwamwache Kristo na kumpa yeye utiifu. Zamani Babeli ulisifiwa sana kwampango wa umwagiliaji wa maji kutoka Mto Frati uliosababisha mafanikio yake.Wakati wa Yohana Dola la Kirumi lilisifiwa sana kwa mafanikio yakeyaliyosababishwa na meli zake kuvuka Bahari ya Kati na kusafirisha bidhaanyingi huko na huko. Katika Waraka wa kwanza Yohana aliwaandikia Wakristomaneno hayo „msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtuakiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomoduniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima,havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaazake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele‟ (1 Yoh.2:15ku).Kwa hiyo, Babeli ni ya zamani, ya sasa, na ya baadaye, Babeli upo wakati wote.Umefananishwa na mji mkuu kwa sababu humo yapatikana kila aina yaushawishi, anasa, utamaduni, uchumi, urembo, ubembe, na kitu chochotekinachoukamata usikivu wa watu na kutawala maisha yao (fikiri hali ya Jiji na mijiya nchi yako). Anguko lake latokeatokea katika mwenendo wa historia na angukolake kubwa la mwisho litatokea katika siku kuu ya hukumu za mwisho. Neno„kahaba‟ linafunua tabia ya Babeli Mkuu na kiini cha dhambi yake ambacho nikwenda kinyume cha upendo wa kweli, upendo safi, usio na unafiki. Nikuusukumia mbali upendo wa ajabu wa Mungu uliodhihirika katika Kristo na KufaKwake kwa ajili ya dhambi zetu pale Msalabani.

k.2 Hapo twaona uvuto mkubwa wa „kahaba mkuu‟. „aketiye juu ya maji mengi‟ina maana kwamba amekuwa na uwezo wa kushawishi watu wa mataifa mengi(k.15). Watu wanapaswa wawe na tahadhari juu yake kwa sababu ni mjanjasana, anaonekana kama ni mzuri sana, kumbe ni kahaba. Fikirini jinsi ambavyowatu wengi wameshindwa kumwabudu na kumtumikia Mungu kwa sababuwameshikwa na mambo „mazuri‟, kwa mfano, michezo, shughuli za bustani,miradi midogodogo, sinema, televisheni; mambo ambayo yenyewe

Page 111: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1481

hayamdhuru mtu, hata hivyo, ni hayo ambayo yamfanya mtu atosheke, asionehaja ya kumwabudu Mungu na kufanya mapenzi yake na kumjali katika maishaya kila siku. Ni kama mtu hana nafasi kwa Muumba na Mwokozi wake, hukuanazo nafasi tele kwa mambo yake mwenyewe. Pia watu „huwaabudu‟ watumaarufu, huwainua juu sana mabingwa wa mpira, waigizaji hodari wa sinema natelevisheni nk. Hayo yote ni kuabudu sanamu, Mungu alisema „msiwe na miungumingine ila Mimi‟. (Fikirini jinsi mtu alivyo tayari kulipa fedha nyingi kwa kiingiliocha kuhudhuria michezo, dansi, sinema nk. huku mtu anapokwenda Kanisanihutoa fedha ndogo kwa shughuli za Kanisa).

k.3 Yohana alichukuliwa na Roho mpaka jangwani ili amwone huyo mwanamkejinsi alivyo hasa. Kuwa „katika Roho‟ ina maana kwamba atakuwa mwepesi wakuyatambua mambo ya kiroho. Katika jangwa utambuzi wa kweli utapatikana, nipale uhalisi wa mambo unapodhihirika. Ataweza kubainisha tabia halisi za huyomtongozi. Ni pale tu atakapokuwa salama asidanganywe na uongo wa Shetanina vitisho vya mnyama na utongozi wa kahaba. Tuliona ya kuwa jangwani nimahali pa watu wa Mungu, mahali wanapohifadhiwa (12:6,14). Wakristo budiwawe wamejitenga na dunia (Yoh.15:11).

Yohana aliona kwamba mwanamke alibebwa na mnyama mwekundu sanaaliyejaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Ina maanakwamba huyo mwanamke ni mbaya sana, amesimamishwa na kuunga mkonokazi za mnyama aliyetoka baharini na mnyama aliyetoka nchini. Ameshirikishwanguvu zao (ndiyo maana ya vichwa na pembe). Ijapokuwa amepambwa kwanguo za rangi za kifalme, nyekundu na zambarau, na kukaa juu ya mnyamamwekundu sana, hata hivyo, ni tofauti sana na „yule mwanamke mwingine‟aliyetajwa katika sura ya 12 bibi arusi wa Bwana Yesu 21:9, ambaye amebebwana mnyama na kuvikwa na jua na utukufu wa mbinguni. Huenda kuketi juu yamnyama ilikuwa ishara ya jinsi alivyotegemea Dola la Kirumi lililomwezesha nakumpatia nafasi tele kwa utongozi wake. Hayo yote ni ishara ya upinzani mkubwajuu ya Mungu utokao kwa siasa, vyama, uchumi, falsafi, dini za uongo nk.Mnyama alijaa majina ya kufuru, ishara ya madai ya MaKaisari kuabudiwa kamaMungu. Vichwa na pembe zimeelezwa zaidi katika k.9-14, 16-17. Ranginyekundu ni rangi ya utukufu pia ya dhambi (Isa.1.18). Huyo mwanamkealionekana kama malkia, amevaa kwa umalidadi sana, naye alikuwa na kikombecha dhahabu mkononi mwake. Alidai kuwanyweshea watu kinywaji kizuri sanaila hakikutuliza kiu yao, aliwadanganya tu. Taswira yote ni ya uvuto mkubwa sanaila kweli yenyewe ni kwamba mle ndani ya kikombe ni „uasherati‟ umejaa uasikwa Mungu wa kweli, Muumba na Mwokozi wa wanadamu. Aitwa kahaba, nawafuasi wake waitwa waasherati, si wazinifu, hawakuwa na uhusiano wa uhalalina Mungu. Yesu aliwaita watu waje Kwake ili wayanywe maji yaliyo hai na walechakula cha uzima (Yn.4:10ku. 6:35ku). Katika siku za Yohana Dola la Kirumi„lililoga‟ watu wa nchi nyingi kwa mafanikio yake, waliona kwamba kwake wapataraha na

Page 112: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1482

maendeleo, ila hasa Dola lilikuwa „mchawi‟ wa kufanya watu wasiitikie wito waInjili na kumwamini Kristo.

k.5-6 Kipaji cha uso kimetajwa mara nyingi, watu wa Mungu walitiwa muhurikwenye vipaji vyao, na wafuasi wa mnyama vilevile walitiwa chapa vipajini.Zamani zile makahaba walivaa utepe kichwani wenye jina lake. Jina la Kahabahalikuwa wazi, lilihitaji kufunuliwa na kutafsiriwa kiroho. Ijapokuwa Yohanaalimwita Babeli, zaidi alikuwa Rumi. Amelewa na damu ya watakatifu namashahidi wa Yesu. Kwa mpango wa Dola watu wa Mungu walipingwa sanahasa kiasi cha baadhi yao kuuawa. Kwa hiyo Babeli, Kahabu Mkuu ni wa hatarisana, na ni ujinga wa hali ya juu ikiwa Wakristo watakosa kumtambua ndipowakalogwa na hila za ushawishi wake. Zaidi ya yote Kahaba ni mwuaji,amewaua Watu wa Mungu wengi, wale ambao walikataa kujiunga naye nakushirikiana naye. Inaonekana wengi wameuawa naye kwa kuwa „amelewa‟ nadamu yao. Kwa hiyo atalipwa kulingana na alivyofanya, maana yeye aliwalevyawatu na uasherati wake (k.2). Yohana alistaajabu ajabu kuu, hata malaikaalimwuliza sababu yake. Yeye alitazamia atapewa maono ya hukumu yake, ilampaka hapo ameonyeshwa „utukufu‟ wake na „ushindi‟ wake na „tabia‟ yake.

Ndipo malaika alimwambia siri ya mwanamke, na ya mnyama aliyemchukua.Twaona uhusiano wa ukaribu sana kati ya mwanamke na mnyama na ni vigumukuwatenga. Wote hutekeleza shabaha ya Shetani. Mnyama alimwiga Kristo(1:4,17,18). Mnyama alikuwako, naye hayuko, naye atakuwapo. Huenda maanayake ni kwamba mateso hutokea mara kwa mara. Kaisari Nero amepita, sasayuko Kaisari Domitiani, ila jambo kubwa la maana ni kwamba Mnyama alitokashimoni na kurudi shimoni!! bali Kristo alitoka mbinguni, ndipo akarudi mbinguni!!Iwapo mnyama, ishara ya upinzani juu ya Kristo una „kuwako kwake‟ maana upomara kwa mara kama jambo moja la kawaida katika mwenendo wa historia yadunia, hata hivyo, mpinzani baada ya mpinzani anakwenda shimoni, ndiomwisho wa kila mmoja wao, ila ni vigumu kwa watu kuutambua mwenendo huo.Ni vema watu wa Mungu wafahamu jambo hilo la kuzuka na kutoweka kwa uovuili watambue kwamba utakapofika mwisho wa mwenendo huo ndipo maovu yotena upinzani wote utamalizika. Si Yohana tu aliyestaajabu, „wakaao juu ya nchi‟pia walistaajabu. Ni faraja kwa Wakristo walioandikiwa katika makanisa sabakuhakikishiwa kwamba majina yao yamo katika kitabu cha uzima kilichoandikwahata kabla ya Dola la Kirumi, hata kabla ya kitu chochote, hata tangu kuwekwakwa misingi ya ulimwengu. Kitu kilichomvuta Yohana kilikuwa „mwisho‟ wamnyama, kufahamu kwa uhakika kwamba anao mwisho ni kutambua ubatili wamadai yake kuwa kama Mungu na kuwa na haki ya kuupata utiifu wa watu ambaoni haki ya Mungu peke yake kuupata. Ni igizo la kumbeza Kristo.

k.9-11 Jambo hilo lilihitaji akili zenye hekima (13:18). Kwa kifungu hicho twaonaYohana alikuwa akisemea Dola la Kirumi na Jiji lake kuu lililojengwa juu

Page 113: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1483

ya vilima saba. Ila pia vichwa saba na milima saba na wafalme saba ni ishara yamfuatano wa watawala. Watano wamekwisha kutawala na kuondoka, ndipommoja yupo, na mwingine hajaja bado. Muda si muda huyo mwingine atakuja,mfano wa Nero, naye atawatesa Wakristo. Ndivyo ilivyo katika mwenendo wahistoria, wamekuwapo wale ambao wamewatesa Wakristo, na mpaka mwishowataendelea kutokea, wakati wote atakuwapo mmoja „wa kuja‟ atakayewaudhiWakristo. Ila jambo la maana ni kuona kwamba wapo kwa muda, nao waondoka,hata yule wa kuja, atakuwapo kwa muda ndipo atakwenda kwenye uharibifu.Mwisho wa kila mmoja ni uharibifu. Ni ishara ya tawala, enzi, mamlaka nauongozi zinazotokea mara kwa mara ambazo zajiinua juu ya Mungu nakumpinga Kristo na wafuasi wake.

k.12ku „pembe kumi‟ ni ishara ya nguvu, baadaye wafalme wa nguvu watatokea,huenda ni wale waliotajwa katika 16:12, wasaidizi wa Mpinga- Kristo, yuleatakayetokea wakati wa mwisho, nao watapewa mamlaka kwa saa moja, yaanikwa muda mfupi, kwa kuwa wamempa mnyama utiifu wao.

k.14 (Ling. na 13:7). Hapo tumepewa habari fupi ya vita kuu ya mwisho(19:6,11-21; 2 The.2:3ku) wafanya vita na Mwana Kondoo naye atawashinda.Mwana Kondoo atawashirikisha wafuasi wake ushindi wake. Hakuhitaji msaadawao ila alipenda wawe naye. Yeye ni Mfalme halisi, wa halali, Bwana waMabwana na Mfalme wa Wafalme.

k.15 Hatari kubwa ya Rumi ilikuwa katika umati wa watu wa aina zote waliovutwakujitia chini ya utawala wake kwa sababu ya faida za kimwili walizozipata kwake,maendeleo, anasa, utajiri, nk. Mfano wa leo ni watu wa nchi zisizo na„maendeleo‟ kutazama nchi za maendeleo hasa za magharibi na kuvutwa namambo wanayoona. Kwa upande mmoja mengine ni ya faida kubwa kwa maishaila mengine yanavuta watu kuipenda dunia na kuuacha utamadumi wao mzurihasa hali ya kuwajali watu na kutunza jamaa zao nk. Ujumbe huo wahusu watuwa mataifa yote, si wale tu walioishi wakati ule.

k.16-18 Ndipo jambo la kushtua lilitokea. Zile pembe kumi, yaani watawalafulani, ambao walikuwa wamejitoa kwa hiari kumsaidia mnyama, wao pamoja namnyama waliamua kumwangusha Kahaba. Wivu na chuki zilisababisha farakanolitokee baina yao na mnyama, yaani katika enzi za uovu ufa ulitokea. Kahabamwenyewe alishambuliwa na zile pembe kumi pamoja na mnyama, naowakammaliza kabisa. Walikuwa wamemkinai. Hawakushauriana naye baliwalitumia „mkono wa chuma‟ yaani nguvu tupu wala hawakutafuta kuisababishakwa kuivika nguo za siasa fulani, au falsafa fulani, au dini au imani fulani, aumawazo fulani, ambayo hapo nyuma ilikuwa desturi yao kufanya kamatulivyoona katika mnyama wa pili kumwunga mkono mnyama wa kwanza (sura13). Yesu alitaja jambo la „Shetani kumtoa Shetani‟ (Mk.3:23-26).

Page 114: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1484

Ndani ya maovu zimo mbegu za uharibifu. Jambo hilo lilitoka kwa Mungu, niMungu aliyewapa „umoja‟ wa kutaka kumwangamiza Kahaba aliyewatongozawatu. Ni mapenzi ya Mungu huyo Kahaba aangamizwe kwa kuwa yeye amekuwasababu ya wengi kuvutwa kumwasi Mungu. Hapo nyuma Joka na mnyamawalifurahi kumtumia Kahaba katika mipango yao ila sasa wamemaliza kazi naye,kumbe wakamwangamiza. Hamna neno lililo nje ya madaraka ya Mungu.Mnyama hawezi kushindana na Mungu na kumshinda, mwishoni, kwa kiasi chaurefu wa kamba anachoruhusiwa atajinyonga. Ajabu ni kwamba mnyamaalimharibu Yule ambaye alikuwa amemtumia katika kuwashawishi watu wasiwewaaminifu kwa Mungu (Isa.10:12). Je! liko wazo la kuwa watu watakinai„mafanikio‟ na „maendeleo‟ yao na kuutambua ubatili wake?

MASWALI1. Kahaba Mkuu aketiye juu ya maji mengi ni ishara ya nini?2. Lugha ya „kahaba‟ na „kuzini naye‟ inaonyesha tabia na dhambi gani?3. Babeli Mkuu ni sawa na Kahaba au vipi? Eleza4. Wakati wa Ufunuo Babeli Mkuu ulikuwa ishara ya? na ulihusikaje na

waumini katika makanisa?5. Ni nani aliyembeba Kahaba na kumtumia?6. Alimtumia kwa shabaha gani?

SURA YA 18 KUANGUKA KWA MJI MKUU BABELI

18:1-8 Hukumu ya BabeliKatika maelezo hayo ya kusisimua twakumbushwa Anguko la Tiro (Eze.26-28)na la Babeli (Isa.13 na 14 na 21; Yer.50 na 51). Ni mmomonyoka wa mfumo wamaisha ya jamii jinsi tunavyoufahamu. Tuliambiwa habari za kuanguka kwakehapo nyuma (14:18) na katika sura 17 malaika alimwelezea Yohana siri yaBabeli na mambo yatakayompata na ya kwamba enzi za uovu baada yakumtumia zitamkinai kisha zitamwangamiza.

Hapo malaika mwingine, mwenye mamlaka kuu ya Mungu alishuka kutokambinguni (ni mara chache malaika wamesemwa kuwa na mamlaka). Nchiikaangazwa kwa utukufu wake kwa kuwa alikuwa ametoka kwa Mungu. Kwasauti kuu alitangaza anguko la Babeli, mji mkuu. Lilikuwa tangazo zito sana hatahivyo malaika aliyelileta aling‟aa kwa sababu kuanguka kwa Babeli ni ushindi waMungu na matimizo ya makusudi yake, ndipo watu watawekwa huru wasinaswenaye. Ijapokuwa malaika alisema „umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu‟kana kwamba Babeli umekwishaanguka, iwapo bado haujaanguka, ila kwauhakika utaanguka (Isa.21:9). Mji mkuu ulionekana hauna watu, bali umekaliwana mashetani na kuwa ngome (gereza) ya roho wachafu na ndege wachafu. Nipicha ya ukiwa na udhilifu mkubwa (Isa.13:10-22; 34:11; Yer.50:39).

Page 115: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1485

k.3 Ni kwa sababu gani umekuwa na hali hiyo mbaya mno? Ni kwa sababu mjiumewapotosha watu, „umewaloga‟ na „uzuri‟ wake ambao kwa njia yake wafalmena wafanya biashara wametajirika, wameishi kwa raha na anasa, „wakiviabudu„vitu‟ badala ya Mungu, Muumba wao (Yer.51:7; Rum.1:20ku). Hapana budiMungu aivunje nguvu yake ya kuukamata usikivu wa watu na kuwashawishi(Dan.5:26). Ni dhahiri kwamba Babeli si mji fulani hasa, bali ni ishara ya jamiinzima ya wanadamu waiishio kwa kujipendekeza tu. Wanadamu wapendakujiunga katika shirika, chama, taasisi, kampuni nk. ili wapate nguvu yakuendesha na kutawala mambo kwa jinsi wapendavyo wenyewe bila kujali hakiza binadamu, kwa kufuliza tamaa na anasa zao, katika hali ya kumdharau Munguna sheria zake. Kwa sababu hiyo Mungu atauhukumu mfumo huo wa jamii nakuuangamiza.

k.4-5 Watu wa Mungu waitwa watoke Babeli: Halafu Yohana akaisikia sautinyingine kutoka mbinguni ikiwaagiza watu wa Mungu watoke Babeli. Sauti hiyoilisema kwa niaba ya Mungu. Iwapo katika k.4 tuna maneno „enyi watu wangu‟kama ni Mungu Mwenyewe anayesema, katika k.5 tuna maneno „na Munguamekumbuka‟ kama si Mungu asemaye. Haidhuru ni nani aliyesema ni waziwatu wa Mungu waitwa wasijihusishe na dunia, wala kuridhiana na hali zilizoko.Bila shaka walijaribiwa kurahisisha maisha yao ili waishi kwa raha kamawengine, wasikose riziki wala kazi pia wasiteswe. Ila iliwapasa waitambue hatariya „Babeli‟. Wakristo waitwa kuishi kwa amani na upendo na jirani zao na kuwamsaada katika jamii, ila pamoja na wito wa kushirikiana na wenzao pia waitwakujitenga na dunia katika hali zote zilizo kinyume cha Mungu (2 Kor.6:14;Efe.5:11; 1 Tim.5:12; Rum.12:2; 1 Yoh.2:15-17). Yohana hakulifurahia anguko laBabeli ila alikuwa na mzigo juu ya Wakristo katika yale makanisa saba ili wawena utambuzi wa kweli jinsi mambo yalivyo hasa. Yohana aliona dhambi za mjimkuu zimerundikana kwa wingi wao hata zimefika mbinguni na saa ya hukumuyake imefika (Mfano wa Mnara wa Babeli zamani (Mwa.11:4; Yer.51:9)).Wakristo walijaribiwa kufikiri kwamba waovu wataendelea tu bila shida kamahakuna anayeyajali maovu yao, watafanikiwa kana kwamba dhambi zaohazitagunduliwa, ila sivyo ilivyo, hali halisi ni kwamba Mungu ameyakumbukamaovu yao na hakika atayahukumu.

k.6-8 Halafu sauti ilitoa wito kwa Babeli kuangamizwa kabisa. Wito huoulipelekwa kwa nani? Ulipelekwa kwa watekelezaji (huenda malaika) wa hukumuza Mungu (Rum.12:19). Ni wito wa kulipa, wito wa kufidia (si wito wa kulipizakisasi) kwa dhambi zake. „amlipe mara mbili‟ haina maana kwamba alipwemaradufu, ila maana yake ni kwamba dhambi zake ni maradufu, kwa hiyo, alipwemaradufu kulingana na kiasi cha dhambi zake. „Kikombe‟ chake cha anasakimegeuzwa kuwa kikombe cha maumivu na huzuni. Hakudhani kwambaatapatikana na shida, hukumu yake ilitokea kama kitu kisichotazamiwa, kwaghafula, kwa siku moja. Aliketi kama malkia, kumbe, kwa kufumba na kufumbua,akawa mjane. Ni dhahiri kwamba Yohana alitaka

Page 116: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1486

wasomaji wake wafahamu kwamba anguko lake ni la haki, linalingana naalivyofanya „mlipeni kama yeye alivyolipa‟ (k.6), „kwa kadiri ya matendo yake‟(k.6b), „kwa kadiri iyo hiyo‟ (k.7). Babeli ulistahili hukumu iliyompata. Yohanaalitaka wasomaji wake wajue kwamba Mungu anazo nguvu za kupambana namaovu, maana Bwana Mungu aliyemhukumu Babeli ni mwenye nguvu. Munguhakutakabari kwa sababu ya nguvu zake ila kwa kuwa alizitumia kwa haki. Zikonguvu za uovu ila yuko mwenye nguvu zaidi yao. Twaona udhaifu wa kila taasisi,kundi, shirika, kampuni, chama nk. vya ustawi wa jamii usiojengwa juu ya Munguna haki yake. Ni neno la kututia moyo katika siku zetu inapoonekana kwamba„nguvu‟ iko mikononi mwa wachache, kampuni kubwa za kimataifa, uthamani wafedha kutawaliwa na masoko ya hisa, hata katika michezo hali mpya imetokeakatika timu za mpira kujiunga na kulipa fedha nyingi kwa „mabingwa‟ nk. nakufanya timu ndogo zishindwe kushiriki katika mashindano makubwa. Twaonamambo mengi yakitawaliwa na fedha, huko wanyonge na maskini wa duniawazidi kuonewa. Upo usemi „matajiri huzidi kutajirika na maskini huzidi kufilisika‟.N‟nani anayeyajali mambo hayo? Mungu mwenye haki ayaona hayo yote nayeatajiingiza na kuuvunja mfumo huo wa jamii. Wakristo wasidanganywe na duniahii mbovu.

18:9-19 Maombolezo ya vikundi mbalimbaliYohana alieleza Anguko la Babeli kwa kuonyesha jinsi lilivyowagusa watumbalimbali na hasa alitaja vikundi vitatu - wafalme wa nchi, wafanya biashara,mabaharia, na wahusika na bidhaa zilizosafirishwa na meli. Kwa njia ya maitikioya vikundi hivi vitatu twajulishwa jinsi anguko la Babeli lilivyokuwa kubwa mno naYohana ameeleza jinsi watu walivyojisikia walipoguswa na hilo anguko, waliitikakwa kufanya maombolezo makuu.

Wafalme walimwombolezea Babeli kwa sababu wameupoteza uwezo namadaraka yao ya kutawala mambo. Ni wao walioidhinisha ubepari, kuwapatiamatajiri na wakuu vitu vya ghali na vya anasa huku wakikosa kuwapatia maskinimahitaji yao ya lazima. Kwa ununuzi wa watumwa na kwa ushindi wa vita wakuuwalijenga nchi kwa kazi za hao watumwa na mateka. Waliruhusu nyumba zamadanguro na michezo ya ukatili. Katika michezo hiyo wanyama kama simba nafahali walifunguliwa ili wapigane na wanadamu wasio na silaha kwa shabaha yahao watu kuuawa. Walitumia watu wasiopendwa na wenzao, na wakati waYohana Wakristo walikuwa miongoni mwao, nao walitupwa uwanjani na kuuawakwa ukatili sana. Ajabu ni kwamba michezo hiyo ilihesabiwa michezo yakuburudisha watu, watu walipiga vigelegele na kushangilia sana. Ndiyo maanaya maneno „wafalme wa nchi waliozini naye na kufanya anasa naye‟.

Wafanya biashara walimwombolezea Babeli hasa kwa sababu wameupotezautajiri wao maana njia ya mafanikio yao imeondolewa, hawana nafasi tenakufanya biashara. Orodha ya vitu vya biashara yao ni dhihirisho jinsi

Page 117: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1487

walivyohusika na wakuu na matajiri na kulisha tamaa zao kwa kuwapatia kilaaina ya vitu visivyo lazima kwa maisha ya kila siku. Tazama orodha ya bidhaa,madini ya dhahabu na fedha, vito vya thamani kama lulu na nguo na vitambaavya bei kubwa na vitu vingi sana hata chakula kizuri na kitamu, chakula chamatajiri. Ndani ya orodha hiyo wanyama wametajwa pamoja na „miili na roho zawanadamu‟. Yaani watumwa wametajwa mwisho kabisa, kama ni takataka, watuwasio na thamani, vitu vya kuchezewa na hao wakubwa katika madanguro nakatika michezo ya kikatili. Wanadamu waliraruliwa na mnyama huku watuwakipiga kelele za shangwe wakifurahia mapigano hayo!!! Vitu ambavyo Yohanaameorodhesha vilipatikana katika masoko ya Rumi wakati ule. Wengiwalifanikiwa na shughuli zao.

Ndipo mabaharia walioleta bidhaa hiyo kutoka nchi za mbali pamoja nawanunuzi na wahusika wote walimwombolezea Babeli kwa sababu wameipotezakazi yao nzuri yenye mapato mazuri.

Ilikuwa shida sana kwa hao wote kusadiki kwamba Babeli na hayo yote kweliyamekwisha. Kila kundi la watu walisimama „kwa mbali‟ na kila kundi walianzamaombolezo yao kwa kusema „ole, ole, mji ule mkuu‟. Kila kundi walitaja „katikasaa moja‟. Kwa ghafula faida yao yote ilipotea. Kila kundi walitafsiri anguko laBabeli kwa jinsi wao wenyewe walivyoguswa. Hawakuupenda mji kwa ajili yakewenyewe bali kwa ajili ya faida waliyoipata kwake. Hawakuwa tayari kuyashirikimaangamizi yake, walisimama kwa mbali.

k.20 Ndipo Yohana alionyesha itikio la Watu wa Mungu. Hao waliitwa kufurahikwa sababu katika kuuhukumu Babeli Mungu amewapatia haki yao. Haowaliumizwa na kudhuriwa hata kuuawa walipoishi katika Babeli na kuushuhudiaBabeli uovu wake. Kwa muda mrefu wamesuburi ili kikwazo kikubwa kwa upandewao kiondolewe, na sasa Babeli umefutwa kabisa.

k.21-24 Yohana alimwona malaika mwenye nguvu akiinua jiwe mfano wa jiwekubwa la kusagia, akalitupa baharini, ndipo akasema „kama hivi, kwa nguvunyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa‟. Nimalaika mwenye nguvu aliyelitenda jambo hilo, tena akalitupa jiwe kubwa, sikana kwamba lilianguka tu, tena hakulitupa nchini bali baharini ili lisionekanetena. Kwa tendo hilo la ishara Yohana alipewa habari ya maangamizi makubwaya Babeli, hata Babeli hautaonekana tena kamwe. Ndipo Yohana aliendelea kwakutaja hali na vitu mbalimbali ambavyo havitakuwepo tena kamwe. Ukimyamkubwa uliupata Babeli. Kwa kusema „tena kabisa‟ mara 6 katika k.21-23Yohana alikaza hali itakayodumu ya Babeli. Hazitakuwepo tena sauti za muziki,ishara ya maburudiko ya watu; hazitasikika tena sauti za wafanya kazi, za watukutengeneza vitu mbalimbali nk; wala hazitasikika tena sauti za watu katikauhusiano wa kifamilia nk; watu hawatafunga ndoa, maana ni Mji wa Mauti si waUhai; wala nuru ya taa haitakuwepo tena. Ni giza tupu na mauti tu.

Page 118: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1488

Pakawa kimya kabisa, hamna sauti ya aina yoyote, ni mwisho kabisa wa Babeli.Anguko la Babeli lilikuwa kamili, lisilotenguka, wala halitengenezeki. Ni mwishowa mfumo wa jamii katika hali ya kumwasi na kumpinga Mungu. Wakati wa YesuYerusalemu ulikuwa mfano wa mfumo huo (Mt.23:29-39; 24:37-42), wakati waYohana ni Rumi, Babeli upo wakati wowote na mahali popote, ni pale ambapowatu waipenda dunia na kuvutwa na tamaa zake kiasi cha kumwacha Mungu.

Ni nini hasa sababu za hukumu yake? Kwanza wakuu wake na wafanya biasharawalikuwa na bidii nyingi sana, walikuwa kama wapelekwa, wakieneza sifa nauzuri wa dunia hii na vitu vyake wakishawishi watu kujitia chini yake. Babeliuliwadanganya watu kiasi cha kuwavuta „kuuabudu Babeli‟ badala ya Muumbawao, kupenda vitu kuliko Mungu mwenye kutoa kila kitu chema. Zaidi ya yoteBabeli uliwatesa na kuwaua watu wa Mungu tangu zamani za kale hata mpakawakati wa Yohana. Hata baadaye mpaka mwisho „Babeli‟ utawaua walewanaosimama imara na kukataa „kulogwa‟ na umalidadi wake.

MASWALI1. Eleza maana ya Anguko la Babeli2. Ni akina nani waliofanya maombolezo makuu juu yake? na kwa sababu

gani?3. Ni akina nani waliofurahia anguko lake? na kwa nini?

SURA 19 MSHINDO MKUBWA HUKO MBINGUNI

19:1-5 Sifa kuu kwa Mungu MshindiMwishoni mwa sura ya 18 tulipata habari ya ukimya mkubwa ulioupata Babelibaada ya hukumu ya Mungu, tuliona kwamba hapakuwa na nuru ya taa walasauti ya aina yoyote, wala ya muziki, wala ya kazi, wala ya shughuli za kawaida,pote palikuwa kimya kabisa.

Baada ya Anguko la Babeli Yohana anawatayarisha wasomaji wake kwa Kujakwa Yesu. Mpaka hapo mengi yamehusu enzi za uovu na mateso ya Wakristo.Waumini wameshauriwa kuvumilia kwa kuwa Mungu ni juu ya yote, nayebaadaye atawapatia haki. Tangu hapo mambo yanaiva, wakati umefika kwaushindi wa Mungu na Kristo wake kudhihirika wazi. Kwa hiyo, mwanzoni mwasura 19 Yohana ametuonyesha mambo ya tofauti sana, mambo ya hukombinguni. Ukimya wa Babeli wafuatwa na mshindo mkubwa wa sauti, tena sautikubwa, ya makutano mengi, umati mkubwa wa watu wa Mungu wakimsifu Mungukwa shangwe kubwa kwa ajili ya anguko la Babeli. Waliuimba wimbo wa Sifa„Haleluya‟. Neno hilo limetumika tena katika v.3,4,6 na ni hapo tu katika AganoJipya ila katika Agano la Kale twalikuta katika Zaburi 111; 112; 113; na 146.Lazima watu wa Mungu wafurahi na kushangilia na kumshukuru Mungu

Page 119: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1489

wanapoona maovu yanashindwa na utu wema unashinda. Hasa wakati wamwisho Mungu atakapowashinda adui zake wote na kuukomesha kabisa uovuwote na kuutimiza wokovu wa watu wake. Umati mkubwa wa watu waliimba„wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu, kwa kuwa hukumu zakeni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu........‟ Mambo mawili yaliyowiana ni msingi wa sifa zao, Mungu kumhukumukahaba, na Mungu kupatiliza damu ya watumishi wake. Katika kumhukumukahaba Mungu amefanya tendo la haki, neno lililokazwa katika 15:3 na 16:7.Ilikuwa haki ahukumiwe, maana aliwapotosha watu na kuwashawishi wampeyeye utiifu usio haki yake kuupata. Ni Mungu peke yake aliyeustahili kwa sababuYeye ni Muumba, Mhifadhi, na Mwokozi wa watu wote. „kwa uasherati wake‟maneno hayo yatoboa wazi dhambi yake ambayo mfano wake ni mtukumnyang‟anya mwingine mke wake wa halali. Tena zaidi ya dhambi hiyokahaba aliwaua wale waliothubutu kumpinga, wale waliodumu waaminifu kwaMungu wao. Katika kumhukumu Mungu amewapatiliza damu yao.

k.3 „moshi wake hupaa juu milele na milele‟ ni ukumbusho wa hukumu yaEdomu (Isa.34:10) ni maneno ya kuthibitisha kwamba hukumu yake imetimilikanayo itadumu.

k.4 Kwa mara ya mwisho katika Kitabu wale wazee ishirini na wanne, na walewenye uhai wanne wametajwa. Hao walikuwa karibu na Kiti cha Enzi,wawakilishi wa uumbaji mzima, hao nao walimsujudu na kumwabudu Mungu nakusema Amina, Haleluya. Kwa hiyo taswira ni ya wote kuunga mkono hukumuza Mungu na kuzikubali kuwa sawa kabisa. Babeli/Kahaba Mkuu amehukumiwana kuangushwa na kukomeshwa.

k.5 Halafu sauti kutoka kile kiti cha enzi ilisikika ikisema „Msifuni Mungu wetu,enyi watumwa wake wote, ....wadogo kwa wakubwa..‟ Wito ulitolewa kwa KanisaZima, watu wote wa Mungu, waliojulikana kwa wasiojulikana, tangu Mitumemaarufu kama akina Yohana na Petro nk. hadi Mkristo asiyejulikana katikashirika ya mahali fulani, wote waliitwa kumsifu Mungu. Ni vigumu kujua sautiilikuwa ya nani, ila ni wazi ilisema kwa niaba ya Mungu, kwa sababu ya maneno„Mungu wetu‟.

19:6-10 Karamu ya Arusi ya Mwana KondooNdipo Yohana aliisikia sauti kubwa, hata alishindwa kuieleza ila kwa kusemailikuwa kama sauti ya makutano mengi, kama sauti ya maji mengi, kama sautiya radi yenye nguvu. Ilisema nini hiyo sauti? Ilisema „Haleluya, kwa kuwa BwanaMungu wetu, Mwenyezi, amemiliki‟. Mwisho wa mambo yote umefika na Munguameshinda; utu wema umeshinda; na watu wa Mungu wameshinda. Kwa walewalio katika makanisa saba waliopatwa na shida za kunyimwa kazi,kudharauliwa, kutengwa na jamaa, na wakati wa kuandikiwa walikabiliwa namateso makali, basi habari hii ya ushindi wa Mungu iliwatia moyo wa kudumukuwa waaminifu mpaka kufa katika kumshuhudia na kumfuata Kristo.

Page 120: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1490

„Bwana Mungu wetu Mwenyezi amemiliki‟. Maana yake Ufalme wa Munguumekuja, Mungu amechukua hatua za kuukomesha kabisa upinzani wote. Niwakati wa Arusi ya Mwana wake, Bibi Arusi. Kanisa lishangilie si kwa sababu yaAnguko la Babeli/Kahaba Mkuu tu, bali zaidi sana kwa Kutokea kwa Bwana naBibi Arusi na Yerusalemu Mpya.

k.7 Hivyo mwisho si kutoweka kwa Babeli kahaba, bali ni kutokea kwa Bibi Arusiwa Mwana Kondoo. Hapo tumepelekwa mbele kwa yale yatakayokuwepo baadaya mwisho wa historia ya sasa. Ufalme wa Mungu utazishika nafasi zotezilizochukuliwa na falme na enzi na tawala za dunia hiyo, ndipo Mungu naMwana Kondoo watatawala yote bila kuwepo kwa upingamizi wowote. Haponyuma wametawala hali wakipingwa. Watu waliitwa tena kufurahi na kushangiliana kumtukuza Mungu kwa „Arusi ya Mwana Kondoo‟. Bibi Arusi ni tofauti sana nakahaba. Yeye amempa Mungu utiifu wake wote na kuwa mwaminifu Kwake. BibiArusi huyo ni nani? Ni jamii ya wale wote wa vizazi vyote waliomwamini nakumfuata Kristo kwa uaminifu. Arusi ni ule wakati wa baada ya Babeli kuanguka,wakati watakapoungana kwa ukamilifu na Bwana wao na kuishi pamoja nayemilele na milele. Kwa sasa wameposwa, Kristo amelipa mahari, ila baadayewataungana kama mume na mke wanavyoungana katika ndoa (2 Kor.11:2;Efe.5:23ku). Kama ambavyo tutakavyoona mbele Yerusalemu Mpya unachukuamahali pa Babeli. Vema tukumbuke majina hayo yote ni majina yanayoashiriajamii mbili, jamii ya waaminifu kwa Mungu Muumba wao na jamii ya waasi waMungu ambaye pia ni Muumba wao. Kusema kahaba au bibi arusi, kusemaBabeli au Yerusalemu Mpya ni mamoja, ni lugha ya kueleza jamii hizo mbili.

k.7-8 Twasoma bibi arusi amejiweka tayari na amepewa kuvikwa kitani nzuriing‟arayo, safi. Halafu tumeambiwa hiyo kitani nzuri ni matendo ya haki yawatakatifu. Yeye amevaa vizuri, Yohana ametumia nusu tu ya sentensikuyaeleza mavazi yake. Yeye huwa tofauti sana na kahaba aliyejivika kwaumalidadi, tazama maelezo marefu katika 17:4ku. Kwa nje alionekana mzuri, ilandani alijaa uchafu. Bibi Arusi amejiweka tayari, pia amepewa kuvikwa(kuhesabiwa haki kwa imani) yote mawili ni sawa kwa Wakristo (Flp.2:12-13;Efe.2:8-10, 5:25-27). Pia wameoshwa katika damu ya Mwana Kondoo (7:9,14).Ni kwa neema tu wameweza kuishi maisha ya haki na kutenda mema. Kwa hiyosi ajabu kwamba hayo yanapotokea mshindo mkubwa wa shangwe unasikikambinguni, hayo yanavuta Haleluya; hayo yastahili Haleluya!!!

k.9 Yohana aliagizwa aandike kwa makanisa saba (sura 2 na 3) (1:11;19; 14:13;21:5) ila alikatazwa asiyaandike mambo ya ngurumo 7 (10:4).

k.9-10 Hapo tunayo „heri‟ nyingine, ya nne (ziko 7 katika Kitabu). Yohanaameandika „Heri walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana Kondoo‟.Kama ambavyo tumeona mara nyingi Yohana huchanganya mifano yake,

Page 121: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1491

ametumia kwa jambo moja mfano wa Bibi Arusi na mfano wa Waalikwa kwenyekaramu ya Arusi. Ndipo malaika alithibitisha hilo jambo kuwa kweli. KishaYohana mwenyewe alishindwa kabisa alipotambua ukweli wa mambo hayo yotena ya kwamba maovu yote na vitisho vyake vimekwisha, haitabaki hata nuktayoyote ya uovu. Kumbe, Kanisa dhaifu, dogo, la kuchukiwa na kushambuliwa,litatokea salama salamini mwisho wa mambo yote. Yohana akataka kumsujudiamalaika aliyesema „heri walioalikwa...‟ ila malaika akamzuia akijiweka pamojanaye kuwa mjoli wake na ndugu wa wote waliomfuata Kristo. Sawa na watu wote,ama ni malaika ama ni wanadamu, ni wajibu wa Yohana kumwabudu Mungu(Mt.4:10) na kumshuhudia Yesu. Ijapokuwa amepata maono hayo kwa njia yamalaika, malaika si asili yake bali ni Mungu. Ni vigumu kujua maana ya manenojuu ya roho ya unabii ila kazi ya Yohana na wote walio na Roho ni kumshuhudiaKristo (Yn.16:13ku). Twaona uhusiano kati ya malaika na Wakristo katikaEbrania 1:13-14.

Kuutambua ukweli wa Babeli kuanguka na kuwa kimya kabisa na kuondolewakabisa ni maono ya faida kubwa ya kutuongoza katika maisha yetu. Yatatawalajinsi tunavyowaza na kukabili mambo yanayotokea katika maisha yetu. Tutaishikwa matumaini na uhakika, kwa ujasiri na ushujaa, na kwa uvumilivu wakati washida na matatizo.

19:11-16 Kristo aliyeshindaKatika sehemu iliyotangulia Yohana alitutayarisha kumwona Bwana Arusi, ilaalipotokea alionekana kama Mpiga Vita shujaa aliyepanda farasi mweupe.Tukumbuke ni taswira, farasi mweupe nk. ni ishara ya uhalisi kimsingi.

k.11 Yohana aliziona mbingu (si mlango tu uliofunguliwa 4:1) zimekuwa wazi nahuyo mpanda farasi mweupe alitokea na kama alijaa uwanja maana Yohanahakutaja kitu kingine. Majina ya mpanda farasi mweupe yalikuwa „Mwaminifu‟(Yeye huzitimiza ahadi zake 3:14; Isa.11:4-5) na „Wa-kweli‟ ufunuo wa tabia zatofauti sana na adui zake wadanganyifu (19:20). Kazi yake ilikuwa kuhukumu nakufanya vita kwa haki, twaona tena mkazo ni juu ya haki, wakati wote Yohanaalitilia mkazo neno la haki kutendeka, hana nia ya ushindi wala kulipiza kisasi ilakutekeleza haki tu. Yohana alikuwa na mzigo sana juu ya Wakristo walioonewana kutendewa kwa ujeuri kinyume cha haki, ni msaada kwao wakijua kwambaBwana wao ni mwenye nguvu na anawapigania. Iwapo mpanda farasi atatokakwa mara ya mwisho ili apingane na uovu Yeye hutoka kila wakati na kupiganana uovu. Farasi mweupe ni dalili ya ushindi.

k.12 „macho yake yalikuwa kama mwali wa moto‟ ishara ya Yeye kujua nakuchunguza mambo yote, Yeye husoma mioyo ya wanadamu na kufahamu niana makusudi yao pamoja na matendo yao wala hamna kitu kilichofichwa Kwakeasikione. „vilemba vingi kichwani‟ ni ishara ya Yeye kutawala mambo yote mahalipote. „ana jina lililoandikwa asilolijua mtu ila yeye mwenyewe‟

Page 122: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1492

maana yake nini? huenda ina maana kwamba kuna mengi tusiyoyajua juu yake.Ni Yeye Mwenyewe tu mwenye kufahamu siri ya Nafsi yake na undani wauhusiano wake na Baba (Mt.11:27). Pia hakuna awezaye „kumpata‟ kwa sababukatika zamani zile ilidhaniwa kwamba wachawi na wafanya ushirikina wakijuajina la mtu walipata uwezo juu yake.

k.13 „Vazi lililochovywa katika damu‟ Wengine wanamaanisha maneno hayoyahusu Kifo cha Yesu alipoimwaga damu yake pale Msalabani ili wauminiwapate wokovu. Ndiyo sababu Yesu ameitwa Mwana Kondoo. Ila wenginewanafikiri maana yake ni vazi lake limetiwa madoa ya damu hata kabla ya kupigavita, ishara ya ushindi atakaopata (Isa.63:1-6; Ufu.14:20). Hivyo damu ni isharaya kushindwa kwa adui zake. Pia Jina lake ni Neno la Mungu, Neno lina nguvukiutendaji, kwa njia ya Neno uumbaji ulifanyika (Mwa.1:3; Zab.33:6; Yn.1:1; 1Yoh.1:1; Ebr.4:12ku).

k.14 Ndipo Yohana alitaja majeshi ya wale waliomfuata ambao pia wamepandafarasi weupe. Hao wamevikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Hao ni akina nani? Amani malaika, ama ni washindi waliotajwa katika 14:4 na 17:14. Mavazi yaohayakuwa na madoa ya damu kwa kuwa wameyaosha katika damu ya MwanaKondoo. Silaha za vita hazikutajwa wala habari ya vita, kwa kuwa ni kiongoziwao Kristo ambaye peke yake huyashinda maovu.

k.15 Huyo mpanda farasi aitwaye Neno la Mungu ana silaha moja tu, upangamkali (1:16;12:48). Upanga mkali hutoka kinywani mwake, Neno lake lina nguvuya utendaji (Ebr.4:12-12; Isa.11:4,9; Rum.11:22). Kwa Neno lake atawahukumuwatu siku ya mwisho (Yn.12:48). Kwa Neno lake atapiga mataifa na„atawachunga mataifa kwa fimbo ya chuma‟ (Zab.2:9). Watu waweza kumpingana kulikataa Neno lake hata hivyo Neno hilo litawarudia na kuwahukumu siku yamwisho, haliepukiki.

„anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi‟(Isa.63:1-6) ni maneno ya kuashiria maangamizi kabisa ya wale wotewampingao Mungu. Ni kuondolewa kwa yote yaliyo kinyume chake. Muda wotewa historia Mungu amevumilia mengi, uumbaji wake umeharibiwa na waovu namapenzi yake yamezuiliwa na enzi na tawala za kiroho na za kibinadamuzilizoudai utiifu wa wanadamu, kinyume cha haki. Huenda maono hayoyanatutisha. Ila ni vema tufikiri juu ya itikio letu. Ikiwa kitu chetu kizuri kikiharibiwaovyo bila sababu au ikiwa ndugu yetu au rafiki yetu anashambuliwa nakujeruhiwa hata pengine kuuawa na mtu mwingine bila sababu. Je! twasikiaje?twafanyaje? Je! twafumba macho na kusema „basi tu, si kitu!‟ Je! twakunjamikono bila kufanya chochote! sidhani.

k.16 Hapo twapewa jina lake lingine ambalo limeandikwa katika vazi lake napaji lake ili lionekane wazi, nalo ni „Mfalme wa Wafalme, na Bwana wa

Page 123: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1493

Mabwana‟. Yohana hataki tubaki na mashaka kuhusu huyo kuwa ni nani. Ni wazikabisa kwamba kwa hali zake zote, kwa kazi zake zote, kwa tabia zake na kwamajina yake, huyo ni Yesu Kristo, Mwana pekee wa Baba, Mwana Kondoo halisi,Mkombozi wa ulimwengu. Yohana anataka tumwaze Yeye kuliko mwingineawaye yote. Yeye ni Mshindi kwa sababu tangu wakati wote na hata kabla yawakati Yeye ni Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana. Hii ndiyo asili yaushindi wake.

19:17-21 Mnyama na Nabii wa uongo waangamizwaYohana alimwona malaika mmoja amesimama katika jua, penye nuru kuu,mahali pa kuuvuta usikivu wa ndege, na kwa sauti kuu aliwaita waje kwa karamukuu ya Mungu ili wapate kula nyama ya wakubwa kwa wadogo, watu mbalimbali,waliomwasi Mungu na kufanya kinyume cha haki yake. Vita hiyo haikutegemeatabaka ya mtu bali ilikuwa vita kati ya haki na udhalimu, ukweli na uongo, Kristona Shetani. (Ling. na k.9 karamu ya arusi ya Mwana Kondoo). Kwa taswira hiyoYohana alitaka kuonyesha maangamizi makubwa ya uovu. Vita imekwisha naimebaki ndege waje na kujishibisha kwa nyama ya wapinzani.

k.19 Ndipo Yohana aliona nini? Aliona enzi za uovu zikikutana tayari kufanyavita na Kristo na majeshi yake. Ziliongozwa na mnyama na pamoja naye niwafalme na majeshi yao (Zab.2:2).

k.20 Ila Yohana hakusema zaidi juu ya vita hiyo. Mara ataja kukamatwa kwamnyama pamoja na nabii wa uongo. Pengine maana yake ni kwamba vita hiyohaikutokea. Iwapo enzi za uovu zinaonekana kuwa na nguvu nyingi, nazozinatisha sana, zinapokutana na Kristo zinaishiwa nguvu (2 The.2:8). Nabii wauongo ni sawa na yule mnyama aliyetoka nchini (sura 13:11ku). Huyoameelezwa kuwa yule aliyefanya ishara zilizowadanganya wale watuwalioipokea ile chapa ya mnyama na kuisujudia sanamu yake. Wote wawiliwalitupwa katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti (20:10,14,15; 21:8). Tena kwalugha hiyo Yohana alitaka kuonyesha maagamizi yao (Mt.13:40-42).

k.21 Wafuasi wa wanyama hao pia waliangamizwa, waliuawa na nguvu ya Nenola Mungu, Neno lile ambalo lilitoa ahadi ya wokovu kwa wote watubuo (Efe.6:17;Ebr.4:12). Mwisho wa wote wanaomwasi Mungu na kuyapinga mapenzi yake niwa kutisha sana. Yohana alitumia lugha ya kimfano kama maneno upanga, vita,ziwa la moto liwakalo, ndege kujishibisha na nyama ya wapinzani. Je! uhalisiwake utakuwa nini ikiwa hiyo lugha imetumika kuumaanisha?

MASWALI1. Ilitokea nini mbinguni Kahaba alipohukumiwa na Babeli ulipoanguka?2. Nani atakuwa badala ya Kahaba Mkuu? Eleza hali ya huyu?

Page 124: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1494

3. Itatokea nini kati ya huyu na Mwana Kondoo? maana yake ni nini?4. Ni nini iliyowapata mnyama wa kwanza na mnyama wa pili ambaye ni nabii

wa uongo? Maana yake nini?

SURA 20 KUFUNGWA KWA SHETANI KWA MIAKA ELFU

Kabla ya kuendelea ni vema kusema kwamba Wakristo hutofautiana katikamaelezo ya sehemu hiyo juu ya Shetani kufungwa miaka elfu. Baadhi yaohufikiri kwamba Kristo atakaporudi Wakristo waliokwisha kufa watafufuka napamoja na Wakristo walio hai wote watanyakuliwa na kukutana na Kristohewani (1 The.4:17) ndipo watatawala pamoja na Kristo hapa duniani kwamiaka elfu. Ndipo baada ya miaka hiyo elfu Shetani atafunguliwa kwa mudamfupi. Kisha wafu wengine watafufuliwa.

Baadhi ya Wakristo wanaamini kwamba Kristo atarudi baada ya miaka hiyoelfu.

Wako wengine wanaofikiri kwamba miaka hiyo elfu si miaka elfu kamili bali nilugha ya kueleza wakati tangu Kuja kwa Kristo mara ya kwanza mpaka karibuna Kuja Kwake tena. Katika 11:2-3 tuliona kwamba Mataifa walipewakuukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili, muda uleule wa mashahidiwawili kuutoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini. Kwa hiyo miaka elfu niishara ya kipindi kilekile.

Inafikiriwa ufufuo wa kwanza unahusu kuzaliwa kwa mara ya pili wakati mtuanapomwamini Kristo, kwa sababu jambo hilo limeelezwa kuwa „kutoka mautiya dhambi kwa kufufuliwa kwa maisha mapya katika Kristo‟ (Rum.6:1ku.Yn.5:24; Efe.2:5; 1 Yn.5:11-12).

20:1-6 Shetani kufungwa kwa miaka elfuKatika sura ya 20 tulipewa habari ya wasaidizi wa Shetani, mnyama wa kwanzana nabii wa uongo/mnyama wa pili kukamatwa na kutupwa katika ziwa la motopamoja na wafuasi wao. Je! habari za „bwana‟ wao Shetani? Kabla ya Shetanikutupwa katika ziwa la moto tunazo habari za „kufungwa kwake‟ kwa miaka elfu.Yohana alimwona malaika akishuka kutoka mbinguni mwenye ufunguo wakuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake, ndipo malaika akamshikaShetani na kumfunga, akamtupa katika kuzimu, akatia muhuri juu yake.

Ni vema tujiulize Shetani alifungwa lini? na kwa kiasi gani? na kwa shabahagani? Katika Maandiko kuna mahali pamoja tu ambapo tuna habari za Shetanikufungwa (Mt.12:26-29, Mk.3:27 Lk.11:21). Yesu alidai kuwa amemfungaShetani wakati alipomtoa pepo katika mtu kipofu na bubu hata akapata kusemana kuona. Halafu Yesu aliendelea kwa kusema kwamba Ufalme wake umekuja.

Page 125: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1495

Ndipo alisema wafuasi wake watafanya vivyo hivyo (Mt.16:19; 18:18, Yn.20:23).Hata hivyo, inaonekana Shetani yu hai akifanya kazi kwa bidii sana. Kwa hiyo inamaana gani kusema amefungwa? Katika k.3 twaambiwa shabaha ya kufungwakwake ilikuwa „asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie‟.Yesu alipozaliwa Mzee Simeoni alitangaza kwamba Yesu atakuwa nuru yakuwaangaza WaMataifa; mamajusi wa mashariki walikuja kumsujudia (Mt.2:1ku)wageni kama akida wa Kirumi (Mt.8:5ku) na mwanamke Mkananayo(Mt.15:21ku) walimwamini; Wayunani walitaka kumwona (Yn.12:20). KatikaSikukuu ya Pentekoste watu wa Mataifa mbalimbali waliyasikia mahubiri yakwanza ya Kikristo (Mdo.2:5ku). Ndipo Injili ilienea mpaka Samaria (Mdo.8:5ku)baadaye Kornelio Mmtaifa aliamini (Mdo.10) kisha Injili ilitolewa moja kwa mojakwa WaMataifa (Mdo.17:30). Nyakati za kutokujua kwao zilikuwa zimepita nailikuwa dhahiri kwamba Shetani hakuweza kuwashika. Wayunani walikuja nakuomba wamwone Yesu na Yesu alipolisikia ombi lao alisema juu ya Shetanikutupwa nje (Yn.12:20-32). Yesu aliwatuma watu sabini ili wahubiri na kutoapepo nk. waliporudi na kutoa habari za kazi zao na jinsi hata pepo walitoka kwawatu kwa neno lao Yesu akasema „nilimwona Shetani akianguka kutokambinguni‟ (Lk.10:1-20). Kwa hiyo maana ya kufungwa kwa Shetani ni kubanwakwake asiweze kuwadanganya watu. Kama mmoja alivyosema, kila mwongofuni ushuhuda wa Shetani kushindwa asiweze kuwadanganya watu. Katika Kitabucha Ufufuo mara kwa mara tumesoma neno „kupewa‟ na kuambiwa juu yamipaka kuwekwa, hakuweza kufanya moja kwa moja kadiri alivyotaka. Hawezikuliangamiza Kanisa wala kuizuia Injili isihubiriwe. Kwa hiyo, hiyo miaka elfu nisawa na vipindi vile vilivyotajwa hapo nyuma, siku 1260, miezi 42, miaka 3 nanusu, wakati, nyakati na nusu ya wakati, ni „Majira ya Injili‟.

k.3 „na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache‟. Pengine muda huohulingana na muda wa mashahidi wawili kuuawa na mnyama kupata jeraha lamauti halafu akawa hai tena, vichwa saba na pembe kumi ni ishara nakuinukainuka kwa maovu. Pia katika 2 The.2:4ku. kuna habari ya „mtu wa uasikufunuliwa‟. Kuja kwa Kristo mara ya pili kutakomesha kuzukazuka kwa uovu (2The.2:8). Neno „apaswa‟ laonyesha kwamba hii ndiyo njia ambayo kwayo Munguatauleta huo mwisho wa maovu yote.

k.4-6 Yohana alitaja viti vya enzi bila kusema vilikuwa vingapi wala kusemavilikuwa wapi, ila twafikiri vilikuwa mbinguni. Hakusema wazi ni akina naniwaliokaa juu yake ila kwa maneno yanayofuata inaonekana ni wale mashahidina wale wasiomsujudia mnyama nk. „wakapewa hukumu‟ pengine ina maanakwamba Mungu alikata hukumu upande wa hao mashahidi kwa sababu Yohanaamekuwa na mzigo juu ya hao kupatiwa haki kwa kuwa wameteswa isivyo halali.Au maana nyingine ni walishirikishwa kazi ya kutoa hukumu. Wakristowalitazamiwa wataamua mambo kati yao (1 Kor.6:2-3).„nikaona roho zao waliokatwa vichwa .. wakatawala pamoja na Kristo miaka

Page 126: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1496

elfu‟. Watu wa Mungu wameishafufuliwa pamoja na Kristo na kutawala pamojanaye kama wafalme na makuhani (Kol.3:1ku; Ufu.3:21) Ufufuo wa kwanza nikuzaliwa kwa mara ya pili, kuokoka (2 Kor.5:8,17). Wasiomwamini Kristo ni wafukatika dhambi (Efe.2:1) iwapo wako hai kimwili, watakapokufa kimwili ni „mautiya pili‟. Twaona Yohana alisema „roho zao‟ si miili yao. Kwa hiyo miaka elfu niwakati uleule wa mashahidi kutoa ushuhuda, na Mwanamke kuishi jangwani(11:3; 12:6,13ku).

Liko wazo tofauti na hilo la juu. Pengine maana ya ufufuo wa kwanza ni kuhusuhao waaminifu wakati wa kufa kwenda mara moja kwa Kristo, waliteswa pamojanaye nao watatukuzwa pamoja naye (Rum.8:17). Tumeona desturi ya Yohanamara kwa mara ni kuwakumbusha wasomaji wake juu ya usalama wa wale waliowaaminifu kwa Kristo iwapo waudhiwa hata kuuawa. Wameonekana katika raha(7:9-17; 14:1-5).

k.6 Hapo Yohana alitaja heri ya tano katika zile saba za Kitabu „heri na mtakatifuni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza, juu ya hao mauti ya pili hainanguvu.....‟ mauti ya pili ni „ziwa la moto‟ (k.14). Heri hizo zililenga kuwatia moyoWakristo katika makanisa saba waliokabiliwa na mateso ili wadumu kuwawaaminifu hata kufa kwa ajili ya Kristo.

20:7-10 Shetani kufunguliwa kwa muda mfupi kisha kutupwa katika ziwa lamoto

Kuelekea mwisho wa Injili kuhubiriwa Shetani aruhusiwa kwa muda mfupi iliaende kuwadanganya Mataifa katika dunia nzima na kukusanya idadi kubwasana ya watu ili wawashambulie watu wa Mungu tena kwa mara ya mwisho.„kambi ya watakatifu‟ na „mji uliopendwa‟ ni lugha ya mifano kueleza watu waMungu. „kambi‟ ni neno liletalo wazo la usafiri, Wakristo ni wasafiri na wagenihapa duniani, kwao ni mbinguni, ni raia wa Ufalme wa Mungu (Ebr.9:14). „mjiuliopendwa‟ ni maneno ya kuonyesha jinsi watu wa Mungu walivyo „jamii‟, watotowa Baba mmoja, watu wa familia moja.

Shetani alikusudia kwa njia ya vita hiyo kumshinda Mungu na watu wake, kumbeilitokea kuwa njia ya kushindwa kwake na Mungu na kusababisha Mungu akateshauri la kufanya hukumu ya mwisho. Hatusikii kwamba walipigana vita. Ni vitaileile iliyotajwa katika 16:12-16; 17:14-18; 19:17-21. Hapo Mataifa yamepewamajina ya Gogu na Magogu (Eze.38:2). Majina hayo hayana maana ya kijiografiaila ni ishara ya upinzani na uasi juu ya Mungu. Sehemu hiyo ni ukumbusho wakushindwa kwa Edomu na kuhuishwa kwa Israeli (Eze.35-39).k.9b „moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala‟ maana yake Mungu Mwenyewealijiingiza kwa nguvu. Uwezo wa Mungu ni mkubwa sana; yule asianaangamizwa kwa ufunuo wa Kuwapo Kwake Bwana Yesu, ambaye atamwuakwa pumzi ya kinywa chake‟ (2 The.2:8) lugha ya kuonyesha urahisi wa

Page 127: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1497

kuondolewa kwake, yatosha tu Yesu atokee. Kwa hiyo, Mungu atakapochukuahatua ya mwisho kuyakomesha maovu, vita imekwisha hata kabla haijaanza.

k.10 Ndipo Shetani alitupwa katika ziwa la moto na kiberiti walipotupwa„wasaidizi wake‟ waliojiunga naye. Si kwamba hao walimtangulia ila adhabu yaoni ileile moja nayo imekwisha kuamriwa. Wamewatesa wale waliothubutu kuwawaaminifu kwa Yesu na tangu hapo wao watateswa milele na milele kwa matesoyanayoendelea moja kwa moja bila kusimama na bila kuwa na mwisho (2The.1:4ku)

20:11-15 Ufufuo wa wanadamu wote na hukumu ya mwishoKisha Yohana aliona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe. Hakusema ni nani aliyeketijuu yake. Bila shaka ni Mungu na hapo nyuma tumeambiwa Kristo ameketipamoja na Baba yake. Katika Agano Jipya twasoma kwamba Baba amempaMwana kuhukumu (Yn.5:21-22; Mt.25:32ku; 2 Kor.5:10). Maelezo ya kiti hichokuwa kikubwa na cheupe huonyesha adhama kuu ya yule aliyeketi juu yake. Nimahali pa haki kufanyika. Huyo hakimu amestahili kufanya hukumu. Ni Mtakatifuna Mwenye haki, hana upendeleo wowote. Yohana hakutaja kitu kinginechochote, tofauti sana na maelezo mengi yaliyotolewa mara ya kwanzakilipotajwa kiti cha enzi (4:2ku). Alitaka kuuvuta usikivu wa wasomaji wake iliwazingatie sana hicho Kiti cha Enzi, na Hakimu aliyekikalia, na wale wakuhukumiwa, maana jambo hilo ni la kipekee, ni zito, lenye kutisha sana, nalolamhusu kila mwanadamu.

Twasoma nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.Kuwako kwa Mungu kulitosha kwa taratibu za kwanza za uumbaji kutoweka.Hazikuweza kusimama mbele zake kwa kuwa zilikuwa zimechafuka sana kupitauwezekano wa kuzitakasa. Zilitoweka ili utaratibu mpya wa mbingu mpya na nchimpya utokee (2 Pet.3:10; Mt.19:28; Rum.8:18- 22).

k.12 Ndipo Yohana aliwataja wale wa kuhukumiwa. Kila mmoja wa wanadamuyumo miongoni mwao, potelea mbali alikufa lini, au wapi, au kwa njia gani, hatawale waliokufa vibaya kwa ajali, hata hao hawataiepa (Rum.14:10; 2 Kor.5:10).Halafu vitabu vilifunguliwa navyo vilishuhudia maisha ya kila mtu, vilikuwa nakumbukumbu za matendo yake. Hukumu yalingana na matendo ya mtu, kanunihiyo imetajwa katika Agano Jipya lote (2:23; 22:12; Rum.2:6)). Ushuhudaulikuwepo wa kutosha kwa kila mtu kuonekana kuwa mwenye hatia (ling.Rum.3:23 „wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu).

Ndipo Yohana alitaja kufunguliwa kwa kitabu kingine, kitabu cha uzima, ambachokimeitwa Kitabu cha Mwana Kondoo (3:5; 13:8; 17:8; 21:27) na wote ambaomajina yao yaliandikwa humo walipita salama katika hukumu. Hao walikuwawamekataa kuridhiana na Shetani, na Mnyama, na Nabii wa uongo,

Page 128: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1498

na Babeli. Dhambi zao zilihukumiwa katika Kristo alipokufa Msalabani, naowalikuwa wameupokea wokovu wake, walikubali kuoshwa dhambi zao katikadamu yake, wakavikwa haki yake, hawakutegemea haki yao wenyewe, na kwasababu hiyo Mungu aliwapokea. Walikuwa mali yake na kwa msaada wa RohoMtakatifu ndani yao waliishi maisha safi na kutenda mema (Efe.2:8-10). Walewatakaoitegemea haki yao wenyewe watakuta kwamba haitatosha kuwaepushana mauti ya pili (Mt.10:28).

k.14 Mwishowe hakitabaki kitu chochote cha nguvu. Hata Mauti na Kuzimuhazitakuwapo tena (1 Kor.15:26:55) zilitupwa katika ziwa la moto pamoja nawote waliokataa kumpokea na kumfuata Kristo. Hukumu itasawazisha nakurekebisha yote. Mungu peke yake amebaki na nguvu yake ni upendo wake.

Ni mwisho wa taratibu za sasa za uumbaji k.11;Ni mwisho wa waasi wote k.15;Ni mwisho wa mauti na kuzimu k.14.

Lakini hukumu hiyo ijapokuwa ni mwisho kwa adui wote na hali zote mbaya piani dhihirisho la ushindi kamili wa Kristo. Vema tusiyawaze maangamizi tu, balitujipe moyo kwa kujua kuwa hayo yote ni utangulizi wa utaratibu mpya, nimatayarisho kwa dahari mpya ambayo haki itakaa ndani yake (2 Pet.3:13). Nimwanzo wa dahari ya utukufu.

Tukumbuke kwamba usemi kama „ziwa la moto‟ nk. ni lugha ya kuashiria haliitakayowapata wote wanaomkataa Kristo na pendo lake. Itakuwa baada ya watukupewa nafasi nyingi za kutubu, hizo hazitapatikana tena (Ebr.9:27). Daimakatika maisha watu hupata nafasi za kuchagua ama Kristo ama Shetani, amakweli ama uongo, ama usafi ama uchafu wa maisha, ama kutenda mema amakutenda mabaya, uchaguzi una kila mtu. Upo utengano mkubwa kati ya watu wakupotea na wa kuokoka.

MASWALIUnaelewaje maana ya Shetani kufungwa miaka elfu moja?Unaelewaje maana ya Shetani kufunguliwa kwa vita ya mwisho?Ni akina nani watakaofufuliwa siku ya mwisho?Ni kwa kanuni gani Mungu atawahukumu wanadamu?Maneno „vitabu vilifunguliwa‟ yana maana gani?Ni akina nani watakaosalamika katika hukumu ya mwisho? na kwa sababugani?

Page 129: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1499

SURA 21 MBINGU MPYA NA DUNIA MPYA

Baada ya „ule mwisho‟ tumefika kwa „mwanzo‟ yaani tumefika katika umilele.Dhambi imeondolewa, uovu umeondolewa, na watenda dhambi wameondolewa,na enzi za uovu zimeondolewa. Hii dahari mpya imeelezwa kwa lugha ya„mbingu mpya na dunia mpya‟ (Isa.65:17; 66:22; Mt.19:28). Washiriki wa daharihii mpya ni wale waliouonyesha ukweli na uthabiti wa imani yao, waliyashindamajaribu na mateso na thawabu yao ni kushirikiana kwa ukaribu sana na Munguna Kristo. Wale wasiokuwa na imani halisi waliomkana Kristo kwa sababu yahofu ya kuteswa watashirikiana na Mjaribu wao katika adhabu ya milele.

21:1-8 Mungu kuwa pamoja na watu wakeTusiwaze „maumbo ya kuonekana‟ ya mbingu mpya na dunia mpya kuwa yanamna gani, ila jambo la maana ni hali zake mpya (Mdo.3:19-21).

k.1b „wala hapana bahari tena‟ bahari ilikuwa ishara ya uovu, misukosuko,masumbufu ya maisha ya wanadamu, na utengano katika Mataifa (17:15) kwakuwa watu hawakupenda kutulia chini ya mamlaka ya Mungu (Isa. 57:20;Zab.65:7). Twakumbuka kwamba mnyama wa kwanza alitoka baharini (13:1).Kwa hiyo bahari haipatani na tabia ya uumbaji mpya. Kwa kusema „hapanabahari tena‟ ina maana kwamba watu wataishi kwa amani na masikilizano,hawatatatizwa tena na shida za maisha. Watu hawaishi baharini, bahari ni yakuvuka kutoka mahali fulani mpaka mahali pengine, bahari haina kazi maadamumtu amefikia mahali alipokusudia kupafikia.

k.2 Ndipo Yohana aliuona mji ule mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ukishuka kutokambinguni kwa Mungu....‟ Utakatifu ni hali yake na tabia ya wale wakazi wake.Mpya kwa sababu hutofautiana sana na mji wa sasa, „Babeli‟. Jina la Yerusalemuni ukumbusho wa ukombozi uliofanyika na Kristo. Yohana alisema YerusalemuMpya ulitoka mbinguni kwa Mungu, na mara baada ya kushuka hamnakutofautisha tena kati ya mbingu na dunia. Kushuka ni thibitisho kwambaYerusalemu Mpya haukuundwa na wanadamu wala haukutokea kwa sababu yambinu na maendeleo ya wanadamu, wala hauwi matimizo ya ndoto zawanadamu. Huo mji ni kazi ya Mungu, ni mji ulioundwa na Mungu. Neno „mji‟linaashiria jamii ya watu wa Mungu katika hali njema ya kushirikiana pamoja.

k.2b „umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe‟.Kama ambavyo tumeona Yohana alitumia mifano mbalimbali katika kueleza kitufulani. Hapo ameufananisha Mji na Bibi Arusi aliyepambwa vizuri sana kwa sikuya arusi yake, siku ya yeye na Bwana Arusi kuungana kikamilifu. Kwa neemayake Mungu amefanya kazi maishani mwa wafuasi wake na kuwaweka tayarikwa siku hiyo ya kuishi pamoja na Bwana wao katika uhusiano wa

Page 130: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1500

ukaribu sana. Kwa hiyo huo mji ni jamii ya wote waliokuwa waaminifu kwa Yesunao wataendelea kuukamilisha uhusiano wao katika uzima wa milele. Jambo lamaana ni ushirikiano wao na Bwana wao na ushirikiano wao kwa wao (Efe.5:26-27; 1 Yoh.3:3).

k.3 Upeo umefika katika Mungu kuwa pamoja na watu wake, Yohana alisikiasauti kubwa kutoka kiti cha enzi ikisema „Tazama, maskani ya Mungu ni pamojana wanadamu.....‟ Neno hilo limesemwa mara tatu kama kutilia mkazo jambokubwa la maana sana la Mungu kuwa pamoja na watu wake. Mungu ni Munguwao. Neno hilo lilikuwa na shabaha ya kuwatia moyo Wakristo katika makanisasaba pamoja na Wakristo wote hasa wale wapatwao na magumu na mateso kwaajili ya Kristo. Vema watazame mbele kwa mwisho wa safari yao ya kufikakwenye Yerusalemu Mpya. Bila shaka maishani mwetu tumejua hali ya furahatuliyosikia tulipofunga safari kwenda mahali fulani, ndipo njiani tulikutana nashida nyingi, tulitaka kukata tamaa juu ya kufika, kisha baada ya taabu tukafikasalama salimini, tukafurahi sana. Itakuwa furaha ya namna gani Wakristowatakapomaliza safari yao na kufika kwa Bwana wao?.

k.4 Ni Mungu Mwenyewe atakayewafariji na kuyafuta machozi yao, hata Yohanaaliandika „kila chozi‟ kuonyesha kwamba Mungu amejua kila jambo la maishayao. Yale magumu waliyopata yatakuwa yamepita, wala hayatatokea tena.Mungu anao mzigo mkubwa juu ya watu wake (1 Pet.5:7). Alipozaliwa Yesualipewa Jina „Imanueli‟ (Mt.1:23) maana yake Mungu pamoja nasi. Ni mwisho wamauti na huzuni na maumivu na yote yaliyowaumiza wanadamu.

k.5-6 Ndipo Mungu Mwenyewe alisema kutoka katika Kiti chake cha enzi. KatikaKitabu hicho mara nyingi „sauti‟ imesema, wakati mwingine imekuwa ya malaika,wakati mwingine haikuwa wazi ilikuwa sauti ya nani. Ni mara chachetumeambiwa wazi kwamba Mungu amesema (1:8; labda 16:17). Hapo Mungualisema, Alisema nini? Alithibitisha kwamba ayafanya yote kuwa mapya. Wakatiwote Mungu hufanya mambo kuwa mapya, ila mwishoni mambo yote jinsiyalivyokuwa yatageuzwa kuwa mapya (2 Kor.3:18; 4:16-18). Tena, Mungualisema hayo kwa uthabiti wa Yeye kutegemewa kabisa, maana alimwambiaYohana „Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli‟ halafu aliendeleakumwambia „Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega....‟ (1:8;22:13). Ni mamboya kuwafaa sana Wakristo katika makanisa saba ndiyo sababu Yohanaaliambiwa ayaandike. Mungu alitamka kana kwamba mambo hayo yametokeatayari, kwa sababu ya uhakika wa kutokea kwake. Mungu ni Mwanzilishi naMtekelezaji na Mwenye kutimiza mipango na makusudi yake yote (Efe.1:11).Tena anao uwezo wa kushibisha „kiu‟ za wanadamu, mahitaji yao ya kiroho naya kibinafsi, tena kwa ukarimu sana bila gharama, budi mtu asikie „kiu‟ nafsinimwake, atambue haja yake ya kushirikiana na Muumba na Mkombozi wake(22:17; Zab.42:1-2; 63:1; Isa.55:1-2; Mt.5:6). Tukiuliza huo mwisho hasa ni nini?Je! ni tukio fulani? hasa mwisho ni Mungu Hai na Kristo wake katika uhusianokamili na watu wake.

Page 131: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1501

k.7 Warithi wa mambo hayo mema ni akina nani? Washindi ndio warithi kamaambavyo tulisoma katika barua saba, kila barua ilimalizika na ahadi kwa„ashindaye‟ (2:7,11,17,26; 3:5,12,21) ahadi kwa yule aliyedumu mwaminifu kwaKristo, yule ambaye hakukubali kujisalimisha kwa kuridhiana na mambombalimbali kama kufukiza uvumba kwenye sanamu ya Kaisari na kusema Kaisarini Bwana, au kuhudhuria hekalu za kipagani na kula vitu vilivyotolewa sadakakwa sanamu nk. Mshindi apata zawadi gani? Zawadi yake ni kuzidishiwaushirikiano wake na Mungu hata apate kuitwa „mwanangu‟ na Mungu.

k.8 Ila si wote walio miongoni mwa washindi, hao watakuwa nje ya baraka hizo,hawatashirikiana vema na Mungu wao, kwa sababu hapo nyuma hawakuwawaaminifu Kwake. Waoga wameonekana kuwa wa kwanza katika orodha.Wasomaji wa Kitabu walihitaji ujasiri mkubwa ili wawakabili adui za Mungu nakusimama imara na kuyakataa madai yao. Twasoma kwamba Mungu hajawapa„roho‟ ya woga bali roho ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi‟ (2 Tim.1:7).Bila shaka neno „waoga‟ liliwaonya Wakristo wasitafute njia nyepesi ya kutokakatika mateso. Katika Injili Pilato aliitwa „mwoga‟ kwa sababu hakuwezakusimama imara wakati adui za Kristo walipomsukuma atoe hukumu ya Yesukuuawa. Baada ya waoga Yohana alitaja wasioamini, watu walioikana imani yao,na wengine kadha wa kadha ni wale wenye maisha na tabia za yule kahaba nayule joka mkubwa na mnyama wa kwanza na wa pili, kwa jumla, waasi.Walishiriki tabia zao nao wataishiriki adhabu yao, sehemu yao ni katika ziwa lamoto, ambayo ni mauti ya pili (20:14).

21:9-22 Yerusalemu, Mji Mtakatifu ukishuka kutoka mbinguniHapo Yohana alipewa kuona hali mpya za maisha ya baadaye. Aliitwa juu nammoja wa wale malaika saba wa vitasa saba vilivyojaa mapigo saba ya mwisho(17:1 Yohana aliitwa kwenda kuona hukumu ya kahaba yaani Babeli). PengineYohana alitaka kuonyesha wasomaji wake kwamba kutokea kwa bibi arusi nakushuka kwa Yerusalemu kumefungamana na kuhukumiwa kwa kahaba nakuanguka kwa Babeli. Kwa kuwa mtu hawezi kuwa mwaminifu kwa MwanaKondoo na kwa Kahaba, hana budi achague yupi wa kumfuata na kumtumikia.Ipo tofauti sana kati ya hukumu ya Babeli na utukufu wa Yerusalemu yambinguni. Twakumbushwa unyenyekevu mkuu wa Mungu, Yeye ndiyeashukaye, na hasa alifanya hivyo Yesu alipokuja duniani na kufa Msalabani kwaajili yetu (Flp.2:5ku). Mji unashuka kutoka kwa Mungu, Mungu ni mjenzi wakehasa. Mwana kondoo ametajwa mara 7 katika sura 21 na 22. Tumeona maranyingi Yohana anatumia mifano tofauti tofauti katika kueleza jambo fulani;„mke/‟mji‟; „Babeli‟/‟kahaba‟ nk.

Kwa maneno „bibi arusi wa Mwana Kondoo‟ na „Mji uitwao Yerusalemu‟Yohana anamithilisha Kanisa la Kristo, Watu wa Mungu waliokombolewa

Page 132: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1502

wakionekana kama Bibi Arusi na kama Mji. Katika maono hayo twaona Kanisala baadaye, Kanisa ambalo limekamilika ambalo Kanisa la sasa ni kivuli chake(21:7). Jamii ya wanadamu wenye kushirikiana vema na Mungu wao kwa njia yaKristo, ushirika wao utaendelea na kukamilika. Ijapokuwa tumezoea kufikiri juuya kuokoka kwa mtu mmoja mmoja, katika Agano Jipya na Agano la Kale watuwa Mungu wamefikiriwa katika hali ya kuwa „jamii‟. Neno „kushuka‟ ni ukumbushokwamba wao ni kazi ya Mungu, ya neema, kwa kuwa Mungu amewajengapamoja kuwa „jengo‟ la Roho (1 Kor.2:9ku; 3:9ku; Zab.46:5). Kwa hiyotunapoendelea kupewa habari za „jengo‟ tukumbuke ya kuwa Mji hasa ni „jamiiya watu‟ waliookolewa na Kristo (Efe.5:26ku). (Inawezekanaje kuwa jengo lamawe, jengo la maili 1,500 lajengwaje?).

11ku Katika Ukiri tumezoea kusema maneno „naamini Kanisa Moja, Takatifu,Katholiko (la mahali pote), na Apostoliko. Katika maelezo yafuatayo twaonaumoja wa jengo, utakatifu wa mji (k.2) ukatholiko wake yaani upana wake wakupokea watu wa aina zote, na hali ya kiapostoliki kwa kuwa umejengwa juu yaushuhuda wa Mitume 12 waliochaguliwa na Yesu na kuwekwa ili wazishuhudiehabari za kweli za Kristo kuhusu maisha yake, hudumu yake, miujiza yake, kufa,kuzikwa, kufufuka na kupaa Kwake. Nao waliagizwa kuzihubiri habari hizo njemakotekote (Mt.28:18ku. Mdo.1:8).

Kwa maelezo yafuatayo twapata kuona uzuri, usalama, umoja, uimara, utukufu,kudumu, na uangavu wa mji mtakatifu. Yote yaashiria utukufu wa Mungu.

k.12 Mji una ukuta mkubwa mrefu, na milango kumi na miwili ni ishara ya kuwaumejengwa juu ya ufunuo wa Mungu katika Agano la Kale na Agano Jipya. Watuwote wa Mungu tangu Israeli ya Zamani hadi Kanisa (Israeli mpya) watakuwemo,yaani hao wenyewe ndio mji. Iwapo mji una mipaka ipo nafasi kwa watu kuingia,sharti ni moja tu, wawe wamempokea Kristo na ukombozi wake. Mitume huitwamitume wa Mwana Kondoo, ukumbusho wa ukombozi. Bila imani halisi mtuhashiriki maishi ya mji huo. Iwapo haikuwa vigumu kuingia maana milangoilikuwapo pande zote kuonyesha kwamba Mungu hana upendeleo (Efe.2:19-22;Lk.13:28-29) hata hivyo milango ililindwa na malaika.

k.15ku Mji ulipimwa na yule malaika aliyesema na Yohana. Hapo nyuma katika11:1-2 tuliona hekalu lilipimwa na behewa nje ya hekalu halikupimwa, ishara yakuwa watu wa Mungu watalindwa wakati wa Kanisa kushambuliwa. Huendawazo hilo lahusu sehemu hiyo pia. Liko wazo lingine la kufikiri ni njia ya kusemakila sehemu ya mji inajulikana kwa Mungu na Yeye yuko kotekote (Zab.139:1-2).Hesabu ilikuwa ileile moja kwa urefu na upana na kwenda juu (mraba) ishara yaukamilifu na utimilifu wake. Katika Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu la zamanikipimo cha urefu na upana na kwenda juu kililingana. Huenda Yohana alionaulinganifu kati ya hekalu la zamani kwa sababu lilikuwa mahali pa Mungukukutana na watu wake na mji huo ambao pia ni „mahali‟ pa Mungu kuunganana watu wake kwa ukamilifu. Kipimo kilikuwa kikubwa sana ishara ya kuonyeshanafasi ni tele.

Page 133: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1503

k.18ku Yaspi na dhahabu safi mfano wa kioo safi, ni ishara ya utakatifu nautukufu wa Kanisa jinsi litakavyokuwa baadaye. Mji ni mzuri mno, Munguameupamba na uzuri usioelezeka, Mji umetoka kwa Mungu nao unamfunuaMungu (1 Yn.3:1-3). Vito na dhahabu ni ishara ya thamani kubwa sana ifaayoMfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana. Vito viliyotajwa vimefanana na vitovilivyokuwamo katika kifuko cha kifuani alichovaa Kuhani Mkuu (Kut.28:15ku).Huenda ni ishara ya Wakristo kuwa „makuhani na wafalme‟ (1:6). Wakristo ni„jengo‟ la Mungu, hekalu lake, naye amefanya kazi ndani yao kwa Roho wake nakuwatayarisha kuwa mke wa Mwana Kondoo. Sisi tumwaminio Kristo ni wathamani sana machoni pake (1 Kor.3:9; Tit.1:10). Imetubidi tujipambe maishayetu na tabia za Kikristo na matendo mazuri.

k.21ku Milango ni lulu nayo pia imepamba mji huo. Twakumbushwa maneno yaYesu katika mfano wa lulu nzuri. Ufalme wa Mungu ni wa thamani sana naunastahili mtu aviache vitu vyote vingine ili ampate Kristo (Mt.13:45-46). Njia yamji ni dhahabu safi, ukumbusho wa heshima kuu ya kifalme ambayo wafuasi waKristo wanaishiriki kwa kuwa ni warithi pamoja naye. Pia neno „njia‟ ni nenolihusulo mawasiliano, katika mji huo mawasiliano yatakuwa mazuri sana, meupe,bila hila yoyote.

k.22 Hekalu la zamani, na kabla yake hema ya kukutania, lilikuwa mahaliambapo Mungu aliahidi kukutana na watu wake (Kut.25:22; 1 Waf.6:11-13).Lakini hamna haja ya hekalu tena kwa sababu kuwemo katika Mji ni kuwapamoja na Mungu na Mwana Kondoo maana wao wamo humo, hamna haja yanjia ya kuwakaribia. Mji umekuwa „Patakatifu pa Patakatifu‟. Shabaha ya Injiliilikuwa kupatanisha Mungu na wanadamu. Mwungano umetokea (Arusi yaMwana Kondoo imefanyika) nao wataishi kama „mume na mke‟ katika uzima wamilele. Wale ambao wamempokea Kristo hawana haja ya kitu kingine chochote.Hekalu lilikuwa ishara ya Mungu kuwepo katika ulimwengu wake aliouumba nakuukomboa nalo lilishuhudia kwamba Mungu alikuwa angali akiendelea kuudaiutiifu wa wanadamu iwapo wamemkaidi na kumwasi.

k.23 Mji hauhitaji mwanga wa jua wala wa mwezi kwa sababu Mungu huangazamji na utukufu wake na Mwana Kondoo ni nuru yake. Hamna usiku wala gizawala chochote kilicho kinyume cha nuru (Isa.60:11). Hata alipokuwapo dunianiYesu alisema „Mimi ndimi nuru ya ulimwengu‟ (Yn.8:12) kwa Yeye watuwautambua uhalisi wa mambo. Uungu wa Kristo waonekana katika Yeye naMungu kuwa pamoja na kuwa „nuru‟ ya huo mji.

k.24-26 Halafu mji huo ni kwa watu wote, mataifa watakuwa huru kutembeandani yake na wafalme kuleta utukufu wao ndani yake. Kitu chochote kilichokizuri, safi, na chema kitaruhusiwa, utamaduni, ustaarabu na fani zote zakibinadamu zitakaribishwa mradi zimetakaswa na kuwekwa chini ya Kristo.Jambo hilo lathibitisha jambo la kila kitu kuumbwa kuwa chema sana mwanzoni

Page 134: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1504

(Mwa.1:31). Wengine huona kwamba maana yake ni utukufu na uangavu waKuwako kwa Mungu utawavuta WaMataifa na Wafalme waje na kumsujudia(Isa.60:11). Tumeishaona waliokombolewa watoka katika mataifa yote (7:9).Tumezoea kuwaza kuokoka kwa mtu mmoja mmoja ila sehemu hiyo yote yavutamawazo yetu kufikiri juu ya wokovu wa „jumuiya‟ mataifa kuletwa kwa Kristo ilimakusudi ya Mungu kwa mataifa yatimizwe (Efe.1:9-11). „haitafungwa kamwe‟hali hizo njema zitaendeleaendelea bila kukoma. Ni uzima wa milele, uzima tele,timizo la ahadi ya Bwana Yesu (Yn.10:10).

k.27 Iwapo nafasi ni tele na mengi yataruhusiwa hata hivyo, kamwe dhambihaitapata nafasi. Ni dhambi tu itakayomharamisha mtu. Injili ni takatifu, ni Injili yawokovu, njia ya mtu kusamehewa dhambi zake na kupewa uwezo wa kushindadhambi. Hivyo awaye yote akataaye kutubu na kusafishwa na damu ya MwanaKondoo haruhusiwi kuingia mle ndani ya mji (Yn.8:24). Msingi thabiti ni ukweli,wote waliouamini uongo wa Shetani na kudanganywa naye watapotea. Yohanaalitaja tena Kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo. Tumaini la kushiriki memahayo yote ni katika Kristo na kazi yake Msalabani.

MASWALI1. Yerusalemu Mpya ni badala ya „Mji‟ gani? na ni nini hasa?2. Baraka kubwa kwa waumini ni nini?3. Ni kitu gani ambacho kimepigwa marufuku katika Yerusalemu mpya?4. Watakaoingia watakuwa watu gani? nao watakuwa na hali gani?5. Maelezo ya jengo la Yerusalemu Mpya yanaisharia nini kuhusu maisha ya

baadaye?

SURA 22 KUJA KWA KRISTO

22:1-5 Uzima teleKatika sura 21 tulipewa habari za „ujenzi‟ wa Yerusalemu na katika sura hiitumepewa habari za maisha yake ya ndani. Tukilinganisha na habari za kwanzakabisa za Biblia twaona mageuzo makubwa yametokea. Katika Mwanzo tunazohabari ya Mungu kuuumba ulimwengu, hapo tunaambiwa habari za Mungukuumba umbaji mpya. Katika Mwanzo tunazo habari ya „Paradiso‟ Bustani yaEdeni na Mti wa Uzima ndani yake (Mwa.2:9-10; 3:1-24). Hapo tuna habari yaMji/Bustani na Mti wa Uzima. Mambo yote mema yaliyopotezwa na Adamu naHawa na wanadamu wote waliozaliwa baadaye, sasa wanadamuwanaomwamini Kristo wanarudishiwa na baraka zaidi ya zile walizokuwa nazohapo nyuma. Nabii Ezekieli alisema juu ya Yerusalemu Mpya (Eze.47:1-12) naZekaria pia alisema juu yake (Zek.14:8).

k.1 Yohana alisema alionyeshwa mto wa maji ya uzima, wenye kung‟aa kamabilauri (ishara ya utakatifu) na mto huo ulitoka katika kiti cha enzi cha Mungu nacha Mwana Kondoo. Asili ya uzima tele ni Mungu na Mwana Kondoo, Kiti cha

Page 135: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1505

enzi ni ukumbusho wa utawala na adhama yao. Yesu hushiriki kabisa Kiti hichocha enzi pamoja na Baba Yake, na maneno hayo ni ushuhuda unaouthibitishaUungu wa Yesu. Yesu aliyafananisha maji ya uzima na Roho Mtakatifuwatakayepewa wafuasi wake (Yn.4:14; 7:37-39). Taswira ni ya uumbajiunaobubujika na uzima tele, kwa njia ya Kristo. Uumbaji unafanywa upya naKristo Mwenyewe. Yeye ndiye huo uzima naye anashikamanisha yote (Kol.1:17).Mti huzaa daima, dalili ya utoshelevu na zaidi ya utoshelevu. Mti ni mti wa uzima,ni ishara ya uzima wa milele (Mwa.2:9; 3:22). Wanadamu walipomwasi Mungukwa kuivunja amri juu ya kuugusa mti wa ujuzi wa mema na mabaya walikataliwahuo mti wa uzima. Yerusalemu Mpya ni mji na bustani pamoja, si bustani tu kamaEdeni ilivyokuwa, kwa sababu Hawa amekuwa „mama‟ amezaa jamii kubwasana (Mwa.3:20). Kama ambavyo tumeishasema Mji ni ukumbusho wawanadamu kuishi katika hali ya jamii. Msingi wa jamii ya watu wa Mungu ni katikaushirikiano wao kwa wao na katika ushirikiano wao na Mungu. Maisha ya Kikristoni maisha ya kujihusisha vema na wengine na kujihusisha vema na Mungu. Maranyingi tumekaza maisha ya binafsi, ya kuokoka wenyewe tu, ambalo ni jambo lalazima, ila lisiwazwe kuwa jambo la kuishia hapo tu. Lengo si mimi niokoke tu,ila mimi niokoke na wengine waokoke ndipo sote tushirikiane vema hapo dunianina zaidi sana katika uzima wa milele.

k.2 „kuyaponya mataifa‟ haina maana kwamba magonjwa na maradhiyatakuwepo, ila ni maneno ya kuonyesha afya na uzima wa maisha ya baadaye.Hali za kwanza hazitajulikana tena.

k.3 Laana iliyokuwa juu ya uumbaji mzima imeondolewa (Mwa.3:17ku.Zek.14:11) hamna upanga wa kuizuia njia ya uzima. Mageuzo makubwayametokea, ziko baraka tele badala ya laana. Hivyo, uumbaji utarudia hali njemailiyokusudiwa na Mungu tangu mwanzo. Mungu atakuwa KATI, Yeye na Kristohushiriki Kiti cha Enzi (Yn.10:30) nao wataongoza yote bila kuwepo au kuinukatena kwa upinzani wa aina yoyote. Watatawala katika upendo. „watumwa wakewatamtumikia‟ neno hilo lina wazo la ibada ndani yake. Wanadamuwatamfurahia Mungu wao sana na kumpa utiifu wao wote bila wasiwasi, kwafuraha na kwa uhuru. Hautakuwapo ushawishi wowote wa kuuvuta usikivu wao.Maisha ya baadaye hayana uvivu, bali msingi wake ni ibada na huduma. Hamnakuchoka, ni kutumika kwa ukamilifu.

k.4 Watamwona uso kwa uso na kumtumikia kwa uhuru na furaha. Ni upeo waheri kumwona Mungu uso kwa uso bila kizuizi chochote. Ila tusifikiri juu ya umbolake hasa kwa kuwa hana umbo kama vitu vinavyoonekana huwa na umbo. Nithawabu ya Mungu kwa wasafi wa moyo (Mt.5:8) „jina lake litakuwa katika vipajivya nyuso zao‟ ishara ya kuwa mali yake. Watazishiriki tabia na hali zake kwaukamilifu (1 Kor.15:49; 2 Kor.3:18; 1 Yoh.3:2). Musa hakuruhusiwa kumwonaMungu uso kwa uso (Kut.33:20ku) ila katika dahari

Page 136: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1506

mpya watumishi wa Mungu watajaliwa heshima hiyo ya hali ya juu. Adamu naHawa walifukuzwa bustanini, hapo watu wakaribishwa katika Mji/Bustani; haoAdamu na Hawa waliharibu „mfano na sura ya Mungu‟ baadaye mfano na suraya Mungu utarudishwa na wafuasi wa Kristo watafanana na Bwana wao nakuushiriki Uana wake na kutawala pamoja naye kama watu walio wafalmepamoja na kuwa watumishi (Rum.8:17). Hatuna haja ya kuuliza „watatawalaakina nani?‟ haina maana ya kutawala juu ya watu fulani bali ina maana ya kuwawashindi.k.5 Hamna usiku, hamna haja ya taa (21:25) Mungu aliye Nuru atawatia nuru,na hali njema zote zitadumu milele na milele.

22:6-22 HitimishoHapo Yohana anafikia kumaliza Kitabu chake, ametoa habari za maonoaliyoyapata, sasa iliyobaki ni kutoa mausia kadha wa kadha hasa juu ya usomajiwa Kitabu.

k.6 Malaika aliusisitiza ukweli wa Kitabu akimwambia „maneno hayo ni amini nakweli‟ kama alivyomwambia hapo nyuma na sawa na Yesu alivyotajwa kuwa(3:14; 19:11; 21:5). Ni ujumbe wa kuaminika, ni ujumbe usiotolewa kwa kusudi lawatu kupanga orodha ya matukio ya historia bali kuwatia Wakristo nguvu yakuyakabili mateso yao. Bwana, Mungu wa roho za manabii ndiye aliyemtumamalaika wake kwa Yohana aliyekuwa miongoni mwa manabii. Tangu zamaniMungu alikuwa ameteua watu ili walete ujumbe wake kwa wanadamu (Ebr.1:2).Mungu ni Mungu wa roho zao mwenye madaraka juu ya fahamu zao na mioyoyao. Waliandika kulingana na tabia zao kibinafsi na kwa ubingwa wao wauandikaji, ndipo chini ya uongozi wa Roho ule ujumbe ulikuwa ni ule ambaoMungu alikusudia kuuleta kwa watu wake. Kwa hiyo ujumbe wao ni wakutegemewa kuwa yale ambayo Mungu alitaka watu wawe nayo (3:14; 19:11).Kwa hiyo Kitabu hicho kizima ni cha kutegemewa, na maneno yake kushikwa, iliwatu katika makanisa saba waelewe kwamba Mungu huwakumbuka katika dhikizao, na kuwashughulikia, na ya kuwa yanayowapata hayawi nje ya mamlaka namapenzi yake, Yeye huzidi kuuleta Ufalme wake na kuzikandamiza chini yakeenzi na mamlaka zote zilizo kinyume chake.

„hayana budi kuwako upesi‟ huenda ina maana kwamba mamboyaliyozungumzwa yatatokea hivi karibuni au yatakapotokea yatatokea „bilakukawia‟ kama kwa haraka. Ipo tofauti kati ya kutokea sasa na kutokea ghafula,na mara nyingi katika habari ya Kurudi kwa Kristo imeelezwa kama Kristoatatokea ghafula bila kufikiri „ghafula‟ ina maana ya „sasa hivi‟.

k.7 Kitabu ni unabii. Hapo Yesu ni msemaji. Alisema nini? Alitoa heri ya sita yaKitabu; „naja upesi, heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa Kitabu hiki‟. Ipobaraka kwa wale watakaoyashika maneno ya unabii wa Kitabu hicho. Kwa kuwasi maneno ya kujua kichwani bali ni maneno yanayohusu Mkristo na

Page 137: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1507

uaminifu wake kwa Bwana wake potelea mbali apatwe na shida gani hatakugharimiwa maisha yake. Baraka si katika kusoma tu, au kuzungumzia mamboyake tu, wala si katika kuyastaajabia maono yake tu, bali ni katika kuyashika.

k.8-9 Kama tulivyoona katika 19:10 Yohana alistaajabu sana alipotambua ukuuna mamlaka ya ujumbe wa Mungu hata akavutwa kumsujudu malaikaaliyemjulisha hayo yote. Akazuiliwa tena, akaambiwa amsujudie Mungu. Malaikani sawa na yeye na manabii (ndugu zake) na wale wayashikao maneno yaKitabu, yaani ni mtumishi wa Kristo, wote wanao wajibu mmoja, kumsujudiaMungu.

k.10 Yohana aliambiwa asiyatie muhuri maneno ya unabii wa Kitabu. Ni muhimunayo yapaswa yasomwe hadharani katika makanisa, watu wasidhani kwambaupo muda mwingi mpaka mwisho, bali kwao muda ni mfupi na katika muda huowamewajibika kumshuhudia Kristo na kuwa waaminifu Kwake. Ni „wakati wamwisho‟ haidhuru „Majira ya Injili‟ yatakuwa ya muda gani. Tangu Kristo Kujamara ya kwanza mpaka aje mara ya pili tumo katika wakati wa mwisho, hamnaufunuo mwingine, hamna tendo kuu lingine la Mungu kufanya. Amefanya yoteyaliyotakiwa kwa wokovu wa wanadamu (Ebr.1:1ku. 1 Yn.2:18).

k.11 Mungu ameufunua „mwisho‟ wa wanadamu. Mwanzoni kabisa Mungualipoumba ulimwengu alitamka maneno „iwe...ikawa...‟ (Mwa.1:3nk). Hapa kilamtu anaambiwa afuate kawaida yake maana wakati utakuja ambapohaitakuwepo nafasi ya kubadili mwenendo. Ni kama neno la kinyumekumwambia mtu „mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu‟. Liko onyo ndani yamaneno hayo kwa kuwa mtu ama hufanya mema, au hufanya mabaya, na kwakujizoeza katika kufanya mema au kufanya mabaya hukomaa katika hali yakekisha hushindwa kuibadili. Tabia ya mtu itaamua mwisho wake. Huenda ndaniya maneno hayo ni mwito wa kubadili kabla ya kuchelewa. Tena ni ukumbushokwa „mwenye haki‟ „azidi kufanya haki‟ kwa sababu ni wale tu wenye kudumumpaka mwisho ambao wataokoka (Mt.10:22). Jua linaloyeyusha vitu fulanihugandisha vitu vingine. Ndivyo ilivyo kuhusu watu, wema na fadhili za Munguhuyeyusha mioyo ya baadhi ya watu, huku wengine huendelea katika ugumu wamioyo yao. Iliyopo tutie maanani hali zetu za wakati huo kwa sababu mbelenihakuna neno katika Maandiko linalotuelekeza kufikiri kwamba nafasi yakuzibadili hali zetu itapatikana baadaye (Ebr.9:27). Leo ni siku ya wokovu, kwahiyo, tusiifanye migumu mioyo yetu (Zab.95:7ku).

k.12 Halafu Yesu alirudia kusema „Tazama, naja upesi, na ujira wangu upamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo‟. Yesu atakapokuja tenaataleta thawabu kwa watu. Thawabu ya nafasi ya kuingia mle ndani ya MjiMtakatifu, Yerusalemu Mpya kwa wale wote waliompokea na kumruhusu afanyekazi ndani yao na kwa njia yao. Neno ujira laonyesha kwamba mtu

Page 138: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1508

hupewa thawabu kulingina na jinsi alivyofanya. Wakati wote Mungu hufanya kwakadiri mtu alivyofanya, hamna upendeleo, yote yamejengwa juu ya haki. Kazi niushuhuda wa nje wa yaliyomo moyoni. Kila mara ambapo jambo la Kurudi kwaYesu limetajwa, ama hapo au katika Injili, limeunganishwa na neno la „kukesha‟na „kuwa tayari‟ hamna habari yoyote inayotueleza tutafiti ni lini.

k.13 Yesu alijiita „Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wamwisho‟ kama Mungu alivyojiita, ukumbusho wa Uungu na Umilele wa Yesu(1:8,17; 2:8; 4:8; 21:6). Kiti cha hukumu ni cha Mungu, pia cha Kristo(Rum.14:10; 2 Kor.5:10). Vitisho vyote pamoja na ahadi zote ni za milele.

k.14-15 Hapo twapewa „heri‟ ya saba, ya mwisho. Heri hiyo ni ya kiInjili. „Heriwazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjinikwa milango yake‟. Kwa kifungu hicho Yohana ameeleza wazi wale walio ndanina wale walio nje ya „mji‟, wale wa kuushiriki uzima wa milele na walewaliofungiwa nje. Kuhusu „wazifuazo nguo zao‟ maneno ni katika hali ya wakatiwa sasa. Waliompokea Kristo waendelee kuosha dhambi zao katika damu yakeya ukombozi iliyomwagika Msalabani (1 Yoh.1:7). Ni tendo hilo tulinalomstahilisha mtu awe na amri ya kuuendea mti wa uzima, yaani kupewauzima wa milele (1 Yoh.5:12). Wema wake peke yake hautoshi aupate huouzima. (3:4; 7:14; 1 Kor.6:11). „nguo zao‟ ni tabia zao.

k.15 Wa nje ni watendao mabaya, ambao wamezuiliwa kwa sababu ya tabia namatendo yao, ila isifikiriwe pengine wataweza kuingia baadaye. Neno lililotumikalamaanisha kwamba wamekataliwa kabisa, wasiingie kamwe. Mbingu mpya nadunia mpya zitakapotokea hamna „nje‟ tena kwa sababu waovu wote pamoja namabwana wao, joka, kahaba, mnyama wa kwanza na mnyama wa pili watakuwawametupwa katika ziwa la moto na kiberiti. Orodha ya waliofungiwa njeinafanana na 21:8. „mbwa‟ ni lugha ya kufananisha baadhi ya wafanya dhambina mbwa wakali waliotembeatembea humo mjini wakiokoteza takataka zake.Waongo si wale wa kusema uongo tu bali na wale walioupenda uongo, ambaohawakuwa na mzigo juu ya kweli. Yesu alimwita Shetani „baba wa uongo‟(Yn.8:44).

k.16 Hapo inaonekana Yesu alisema tena „Mimi Yesu nimemtuma malaika wangukuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa‟ Halafu alitia sahihi yake kwakutamka „Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi; ile nyota yenye kung‟aaya asubuhi‟. Kwa maneno hayo Yesu alithibitisha kwamba Kitabu kizima ni kwaajili ya makanisa, si zile barua saba tu. Hivyo ujumbe umetoka kwa YesuMwenyewe, maono na yote yaliyomo. Yeye ni ufunguo wa historia nzima yaWatu wa Mungu tangu watu wa Agano la Kale mpaka Kuja Kwake duniani. Yeyeni Masihi aliyeahidiwa katika Maandiko. Pia Yeye ni Nyota inayoashiria daharimpya itakayopambazuka atakapokuja kwa mara ya pili (Hes. 24:17; Rum.13:12;2 Pet.1:19). Maisha ya sasa ni matayarisho kwa siku

Page 139: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO 1509

ile kuu ya Kuja Kwake na kwa maisha mapya yatakayoifuata. Mungu anatakatuwe tayari, tuandae kwa ajili yake.

k.17 Ziko „njoo‟ mbalimbali, wala haiwi wazi sana kila mmoja inamhusu nani.Kwanza „Roho na Bibi Arusi wasema Njoo‟. Je! ni kumwita Yesu Aje? au nikuwaita watu waje kwa Yesu? Halafu „asikiaye na aseme, Njoo‟ Je! asikiayeanamwita Kristo aje, au mtu aje kwa Yesu? Ila maneno yafuatayo „Naye mwenyekiu na aje....‟ hapo ni wito kwa watu kumjia Yesu na kuupokea wokovu wake. Nijuu ya kila mtu kuitika, kwa kuwa wokovu ni bure, lazima mtu awe na „kiu‟ yaaniawe anasikia hamu sana. Kwa hiyo huenda mambo mawili yamewekwa kwapamoja, Kuja kwa Kristo mara ya pili na watu kumjia Kristo ili waushiriki Ufalmewake.

k.18-19 Mwaliko huo hufuatwa na onyo kali sana kwa kila mtu mwenye kuyasikiamaneno ya unabii wa Kitabu hicho. Onyo ni kwa mtu atakayeyaongeza na kwamtu atakayeyapunguza yaliyoandikwa humo. Maana yake hasa ni kuwaonyawatu juu ya kuupuuza au kuupotosha ujumbe huo na kutokuutia maanani. Mtuhawezi kupekuapekua mambo yake kwa kupenda mambo kadha na kuyawekakando mambo mengine. Adhabu ni kali sana, mapigo kuongezewa nakuondolewa sehemu katika mji mtakatifu na kunyimwa baraka za baadaye. Kwanini? kwa sababu Kitabu hicho kimejumlisha na kuuthibitisha ufunuo uliomokatika Biblia nzima. Ni Yesu Mwenyewe ashuhudiaye ukweli wa Kitabu. Kamatulivyoona mwanzoni mwake, Ufunuo ulitoka Kwa Mungu mpaka Yesu, kutokakwa Yesu mpaka kwa malaika, kutoka malaika mpaka kwa Yohana (1:1-2; 22:6;Yn.17:8). Ni onyo kwetu ili tuwe na tahadhari jinsi tunavyoufanyia kazi ujumbe waKitabu. Tukifikiri kwamba yaliyomo hayatoshi kwa wokovu, au kama tukifikirikuwa mengine hatuna haja kuyatimiza, ni kana kwamba kimawazo tunajifanyakama tunajua zaidi ya Mungu, hata kiutendaji tutakuwa tunadai kwambatunafahamu zaidi Yake. Tukifanya hivyo kwa kusudi twafanya dhambi juu yaRoho Mtakatifu. Hatuwezi kuyakwepa mambo yaliyomo.

k.20 Ahadi ya Kristo Kuja upesi. Tumeishaona kwamba neno la ushuhuda nineno muhimu katika Kitabu hicho na hapo tena Yesu Mwenyewe amelitumiakwa kutuhakikishia Kuja Kwake, tena kwa upesi. Kama ambavyo tumeona haponyuma kuhusu neno „upesi‟ tusiliwaze kama linahusu wakati tu bali lifikiriwakuwa neno la kusukuma mtu akate shauri kumpokea na kuwa mwaminifu kwaKristo maadamu yu hai. Yesu alikuwa thabiti juu ya uwezo wake wa kuzitimizaahadi zake na kuitawala historia ya wanadamu na kuuleta Ufalme wake juu yadunia nzima.

Itikio „Amina; na uje, Bwana Yesu‟ laeleza shauku ya kila Mkristo anapotazamiaKuja kwa Mwokozi na Bwana wake. Anataka sana Yesu aje (1 Kor.16:22).

Page 140: Ufafanuzi Wa Agano Jipya Ufunuo - Home - African Pastors ...d)Shabaha ya Kitabu e)Ujumbe wa Kitabu f) Mtindo wa Kitabu UFAFANUZI SURA 1 KRISTO YU KATI YA MAKANISA SABA 1: 1-3 Wito

UFUNUO1510

k.22 Yohana alifunga na baraka ya „Neema‟ kwa wale walio katika makanisaambao watasikia maneno ya unabii huo yakisomwa hadharani katika shirika zao.Twaokolewa kwa neema, kwa neema twapewa Roho kuwa msaidizi wetu ilituishi maisha ya Kikristo, na kwa neema twatazamia kuyashinda majaribu yetuyote na kumaliza safari yetu na „kufunga ndoa‟ na Kristo na kuishi naye katikaYerusalemu Mpya.

MASWALI1. Taswira ya mwisho aliyopewa Yohana ilionyesha nini juu ya maisha ya

baadaye?2. Ilileta habari ya kuondolewa kwa ............zote zilizosababishwa na

..............la wanadamu.3. Ni onyo gani lililotolewa?

Onyo hilo lilithibitisha nini kuhusu Kitabu hicho?4. Kitabu kilimalizika na wito gani?

MASWALI KUHUSU KITABU KIZIMA.1. Umejifunza nini kumhusu Mungu?2. Umejifunza nini kumhusu Kristo?3. Umejifunza nini kuhusu jambo la hukumu?4. Umejifunza nini kuhusu jamii ya Kikristo?5. Kwa nini Mwana Kondoo ametajwa sana katika Kitabu hicho?6. Ni matatizo gani yanayowakumba Wakristo wa leo hasa katika maisha ya

kumfuata?7. Watasaidiwaje na ujumbe wa Kitabu hicho?